"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, June 12, 2009

Walevi wa kazi!

Retirement HomeKama mwanamke una mume ambaye ni mlevi wa kazi jambo la msingi ni kukumbuka kwamba haina haja kuanza kuzozana au kukefyakefya kila usiku akichelewa kirudi, au kumkasirikia au kumnunia au kupigishana kelele.
Why?
Kwa sababu siku inayofuata anaweza akalala hukohuko ofisini kukwepa kelele zako.

Hakuna mwanaume anayeoa mke ili akirudi nyumbani apigiwe kelele, au anuniwe au akute mke amevimba mashavu kwa hasira, kwa nini asiende pangoni ?
Utafanyeje kama mume ni mlevi wa kazi?
Jambo la kwanza ni muhimu kufahamu kwanza sababu za yeye kuchelewa;
Je, anataka kupata promotion kazini?
Anafanya overtime?
Au amepata deal la kazi kwa muda au bosi amempa kazi ambayo ina deadline?
Je, mume wako ni boss kazini so inabidi ahakikishe kazi zimefanywa?
Je ni kazi ya muda au muda mrefu?

Je, mume anakwepa kuwa nyumbani labda kuna tatizo katika mahusiano?
Au kuna kubishana kuhusu kipato hivyo anajitahidi aweze kufikia pale wewe unataka?
Au yupo addicted na kazi tu?

Inawezekana anatumia muda mwingi kazini kwa sababu ni majukumu na ni kwa faida yako na familia kwa ujumla.
Hivyo inabidi uwe makini kujua sababu kwanza kuliko kuanza kupiga kelele.

Jambo la pili na la msingi ni kukaa pamoja kama mke na mume kwa upendo na kuzungumza kwa pamoja na kwa upendo suala la yeye kuchelewa kurudi na zaidi kwamba familia ni muhimu.

Jambo la tatu ni kuhakikisha unawasiliana naye na kuimarisha mawasiliano katika ndoa.
Kama ni wakati wa kuwa na mawasiliano naye basi ni wakati huu kwani anatakiwa kujua anahitajika nyumbani pamoja na kupenda kazi kote na kwamba familia pia ni muhimu.

Pia ukigundua ni mlevi wa kazi na kwamba anawaza na anategemea raha ya maisha miaka 47 ijayo kwenye retirement home basi hakikisha unamwandalia chakula chake (dinner /supper)mapema sana ili akirudi late usiku akikute (kimeganda) kesho atawahi zaidi.

Ikishindikana, kama kuna retirement home tafuta weekend moja nenda naye na mkifika huko tafuta wale wazee wa pale; kaa nao na wawape uzuri na furaha ya maisha uzeeni usisahau kuwauliza jinsi wanavyo-enjoy kuwa mwili mmoja angalau mara 4 au 3 kwa wiki na pia jinsi wanavyofurahia kucheza na watoto wao; anaweza kupata mawazo mapya.

Zaidi ya yote Muombee kwa Mungu!

2 comments:

angel said...

hy
mh yaan leo naona unanisema mimi kabisa mume wangu mtarajiwa ni mkaguzi wa mahesabu mda mwingi yupo kazin na safarini,hua namkosa sana na ye anaelewa hilo
sasa nawaza hapa bado tupo kwenye relationship and what about marriage?
tuna relationship ya miaka mingi karibu 8 yrs
najitahid kuzoea japo napata shida
asante kaka
angel

Anonymous said...

Dada Angel,

Jambo la msingi ni kukaa pamoja na kuzungumza kwa upendo na hekima ya juu sana kuangalia ni jinsi gani kila mmoja anamuhitaji mwenzio na mtaweza vipi kuhakikisha haileti shida.
Pia Omba Mungu maana wakati mwingine kwenye ndoa ni tofauti na uchumba.

Upendo daima