"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 31, 2009

There is more hunger for love and appreciation in this world than for bread.
~ Mother Teresa

Kelele kitandani!

Kwa mwanaume hakuna kitu kinakuwa sexy kama mwanamke ambaye anakuwa loud kitandani na si kuwa na vikelele tu bali kujihusisha moja kwa moja kwa mwanamke katika kuongea maneno matamu
(wengine huita dirty words hata hivyo hakuna dirty words hapa isipokuwa sweet words)

Mwanaume akiwa kwenye game anapenda sana kujua mke wake anajisikia vizuri kwa kile anafanya na kwamba mwanamke anaonesha total participation, pia vile mke unatamka jina la mume wako kwa manung'uniko ya kimahaba huleta raha sana pamoja na vikelele vingine kama vile ooooh! aaah! mmmh! nk humpa uwezo zaidi mume kuendelea kukurusha kwa namna ya ajabu na kuweza kukurishidha inavyotakiwa.

Kawaida mume huaanza kukuuliza kama kile anafanya unakipenda na kwa njia ni vizuri wewe mwanamke kumweleza vile unajisikia na unaweza kuji-express kwa uwezo wako wote na hapa ndipo unaweza kuongea sweet word zote (ulizojufunza au kadri feelings zako zinavyokupa taarifa kwenye kiungo kile kinapata raha au kinaguswa kwa mguso mtamu zaidi) si unajua mapenzi ni sana na msanii mzuri anajua nini aongee na aongee namna gani na mwanamke umejaliwa kuwa na sauti ambayo kwa miguno na kulalamika kimahaba mnaweza kuwa na sherehe nzuri sana ya kuwa mwili mmoja.

Kuwa kitandani ni opportunity kubwa sana mke kuweza kuonesha umaridadi wake haina haja kushona mdomo au kubaki kimya kama vile mume amelala na gogo badala jitume kwa maneno na matendo, huu ni uwanjawako, mume wako, jipe raha na enjoy raha ya mwili.
Piga kelele kwa raha zako na unaweza kutamka kitu kizima kizima bila woga maana huyo ni mume wa ujana wako.

Wanaume nao wakati mwingine huwa insecure kama wanawake wakiwa kitandani hivyo kumtia moyo kwa miguno na vikelele vya kimahaba huweza kumpa ushahidi kwamba una-enjoy kile anafanya na kwamba skills zake na utaalamu wake mke unampa credit naye atajisikia vizuri na kufanya zaidi na hata kujifunza siku nyingine afanye kwa ufundi zaidi.
Hivyo usiogope kuwa mbunifu, lazima uwe mshangiliaji mzuri kwenye mechi na mumeo na hiyo itakuhakikishia furaha zaidi wakati wa kuwa mwili mmoja.
Utakuwa rated 5 stars woman au kama ni shule basi maksi zako ni zaidi ya 95%

Mambo ya kuzingatia
Hata kama wanaume huwa tunafurahia sana mke kuwa noise kitandani ni muhimu kuwa makini na sauti kwani kupiga kelele kama unapigwa na majambazi si ustaarabu kwani mtaa mzima unaweza kuhamaki na kuja kutoa msaada kumbe watu mnapeana raha zenu au mnaweza ku-attract mijitu inayopenda kupiga chabo bure.
Ni vizuri hakikisha chumba kina Mfumo mzuri wa kuchuja sauti kwani mnaweza kushtakiwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria cha Antisocial behaviour order kwani baadhi ya nchi zinafuata na mnaweza kuishia jela au mkajenge nyumba yenu huko shamba mpigiane mikelele yenu.
Wanasayansi wanasemaje kuhusu mwanamke kupiga kelele kitandani?
Wanasayansi wa kijerumani katika utafiti wao wamegundua kwamba mwanamke anapokuwa na kelele kitandani wakati wa kuwa mwili mmoja mwanaume huwa na asilimia 59 za kukojoa (siyo mkojo) tofauti na asilimia 2 kwa mwanamke kuwa kimya na pia mwanamke huwa na kilele zaidi kitandani akiwa fertile na kwa mwanamke kuwa na kilele speed ya mwanaume na uwezo wa kusugua huongezekana maradufu wakati wa kuwa mwili mmoja.
Nakutakia weekend Njema!

Thursday, July 30, 2009

Your wife/husband is God’s creation.
If you reproach him/her, you are not condemning him/her but Him who made him/her.
John Chrysostom
(Picture - thehappyguide.com)

Chunga sana mdomo wako!

Sisi wote huwa tunaongea na marafiki na watu wa karibu kuhusu ndoa zetu, hata hivyo mambo tunayowaambia marafiki ni muhimu sana na huweza kuleta matokeo mazuri sana au mabaya sana kwa ndoa zetu.
Pia duniani tunatofautiana sana hasa kutokana na tamaduni zetu kwa mfano mzungu mara nyingi hana siri haijalishi ni siri ya kitu gani anaweza kukwambia kitu kinachohusu mume wake au mke wake kiasi ambacho unaweza kushangaa na tukirudi kwenye jamii zetu za kiafrika nasi kwa kutunza siri tunajua.
Kuna wakati kutunza siri ni upuuzi kabisa kwani ni siri ambazo ukificha mwisho wake kuna madhara makubwa sana.
Kwa mfano kuficha siri kwamba kabla hujaoana na huyo umeoana naye hukuwahi kuwa na mtoto wakati mtoto unaye na yupo na bibi yake kijijini, hiyo ni hatari kwani siku akigundua ni kweli trust kwako itapotea.

Leo tuangalie hili la kuongea siri za nyumbani kwako na mume wako au mke wako na mmoja wenu anaenda kzimwaga kwa marafiki zake, au wafanyakazi wenzake au mama yake au baba yake au ndugu zake kwa kukuzunguka na anaongea hayo mambo kiasi kwamba ungekuwepo asingethubutu kuongea.
Kulinda siri za mume wako au mke wako ni jambo muhimu sana hasa katika kuimarisha trust katika ndoa.
Bahati mbaya ni kwamba wapo wanandoa ambao wao kutoa siri za mke au mume kwa rafiki au watu baki kwake si tatizo ni kama mdomo una washa.

Yaani kitu kidogo tu mfano kuzozana kidogo tu na mume au mke usiku, ile kuamka asubuhi tayari umeshawambia baba, mama, ndugu, majirani na wafanyakazi wenzake kwamba jana mlizozana wakati wala hakuna faida anayopata na anadhani kuwaambia wengine basi yeye anafaa sana kumbe nao huishia kumdharau.

Unapokuwa ni mwanandoa mtoa siri nje unapoteza hadhi yako ya kuwa mwanandoa.
Ni kama unatengeneza kilema kwa partner wako hasa kwa wale unawaambia siri zenu.
Ndiyo, kuna wakati na pia ni muhimu kushirikisha wengine struggles za ndoa hasa mtu wa karibu ambaye unaamini anaweza kukushauri na kukusaidia lakini si kumwaga siri kwa kila mtu.

Ulimwengu wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa anatoka asubuhi na mapema kwenda kutafuta riziki na mke alikuwa na muda nyumbani kuendelea na kazi zake na watoto.

Siku hizi kila mmoja anaaondoka asubuhi na mapema kwenda kazini na huko kazini anatumia muda mwingi kuliko nyumbani, kubwa zaidi ni kwamba kazini anashinda na mke wa mtu au mume wa mtu au wanaume na wanawake ambao si mume wala mke au watoto.

Tafiti nyingi zinaonesha wanandoa wengi sasa wanatumie muda mwingi zaidi kazini kuliko kuwa na familia hii ina maana mwanandoa anatumia muda mwingi wa kazi kushinda na mke wa mtu au mume wa mtu na kama huyo mke wa mtu ndo amekuwa mtu wa kumwagia siri zake za nyumbani au chumbani kwake na mwenzi wake anakuwa ana date na huyo mke wa mtu au mke wa mtu bila kujua.
Kwani ku-share siri ni moja ya kuwa intimate na mtu ndiyo maana sasa tunakuwa na matukio mengi ya ofisi romance kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Hivyo chunga sana mdomo wako!
Muhubiri 3:7
... wakati wa kunyamaza na wakati wa kuongea kila kitu kina majira na wakati wake.

Wednesday, July 29, 2009

Kwa hivi utamtembelea jela tu!

Lily/EmmanuelNI JUKUMU ULILOPEWA NA MUNGU WEWE MZAZI KUHAKIKISHA WATOTO WANAKUWA NA NIDHAMU NA TABIA NJEMA.
Kujisahau na kufanya mambo yafuatayo unaweza kujikuta mtoto wako anaishia mikononi mwa polisi na anaishi jela baada ya kuachana na kuwa mtoto.
Na ukifanya yafuatayo ni kweli hutakosa muda wa kwenda kumtembelea jela.
Hakikisha unampa mtoto wako vitu vyote anavyovitamani.
Akikua na mtazamo wa aina hii atajua kwamba ni kweli duniani inaweza kumpa chochote anachotaka.

Ukiona ameanza kujifunza maneno mabaya na machafu, mchekee tu, hii inamfanya ajione yupo smart sana pia itampa nguvu ya kujifunza maneno mengine na sentensi zingine zenye maneno ya aina ileile ambayo siku moja yanaweza kukutikisa kama si kukufanya uzimie.

Hakikisha humpi nafasi ya kuwa na uhusiano wa kiroho (training). Subiri hadi awe na miaka 21 atakapoamua mwenyewe kujiunga na dini au kuchagua mwenyewe masuala ya kiroho au afuate na aishi vipi kiroho.

Hakikisha unakwepa wa nguvu zako zote kumtamkia kwamba “umekosea” ili usimsababisha ajisikia hatia. Mwambie ana akili sana kiasi kwamba hawezi kukosea kitu chochote.
Hii itamsaidia kujua ni kosa au si kosa kuvunja mlango wa gari lililoegeshwa na kukamatwa na polisi.

Hakikisha unamsaidia kazi zote hadi kuondoa sahani au vyombo wakati amemaliza kula au kumfulia nguo hadi akiwa na miaka 21 pia mwambie asijali sana kwani wenzake watakuwa wanamsaidia kazi mbele ya safari.

Hakikisha baba na mama mnazipiga mbele ya mtoto siku zote, msithubutu kupigana au kuzozana bila yeye kuwepo kwani kwa njia hii mtoto wenu (watoto) hatashangaa sana au kuumia sana siku mkiachana.

Mpe mtoto wako pesa zote anazohitaji kwa ajili ya matumizi yake, usimshawishi kutafuta pesa zake, kwa nini apate shida kupata pesa kama unavyofanya wewe? Ni mtoto wako mwache afurahie matunda ya kuwa na mzazi mwenye pesa, jitahidi kufanya hivi hadi afikishe miaka 21 hapo unaweza kuanza kubana au kumpa pocket money pungufu.

Hakikisha hakuna siku ana njaa, mpe kila aina ya chakula ambacho tumbo lake linaweza kubeba, pia kila kinywaji ambacho yeye anapenda hata kama unaweza kuagiza mbali kwani ni mtoto wako lazima umpe kitu roho na mwili vinapenda au vinatamani.

Usikubali majirani, walimu au polisi kuingilia maisha ya mtoto wako kwani hawa hawana uchungu na mtoto wako, mwenye uchungu na mtoto ni wewe mzazi, isitoshe mtoto ni wako si wao au jamii au jamhuri.

Siku ukiona amekasirika hakikisha unamuomba msamaha na mhakikishie kwamba hutarudia tena yeye za zaidi ya yote yeye ndiye yupo sahihi wakati wote.

Kama hujapata mtoto bado akishazaliwa tu hakikisha unampa jina ambalo hata wanafunzi wenzake wanaweza kumtania majina kama “Shida, Mateso, Chuki, Luleho (wabena mpo?), Fisi, Maskini, Sinahaki nk ilimradi tu likitamkwa jina lake lazima ataniwe.

NB:

Mlee mtoto katika njia ipasayo, Naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

Mithali 22:6

Tuesday, July 28, 2009

“Woman was taken out of man; not out of his head to top him, nor out of his feet to be trampled underfoot;
but out of his side to be equal to him, under his arm to be protected, and near his heart to be loved”

Kwa nini wanaume tu!

..............Wapendeni wake zenu kama Kristo anavyolipenda kanisa!Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake.
Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume.

Kwa nini Biblia imesisitiza zaidi ya mara nne mwanaume kumpenda mke na mara moja tu mke kumpenda mume na kumtii?
Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana.

Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama, nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alilalamika kwamba
“Without love I have no life” wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali.

Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa!
Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume.

Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali.

Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa!

Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume.

Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake.

References:
Ephesians 5:25
Ephesians 5:28-33
I Peter 3:7
Colossians 3:19
Proverbs 31:28-29

Monday, July 27, 2009

“To wish you were someone else is to waste the person you are.”
By Lazarus Mbilinyi

Ni mtazamo wako tu!

Walikatakata wakaondoa hivi lakini bado wakawa na furaha ajabu!Mithali 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.

Pia kuna msemo wa kingereza usemao
‘ A person never rises above his expectations”
Kwa maana kwamba ukitegemea kushindwa, kufanikiwa ni kitu kisichowezekana.
Pia ukitegemea kufanikiwa unaweza kufanikiwa kiwango chochote unachotaka, kwani upo hivyo kutokana na unavyowaza na kuweka mtazamo wako.

Tunapokuja kwenye suala la mahusiano (kufanya mapenzi katika ndoa au kuwa mwili mmoja au tendo la ndoa kwa mwanamke kuwa na IQ kubwa au vipaji (talents) au umri mzuri katika ndoa havina maana sana ukilinganisha na mental attitude uliyonayo kuhusiana na suala la kufanya mapenzi.

Wapo wanawake walioolewa (si wote) ambao ni warembo, wamesoma, ni portable, matiti katika size inayong’ang’aniwa na wanaume, wana vipaji vya ajabu na umri sahihi wa kuwa kwenye ndoa na sifa zingine kedekede zinazofanya aonekane mwanamke wa nguvu, lakini linapokuja suala la mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja wamekuwa si lolote na aibu tupu kama si kukatisha tamaa kwa waume zao.

Kwa upange mwingine wapo wanawake (si wote) kwenye wapo wapo tu na sura zao, wajasoma, IQ ni ndogo, wapo overweight, vifua flat kama wanaume, hawana hata uwezo wowote katika jamii; hata hivyo linapokuja suala la mapenzi au kitandani ni moto wa kuotea mbali na wanawapa waume zao vitu vya uhakika kitandani.

Na wapo ambao anaweza kuwa kwenye kundi lolote hapo juu na akawa zero kitandani au akawa moto kitandani.

Je, ni nini siri ya mwanamke kuwa moto kitandani na mume wake?
Ukweli si size wala shape wala appearance ya mwanamke ndiyo inayo dhihirisha ufundi wake kitandani bali mtazamo (attitude) kuhusu tendo la ndoa (sex) ndio msingi unaoweza kuelezea mafanikio na kushindwa kitandani.

Kama mwanamke anaamini kufanya mapenzi ni uchafu au ni kitu kibaya au mtazamo wowote potofu katika ndoa hataweza kuleta furaha ya kweli.
Kama anaamini mapenzi katika ndoa ni legalize rape basi hata siku moja hataweza kufurahia mapenzi atakuwa anajiona anabakwa kila siku.

Kama anaamini matiti yake ni madogo sana au makubwa kupita kiasi ambacho hawezi kufurahia kufanya mapenzi ni kweli hataweza kufurahia na anaweza kukosa feelings za kweli kuhusu mapenzi ndani ya ndoa.
Kama anaamini skills zake katika kufanya mapenzi ni pungufu basi hataweza kufurahia raha ya kuwa mwili mmoja.
Kama anaamini mwili wake upo ovyo kiasi kwamba hawezi kuwa uchi mbele ya mume wake basi ni dhahiri faragha na mumewe imeingiliwa.

Katika utafiti ambao ulihusisha wanaume ambao sehemu zao za siri ziliondolewa testicles (mapumbu) na wanawake ambao waliondolewa visimi (clitoris) na kuwachunguza wanavyofanya (enjoy) mapenzi na partners wao; ilikuja kujulikana kwamba walifurahia kufanya mapenzi sawa na wengine ambao wapo salama.
Hii ni kudhihirisha kwamba organs (kisimi na pumbu) hazikuwa msingi wa wanandoa kufurahia mapenzi bali jinsi wanavyofikiria au mtazamo wao kuhusu tendo la ndoa.

Hii ina maana unaweza kuwa na size, shape na appearance tofauti au yenye hitilafu kwa mtazamo wa jamii lakini ukiwa na mtazamo (binafsi) mzuri kuhusu mapenzi unaweza kufurahia tendo la ndoa kwa njia ya ajabu sana na unaweza kuwa moto kitandani na mumeo kukufurahia.

Sunday, July 26, 2009

Je, kwa urembo tu utampata?

Kuna usemi kwamba jinsi mwanamke anavyovutia physically kwa mwanaume ndivyo mwanaume humuhitaji zaidi.

Ukweli ni kwamba jinsi usivyokuwa concerned sana na physical appearance ndivyo mwanaume atakuhitaji zaidi na kama ndo dating unaweza kuona mwanaume anakuganda hadi inakuwa ndoa.

Nahisi unadhani hii haijakaa sawa hata hivyo subiri kidogo tuchambue.
Inaweza kuwa kweli kwamba Ukitaka kumvutia mwanaume ni muhimu kujipamba haswaa na kuvaa nguo ambazo zinaweza kumvuta mwanaume yeyote kwani ugonjwa wa wanaume wengi ni kile anaona.

Mwonekano wako unaweza kumvuta mwanzoni lakini hiyo haiwezi kukupa ticket kwamba atadumu na wewe au atakuona unafaa kuwa mke ndani ya nyumba ambaye kila siku atakuwa anasumbua suala la kutojiamini na uzuri wake wa nje.

Wapo wanawake warembo wengi sana wanaojua kujipamba kuanzia kucha za miguu hadi nywele kichwani, bado wapo single na wanaume wamekuwa wakipita na kukimbia.
Why?

Kawaida mwanaume huvutiwa sana na mwanamke ambaye emotionally anakuwa kawaida kuhusu anavyoonekana.
Mwanamke ambaye anahitaji sifa na attention kutoka kwa mwanaume kila mara kuhakikishiwa anapendeza wanaume wengi hukwepa kwa kuogopa kuishi nao maana ni usumbufu.
Ni wazi kwamba mwanaume huvutiwa na hupenda kuangalia uzuri wa nje wa mwanamke (beautifulness) na wakati huohuo pia mwanaume huwa turned off emotionally na mwanamke ambaye anapenda appended kwa sababu ya uzuri wake.

Mwanamke akiwa ana act au kuonekana anapenda kujisikia vizuri tu kwa sababu ya urembo wake wa nje mwanaume huhisi mwanamke mwenye uhitaji wa aina hii ni usumbufu na mara moja huanza kujitoa au kukimbia kabisa.

Mwanaume huvutiwa na kudumu na mwanamke ambaye kwanza anajisikia vizuri kuhusu uzuri wake awe amependeza au hajapendeza ila anajiamini na kwamba kama alivyo ndiye yeye. Pia kuna mambo mengine yanayofanya mwanaume avutiwe na kubaki na mwanamke kama vile tabia, ufahamu na mitazamo mbalimbali kuhusu maisha na kwamba kama wataishi pamoja huyo mwanamke atakuwa msaada kwa mwanaume kufikia malengo yake ya maisha na mafanikio si urembo tu.

Mwanamke huhitaji kupendeza na kujipamba kwa kadri anavyoweza hata hivyo bila kujiamini kwanza na kutokuwa too much concerned kuhusu urembo wake bado mwanaume huona si good marriage material au good relationship material.

Saturday, July 25, 2009

Weekend Njema!

Swali:
Mtaalamu au mtu anayetumia vifaa vilivyopo kwenye picha hujulikana kwa jina gani?

Friday, July 24, 2009

Vizuizi vya kufika kileleni!

Wanawake wengi huolewa wakiwa na uhakika kwamba mwanaume anayeoana naye anajua misingi ya masuala ya tendo la ndoa, ukweli ni kwamba wanaume wengi bado huwa hawajui chochote kuhusiana na masuala haya. Kutokuwa na ufahamu wa kutosha huwa kikwazo kikubwa na hukatisha tamaa wanandoa wote na kuna wakati wanaweza kujikuta wapo njia panda.

Tendo la ndoa au kuwa mwili mmoja ni muhimu kwa ajili ya kuijaza dunia pia ni muhimu sana kwa ajili ya mwanamke kupata raha kutoka kwa mume wake kupitia tendo takatifu la ndoa hasa anapofika kileleni wakati wa kuwa mwili mmoja.

Hata hivyo kuna asilimia kubwa sana ya wanawake hawajui kufika kileleni ni kitu gani na pia hata kama amewahi kufika basi ni mara chache na kubwa zaidi hajui kwa nini hawezi kufika kileleni akiwa na mume wake.

Sababu Zifuatazo ni moja ya mambo yanayochangia kwa kiwango kikubwa mwanamke kushindwa kufika kileleni (orgasm)

UJINGA
Kuna wanawake wanajua au wanafahamu baadhi ya mashine kama vyerehani lakini ukiuliza kuhusu viungo vyake vya uzazi hajui. Hali huwa mbaya zaidi pale mume na mke wote hawajui chochote kuhusu utendaji wa kazi wa viungo vyao za uzazi na hasa vile vinahusika na kuwa mwili mmoja.

Ni kweli katka zama za giza suala la mwanamke kufika kileleni lilikuwa halijulikani na mwanaume alikuwa anamtumia mke wake kwa raha zake na kujibinafsisha.
Hivyo ni muhimu mume na mke kufahamu utendaji wa viungo kuhusiana na suala zima la kuwa mwili mmoja. Kama hujui kisimi kipo wapi na kina kazi gani itakuwa ngumu sana kukufanyia kazi ili kitoe raha inayotakiwa au kusudiwa.

UNENE
Wanawake wengi ambao wana unene wa kupindukia pia hushindwa kujiamini au kuwa huru (self image) matokeo yake wakati wa kuwa mwili mmoja huhisi mume wake atachukia umbo jipya ambalo bibie kajiongezea hivyo anaweza kuanza tabia za kuogopa kuwa uchi mbele ya mume wake na matokeo ni kuwa disconnected kwenye feelings na tendo la ndoa na hata kama wakifanya anafanya kwa kujificha kwa mume wake (anaogopa kuonesha nyama zembe).
Na asilimia kubwa na overweight ni tamaa yao ya kufukia chakula bila utaratibu.
Anyway, kwanza hakuna uhusiano wa wewe kuwa fat na kuenjoy kuwa mwili mmoja na mume wake tatizo ni wewe tu hujiamini.

KUZUBAA
Wapo wanawake ni wazubavu wa hali ya juu wakati wa kuwa mwili mmoja. Wakati wa kuwa mwili mmoja analala tu kama gogo na kuacha mwanaume mchoyo na mbinafsi anajishughulishe na kumaliza hamu yake na kujiondokea kama vile hakuwa na kiumbe chenye uhai.
Tendo la ndoa ni contact sport (mchezo wa kugusana) ambao huhitaji watu wawili ambao wote wanashambulia kiwanja kwa juhudi zao zote.
Mwanamke anavyokuwa active ndivyo ataweza kutoa mwitikio wa wapi anajisikia utamu na kufurahia na hatimaye kufika kileleni. Wanaume ndiyo hufika kileleni haraka kwa sababu huwa active (ni genius) huwa hawazubai mke akishakuwa naked. Na mwanamke naye akichangamka urahisi wa kufika kileleni huwa mkubwa.

HATIA
Kuwa na hatia ya jambo lolote husababisha kufunga kwa hisia za ndani na kuzuia kuweka kufika kileleni.
Inawezekana unatembea na hatia ya mambo fulani uliyoyatenda katika maisha yako na yanakupa wakati mgumu kuwa free katika moyo wako.
Wakati mtu anakuwa amesamehewa dhambi zake, ufahamu wake (conscience) huwa huru na matokeo yake anakuwa ameondoa vizuizi vya kutofika kileleni.

MUDA
Kitu chochote cha kinachoridhisha huhitaji muda na tendo la ndoa halina msamaha. Zamani za kale (giza) kazi ya mwanamke ilikuwa ni kuzaa watoto tu linapokuwa suala la kuwa mwili mmoja na sex kati ya mke na mume ilikuwa sekunde 30 hadi dakika 3, lakini leo wanawake wamekuwa na uwezo wa kufurahia kuwa mwili mmoja na kupata raha at maximum.
Mke anahitaji zaidi ya dakika 10 hadi 15 kufikia kileleni na pia mwanaume anatakiwa kutoa movement za in and out kwenye uke angalau mara 75.

KUCHOKA
Ili kuwa na tendo zuri la kuwa mwili mmoja kiasi ambacho mke afike kileleni bila tatizo kitu cha msingi ni mume na mke kuwa na muda wa kutosha baada ya kupumzika.
Mke ambaye amechoka kwa kazi na majukumu hawezi kutoa cheche kitandani kwani amechoka.
Ni muhimu kuwa mwili mmoja baada ya wanandoa wote kuwa huru bila uchomvu wa aina yoyote.

MISULI DHAIFU
Inajulikana kwamba 2/3 ya wanawake ambao hawawezi kufika kileleni wana tatizo ya ulegevu au udhaifu wa misuli kwenye uke na ni rahisi sana kuondoa hili tatizo bila gharama kwa kufanya mazoezi ya kegel.

UBABE
Kumetokea wanawake ambao sasa nao wanakuwa kama wanaume hataki ku-surrender kwa mume wake, wanapenda kuwa viongozi wa kila kitu, wanapenda kutoa maamuzi, wana dominate kila kitu katika ndoa matokeo yake hata likija suala la kuwa mwili mmoja hataki kujikabidhi kwa mume wake kikamilifu ili amshughulikie kwa kusaidiana kupeana raha ya kuwa mwili mmoja.
Hawajikubali kama wao ni wanawake wanaohitaji mwanaume kumpa raha ya mwili mmoja matokeo yake feelings zao zipo disconnected na hata wakiguswa hakuna kitu.

Zipo sababu nyingi sana (click hapa) ambazo huweza kuzuia mwanamke asifike kileleni wakati wa kuwa mwili mmoja.
Je, wewe unadhani nyingine ni zipi?

Thursday, July 23, 2009

Picha kwa hisani ya servneinup Let your fountain be blessed, and rejoice in the wife of your youth, a lovely deer, a graceful doe.
Let her breasts fill you at all times with delight;
be intoxicated always in her love.

Proverbs 5:18 - 19

Haraka na rahisi

Kuna usemi wa zamani unaohusiana na biashara ambao unasema kwamba haiwezekani ukatengeneza bidhaa au huduma ambayo huwa nzuri, hupatikana haraka na ikawa rahisi kwa wakati mmoja.
Kwani bidhaa nzuri na rahisi haiwezi kupatikana haraka, na bidhaa nzuri inayopatikana haraka haiwezi kuwa rahisi hata kidogo na bidhaa inayopatikana haraka na rahisi haiwezi kuwa nzuri kamwe.

Hivyo basi huwezi kupata vyote vitatu bila kuvunja kanuni ya uzuri, uharaka na urahisi lazima kimoja kitolewe sadaka.

Je, unaweza kumpata mchumba kwa haraka, kirahisi na mzuri?

Unadhani kuna hasara na faida gani kama utampata kirahisi, haraka na mzuri?

Wednesday, July 22, 2009

“A kiss is an upper preparation for a lower invasion that will lead to further penetration in fast acceleration that will build the next generation”

Hii imepitwa na wakati!

Eti kwa fimbo mke hujifunza; ni aibu na imepitwa na wakati!Spouse abuse (mke na mume kutukana na kupigana) ni tabia mbaya sana katika ndoa na ina ugumu kuielezea kwa sababu inahusisha kuumizwa kimwili (Physical) na tukuko (emotions).
Abuse ya kimwili huhusisha kupigana ngumu, makofi au kutumia vitu kama mwiko, mikanda, fimbo na kitu chochote ambacho huwa karibu baada ya hasira kupanda.

Kwa upande mwingine abuse ya emotions huhusisha kutukunana kwa maneno ya aibu hata mbele ya public, kupeana maneno ya dharau na wakati mwingine hii shughuli huvuta mtaa mzima na watu kuanza kushangaza wanandoa wanavyochambuana kama karanga hata siri za ndani.
Suala la spouse abuse hutokea kila tamaduni, kila rangi za watu kila dini, waliosoma na ambao hawajasoma, maskini na matajiri.

Tabia ya kuwa abusive kwenye ndoa huanza tangu utoto hasa wala ambao wamekulia familia ambazo wazazi walikuwa ni abusive kati yao na kwa watoto pia.
Watu ambao ni abusive huwa hawajiamini na hutafuta security kwa kuwa abusive wa wapenzi wao na wengine kutokana na jadi zao huamini ndivyo mwanaume au mwanamke anatakiwa kuwa ingawa ukweli ni kwamba tabia hizi zimepitwa na wakati na hazifai ukiacha kwamba hakuna ustaatabu wowote.

Jamii kwa sasa zimepiga hatua katika suala la spouse abuse pia sheria zimeanza kutumia meno kusaidia kupunguza tabia za wanandoa kuumizana ingawa hadi mmoja wao atakapotoa taarifa kwamba anaumizwa vinginevyo huwa ni suala la wao wenyewe.
Zamani mwanaume alikuwa ni ruler na mamlaka yoyote haikuwa na business yoyote kwenye himaya yake.
Mke mwenyewe amemnunua kwa mahari na anamtumia kama kifaa chochote kinachonunuliwa na mwanamke hakuwa na uwezo wowote.

Hata hivyo suala hili huwa gumu kwani pamoja na kuwa abused bado kuna wanandoa huamua Kula jive kwa maana kwamba hawapendi jamii ijue nini kinaendelea katika kuta nne za nyumba zao, wengine hata wamevunjwa viungo bado hudanganya (hospitalini) kwamba wamepata ajali zingine na si kupigwa na wanandoa wenzao.

Biblia inaasemaje kuhusu spouse abuse?
Hakuna sehemu katika Biblia ambapo inaruhusu mwanaume au mwanamke kumkalia mwenzake katika ndoa isipokuwa kila mwanaume kuonesha ule upendo wa Kristo anavyolipenda kanisa kwa mke wake.

Ninyi wake watiini waume zenu kama ipendezavyo katika Bwana, ninyi waume wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
(Kolosai 3: 18 – 19)

Hapa Biblia inazungumzia ule upendo wa kujisadaka (sacrificial/unconditional) na kila aina yoyote ya abuse ni kinyume na huu upendo wa mwanaume kutoa uhai wake kwa ajili ya mke wake.

Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Efeso 5:22

Hapa wanaume wengi hujiona wamepewa tiketi au lungu kwa ajili ya kuwakalia wake zao hata hivyo Biblia inaelezea kitendo cha mwanaume kutoa upendo wa kweli ambayo husababisha mwanamke kuukubali kwa kutii.


Tuesday, July 21, 2009

Hupunguza Msuguano!

Ukiona yupo nervious, mhudumie vizuri!Wakati mwingine mwanaume hujikuta amekuwa mkali, majibu ovyo na mkato, violent na mwenye hasira kumbe tatizo ni kutotoshelezwa kimapenzi na mke wake, acha wale wanaume ambao ukali kwao ni nature.
Pia wapo wanawake ambao huwa violent maofisini hasa kama ni boss (siyo wote lakini) hata kitu kidogo tu kwake inakuwa issue.

Moja ya matokeo ya kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha, mke na mume kuridhishana na kila mmoja kuridhika na mwenzake ni kupunguza misuguano katika ndoa.
Mwanaume ambaye anapata huduma inayomridhisha kimapenzi huwa ni mwanaume aliyetulia (contented)
Hii haina maana kwamba matatizo makubwa yatatoweka yenyewe au kwa kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha basi ada ya shule watoto itapatikana haraka au itasaidia budget kuwa shwari.

“Mume wangu huwa mtulivu na mwenye ushiriakiano mzuri pale tu masuala la mapenzi yanapokuwa shwari na kurishidhana kimahana kwa kiwango cha juu kiasi kwamba hata kelele za watoto zinakuwa hazimsumbui au anakuwa mvumilivu, hata hivyo kukiwa na ukame wa kimapenzi mambo huwa tofauti”.
Mwanamke mmoja anayemjua mume wake vizuri alielezea.

Wapo wanaume wengi hawafahamu kwamba baadhi ya matatizo yanayokuwa nayo nyumbani na kazini yanaweza kuwa traced kwa kutokana na utoshelevu wa tendo la ndoa wanavyopeana mke wake pia mke mwenye hekima na busara huweza kutambua namna mume wake ana-behave nyakati tofauti na anajua dawa yake ni ipi.

Katika ulimwengu wa ndoa wakati mwingine matatizo madogo madogo huweza kupungua size kutokana na hali ya nzuri ya utendaji kitandani.
Hii ina maana kuna mizozo mingi ingekuwa haisikiki katika ndoa kama kila mmoja angejua kwamba kumridhisha mpenzi kimahaba inaweza kuwa dawa tosha.

Kuridhishwa kwa tendo la ndoa pia husaidia nervous system ya mwananmke kuwa relaxed.
Wapo wanawake kutokana na kukosa huduma au kuhudumiwa vizuri na waume zao hadi kuridhika kimapenzi wamekuwa wakali, wenye vurugu, visilani na hata maofisini kama ni boss kuwaka moto kwa kila mfanyakazi pasipo sababu ya msingi acha wale wanawake ambao ni wakali by nature.

Mfumo wa fahamu wa mwanamke umeunganishwa moja kwa moja na viungo vya uzazi na kila mwanamke kutoka kila aina ya maisha duniani ameumbwa kuwa na uzoefu wa kupokea furaha ya Ku-relax kupitia kitanda cha ndoa (sex).
Hivyo basi mwanaume anayejua raha ya mwanamke kuwa relaxed anakuwa mjanja kuhakikisha kitanda kinakuwa na moto wa kutosha.

Kwa habari zaidi soma hapa

Monday, July 20, 2009

Nitajuaje tayari!

Nitajuaje moto umewaka?Swali:
Nitajuaje mke wangu amesisimka vya kutosha na kwamba uke wake upo tayari kupokea uume wangu?
Jibu:
Ukweli ni kwamba mwanamke huwa tayari pale tu ukiwa na muda wa kutosha kuhakikisha amesisimka kiasi cha kutosha mwili mzima.
Mwelezo au dalili au alama (sign) kwamba (mwanamke) yupo tayari au amesisimka kiwango cha kutosha si kuwepo kwa majimaji ya uke tu (secretion/lubrication), au chuchu kusisimka na kuwa ngumu au kulegea kwa macho yake tu, au yeye kutoa miguno, kelele au sauti zinazoonesha anapata raha fulani, bali ni pamoja na kukua au kuongezeka maradufu kwa uke na kuta za uke kukuhakikishia kwamba uke upo tayari kupokea uume wa size na shape ya aina yoyote bila tatizo.

Sunday, July 19, 2009

The best prove of love is trust.

Saturday, July 18, 2009

Kukosa Uzazi -- Mwisho

Emmanuel/LorieKukosa uzazi huweza kuathiri ndoa katika njia nyingi, hii ni pamoja na kuweza hata kufikia hatua mume na mke kutengana na kwa upande mwingine huweza kusababisha mume na mke kuwa na bond imara kuliko kawaida.

Je, kukosa uzazi huweza kuathiri wanandoa kivipi?
Kutounganishwa ki-emotions:
Hii hutokana na ile hali ya mwanandoa mmoja kutaka kuongea kutoa hisia zake au kuongea kile anapenda na mwingine kushindwa kumwelewa mwenzake na kuhisi hamjali.
Kutokana na tatizo lililopo wanandoa hujikuta wapo disconnected katika hisia zao na kama mwanaume ndiye mwenye tatizo wakati mwingine inakuwa ngumu zaidi kuongelea kwani wanaume (wachache) huwa wabishi linapokuja suala la uzazi.

Suala la gharama (Pesa).
Kulipia gharama za kimatibabu kuhusiana na suala la kukosa uzazi (infertility) kama vile IVF (in vitro fertilization) kufanya vipimo huweza kutikisa sana ndoa yoyote iliyo imara na wanandoa huiweza kujikuta wakiwa na mzigo wa deni wakati hata mimba haijatungwa bado.
Huwa ni jambo la busara kujadili pamoja mke na mume ni namna gani wanaweza kufikia makubaliano wapi pesa zitapatikana na watalipa vipi.

Tofauti ya malengo ya maisha
Inawezekana mmoja kati ya wanandoa ambao wanatatizo la infertility anapenda kuwa na mtoto tena ile ya kupindukia na kama ni mwanaume wengine hali huwa tete kabisa katika ndoa.
Utofauti wa mitazamo huweza kuleta friction kubwa hata hivyo kuwa mume na mke ni pamoja na kukubaliana malengo ya maisha na kuimarisha bond ya ndoa.

Hata hivyo siyo tatizo la kukosa uzazi ndilo hudhoofisha ndoa bali jinsi unavyokabiliana na tatizo la kukosa uzazi ndicho kinachoweza kudhoofisha ndoa yako.

Kwanza kubali na kujikubali kwamba hii ni njia ndefu katika maisha na utaweza kukabiliana nayo.
Kubali kwamba unaweza kuishi maisha marefu kabla ya kupata watoto.
Hukuolewa au kuoa ili upate watoto bali kuwa na maisha pamoja na mwenzi wako katika hali zote hadi kifo kitakapowatenganisha na watoto ni matokeo au zawadi kutoka kwa Mungu na ipo siku Mungu atatimiza ahadi yake kwako kwani Mungu si mwanadamu.

Kuna wakati mmoja wenu au wote kwa pamoja mnaweza kupata habari zinazokatisha tamaa kutokana na tatizo lililopo, jambo la msingi ni kila mmoja kumsikiliza mwenzake ili kuhakikisha anajikisikia vizuri katika feelings zake.

Kuwa msikilizaji mzuri wa hisia za mwenzako, usitegemee mwenzi wako atasoma akili yako na kujua unahitaji kitu gani ni vizuri kila mmoja kujieleza vizuri kwa mwenzake anahitaji kitu gani kuliko kubaki kimya na baadae kuanza kulalamika kwamba hakujali.

Ni vizuri kuishi kwa kuridhika na kile kilichopo kuliko kuishia kwa kuangalia kile ambacho kinakosekana kwenye ndoa au mahusiano yenu. Kuwa na muda wa pamoja na kufurahia kwa pamoja furaha ya ndoa huweza kutoa ahueni kutokana na tatizo la kukosa uzazi.

Weka mipaka
Kama wazazi wako au ndugu zako wanapenda sana kuingilia ndoa kwa namna ambayo inaonesha kunaweza kuzua mgogoro zaidi ni muhimu kuwa makini kuweka mipaka ya uhakika.
Wanaume wengi ikitokea mke anashindwa kupata mimba wazazi wao au ndugu huja juu hata kumshauri kijana wao achane na huyo mwanamke.
Mwanaume lazima usimame imara kuhakikisha unamlinda mke na kuzidi kumpenda kwa kuhakikisha mnakuwa kitu kimoja.

Friday, July 17, 2009

Mwambie "Switch me on"

Kuna Swali ambalo liliulizwa na dada yetu kuhusu mume wake na dada GBennett amechangia kujibu swali kwa kumshauri kufanya mambo mbali mbali kama unavyoweza kusoma hapo chini

Swali lilikuwa:
Mimi ni dada nimeolewa nina kama 12 yrs ya ndoa na nina motto, mume wangu mzito sana kimapenzi kwanza huwa haonyeshi kuwa anataka tendo la ndo.
Ni mimi tu huwa najitahidi kuhitaji ninapojisikia hamu na pia yeye ni mzito kuniandaa hivyo hunipasa kumuandaa yeye na huwa anajilaza tu hafanyi kitu mpaka naamua kujishughulikia na ninamshukuru Mungu nafika kileleni kwa staili ambayo nikiitumia inanifikisha.

Je, nifanyeje ili nifurahie penzi la mume wangu no kises na kukumbatiwa yaani sijui ana tatizo gani?

Jibu
Shalom dada muuliza swali!
Napenda kukupongeza sana kwa kuuliza swali zuri na pia ili wengi tujifunze jinsi ya kuridhishana katika ndoa zetu.
Pia tujifunze kamba tukishirikiana mume na mke huku tukimuomba Mungu aonekane katika eneo au katika hii idara ya kuridhishana chumbani basi ndoa zetu zitakuwa rah asana.
Mimi ninachotaka kukushauri ni kwamba uwe mtu wa maombi sana, kwa maana kwamba ndoa inahitaji maombi mno na Mungu hujibu na unaweza kuhamisha kila mlima unaojitokeza katika ndoa.

Amka hata usiku wa manane omba kwa ajili yako na mumeo pia, mwambie Mungu amfungue na ampe ubunifu kwenye tendo la ndoa kwani Mungu ndiye ambaye alibuni sex katika ndoa na anajua kwa kupitia tendo la ndoa mke na mume huwa na wakati mzuri kujenga bond ambayo itawawezesha kuwa wazuri katika mahusiano ya mwili na roho.

Mimi huwa naomba ulimi wa mume wangu Yesu aufanye uwe mtamu na wa maneno matamu zaidi ya asali, tembea ya mume wangu ionyeshe utukufu, imani yake iwe kwa kristo, tamaa yake iwe kwangu tu, Mungu ampe ubunifu kwenye tunapokuwa mwili mmoja, anifanye nijisikie nipo paradiso, Mungu anifanye nitosheke nae, naomba Mungu anifanye niwe mtamu sana kwa Mume wangu, Niwe namvutia nay eye ananivutia, amfanye atosheke na mimi mkewe na kwamba kila siku niwe mpya kwake.

Dada lazima ufanye maombi ya namna hii, kabla ya tendo ombeni Mungu katika jina ya Yesu Kristo tendo la ndoa liwe tamu sana na kila mmoja aridhike, na baada ya hekaheka za kujiburudisha mshukuru Bwana kwa kuwafanya mjisikie raha.
Pia siku unayotaka tendo la ndoa uwe unapenda sana kuzungumza masuala ya mapenzi na mumeo mara kwa mara mkiwa wawili, weka utani utani kwa mumeo (hakikisha unatoa utani ambao hauwezi kumkwaza maana kuna watu wamelelewa tofauti).

Mfano mimi huwa namtania mume wangu na yeye anapenda sana na naamini huwa inampa matayarisho kwenye ubongo wake, kuna wakati namwambia leo nataka unitafune, hahahahah! Au leo namwambia typwritter haina red ribbon vipi utafanya typing?

Ni muhimu kuwa mbunifu dada, mnaweza mkawa mnaangalia TV halafu ukazima kusudi na ukamnong'oneza “switch me on” au unazima TV UNAENDA CHUMBANI HUKU UNAKUWA UMEANDIKA KIKARATASI KINASEMA “SWITCH ME ON” UNAMPA MKONONI AU UNAWEKA PEMBENI YAKE MAHALI ANAWEZA KUONA, utashangaa smile atakalotoa na lazima mtakuwa na wakati mzuri sana.

Pia waweza andika ka-note na kusema “Umebeba funguo, furaha ya maisha yangu yote” au “nakupenda sana I am proud of you” halafu unaweka kwenye mfuko wa shati lake analovaa asubuhib akienda kazini, au kama mmebarikiwa usafiri unaweka kwenye gari kwa siri kiti anachokalia kabla hajaenda kuendesha gari,au kwenye suite case yake, msifie mwambie yeye ni lulu ktk viumbe amezidi wote, kumbushaneni wakati mnaapa kanisani, rudieni viapo vya harusi yenu tena unaigiza sauti kama ni nzito igiza kuapa kwa kutumia sauti yake atacheka sana hapo hayo ni ktk kuwekana sawa ili aanze kukuchokoza yeye mfikie lengo la kuingia paradise.

Mwambie nakupenda wakati wotena asubuhi akienda kazini mwambie nakupenda na mpige busu usisubiri yeye kukupigia busu kila siku, akipiga simu baada mchana mwambie nakupenda akirudi home mwambie nakupenda yani nakupenda ni wakati wote pia unaweza kumtumia Text message muda wowote ukimkumbuka kwa njia hii itakuwa rahisi wewe na yeye kuweza kuongea mambo ya faragha kwa urahisi kwani mtakuwa mmevunja ukuta unaowafanya msiongee issue za chumbani.

Samahani nashindwa kutafsiri kwa kiswahili baadhi ya maneno hata hivyo naamini ujumbe kamili au wazo kamili umelipata.

Nakutakia mafanikio katika yale unahitaji kwa mume na nina imani kubwa Mungu atafanya na zaidi utafurahia ndoa yako kwani hakuna kitu kitamu duniani kama ndoa au mume na mke ambao wanatoshelezana idara zote.

Ukweli ni kwamba tofauti zilizopo kati ya mume na mke husaidia kutuweka karibu na kuwa kitu kimoja.

Ubarikiwe sana na Bwana
MS GBennett

Mwenzenu Mara Moja Kwa Wiki Mbili!

Akifurahi Hawezi Kulalamika! Mimi ni mwanaume mwenye miaka 32 najisikia kupenda sana tendo la ndoa niwe nifanya mara kwa mara, lakini mke wangu amekuwa hapendi kabisa.
Je, nitafanya nini ili kubadilisha hii hali kwani kwa wiki mbili tunafanya mara moja na hiyo moja ni kwa kulazimishana?

Kwanza asante kwa swali suri ambalo linasumbua wanaume wengi duniani ndani ya kuta nne za vyumba vyao.
Pili lazima ufanye analysis je, unampenda au unamtumia tu huyo mke wako?
Why?
Uzoefu unaonesha kwamba hata mwanamke asipofika kileleni bado huweza kufurahia tendo la ndoa (kuwa mwili mmoja) ikiwa tu mwanaume atakuwa mwororo (tenderness), ukaribu (closeness), anayeonesha upendo, anaye jali na mwenye mawasiliano mazuri na mke wake na mwanamke kujisikia anapata real love.

Ukweli ni kwamba mwanaume ambaye ni mbinafsi (selfish) na hajifunzi sanaa ya mapenzi ndani ya ndoa na anamtumia mke wake kutimiza mahitaji yake ya tendo la ndoa (sex) tu hawezi kujenga hamu ya mwanamke kuhitaji huduma ya kuwa mwili mmoja.

Labda kuwa na medical problems au matitazo ya ndani ya emotions zake (deep rooted) hasa kutokana na maisha yake ya nyuma (past life hata kabla hujamuoa) kama vile kubakwa au kudhalilishwa na mwanaume au ndugu wa karibu katika familia, hivyo kisaikolojia ameathirika.

Bottom-line ni kwamba maisha ya kimapenzi ya wanawake wengi katika ndoa huelezea (reflect) jinsi wanaume wanavyo wahudumia katika mzunguko mzima wa maisha yao ya kila siku ya wawili waliooana.

Ni mara chache sana kukutana na wanandoa wanaohitaji ushauri wa masuala ya tendo la ndoa, kama mwanaume anampa mke wake upendo wa kweli ambao mwanamke huhitaji hata kabla ya kuingia chumbani.
Mwanaume ambaye anajifunza sana ya mapenzi (kile mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume), ambaye anamjali mwanamke, ambaye anakuwa na muda wa kutosha kumuandaa (foreplay) na anayehakikisha mwanamke anaridhika na raha ya kuwa mwili mmoja (kudumu kwa muda mrefu wakati wa kuwa mwili mmoja) na kuendelea kuwa naye hata baada ya wote kufika kileleni (siyo unaenda ICU bila taarifa) huwezesha mwanamke kuvutiwa na tendo la ndoa na kujikuta anahitaji kila wakati bila kulazimishwa.

“Acha ile mume wangu anafanya kuniandaa kwa muda unaotosha, mimi huwa napenda sana kila kitendo cha yeye kuendelea kunikumbatia na kunishikashika kwa wororo (tenderness) hata baada ya kufika kileleni”
Luciana aliongea kwa wazi kile anakipata kwa mume wake James.

“Waaambie wanaume umuhimu wa mwanaume kumhudumia (maneno, tabia, upendo, mawasiliano) vizuri mwanamke wakati wa mchana kwani huweza kuathiri kwa kiasi kikubwa sex life usiku”
Grace alitoa haya maelezo kujibu swali kwa nini wanawake wengi hujikuta wamepiga password feelings zako kuhusiana na kutamani tendo la ndoa na waume zao

Mengineyo:
Kwanza chunguza ratiba yako ya kazi na ratiba yake ya kazi na analyse mgawanyo wa kazi uliopo na pia angalia kama huwa anachoka sana jioni au usiku kutokana na majukumu au kazi anazofanya.

Chunguza kama kuna aina yoyote ya mgogoro au matatizo ambayo hayajaweza kupewa solutions kwa muda mrefu na limekuwa donge moyoni mwake.

Je, unafahamu vizuri past life yake kimahusiano au kimapenzi na hakuna tatizo lolote la kisaikolojia au tabia ambazo amerithi kutoka kwao, wengine huamini sex ni uchafu hata baada ya kuolewa au kuoa.

Jichunguze kwanza mwenye ni kiasi gani umetengeneza mazingira ya yeye kupenda kuwa mwili moja kwani mwanaume yupo sex oriented wakati mwanamke yupo romance oriented.
Mwanamke romantic life kwanza then sex ingawa mwanaume hutaka sex kwanza.

Mwisho n muhimu kuliko yote, muombe Mungu akupe hekima na busara uongee naye kwa upendo wa hali ya juu na kwa uwazi kabisa, ukielezea ndoto yako katika suala la kuwa mwili mmoja na nini unapenda na nini unakosa, kwa kuwa ni mke wako ni wewe tu ndiye unaweza kuongea naye kwa urahisi kuliko mtu wa nje.
Naamini wengine wenye uzoefu wanaweza kukushauri zaidi!
Mungu akubariki sana!
+++++++++++++++++++++

Thursday, July 16, 2009

Mahali popote!

Hata njia za train wengine wametumia Swali:
Tuna miaka mitano (5) katika ndoa yetu na siku zote tumekuwa tunafanya tendo la ndoa kitandani tu, je ni sehemu zingine zipi zinaweza kutumika kwa wanandoa kufurahia kuwa mwili mmoja?

Jibu:

Ni kweli kitandani ndiyo sehemu ambayo ni rahisi (convenient), inayofaaa, inayotoa fursa na maalumu kwa wanandoa wengi kufurahia kufanya mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja. Hata hivyo si sehemu ambayo wengi hutumia kufanya mapenzi.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 90 ya wanandoa wanaofanya mapenzi huwa kitandani wapo wanandoa hutafuta sehemu zingine kutokana na mood au pale wanataka kitu kipya.

Ni busara na hekima sana kuwa creative na kufanya kitu kipya hasa wawili wakikubaliana na ikiwa tu hakuna tatizo litakalotokea kuharibu privacy yenu, kukamatwa, kudakwa au hata kushitakiwa kwani kuna sehemu watu hawaruhusiwi hata kama ni mke na mume.

"So, Sex is everywhere"

Hapa si suala tu la kuwa na sehemu tofauti za wawili kuwa na faragha bali aina za milalo na pia ubunifu kuhakikisha kwamba shughuli nzima ya kuwa mwili mmoja haiwi na utaratibu unaojirudia miaka nenda rudi.

Naamini hata wewe unayesoma hapa sasa hivi inawezekana umewahi tumia sehemu ambayo ukikumbuka unaishia kucheka hata hivyo ilikuwa ni kumbukumbu nzuri ndiyo maana umeishia kutabasamu.

Baadhi ya sehemu ni:
Kwenye shamba la mahindi, msituni, jikoni, bafuni, sebuleni, sakafuni, mezani, kwenye backyard huku kukiwa na nyota angani, kwenye gari, kwenye boat, chumba chochote kwenye nyumba yako, swimming pool, mlimani, kwenye mvua, beach nk.
Naamini wapo ambao wamewahi tumia sehemu zingine zaidi ya hizo.

Zifuatazo ni sehemu hatari kabisa kwa wawili kuwa mwili mmoja.
Beach
– kujisahau huweza kusababisha kubebwa na mawimbi, kumbuka ile issue ya tsunami.
Ofisini – kama ni ofisi yako au ofisi yenu na mke wako au mume wako it is ok, ila kama ni vinginevyo utaacha evidence ambayo lazima utafukuzwa kazi.
Makaburini (graveyard)- hata haielewiki watu wapoje, lazima akili iwe inaenda mwelekeo tofauti na binadamu wengine, hata hivyo tumeyasikia.
Kanisani – ni aibu na kukosa maadili hata hivyo tumesikia watu wanaenda church pews kutimiza haja zao za kimwili.
Kitandani au chumbani kwa wazazi wako – subiri ukamatwe ndo utajua kuwa ni risk kiasi gani.
Kwenye reli – mahaba yakinoga mnaweza kusagwa na train.

Pia ulimwengu wa sasa security Camera zinawekwa kila sehemu hivyo bila kuwa makini unaweza kushangaa issue zako zipo hewani bila kujua.

Wednesday, July 15, 2009

Kuishi Pamoja Kabla ya Kufunga Ndoa

Kuishi Pamoja Kabla ya Kufunga Ndoa Kunaua Ladha ya Ndoa

Kuishi pamoja kabla ya ndoa kunaua ladha ya ndoa na wapenzi wanaoishi pamoja kabla ya kufunga ndoa, ndoa zao huwa hazidumu muda mrefu kulinganisha na ndoa za wapenzi ambao huanza kuishi pamoja baada ya ndoa.
Kwa habari zaidi soma mtandao wa NIFAHAMISHE wenye habari nyingi zinazoweza kukufanya kufahamu mambo mengi yanayotokea duniani na pia uweze kuelimika.

Kukosa Uzazi

Emmanuel Lazarus Suala na kutopata mtoto (mimba) ni gumu sana na ugumu huongezeka zaidi kutokana na design ya ndoa za kiafrika ambazo suala la ndoa huhusisha jamii nzima kutaka kujua una mtoto au huna na ndugu huenda mbali zaidi kwa kutaka kujua sababu ambazo zinafanya wanandoa msiwe na mtoto.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba mwanamke ambaye ana tatizo la kushindwa kupata mimba (mtoto) huwa na wakati mgumu sawa na maumivu (kisaikolojia) ya mwanamke ambaye anaumwa Cancer au UKIMWI au ugonjwa wowote ambao ni Chronic.

Inawezekana kuna wakati unawaza sana hadi unajisikia uncomfortable kwa kuanza kufikiria hili suala na zaidi kuna wakati unapokea ushauri ambao hauna tija yoyote na unakupa stress zaidi na kubwa kuliko yote ni pale ambapo hata huyo ambaye alisema atakupenda katika hali zote hadi kifo kitakapowatengenisha anakupa maneno au matendo ya masimango hadi unatamani usingekuwepo duniani.

Pia inawezekana umemuomba Mungu hadi umefika mahali unajiuliza kama kweli Mungu anakuona au hayupo au anaupendeleo.
Ukweli ni kwamba Mungu bado ana mpango na maisha yako na anakuwazia mema na ni mwaminifu kutimiza ahadi zake kwako.
Pia hupo peke yako wapo wanandoa wengi ambao wanapita katika njia hii na zaidi ya yote ndoa zao zipo imara na zenye furaha ya kweli.

Kukosa uzazi (infertility) ni nini?
Wataalamu wana elezea kwamba kukosa uzazi ni uwezo wa kukosa kupata mimba kwa muda wa mwaka mmoja (miezi 12) wa kujaribu kupata mimba bila kutumia aina yoyote ya uzazi wa mpango.
Hata wanawake ambao hupata mimba na kuishia kutoka (miscarriage) pia hujulikana kama ni kukosa uzazi.
Wengine huita ni kuwa tasa na wengine huita ni ugumba (haya Maneno ni mazito sana ziwezi kuyatumia pia yanachanganya maana)

Kupata mimba ni mnyororo wa matukio tofauti kwani ili kupata mimba mwanamke anahitaji kutoa yai kutoka katika moja ya ovary zake (ovulation), na yai lazima lisafiri kwenda kwenye uterus (womb) kupitia fallopian tube na wakati huophuo liweze kuungana na mbegu ya mwanaume na kuwa fertilized na kukaa ndani ya uterus (implantation).
Kukosa uzazi huweza kutokea iwapo kutakuwa na hitilafu katika moja ya hatua zilizotajwa hapo juu.

Je, kukosa uzazi ni tatizo la wanawake tu?
Hapana, tatizo la kukosa uzazi si wanawake tu bali hata wanaume. moja ya tatu (1/3) ya tatizo la kukosa uzazi ni wanawake (female factor) wakati moja ya tatu (1/3) ni wanaume (male factor).
Na 1/3 inayobaki husababishwa nje ya sababu za mwanamke au mwanaume.

Nini husababishwa mwanamke kukosa uzazi?
Tatizo kubwa kwa mwanamke ni ovulation, kitendo cha yai kushindwa kuwa fertilized na moja wapo ya sign kwamba yai lake halitaweza kuwa fertilized ni kutakuwa na siku zake (MP)
Pia zipo sababu ndogondogo ambazo husababisha kukosa uzazi nazo ni
Kufunga kwa fallopian tubes kunakosababishwa na magonjwa.
Matatizo (physical) ya uterus kama vile kutoa mimba.

Pia vitu kama umri, mlo hafifu, kuwa overweight au underweight, sigara, pombe, magonjwa ya siri (STD), madawa (sindano za mpango wa uzazi) na matatizo ya afya yanayosababisha kubadilika kwa homoni.

Nini husababishwa mwanaume kukosa uzazi?
Mara nyingi mwanaume hukosa uzazi hasa kutokana na:-
Tatizo la kushindwa kutengeneza mbegu (sperms) – huzalisha kiwango kidogo sana au hakuna kabisa.
Tatizo la sperms kushindwa kulifikia yai na kufanya fertilization- inawezekana sperms zina shape au structure inayozuia kuweza kulifikia yai.
Wakati mwingine mwanaume anazaliwa na tatizo ambalo huathiri sperms zake na wengine tatizo huanza baadae ktk maisha kutokana na kuugua au injury. (kama vile cystic fibrosis)

Nini huongeza uwezekano wa mwanaume kukosa kizazi?
Ukweli ni kwamba uwingi na ubora wa sperms za mwanaume huweza kuathiriwa sana na afya yake na life style.
Vitu ambavyo huweza kupunguza uwingi na ubora wa sperm ni kama vile”
Pombe, madawa (drugs), kuvuta sigara, mionzi (chemotherapy), umri, matatizo ya afya, sumu kutokana na mazingira (lead, pesticides)
Bottom line:
Issue ya kupata mtoto ni issue sensitive mna kwa wanandoa, ni Mungu peke yake anayeweza kuwa na solution kwani pamoja na kuwa na kiwango cha juu sana cha technology bado suala la kupata mtoto limekuwa gumu (infertility).
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana
(Mathayo 19:26)

Tuesday, July 14, 2009

Tujadili basi!

Kama una aibu unaweza kujifunika, lakini lazima issue iongelewe! Sex ni somo au kitu ambacho ni exciting duniani, hata hivyo ni kitu kigumu sana na husumbua sana kujadili na hii inatokea mara nyingi kwa wale walio kwenye ndoa.

Mwanaume na ujanja wake wote kuna wakati hujikuta ananywea kuongelea suala la sex au kumshirikisha mke mpenzi nini wafanye ili wanapokuwa mwili mmoja kuwa na kuridhika kwa kila mmoja.
Pia wapo wanawake huogopa kuongea bayana na wazi kile wanahitaji kwa mume au mahusiano na kwa kuwa kuna stima kubwa kwa mwanamke kuwa passive kwenye ndoa matokeo kila mmoja anakula jiwe na wote huishia kuumia na kuugulia wakati wanandoa wengine duniani wanaongea na kuweka sawa mambo yao chumbani bila woga.

Kawaida unavyochelewa au kuacha kuongelea issue hii ya sex kwenye kuta nne za chumba chenu ndivyo inazidi kuwa ngumu zaidi na huzidi kuwapa disconnection ya feeling kwenu wawili.

Jambo la msingi ni kufanya haya Yafuatayo:-
Omba Mungu akupe hekima na busara ili uweze kujadiliana na mume wako au mke wako kwa upendo na wazi issue hii, wewe unadhani uliondoka kwa wazazi wako kuja kwake ili iweje kama si kupata mtu ambaye atakupa hitaji la mwili wako.
Hii issue ni muhimu kuijadilia kama mnavyojadili mipango mingine ya familia kama fedha na miradi.

Tafuta muda ambao wewe na mwenzi wako mnaweza kukaa chini na kujadili, tafuta sehemu ambayo imetulia na hamuwezi kusumbuliwa na kitu chochote.

Muhakikishie kwamba unampenda na onesha msingi wa upendo ulio nao kwake, elezea hisia zako halisi na kwamba kuna kitu ambacho hukipati katika maisha ya ndoa, na kwamba ungependa muongelee na ukipate.

Hatua kubwa na ya msingi ni kwa wote kukubali kwamba kuna tatizo.
Ukweli ni kwamba ukiona unashindwa kuongelea issue za sex kwenye ndoa, maana yake mnashindwa kuongelea mambo mengi ya msingi.
Pia kuongelea suala la sex ndani ya ndoa huweza kuwaweka karibu zaidi na wanawake hupenda sana hii topic kwani huonesha mwanaume anajali.

Tegemea kupata solution na uwe positive kwani unaweza kushinda tatizo lolote kwa kumtegemea Mungu

Wafilipi 4:13.

Monday, July 13, 2009

Nimepata swali lifuatalo ni nimeruhusiwa kulirusha na kila mmoja aweze kusoma na kama inawezekana kutoa maoni.
Swali:
Je, Ni kweli kwamba kisimi, kinembe (clitoris) ni kiungo pekee ambacho mume ni lazima aguse (chezea) ili mke asisimke na kuwa tayari kuwa mwili mmoja?

Jibu:
Si kweli.
Mwanamke si Channel za radio kwa maana kwamba ukibonyeza kitufe pale station inapatikana basi utapata frequency na kuanza kufaidi matangazo yake (muziki au bahari).
Mwanamke ni kiumbe ni kiumbe cha tofauti ambacho hutawalaliwa na hisia (emotions, mood na feelings).
Pia wanawake wote hutofautiana na hata huyo mmoja huweza kuwa tofauti kila siku hii ina maana kwamba kama jana alisisimka sana ulipomchezea kisimi si kanuni kwamba na leo atasisimka kwani inaweza kuwa katika mzunguko wake basi matiti ndiyo yanasisimka zaidi au G-Spot ndo anasisimka zaidi nk.
Ni jukumu la wewe mwanaume kuwa sensitive na smart kujua hitaji lake au ni kiungo gani kwa huo anasisimka zaidi.

Kuchezea kisimi chake si kanuni au sheria au utaratibu ambao umewekwa na kwamba usipofanya basi hakuna kusisimka, ingawa ni kweli mwanamke huweza kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi zaidi wakati mwingine kuliko kutwanga na kupepeta kwenye kinu.
Mwanamke anahitaji maandalizi kwanza, anahitaji busu, caring, anahitaji mwanaume mwororo, gentle, loving, anayebembeleza, mwanaume mwenye mikono slow na mwenye mwendo wa kube kuzunguka (kumtembelea) kiwanja kizima cha mwili wake kabla ya kufika huko kwenye kisimi.

Ni muhimu kwenda sehemu zingine za mwili kwanza kama matiti (chuchu) na sehemu zingine kuanzia zile ambazo zinasisimka kidogo hadi zile ambazo ukimgusa mwili wake unapata joto kiasi cha yeye kutoa ukelele ambao utajua kweli tumeanza kupanda mlima na kileleni tutafika.
Wanawake wengi (siyo wote) hulalamikia kitendo cha mwanaume kuwa na full speed kwenda kwenye kisimi bila kupita maeneo mengine kiasi ambacho huwa ni kuumia au kuumizana kwani kisimi huwa hakijawa tayari kupokea msisimko.

Kumbuka hili eneo lina zaidi ya nerves 8,000 hivyo ni muhimu kuguswa wakati ambao eneo lipo tayari na evidence kwamba kupo tayari ni eneo zima la south pole kuwa wet.
Kupeleka vidole vyako vikavu na bado kukavu huweza kuumiza badala ya kutoa raha.

Unataka kujifunza zaidi kumpa mpenzi wako kitu cha tofauti soma hapa

Ni jinsi ya kutumia tu!

Wanaume wengi na wanawake wengi huhofia sana size ya baadhi ya viungo vinavyohusika na uzazi (genital).
Wanaume wako concerned na size ya uume linapokuja suala la mapenzi, wakati wanawake wao wako concerned na size ya matiti na uwezo wa uke kuhimili uume mrefu, kwa bahati mbaya ujinga wa aina hii huzalisha hofu, mashaka na woga ambao hupelekea kutojiamini linapokuja suala la mapenzi.

Ukweli ni kwamba haijalishi mwanaume ni mrefu au ni mfupi au ni mnene kiasi gani urefu wa uume huwa si zaidi ya inches 6, na kiasi cha inches 3 tu za urefu wa uume wowote huweza au zinatosha kabisa kumfurahisha mwanamke kimapenzi na akaridhika.
(hapa muhimu ni skills jinsi ya kutumia sticks na si urefu wa sticks).

Pia haijalishi mwanamke ni mrefu kiasi gani au ni mfupi kiasi au ni mnene kiasi gani wanawake wote huwa na uke ambao hauwezi kuwa mpana zaidi au pungufu ya inches 1.

Utafiti unaonesha kwamba mwanaume mrefu sana akioana na mwanamke mfupi sana wanaweza kufurahia mapenzi (sex) sawa na wale ambao mwanaume na mwanamke wana urefu sawa.
Tofauti ya urefu wa kimo kati ya mwanamke na mwanaume huweza kuleta shida au matatizo wakati wa kupeana kisses wakati wa kuwa mwili mmoja.

Pia suala la mwanamke kuwa na matiti makubwa sana au madogo sana huwa na usumbufu wa aina yake kwa wanawake hasa wale wambao hawajaolewa.
Hata hivyo jambo la msingi ni kujiamini kwamba na kufahamu kwamba kuwa na matiti makubwa sana au kidogo sana maana yake huna tatizo na unaweza kuvutia na kuwa sexy sawa na wengine tatizo ni attitude yako.

Ubunifu wa Mungu kiuumbaji Kumefanya kusiwe na tatizo katika tofauti ya kimo (size) linapokuja suala la mapenzi au kuwa mwili mmoja.

Friday, July 10, 2009

ARE YOU SINGLE
Love is like a butterfly.
The more you chase it, the more it eludes you.
But if you just let it fly, It will come to you when you least expect it.
Love can make you happy but often it hurts.
Love is only special when you give it to someone who is really worth it.
Take your time and choose the best.

ARE YOU NOT SO SINGLE
Love isn't about becoming somebody else's "perfect person".
It's about finding someone who helps you become the best person you can be.

ARE YOU PLAY TYPE
Never say "I love you" if you don't mean it.
Never talk about feelings if they aren't there.
Never touch a life if you mean to break a heart.
Never look someone in the eye if all you do is lie.
The cruellest thing a man can do to a woman:
Is to let her fall in love when he doesn't intend to catch her fall.
It works both ways.

ARE YOU ENGAGED
The true measure of compatibility is not the years spent together, but how good you are for each other.

ARE YOU MARRIED
Love is not about "it's your fault", but "I'm sorry"
Not "where are you", but "I'm right here"
Not "how could you", but "I understand"
Not "I wish you were", but "I'm thankful you are"

ARE YOU HEARTBROKEN
Heartbreaks last as long as you want and cut as deep as you allow them to go.
The challenge isn’t how to survive heartbreaks but to learn from them.

ARE YOU POSSESSIVE
It breaks your heart to see the one you love Happy with someone else
But it ' s more painful to know that the one you love Is unhappy with you.

ARE YOU AFRAID TO CONFESS
Love hurts when you break up with someone.
It hurts even more when someone breaks up with you.
But love hurts the most:
When the person you love has no idea how you feel about him/her

ARE YOU STILL HOLDING ON
A sad thing about life is when you meet someone and fall in love, only to find out in the end that it was never meant to be, and that you have wasted years on someone who wasn't worth it.
If that person isn't worth it now, she/he's not going to be worth it a year or 10 years from now.
Source: Mtandao

Thursday, July 9, 2009


Usijidanganye!

Fikiria wewe ni mkulima na unataka kutumia jembe la kukokotwa na ng’ombe kwa ajili ya kulima shamba.
Kwa kuwa una Ng’ombe mmoja (dume) na Mbuzi mmoja (beberu) unaamua kuwafunganisha nira (yoke) ili uwatumie kukokota jembe na shamba lilimwe.

Ukweli huu ni uvivu wa kufikiri na ni kutaka kusababisha maafa.
Anyway mtu yeyote mwenye akili timamu atajua ubongo wako una matatizo kwani haijawahi tokea mbuzi na ng’ombe wakafungwa nira pamoja na shamba likalimwa.

Linapokuja suala la ndoa au mahusiano wapo watu ambao huamini kufungwa nira pamoja na mtu wa imani tofauti haina tatizo kama kwa ng’ombe na mbuzi kufungiwa nira moja na tayari kwa kulimba shamba.

Kama hujaunganishwa na mwenzi wako katika suala la kiroho basi mahusiano yako yanaelekea kwenye maafa.
Jinsi unavyoamini kuhusu Mungu, jinsi unavyoomba, jinsi unavyosherehekea holidays, kitabu gani unaamini ni kitakatifu, kuamini katika ubatizo upi ni moja ya components zinaweka mfumo wa kiroho wa maisha yako.

Kama hamuwezi kutazamana jicho kwa jicho kwenye maeneo haya basi unachukulia juu juu kile ambacho ni msingi moyoni mwako na umepofushwa na fall in love ila siku ukianza kuona you will be too late to catch the bus.

Kiroho chako na jinsi unavyoji-express ni kitu cha undani katika maisha yako na maumivu ya kichwa au kukatishwa tama kutajitokeza iwapo wawili watashindwa kuwa connect kwenye eneo muhimu kama hili.
2 Corinthians 6:14

Wednesday, July 8, 2009

Ukuni wa Asubuhi!

Moja ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika suala la tendo la ndoa (kuwa mwili mmoja) ni kitendo cha mwanaume kupenda kufanya mapenzi (sex) asubuhi anapoamka na mwanamke kuweka muda maalumu (reserve) kufanya mapenzi usiku kabla ya kulala.

Kwa mwanaume kupenda sex asubuhi huchochewa na kitendo cha kusimamisha bunduki yake zaidi ya mara tano usiku na anapoamka asubuhi (kitaalamu wanaita Nocturnal penile tumescence – NPT) na wengine huita morning glory au morning wood.
Hii kitendo cha mwanaume kuamka huku amesimamisha (erection) kwanza ni kuonesha kwamba ni rijali na pili hupelekea kuwa na sababu nzuri ya kumshawishi mke kuwa na morning glory kabla ya kuwahi kazini.

Hata hivyo mwanaume anahitaji kuwa makini kwani mke anaweza kuwa hata hajafungua macho na mzee anataka, approach unayotumia ni muhimu ili na yeye aweze kukubaliana na kufurahia kupeana one for the road.

Wengine Wanasema kufanya mapenzi asubuhi huweza kuelezea good day na great day.

Ukweli ni kwamba homoni za testosterone huhusika na masuala ya sex kwa mwanaume moja kwa moja na ingawa hizi homoni zinapatikana kwa mwanamke bado mwanamke ana homoni zingine zinazomsaidia masuala ya sex.

Hizi homoni hupenda na kushuka kwa vipindi tofauti yaani mchana usiku na asubuhi, kuongezeka kwa homoni huwa mkubwa wakati wa asubuhi basi utapenda kuwa na sex asubuhi kuliko usiku na kama huongezeka usiku basi utapenda sex usiku na kama huongezeka mchana basi utapenda sex mchana hii ni pale tu kuongezeka kwa homoni kunapokupa libido.

Bottom line ni kwamba binadamu ni complex individuals, hata kama homoni huweza kuathiri tabia zetu linapokuja suala la mapenzi bado si factor muhimu inayotakiwa kuzingatia jinsi tunavyopenda na kuishi na wapenzi wetu.

Je, ungeambiwa (wewe unayesoma sasa hivi hapa) uchague ile ya usiku au ile ya mchana au ile ya asubuhi ungechagua ipi?

Tuesday, July 7, 2009

Ya kwako ni Ipi!

Ni vizuri kufahamu kwamba ili mahusiano yadumu kuna umuhimu wa wapendanao kuwa na asilimia kubwa ya kufanana kwa tabia kuliko kuwa tofauti.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za mahusiano ambayo baada ya muda mwanandoa huweza kujikuta ndoto zinayeyuka.

Mahusiano ya hasira.
Hapa mtu anaenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye ni tofauti kabisa na familia yake kwa kila kitu na lengo ni kuikomoa familia yake (wazazi na ndugu) kwa sababu una hasira nao.
Kuna njia za kupamba na hasira lakini si katika kuoa au kuolewa kwani mwenye kuumia ni wewe.
Pambana na hasira zako kwa njia zingine pia jifahamu na uwe na moyo wa kusamehe ndo kuonesha maturity lakini si hasira na kwenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye yupo tofauti na wewe mwenyewe kwa lengo la kuwakomoa wazazi.

Mahusiano ya kimishenari
Haya ni mahusiano ambayo mmoja hujaribu kubadilisha dini ya mwenzake ili aoe au kuolewa “Usipobadilisha dini sikuoi au huwezi kunioa”,
Je, akikubali kubadilisha dini then akakuoa na baada ya kukuoa akaacha dini yako itakuwaje? Utajuta!
Ukweli ni kwamba mahusiano ya aina hii hayawezi kuwa na afya mbele ya safari kwani mmoja huwa na agenda ya siri (anaweza kusema ndiyo nimekubali kumbe moyoni hajakubali kabisa anakutaka wewe tu siyo dini yako) na bahati mbaya zaidi ukishaingiza mambo ya dini kwenye ndoa ni ngumu sana kuvunjika.
Unachanganya emotions za mapenzi na dini?
Romance na dini?
Atakukubali kubadilisha ila mbele ya safari (siyo mwisho) mmoja huangukia pua.

Mahusiano ya kutoa sadaka
Wengi hasa wanawake (si wote) huamua kujitoa sadaka kumpenda mwanaume ambaye hapendeki kwa malengo kwamba siku moja atanipenda asilimia 100.
Huu ni uhusiano kama wa mgonjwa na nesi kwa maana kwamba hujitoa kupenda, kufariji, hata kumtunza mpenzi wake kimavazi, chakula, pesa akitegemea atakuja kupendwa zaidi au kuolewa wakati huohuo anayefanyiwa wala hana mpango (wajinga waliwao).
Mahusiano ya ana hii huwa so exciting mwanzoni hata hivyo mwisho wa safari anayejitoa sadaka huona amedanganywa na kutumiwa.

Mahusiano Exotic
Haya ni mahusiano ya watu ambao kunatofauti kubwa sana ya utamaduni na mila.
Ni kweli mahusiano ya aina hii huwa exciting na adventurous.
Hata hivyo kuna wakati hukosa ladha, hivyo jambo la msingi kabla ya kuwekeza muda wako, nguvu zako, pesa zako kwenye haya mahusiano ambayo unaenda nchi za mbali kubeba exotic species hakikisha umefikiria miaka 50 ijayo.

Mahusiano ya tofauti ya umri uliokithiri
Hapa kunakuwa na tofauti kubwa sana ya umri wa wahusika, ni kweli age is just a number hata hivyo haiko hivyo wakati wote.
Kupishana miaka zaidi ya 20 kuna matatizo yake.

Hata kama unataka kuishi na mama au baba si suala la mke au mume kwani kuna wakati wanandoa huhitaji kuwa na fun ambazo kwa umri kupishana sana ni ngumu.
Hata tukiacha sababu ya kisaikolojia za tofauti kubwa ya umri suala la kupishana sana umri ni moja ya mahusiano yenye tofauti kubwa kuliko kufanana.

Mwanzoni inaweza kuwa raha kwani mwenye umri mkubwa anaweza kuwa amejijenga hata hivyo baada ya muda anaweza kukugeuka kwa hivyo vitu vyake, zaidi anakuwa hana energy kwa baadhi ya shughuli pia kuna kupishana sana katika interest kwani mwingine anakuwa wa miaka ya 47 iliyopita na mwingine kizazi kipya au unaweza kuona mwenzako ni kama mtoto au ana IQ ya kitoto kila siku.

Sunday, July 5, 2009

Mwingine akipewa zawadi hujiona anapendwa, mwingine hudhani unapoteza pesa! Mwanaume na mwanamke hutofautiana katika mambo mengi na hufanana katika mambo mengi pia.

Unapokuwa kwenye mahusiano ni jambo la msingi kufahamu kwamba hata kama kuna
tofauti bado kwa kuzikubali tofauti zilizopo na kumfurahia mwenzi wako ndoa huwa kitu cha kuridhisha zaidi kuliko kuendelea kujitahidi kumbadilisha mwenzi afuate misimamo na misingi uliyotoka nayo kwenu.

Baadhi ya tofauti na kufanana ni kama ifuatavyo:
Wanaume ni wajenzi na creators, huchukua risk na majaribio mara kwa mara wakati wanawake huchagua knowledge ambayo ni ya thamani na kuitumia generations to generations.
Wanaume huwa huru katika mawazo yao na utendaji wakati wanawake hupenda kufuata mawazo yanayopendekezwa na wengine.

Wanawake hupenda ku-criticize wao kwa wao wanaume huridhika na wenzao na utendaji wao.
Mwanaume na mwanamke wote huwa na chanzo cha kuridhika wakati mwanaume ni kazi na kipato kwa mwanamke ni familia na watoto.

Wanaume hujikuta katika kutekeleza malengo yao na kuwa kitu muhimu kwao wakati wanawake suala la mahusiano ya wengine huwa muhimu na msingi zaidi.
Wanaume huugua mara mbili zaidi ya wanawake ingawa wanawake huwa concerned na afya zao kuliko wanaume.

Wanawake huweza kuvumilia maumivu na kazi zenye usumbufu kuliko wanaume.
Wote mwanaume na mwanamke ndani yao kuna aina ya ubinafsi (selfish) na kukiwa na issue kila mmoja huwa na njia yake hivyo Usipoteze muda kwa kujaribu kumbadilisha kwa kuingiza sheria zako mpya na misimamo yako uliyotoka nayo kwenu kwa mke au mume au mpenzi wako badala yake furahia tofauti zilizopo na ndoa itakuwa na raha zaidi.

Wote mwanaume na mwanamke huwa na tabia ya kujitolea kuji-sacrifice vitu anapenda, au misingi yake ili kumfurahisha mpenzi wake mwanzoni mwa uchumba au dating.
Hata hivyo kwa kadri relationship inavyozidi kwenda huanza kujilinda mwenyewe na kuwa selfish tena.

Ndani ya kila mwanaume na mwanamke kuna sehemu inahitaji upendo (love) hata jitu katili kama Hitler alikuwa anayeyuka mbele ya love kutoka kwa mwanamke, wote tunahitaji caring, support, msaada na kutiwa moyo tukiwa wagonjwa au kujisikia tupo low emotionally au tunapofanya makosa, ingawa ni kweli mwanamke huhitaji company zaidi na caring zaidi kuhusiana na feelings zake wakati mwanaume huhitaji zaidi caring kwa tabia zake za nje kama usafi.

Wanaume hupenda kuwalinganisha wanawake na wanawake hupenda kuwalinganisha wanaume, wanaume huwapanga (rate) wanawake kwa appearance zao wakati wanawake huwapanga (rate) wanaume kwa wallet ilivyojaa (wealth), status katika jamii, mwonekano na sehemu ambazo watu wote wana magari basi mwanaume huwa rated kwa aina ya gari analoendesha.

Wote mwanaume na mwanamke huwa na mzunguko wa mood na kwamba baadhi ya siku katika mwezi kila mmoja huwa emotional.
Kwa wanawake hii ni kutokana na kiwango tofauti cha liquid kwenye mwili na utendaji wa ubongo siku wakiwa mwezini, hata kama wanaume hawapati siku moods zao zina mzunguko pia na kama mwanamke anamjua vizuri mume wake anaweza kujifunza na kufahamu signal na zaidi jinsi ya kumkubali.

Wote mwanaume na mwanamke wana wivu (jealous), ndani kabisa ya mwanaume na mwanamke kuna kiasi sawa na wivu wa mambo ya mapenzi tofauti ni kwamba wanaume huweza kuficha vizuri zaidi ya wanawake.
Wote mwanaume na mwanamke hutilia mashaka mahusiano (suspicious) tofauti ni kwamba mwanamke huwa mwepesi kuhisi mwanamke mwingine anaingilia mahusiano yake ni mume wake kwa kuangalia kubadilika kwa mumewe wakati mwanaume hupuuza au huchukua muda mrefu kujua mwanaume mwingine anaingilia mke wake.