"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 30, 2009

Chunga sana mdomo wako!

Sisi wote huwa tunaongea na marafiki na watu wa karibu kuhusu ndoa zetu, hata hivyo mambo tunayowaambia marafiki ni muhimu sana na huweza kuleta matokeo mazuri sana au mabaya sana kwa ndoa zetu.
Pia duniani tunatofautiana sana hasa kutokana na tamaduni zetu kwa mfano mzungu mara nyingi hana siri haijalishi ni siri ya kitu gani anaweza kukwambia kitu kinachohusu mume wake au mke wake kiasi ambacho unaweza kushangaa na tukirudi kwenye jamii zetu za kiafrika nasi kwa kutunza siri tunajua.
Kuna wakati kutunza siri ni upuuzi kabisa kwani ni siri ambazo ukificha mwisho wake kuna madhara makubwa sana.
Kwa mfano kuficha siri kwamba kabla hujaoana na huyo umeoana naye hukuwahi kuwa na mtoto wakati mtoto unaye na yupo na bibi yake kijijini, hiyo ni hatari kwani siku akigundua ni kweli trust kwako itapotea.

Leo tuangalie hili la kuongea siri za nyumbani kwako na mume wako au mke wako na mmoja wenu anaenda kzimwaga kwa marafiki zake, au wafanyakazi wenzake au mama yake au baba yake au ndugu zake kwa kukuzunguka na anaongea hayo mambo kiasi kwamba ungekuwepo asingethubutu kuongea.
Kulinda siri za mume wako au mke wako ni jambo muhimu sana hasa katika kuimarisha trust katika ndoa.
Bahati mbaya ni kwamba wapo wanandoa ambao wao kutoa siri za mke au mume kwa rafiki au watu baki kwake si tatizo ni kama mdomo una washa.

Yaani kitu kidogo tu mfano kuzozana kidogo tu na mume au mke usiku, ile kuamka asubuhi tayari umeshawambia baba, mama, ndugu, majirani na wafanyakazi wenzake kwamba jana mlizozana wakati wala hakuna faida anayopata na anadhani kuwaambia wengine basi yeye anafaa sana kumbe nao huishia kumdharau.

Unapokuwa ni mwanandoa mtoa siri nje unapoteza hadhi yako ya kuwa mwanandoa.
Ni kama unatengeneza kilema kwa partner wako hasa kwa wale unawaambia siri zenu.
Ndiyo, kuna wakati na pia ni muhimu kushirikisha wengine struggles za ndoa hasa mtu wa karibu ambaye unaamini anaweza kukushauri na kukusaidia lakini si kumwaga siri kwa kila mtu.

Ulimwengu wa sasa umebadilika sana tofauti na zamani ambapo mwanaume alikuwa anatoka asubuhi na mapema kwenda kutafuta riziki na mke alikuwa na muda nyumbani kuendelea na kazi zake na watoto.

Siku hizi kila mmoja anaaondoka asubuhi na mapema kwenda kazini na huko kazini anatumia muda mwingi kuliko nyumbani, kubwa zaidi ni kwamba kazini anashinda na mke wa mtu au mume wa mtu au wanaume na wanawake ambao si mume wala mke au watoto.

Tafiti nyingi zinaonesha wanandoa wengi sasa wanatumie muda mwingi zaidi kazini kuliko kuwa na familia hii ina maana mwanandoa anatumia muda mwingi wa kazi kushinda na mke wa mtu au mume wa mtu na kama huyo mke wa mtu ndo amekuwa mtu wa kumwagia siri zake za nyumbani au chumbani kwake na mwenzi wake anakuwa ana date na huyo mke wa mtu au mke wa mtu bila kujua.
Kwani ku-share siri ni moja ya kuwa intimate na mtu ndiyo maana sasa tunakuwa na matukio mengi ya ofisi romance kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.
Hivyo chunga sana mdomo wako!
Muhubiri 3:7
... wakati wa kunyamaza na wakati wa kuongea kila kitu kina majira na wakati wake.

6 comments:

Anonymous said...

Tumsufu Yesu Kristu!
Nimependa sana mada yetu ya leo siri ni kitu muhimu sana katika mahusiano hasa ambayo unajua hii ni kwa kujenga uhusiano imara.
yaani wanafundishaga vitu vingi kwenye kitchen party zetu wanasahau kuhusu utunzaji wa siri,na ndoa nyingi huvunjika kutokana na hili.

nilichogundua kwenye ndoa zetu tunatoa sana siri nje kwa sababu mume au mke bado wana ile deep shy kiasi kwamba unashindwa kuwa na mumeo kama best friend wako mnapeana siri zenu yaani ukimfanya mumeo hivo au mke hutaitaji mtu wa kumpa siri zako, mfano mimi nikikwazwa au nina furaha yangu wa ni mr kama ndio kazima cm simpati yaani ntahaha kiasi kwamba hata kazi hazitaenda mpaka nimwambie hata akinishushua lakini nimetua mzigo,rafiki wa kawaida ongea mambo ambayo hata mwenza wako akisikia ya kawaida mwingine ambaye unaweza kumpa siri zako kwa msaada ni mzazi maana mzazi hawezi akamuangamiza mwanae kwa ushauri mbovu.Kitu kingine ni kuongea na Mungu ni kitu kizuri sana umekwazika ingia chumbani piga goti lako mweleze.

Mwisho mimi nikigombana na mume wangu nasubiri kaingia kitandani maana hata kusali wote anakuwa kanuna basi nasali huku anasikia maombi yangu namuombea natubu huku anasikia, asubuhi anaamka hasira zimekwisha.

Mama P

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P.
Hongera sana kwa approach yako ni muhimu sana mume au mke kuwa rafiki yako na kwamba mnaweza kuongea kitu chochote bila wasiwasi. Pia kuwa makini na maneno tunaongea na ndugu zetu au marafiki zetu au wazazi wetu kuhusu wapenzi wetu na swali muhimu la kujiuliza ni je, hiki ninachoongea kuhusu mke/mume wangu yeye mwenyewe angekuwepo ningeongea mbele yake na akajisikia vizuri.
Ndoa ni process na huhitaji efforts ili iendelee kukua na kuleta feelings nzuri kati ya wanandoa, kuongelea mambo mabaya kuhusu mpenzi wako mbele za watu wengine haijengi bala ni aibu pia, wakati huohuo kumpa credit au sifa mwenzi wako mbele za watu ni muhimu na raha na inajenga uwe peke yako au pamoja.
Mke au mume ni namba moja kwa kila kitu na ni rafiki yako na kuongea naye siri zenu pamoja.
Pia bila kusahau kuombeana kwani maombi huweza kufanya kile Mungu anaweza kufanya.

Upendo daima.

Anonymous said...

Bwana Yesu asifiwe
majibu ya matatizo yanatoka kwa Mungu, nakumbuka huko nyuma nilipita kwenye mapito flani kwenye ndoa yangu Mume wangu alinikataa akawa hanitaki kabisa, kwa kweli niliona hakuna mwananadamu wa kunisaidia isipokuwa Mungu ndo mtetezi wangu, namshukuru Mungu sikumwambia Mtu kwa msaada wa ushauri, ilikuwa ni kufunga na kuomba sana na Yesu alijibu kwa mda mfupi sana, Mume akarudi na kuniona mimi ni mke wa thamani sana kwake na ananipenda mno. kweli Mungu ndo msaada pekee hata washenga wa harusi hawawezi kusaidia inafika wakati ni wewe na Mungu tu na hapo ndo Mungu anapoonekana kwa kishindo.

MAMA D

Lazarus Mbilinyi said...

Mama D.

Umeongea kitu halisi na njia sahihi ambayo tunatakiwa kuchukua pale tukikutana na matatizo katika ndoa zetu.
Ni kweli katika hali ya kawaida huwezi kumbadilisha mume au mke ila unaweza kumuathiri (positive au negative) kutokana na tabia yako.

Lakini Ukimuomba Mungu ambaye ndiye ailiyemuumba basi anaweza kumbadilisha na kuiweka ndoa kwenye mstari tena zaidi ya binadamu yeyote.
Ni kweli mshenga, wasimamizi na hata washauri ni muhimu sana hata hivyo anayejua vizuri yale unapitia ni Yesu peke yake maana maana anajua in and out bila illusions yoyote.

Kwa Mungu hakuna lisilowezekana hata ndoa iwe katika hali tete namna gani kwa maombi ya kufunga na kuomba inawezekana na baada ya yote ndoa hufufuka na kuwa kwenye raha mpya, muhimu hakuna kulala tena bali ni kuhakikisha efforts zinaongezwa kuipa afya ndoa na kwa njia hiyo ndoa zetu zitakuwa mfano na zaidi zitampa Mungu utukufu.

Upendo daima

Anonymous said...

SHALOM KAKA LAZARUS,
UTUNZAJI WA SIRI NI MUHIMU SANA TENA SANA, HATA KAMA MTU UNAPITIA WAKATI MGUMU KIASI GANI KWENYE NDOA YAKO LAZMA UTUNZE SIRI TU, HATA HIVYO LAZMA TUOMBE HEKIMA SANA MUNGU ATUFUNGE VINYWA VYETU.

MWANADAMU HAWEZI KUPA MSAADA WA KUSOLVE SHIDA UNAYOPITIA KWA UKAMILIFU KAMA HUTAAMUA KUMSHIRIKISHA MUNGU, MAANA KWAKE HAMNA GUMU LA KUMSHINDA.

WAPENDWA HILI SOMO LA UTUNZAJI SIRI NI SENSITIVE SANA TUSIWAMBIE HATA WAZAZI WETU HAYAWAHUSU, KWANI MUNGU ALIPOSEMA MTAAMBATANA NA MKEO/MUMEO KUWA MWILI MMOJA ALISEMA NA MAMA, BABA, SHANGAZI,MJOMBA, TUSIFUNZE KUWEKA WIGO HUSUSANI NDOA, INAMUHUSU MUME MKE NA MUNGU NDO FOUNDER. LOLOTE LITOKEALO MUNGU NDO WA KUSOLVE MAANA YEYE NDO BABA YETU ALITUPA BARAKA WA KUWA MWILI MMOJA.
HATA BIBLIA INASEMA PASIPO MUNGU HATUWEZI FANYA LOLOTE NA TUNAYAWEZA YOTE KTK YEYE ATUPAYE UWEZO NA NGUVU.

NAUNGANA NA MAMA P HAPO JUU MUME/MKE NI BEST FRIENDS HAMNA LA KUFICHANA LOLOTE, MUME WANGU NI LULU KWANGU NA ZAWADI YA PEKEE AMBAYO MUNGU AMENIPA, MAMBO YANGU ANAYAJUA YOTE NA MIMI YAKE NAYAJUA HAKUNA SIRI.

TUPENDE KUJIFUNZA KUPITIA ANOINTED BOOKS, MKE/MUME MWEMA ANAPASWA AWEJE NA MAENEO KAMA HAPA KWA KAKA LAZURUS NA KWINGINEKO KUNAKOJENGA LKN ZAIDI YA YOTE MUNGU NDO ANAESHIKILIA NA KUIMARISHA NDOA ZETU NA SI KWA UTASHI, USOMI AU HADHI YA MTU.

MBARIKIWE SANA

MS GBENNETT

Lazarus Mbilinyi said...

Wapendwa!

Ni kweli kuna wengine wameangamiza ndoa zao kwa kuwa waropokaji wa mambo yao ya ndani (mke na mume) kwa wengine kwani si wote wanapenda mafanikio ya ndoa yako.

Hata hivyo Mungu ni mwema anayetupa hekima na maarifa na kugundua ujanja wa adui.

Mbarikiwe na Bwana

Upendo daima