"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 23, 2009

Haraka na rahisi

Kuna usemi wa zamani unaohusiana na biashara ambao unasema kwamba haiwezekani ukatengeneza bidhaa au huduma ambayo huwa nzuri, hupatikana haraka na ikawa rahisi kwa wakati mmoja.
Kwani bidhaa nzuri na rahisi haiwezi kupatikana haraka, na bidhaa nzuri inayopatikana haraka haiwezi kuwa rahisi hata kidogo na bidhaa inayopatikana haraka na rahisi haiwezi kuwa nzuri kamwe.

Hivyo basi huwezi kupata vyote vitatu bila kuvunja kanuni ya uzuri, uharaka na urahisi lazima kimoja kitolewe sadaka.

Je, unaweza kumpata mchumba kwa haraka, kirahisi na mzuri?

Unadhani kuna hasara na faida gani kama utampata kirahisi, haraka na mzuri?

6 comments:

Anonymous said...

shalom,
naweza uchangia kwamba kama kijana au binti amemshirikisha Mungu kwenye swala zima la kupata mchumba au mke au mume inategemea anaweza pata haraka kutokana na maombi yake au akachelewa kupata pia, kuna wengine wanasema anataka ndani ya miezi hii 6 apate mchumba na kweli anapata na ndani ya miezi 6 ijayo awe ameoa au kuolewa na kweli inatokea anafunga ndoa. kaka lazarus mi nadhani ni swala la mtu binafsi kuhusu mda mrefu au mfupi kiasi gani anataka apate huyo mchumba. wengine wanataka wachunguze mpaka kabila lake ,ukoo anaotoka, ni mtu wa kiroho kiasi gani n.k.

cha msingi ni kumshirikisha Mungu katika uchaguzi tena ikiwezekana mwambie Mungu haja ya moyo wako, Mungu anasema tutoe hoja za nguvu na tupewe haki yetu.

kuna wengine kutokana na umri kuona umesonga anaamua awaridhishe ndugu na jamaa yake kukubali tu yeyote ajae mbele yake, ambae si chaguo la Mungu kwake na hii imewagharimu wengi sana na wengi wameishia kutalikiana na kuumia hata kufa pasipo mpango wa Mungu wao kufa

ushauri wangu ni kwamba wapenzi tusiombe mchumba, bali tuombe mke au mume maana anapokuja unajua kabisa huyu ni mume niliyeomba lakini ukiomba mchumba watakuja wengi sana sasa utaanza tena kuhangaika yupi ni yupi kwa kulinganisha vigezo vyako binafsi ujuavyo, na wengi wameumia sana unakuta mwanamme anadate na wasichana 10 eti wote anawachunguza ndo nini hii? yani hata vijana wanaojiita wa kiroho wanafanya mchezo huu nimeona kwa macho yangu.

ushauri ni kwamba wewe kijana au binti kama unapenda siku moja uwe na ndoa yako mwombe Mungu akupe mume mwema au mke mwema mwambie YESU jinsi mumeo au mkeo unayemtaka na hakika utapewa hivyo hivyo jinsi ulivyoomba na biblia yanasema awazavyo mtu ndivyo atakavyokuwa na uombacho ndicho upewacho. mimi niliomba Mungu anipe mume na sio mchumba na kweli nilivyoomba ndivyo Mungu akanipa the best husband in the world

mbarikiwe sana

MSGBennett

Anonymous said...

Bwana Yesu atukuzwe!unajua nini kaka Mbilinyi ukitaka mchumba wa haraka mwenye mvuto aaaa mbona mara moja unapata, ila mchumba ambae unategemea awe ndio mkeo mama wa watoto wako lazma utumie muda na mazingira nayo ni muhimu kuzingatia nikiwa na maana point ya kwanza ya makutano na huyo binti.

sasa nianze na madhara ya mchumba wa haraka:migogoro katika ndoa yenu haitaisha kwa maana hamkujuana tabia
Faida itakuwa ni kuwaonyesha watu tu kuwa mkeo kisura ni mzuri yaani wasifu wa nje.

Mama P,

angel said...

hy
its not easy to get all those 3 compliments das y we human beings we are not perfect kila m2 anao upungufu flan even me
thanx kaka mbilinyi

Lazarus Mbilinyi said...

Nami naungana na waliotoa mchango hapo juu.

Suala la msingi ni kwamba siku za leo ndoa nyingi zimekuwa zinaishia kwa mwanandoa mmmoja kukimbia au kumwacha mwenzake au kuishi kwa kuruvugana, au kuwa na kajehanamu kadogo nyumbani kwa sababu watu hawapo makini kutafuta mchumba (mke au mume) na tunaishia kulaumu kwamba ndoa ni mbaya wakati wabaya ni sisi wenyewe tunaoingia kwenye ndoa kwa kutafuta wachumba kirahisi na haraka tukidhani ni wazuri.
Muda unaotumia na nguvu unazotumia na resources unazotumia huku ukimshirikisha Mungu huweza kutoa picha kamili ya ndoa yako hata kabla hamjaoana na walio na hekima na busara akikuuliza jinsi ulivyopata mchumba na muda umetumia anaweza kukwambia ndoa yako itakuwaje.
Tungejua msingi wa ndoa ni katika kutafuta yule utaingia naye kwenye ndoa basi tungetumia vyote tunaweza au tunavyo kuhakikisha tunapata candidate wa uhakika ambaye hata katika dhoruba na shida mtapendana na kusonga mbele na zaidi ndoa yenu kumpa Mungu utukufu.

Siku hizi vijana wanaangalia pesa, urembo ambao ni wa muda, kazi nzuri, utanashati na vitu vingine ambavyo miaka 40 ijayo havina maana yoyote.

Ndoa kama institution ni nzuri ila candidates ndiyo wenye shida na matatizo na matatizo mengi hutokana na wanavyochaguana kuingia kwenye ndoa.

Upendo daima

fikirikwanza said...

There is not formular as a guide for this matter.

fikirikwanza said...

There is not formular as a guide for this matter.