"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 22, 2009

Hii imepitwa na wakati!

Eti kwa fimbo mke hujifunza; ni aibu na imepitwa na wakati!Spouse abuse (mke na mume kutukana na kupigana) ni tabia mbaya sana katika ndoa na ina ugumu kuielezea kwa sababu inahusisha kuumizwa kimwili (Physical) na tukuko (emotions).
Abuse ya kimwili huhusisha kupigana ngumu, makofi au kutumia vitu kama mwiko, mikanda, fimbo na kitu chochote ambacho huwa karibu baada ya hasira kupanda.

Kwa upande mwingine abuse ya emotions huhusisha kutukunana kwa maneno ya aibu hata mbele ya public, kupeana maneno ya dharau na wakati mwingine hii shughuli huvuta mtaa mzima na watu kuanza kushangaza wanandoa wanavyochambuana kama karanga hata siri za ndani.
Suala la spouse abuse hutokea kila tamaduni, kila rangi za watu kila dini, waliosoma na ambao hawajasoma, maskini na matajiri.

Tabia ya kuwa abusive kwenye ndoa huanza tangu utoto hasa wala ambao wamekulia familia ambazo wazazi walikuwa ni abusive kati yao na kwa watoto pia.
Watu ambao ni abusive huwa hawajiamini na hutafuta security kwa kuwa abusive wa wapenzi wao na wengine kutokana na jadi zao huamini ndivyo mwanaume au mwanamke anatakiwa kuwa ingawa ukweli ni kwamba tabia hizi zimepitwa na wakati na hazifai ukiacha kwamba hakuna ustaatabu wowote.

Jamii kwa sasa zimepiga hatua katika suala la spouse abuse pia sheria zimeanza kutumia meno kusaidia kupunguza tabia za wanandoa kuumizana ingawa hadi mmoja wao atakapotoa taarifa kwamba anaumizwa vinginevyo huwa ni suala la wao wenyewe.
Zamani mwanaume alikuwa ni ruler na mamlaka yoyote haikuwa na business yoyote kwenye himaya yake.
Mke mwenyewe amemnunua kwa mahari na anamtumia kama kifaa chochote kinachonunuliwa na mwanamke hakuwa na uwezo wowote.

Hata hivyo suala hili huwa gumu kwani pamoja na kuwa abused bado kuna wanandoa huamua Kula jive kwa maana kwamba hawapendi jamii ijue nini kinaendelea katika kuta nne za nyumba zao, wengine hata wamevunjwa viungo bado hudanganya (hospitalini) kwamba wamepata ajali zingine na si kupigwa na wanandoa wenzao.

Biblia inaasemaje kuhusu spouse abuse?
Hakuna sehemu katika Biblia ambapo inaruhusu mwanaume au mwanamke kumkalia mwenzake katika ndoa isipokuwa kila mwanaume kuonesha ule upendo wa Kristo anavyolipenda kanisa kwa mke wake.

Ninyi wake watiini waume zenu kama ipendezavyo katika Bwana, ninyi waume wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
(Kolosai 3: 18 – 19)

Hapa Biblia inazungumzia ule upendo wa kujisadaka (sacrificial/unconditional) na kila aina yoyote ya abuse ni kinyume na huu upendo wa mwanaume kutoa uhai wake kwa ajili ya mke wake.

Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Efeso 5:22

Hapa wanaume wengi hujiona wamepewa tiketi au lungu kwa ajili ya kuwakalia wake zao hata hivyo Biblia inaelezea kitendo cha mwanaume kutoa upendo wa kweli ambayo husababisha mwanamke kuukubali kwa kutii.


No comments: