"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 21, 2009

Hupunguza Msuguano!

Ukiona yupo nervious, mhudumie vizuri!Wakati mwingine mwanaume hujikuta amekuwa mkali, majibu ovyo na mkato, violent na mwenye hasira kumbe tatizo ni kutotoshelezwa kimapenzi na mke wake, acha wale wanaume ambao ukali kwao ni nature.
Pia wapo wanawake ambao huwa violent maofisini hasa kama ni boss (siyo wote lakini) hata kitu kidogo tu kwake inakuwa issue.

Moja ya matokeo ya kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha, mke na mume kuridhishana na kila mmoja kuridhika na mwenzake ni kupunguza misuguano katika ndoa.
Mwanaume ambaye anapata huduma inayomridhisha kimapenzi huwa ni mwanaume aliyetulia (contented)
Hii haina maana kwamba matatizo makubwa yatatoweka yenyewe au kwa kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha basi ada ya shule watoto itapatikana haraka au itasaidia budget kuwa shwari.

“Mume wangu huwa mtulivu na mwenye ushiriakiano mzuri pale tu masuala la mapenzi yanapokuwa shwari na kurishidhana kimahana kwa kiwango cha juu kiasi kwamba hata kelele za watoto zinakuwa hazimsumbui au anakuwa mvumilivu, hata hivyo kukiwa na ukame wa kimapenzi mambo huwa tofauti”.
Mwanamke mmoja anayemjua mume wake vizuri alielezea.

Wapo wanaume wengi hawafahamu kwamba baadhi ya matatizo yanayokuwa nayo nyumbani na kazini yanaweza kuwa traced kwa kutokana na utoshelevu wa tendo la ndoa wanavyopeana mke wake pia mke mwenye hekima na busara huweza kutambua namna mume wake ana-behave nyakati tofauti na anajua dawa yake ni ipi.

Katika ulimwengu wa ndoa wakati mwingine matatizo madogo madogo huweza kupungua size kutokana na hali ya nzuri ya utendaji kitandani.
Hii ina maana kuna mizozo mingi ingekuwa haisikiki katika ndoa kama kila mmoja angejua kwamba kumridhisha mpenzi kimahaba inaweza kuwa dawa tosha.

Kuridhishwa kwa tendo la ndoa pia husaidia nervous system ya mwananmke kuwa relaxed.
Wapo wanawake kutokana na kukosa huduma au kuhudumiwa vizuri na waume zao hadi kuridhika kimapenzi wamekuwa wakali, wenye vurugu, visilani na hata maofisini kama ni boss kuwaka moto kwa kila mfanyakazi pasipo sababu ya msingi acha wale wanawake ambao ni wakali by nature.

Mfumo wa fahamu wa mwanamke umeunganishwa moja kwa moja na viungo vya uzazi na kila mwanamke kutoka kila aina ya maisha duniani ameumbwa kuwa na uzoefu wa kupokea furaha ya Ku-relax kupitia kitanda cha ndoa (sex).
Hivyo basi mwanaume anayejua raha ya mwanamke kuwa relaxed anakuwa mjanja kuhakikisha kitanda kinakuwa na moto wa kutosha.

Kwa habari zaidi soma hapa

2 comments:

Anonymous said...

habari wapenzi wote wa blog hii,
mimi napenda tu kuchangia kuhusu ni kwa jinsi gani waweza epuka migogoro ndani ya ndoa.
kama nilivyokwisha eleza hapo awali ndoa inahitaji maombi sana tena sana, yani inatakiwa utenge muda maalumu kwa ajili ya kuombea ndoa yako, i mean mume, mke na watoto + ofisi yako kama mwajiriwa/biashara yako.

kwanini nazungumzia sana maombi, unapomwomba sana MUngu shetan hana jeuri ya kukuvuruga, maana unaomba unabana sehemu zote hana nafasi.

ntatoa mfano mimi huwa naombea ndoa yangu,inakuja swala la nyumba tumebarikiwa kuwa na nyumba zetu naombea pia nyumba nazifunika kwa damu ya Yesu na kila aina ya majanja yeyote yawe moto, kimbunga na makusudi ya shetan yanavunja kwa damu aya Yesu, alaf naombea usafir nazindika magari yote kwa damu ya Yesu,alaf naombea ofisi yangu nateketeza kila roho za mafarakano, wivu,chuki, husda,vijicho,hasira,wizi,uchawi na maonevu kwa jina la Yesu,nafunika ofisi kwa damu ya YESU nafanya hivyo kwa ofisi ya mume wangu pia maombi hayo hayo. naombea watoto, ndoa yangu nazindika kwa damu ya Yesu, nafanya toba kwa nafsi yangu na mume wangu na watoto, kila kisicho mpango wa Mungu nakivunja kwa jina la Yesu, roho ya ugomvi, kiburi,hasira,jeuri nazivunja pia.

sasa kutokana na maombi kama haya unakuwa umemmaliza shetan kila mahali hana nafasi kujipenyeza utakuta huwezi patwa na hasira au ghadhabu unashangaa unaishi vizuri na mumeo mkiwepo ndani na hata baada ya kurudi kazini hamna mtu mwenye hasira kwa ajili ya kukwaza ofisini maana tayari nilishaweka ulinzi wa Mungu ofisini,nyumbai namkila mahali mapema usiku wa manane niamkapo kuomba.

namaliza kwa kusema ili kuepuka hasira na ugomvi ndani ya nyumba zetu lazma ujitoe mhanga wa kuamka panapo utulivu, na mda mzuri ni usiku wa manane uombe ili Mungu awape rehema, na haya maombi ni ya mtu binafsi sio na jumuia, haya wamama wenzangu na wababa tuchangamke hapo.

mbarikiwe sana

MS GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana kwa comments zako kwani mnaisha ya kiroho (maombi) huweza kuimarisha maisha ya kimwili (kuridhishana).

Ubarikiwe sana na Bwana kwa kujitoa kutoa maoni yenye kuonesha upo makini na unapenda sote tuwe na ndoa zenye kumpa Mungu utukufu.

Upendo daima