"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 4, 2009

Huweza kuteka moyo wake!

Mwanamke hutumia kiasi cha uhakika cha pesa wakati mwingine na muda wa kutosha kuhakikisha mwonekano wake unampa jina la sifa.
Wakati huohuo mwanaume huweza kuitwa handsome kama ataonekana tofauti kidogo na gorilla (joking) ili mradi awe na sifa za msingi zinazoonesha yeye ni best seed.

Wanawake hupenda (si wote) mwanaume ambaye anaonesha yeye ni strong, ni mwanaume (masculine), wealth, status katika jamii na anayeweza kuwa kiongozi wa familia kiroho na kimwili.

Wapo wanaume ambao kuwa na kichaka cha ndevu ni kuonesha identity au image yao nao ni wachache, wanaume wengi hunyoa na wapo wanawake wanapenda wanaume wenye chaka la ndevu na wapo wanaopenda wanaume walionyoa videvu na kuwa soft (si videvu tu bali).

Ni mara chache sana kumpata mwanamke ambaye hajakiona kioo (mirror) kwa siku tatu na inawezakana hata hivyo wanawake hupenda mwanaume ambaye naye anatumia bathroom mara kwa mara kuhakikisha anauweka mwili wake katika hali ya usafi na kuvutia, pia ulimwengu huu wa cosmetics itakuwa ajabu mwanaume kushindwa kuwa smart, clean and fresh kwa mavazi na mwili.

pia hilo la usafi ni sambamba na usafi wa meno, mikono na kucha, mwanaume mwenye vidole safi vyenye kucha safi huwa na mvuto kwa mwanamke yeyyote na mwili safi ni mvuto pia na kuonesha kweli unajali afya yako na yule unampenda.

Pia hakuna kitu husumbua kama mwanaume mvuta sigara (sipo kwenye anti-tobacco campaign lakini kila mtu anayevuta sigara lazima awe mwangalifu kwa watu aliokaribu nao) nguo zinanuka sigara, mdomo unanuka sigara, na vidole vimeongua kwa sigara halafu unalalamika huna mvuto kwa mpenzi wako. Unategemea kuwa na tabia kama hii na mwanamke afurahie, labda naye awe mvuta sigara kama gari la moshi.

Mwanaume yeyyote ambaye ni mtu wa mwisho kuondoka baa asitegemee kuwa na relationship inayoridhisha kwani hakuna mwanamke anaweza kuvumilia mwanaume mlevi kiasi hicho.
Wanawake wengi hupenda zawadi bila kujali ni zawadi ya aina gani hivyo Ukitaka kupata moyo wake ni vizuri kumpa surprise ya zawadi yoyote na hiyo ni kuonesha unamjali.

Mwanamke hupenda caring and attention labda awe feminist, mwanamke hupenda kufunguliwa mlango apite, awekewe kiti aketi, kumsaidia kushika vitu vyake kama koti au handbag lake kama anafanya kitu nk.

Mwanamke hupenda mwanaume ambaye ana share naye interests na dreams za maisha, anapenda kusikilizwa kwa kujali anapoongea.

Kumbuka usijaribu ku-pretend, uwe wewe na uwe honest ina mwanamke atakufurahia hata kama kuna wanawake bila kumpa uwongo haridhiki kama kweli unampenda hata hivyo hiyo si kanuni bora kwani mwisho wa reli data zikigoma na akajua kwamba hukuwa mkweli trust inaondoka na huwezi kuirudisha na unaweza kupoteza kitu cha thamani.

No comments: