"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 15, 2009

Kukosa Uzazi

Emmanuel Lazarus Suala na kutopata mtoto (mimba) ni gumu sana na ugumu huongezeka zaidi kutokana na design ya ndoa za kiafrika ambazo suala la ndoa huhusisha jamii nzima kutaka kujua una mtoto au huna na ndugu huenda mbali zaidi kwa kutaka kujua sababu ambazo zinafanya wanandoa msiwe na mtoto.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba mwanamke ambaye ana tatizo la kushindwa kupata mimba (mtoto) huwa na wakati mgumu sawa na maumivu (kisaikolojia) ya mwanamke ambaye anaumwa Cancer au UKIMWI au ugonjwa wowote ambao ni Chronic.

Inawezekana kuna wakati unawaza sana hadi unajisikia uncomfortable kwa kuanza kufikiria hili suala na zaidi kuna wakati unapokea ushauri ambao hauna tija yoyote na unakupa stress zaidi na kubwa kuliko yote ni pale ambapo hata huyo ambaye alisema atakupenda katika hali zote hadi kifo kitakapowatengenisha anakupa maneno au matendo ya masimango hadi unatamani usingekuwepo duniani.

Pia inawezekana umemuomba Mungu hadi umefika mahali unajiuliza kama kweli Mungu anakuona au hayupo au anaupendeleo.
Ukweli ni kwamba Mungu bado ana mpango na maisha yako na anakuwazia mema na ni mwaminifu kutimiza ahadi zake kwako.
Pia hupo peke yako wapo wanandoa wengi ambao wanapita katika njia hii na zaidi ya yote ndoa zao zipo imara na zenye furaha ya kweli.

Kukosa uzazi (infertility) ni nini?
Wataalamu wana elezea kwamba kukosa uzazi ni uwezo wa kukosa kupata mimba kwa muda wa mwaka mmoja (miezi 12) wa kujaribu kupata mimba bila kutumia aina yoyote ya uzazi wa mpango.
Hata wanawake ambao hupata mimba na kuishia kutoka (miscarriage) pia hujulikana kama ni kukosa uzazi.
Wengine huita ni kuwa tasa na wengine huita ni ugumba (haya Maneno ni mazito sana ziwezi kuyatumia pia yanachanganya maana)

Kupata mimba ni mnyororo wa matukio tofauti kwani ili kupata mimba mwanamke anahitaji kutoa yai kutoka katika moja ya ovary zake (ovulation), na yai lazima lisafiri kwenda kwenye uterus (womb) kupitia fallopian tube na wakati huophuo liweze kuungana na mbegu ya mwanaume na kuwa fertilized na kukaa ndani ya uterus (implantation).
Kukosa uzazi huweza kutokea iwapo kutakuwa na hitilafu katika moja ya hatua zilizotajwa hapo juu.

Je, kukosa uzazi ni tatizo la wanawake tu?
Hapana, tatizo la kukosa uzazi si wanawake tu bali hata wanaume. moja ya tatu (1/3) ya tatizo la kukosa uzazi ni wanawake (female factor) wakati moja ya tatu (1/3) ni wanaume (male factor).
Na 1/3 inayobaki husababishwa nje ya sababu za mwanamke au mwanaume.

Nini husababishwa mwanamke kukosa uzazi?
Tatizo kubwa kwa mwanamke ni ovulation, kitendo cha yai kushindwa kuwa fertilized na moja wapo ya sign kwamba yai lake halitaweza kuwa fertilized ni kutakuwa na siku zake (MP)
Pia zipo sababu ndogondogo ambazo husababisha kukosa uzazi nazo ni
Kufunga kwa fallopian tubes kunakosababishwa na magonjwa.
Matatizo (physical) ya uterus kama vile kutoa mimba.

Pia vitu kama umri, mlo hafifu, kuwa overweight au underweight, sigara, pombe, magonjwa ya siri (STD), madawa (sindano za mpango wa uzazi) na matatizo ya afya yanayosababisha kubadilika kwa homoni.

Nini husababishwa mwanaume kukosa uzazi?
Mara nyingi mwanaume hukosa uzazi hasa kutokana na:-
Tatizo la kushindwa kutengeneza mbegu (sperms) – huzalisha kiwango kidogo sana au hakuna kabisa.
Tatizo la sperms kushindwa kulifikia yai na kufanya fertilization- inawezekana sperms zina shape au structure inayozuia kuweza kulifikia yai.
Wakati mwingine mwanaume anazaliwa na tatizo ambalo huathiri sperms zake na wengine tatizo huanza baadae ktk maisha kutokana na kuugua au injury. (kama vile cystic fibrosis)

Nini huongeza uwezekano wa mwanaume kukosa kizazi?
Ukweli ni kwamba uwingi na ubora wa sperms za mwanaume huweza kuathiriwa sana na afya yake na life style.
Vitu ambavyo huweza kupunguza uwingi na ubora wa sperm ni kama vile”
Pombe, madawa (drugs), kuvuta sigara, mionzi (chemotherapy), umri, matatizo ya afya, sumu kutokana na mazingira (lead, pesticides)
Bottom line:
Issue ya kupata mtoto ni issue sensitive mna kwa wanandoa, ni Mungu peke yake anayeweza kuwa na solution kwani pamoja na kuwa na kiwango cha juu sana cha technology bado suala la kupata mtoto limekuwa gumu (infertility).
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana
(Mathayo 19:26)

No comments: