"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 29, 2009

Kwa hivi utamtembelea jela tu!

Lily/EmmanuelNI JUKUMU ULILOPEWA NA MUNGU WEWE MZAZI KUHAKIKISHA WATOTO WANAKUWA NA NIDHAMU NA TABIA NJEMA.
Kujisahau na kufanya mambo yafuatayo unaweza kujikuta mtoto wako anaishia mikononi mwa polisi na anaishi jela baada ya kuachana na kuwa mtoto.
Na ukifanya yafuatayo ni kweli hutakosa muda wa kwenda kumtembelea jela.
Hakikisha unampa mtoto wako vitu vyote anavyovitamani.
Akikua na mtazamo wa aina hii atajua kwamba ni kweli duniani inaweza kumpa chochote anachotaka.

Ukiona ameanza kujifunza maneno mabaya na machafu, mchekee tu, hii inamfanya ajione yupo smart sana pia itampa nguvu ya kujifunza maneno mengine na sentensi zingine zenye maneno ya aina ileile ambayo siku moja yanaweza kukutikisa kama si kukufanya uzimie.

Hakikisha humpi nafasi ya kuwa na uhusiano wa kiroho (training). Subiri hadi awe na miaka 21 atakapoamua mwenyewe kujiunga na dini au kuchagua mwenyewe masuala ya kiroho au afuate na aishi vipi kiroho.

Hakikisha unakwepa wa nguvu zako zote kumtamkia kwamba “umekosea” ili usimsababisha ajisikia hatia. Mwambie ana akili sana kiasi kwamba hawezi kukosea kitu chochote.
Hii itamsaidia kujua ni kosa au si kosa kuvunja mlango wa gari lililoegeshwa na kukamatwa na polisi.

Hakikisha unamsaidia kazi zote hadi kuondoa sahani au vyombo wakati amemaliza kula au kumfulia nguo hadi akiwa na miaka 21 pia mwambie asijali sana kwani wenzake watakuwa wanamsaidia kazi mbele ya safari.

Hakikisha baba na mama mnazipiga mbele ya mtoto siku zote, msithubutu kupigana au kuzozana bila yeye kuwepo kwani kwa njia hii mtoto wenu (watoto) hatashangaa sana au kuumia sana siku mkiachana.

Mpe mtoto wako pesa zote anazohitaji kwa ajili ya matumizi yake, usimshawishi kutafuta pesa zake, kwa nini apate shida kupata pesa kama unavyofanya wewe? Ni mtoto wako mwache afurahie matunda ya kuwa na mzazi mwenye pesa, jitahidi kufanya hivi hadi afikishe miaka 21 hapo unaweza kuanza kubana au kumpa pocket money pungufu.

Hakikisha hakuna siku ana njaa, mpe kila aina ya chakula ambacho tumbo lake linaweza kubeba, pia kila kinywaji ambacho yeye anapenda hata kama unaweza kuagiza mbali kwani ni mtoto wako lazima umpe kitu roho na mwili vinapenda au vinatamani.

Usikubali majirani, walimu au polisi kuingilia maisha ya mtoto wako kwani hawa hawana uchungu na mtoto wako, mwenye uchungu na mtoto ni wewe mzazi, isitoshe mtoto ni wako si wao au jamii au jamhuri.

Siku ukiona amekasirika hakikisha unamuomba msamaha na mhakikishie kwamba hutarudia tena yeye za zaidi ya yote yeye ndiye yupo sahihi wakati wote.

Kama hujapata mtoto bado akishazaliwa tu hakikisha unampa jina ambalo hata wanafunzi wenzake wanaweza kumtania majina kama “Shida, Mateso, Chuki, Luleho (wabena mpo?), Fisi, Maskini, Sinahaki nk ilimradi tu likitamkwa jina lake lazima ataniwe.

NB:

Mlee mtoto katika njia ipasayo, Naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

Mithali 22:6

6 comments:

Anonymous said...

BWANA yESU ASIFIWE!
Mh leo hiki ulichotuandikia kwa malezi ya mtoto mbona sijakuelewa kabisa akitaka pesa kwa matumizi ya mpe tuu tena hapo ni under 21 realy akiongea maneno ya ovyo mchekee mbona kama yote ni kinyume ktk malezi au sijakuelewa vzr? nitafsirie vuri zaidi naona sijakupata leo.
ATUKUZWE MUNGU!

Mama P!

Anonymous said...

shalom kaka lazarus,
napenda kuanza kuzunngumzia majina tuwapayo watoto wetu, kwa kweli hata biblia kwenye kitabu cha mithali inasema ni heri kuchagua jina lililo jema, na tena maandiko yanasema uzima ya mauti viko kwenye nguvu ya ulimi wetu, si haki kabisa hata kama mzazi ulipitia kipindi kigumu kiasi gani umwite mtoto wako majina kama shida, huzuni,sina haki, siyawezi, hakika mtoto wako atakuwa vivyo hivyo kama jina lake linavyotamkwa.
mifano mingi tu ipo hata kwenye maandiko kama yabesi maana yake huzuni alikuwa mtu wa huzuni tu, nabali maana yake ni mpumbavu na alikuwa mpumbavu tu.

kaka pia naungana na wewe kwamba tu walee watoto wetu katika njia ipasayo, sisi kama wazazi na wengine wazazi wa kesho lazma tuombe sana hekima na busara toka kwa Mungu jinsi ya kuwa wababa wema na wamama wema kila leo, na tuombe Mungu atufundishe jinsi ya kuwalea watoto wetu katika njia inayompendeza Mungu, kwa kufanya hivi nguvu ya MUNGU itakuwa katikati yetu.

naendelea kusisitiza kwa kusema wazazi wote tuna majukumu ya kulea familia zetu ila wanawake tusizubae jamani, watoto mara nyingi wako chini ya uangalizi wa mama sasa ukizubaa tu unaharibu, ebu wanawake wenzangu tushike jukumu la kusimama kumwomba Mungu kwa ajili ya familia zetu, lazma baba wa watoto wako umwombee sana Mungu amfanye kuwa baba mwenye hekima na anaelea familia ktk njia nzuri imependezayo Mungu.

hii imekuwa shida kwa familia nyingi mama anataka watoto walelewe ktk njia iwapasayo sasa unakuta baba anataka watoto wapewe ruksa kwa kila kitu kufanya.
mimi huwa napenda kuzungumza kwa mifano sana ilikuwa xmas flani yapata miaka zaidi ya 10 nilialikwa kwa aunt yangu sasa aunt ni mtu wa kiroho mumewe alikuwa si kiroho na ilikuwa shida maana mama anawakanya watoto wakikosea baba anawakumbatia tu kuona kama wanayofanya ni mazuri, mtoto wa aunt yangu 6 yrs alimkata kaka yake kwa wembe usoni walibishana akamrarua kwa wembe, mnafahamu kwa malezi ya kitz aunt alimkamata mtoto na kumfungia chumbani kwake na kuanza kumrudi kwa kumchapa fimbo, mumewe alikuwa hayupo aliporudi akasikia mtoto analia na yeye hapendi watoto wake walie au waadhibiwe, ilikuwa ugomvi mkubwa kwa mkewe kwanini amwadhibu mtoto yani ilikuwa arushe ngumi zirudi kwa mkewe bahati nzuri mlango ulikuwa umefungwa, nimependa nitoe kisa hichi kama changamoto kwa wazazi kuna methali ya kiswahili inasema mtoto mleavyo ndivyo akuavyo. tuombee watoto wetu kabla hata mimba haijatungwa wawe wanadhiri wa Mungu.

mbarikiwe sana

MS GBennett

Anonymous said...

Sorry sorry nimeprint nikasoma nimetulia hapo mwanzoni ndio palini changanya sasa nimekuelewa ni kweli ukimlea hivyo utakuwa kila wk end ni kumsalimu mtoto segerea.Please dont retreave my first msg.

mama P

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P.

Pole sana hiyo topic nimeieleze kinyume chake, hii ina maana kwamba huruhusiwi kufanya hayo, ukiruhusu yao kuna uwezekano asilimia 99 mtoto wako ataishia jela.

Ukitala kulea mtoto wako vizuri lazima ufanye kinyume na hayo maelezo.

Upendo daima

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P na Dada Gbennett,
Asante sana kwa mchango wa mawazo ni kweli wazazi wote mke na mume tunajukumu la kuhusika moja kwa moja na nidhamu za watoto na tunatakiwa kuwalea na kushirikiana pamoja wote bila kumwachia mke au mume kwani ni kweli wakati mwingine mama anasema hiki na baba anasema hiki na kwa kuwa mtoto ni mtoto hupenda kushika yale ya mzazi ambaye anaonesha kuwa laini. Future ya mtoto ni sasa na hakuna wakati mgumu kwa jamii ya watoto kama ulimwengu wa leo na zaidi ya kulea watoto katika misingi ya Kikristo bado dunia sasa unawavuta watoto na kuwapa mambo ya hatari kuliko miaka 10 iliyopita na zaidi tuwe na maombi maalumu kwa ajili ya watoto wetu.

Mungu awabariki wazazi wenzangu.

Upendo daima

Anonymous said...

Bwana apewe sifa, MMENENA VEMA. Mbarikiwe,

Msafiri