"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 28, 2009

Kwa nini wanaume tu!

..............Wapendeni wake zenu kama Kristo anavyolipenda kanisa!Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake.
Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume.

Kwa nini Biblia imesisitiza zaidi ya mara nne mwanaume kumpenda mke na mara moja tu mke kumpenda mume na kumtii?
Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana.

Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama, nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alilalamika kwamba
“Without love I have no life” wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali.

Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa!
Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume.

Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali.

Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa!

Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume.

Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake.

References:
Ephesians 5:25
Ephesians 5:28-33
I Peter 3:7
Colossians 3:19
Proverbs 31:28-29

2 comments:

Anonymous said...

Bwana Yesu asifiwe sana! Yaani u'r very very very genius kaka Mbilinyi wanaume wangekuwa wanalielewa hilo ndoa zisingevunjika hata kidogo sisi wanawake ni wepesi sana kudanganyika.Kitu muhimu mke kwa mumewe ni upendo tuuuuuu jamani tena hata ukimwonyesha ule wa uwongo uwongo anakubali na hicho ndio kinasababisha atoke nje ya nyumba kutafuta huo upendo na kusifiwa tu wewe ni mzuri sana sijui mumeo analitambua hilo nje huko akiambiwa hivo tu umemmaliza kabisaaa.Ubarikiwe sana!

Mama P

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,
Amnina kubwa!

Ni kweli mwanamke akijua anapendwa na mume wake anaweza kufanya chochote kumfurahisha huyo mume. Na wanaume tungejua hii siri basi ndoa zetu zingekuwa paradiso za uhakika.
Pia kumpenda mke si gharama kwani haihitaji pesa ili umpende basi kujua nini umwambie na ufanye kukidhi hitaji lake la kupendwa.

Kwa niaba ya wanaume wenzangu naamini tutajitahidi kufanyia kazi ili wake zetu mfurahie kuolewa na wanaume kama sisi ambao kwanza tunamjua Kristo na pia tunapenda kuwa kama Kristo katika ndoa zetu.

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima