"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 16, 2009

Mahali popote!

Hata njia za train wengine wametumia Swali:
Tuna miaka mitano (5) katika ndoa yetu na siku zote tumekuwa tunafanya tendo la ndoa kitandani tu, je ni sehemu zingine zipi zinaweza kutumika kwa wanandoa kufurahia kuwa mwili mmoja?

Jibu:

Ni kweli kitandani ndiyo sehemu ambayo ni rahisi (convenient), inayofaaa, inayotoa fursa na maalumu kwa wanandoa wengi kufurahia kufanya mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja. Hata hivyo si sehemu ambayo wengi hutumia kufanya mapenzi.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 90 ya wanandoa wanaofanya mapenzi huwa kitandani wapo wanandoa hutafuta sehemu zingine kutokana na mood au pale wanataka kitu kipya.

Ni busara na hekima sana kuwa creative na kufanya kitu kipya hasa wawili wakikubaliana na ikiwa tu hakuna tatizo litakalotokea kuharibu privacy yenu, kukamatwa, kudakwa au hata kushitakiwa kwani kuna sehemu watu hawaruhusiwi hata kama ni mke na mume.

"So, Sex is everywhere"

Hapa si suala tu la kuwa na sehemu tofauti za wawili kuwa na faragha bali aina za milalo na pia ubunifu kuhakikisha kwamba shughuli nzima ya kuwa mwili mmoja haiwi na utaratibu unaojirudia miaka nenda rudi.

Naamini hata wewe unayesoma hapa sasa hivi inawezekana umewahi tumia sehemu ambayo ukikumbuka unaishia kucheka hata hivyo ilikuwa ni kumbukumbu nzuri ndiyo maana umeishia kutabasamu.

Baadhi ya sehemu ni:
Kwenye shamba la mahindi, msituni, jikoni, bafuni, sebuleni, sakafuni, mezani, kwenye backyard huku kukiwa na nyota angani, kwenye gari, kwenye boat, chumba chochote kwenye nyumba yako, swimming pool, mlimani, kwenye mvua, beach nk.
Naamini wapo ambao wamewahi tumia sehemu zingine zaidi ya hizo.

Zifuatazo ni sehemu hatari kabisa kwa wawili kuwa mwili mmoja.
Beach
– kujisahau huweza kusababisha kubebwa na mawimbi, kumbuka ile issue ya tsunami.
Ofisini – kama ni ofisi yako au ofisi yenu na mke wako au mume wako it is ok, ila kama ni vinginevyo utaacha evidence ambayo lazima utafukuzwa kazi.
Makaburini (graveyard)- hata haielewiki watu wapoje, lazima akili iwe inaenda mwelekeo tofauti na binadamu wengine, hata hivyo tumeyasikia.
Kanisani – ni aibu na kukosa maadili hata hivyo tumesikia watu wanaenda church pews kutimiza haja zao za kimwili.
Kitandani au chumbani kwa wazazi wako – subiri ukamatwe ndo utajua kuwa ni risk kiasi gani.
Kwenye reli – mahaba yakinoga mnaweza kusagwa na train.

Pia ulimwengu wa sasa security Camera zinawekwa kila sehemu hivyo bila kuwa makini unaweza kushangaa issue zako zipo hewani bila kujua.

2 comments:

Anonymous said...

Bwana Yesu asifiwe kaka!Yaani kaka nimefurahi sana kwa majibu mazuri uliyonishauri kuhusiana na tatizo la mume wangu juzi.nitajitahidi kuyafanyia kazi yale ulionishauri hivi samahani una kipaji kiasi gani na haya maswala ya ndoa na nikuonavyo uko tu sawa na mume wangu i mean u'r age, una kipaji sana. sasa usione kimya watu hatutoi maoni kny blog yako kwa maana inajitosheleza mno.pia ningependa kama ikiwezekana ni vizuri zaidi ukatupa kama semina flani hivi ya ndoa nikiwa na mr au unaonaje maana kumpata mwenyewe inakuwa ngumu ila tuanze wote nae halafu tujenge mahusiano ya wewe kuongea nae mkiwa wawili coz nampenda sana mume wangu maana ndie Mungu amependa niwe nae lazma nijitahidi anipe vile ambavyo nakosa na viko ndani ya uwezo wake zaidi kimwili.Mungu azidi kukubariki.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada,
Asante sana kwa maoni yako na yote umeongea.
Ni huwa inaleta matokeo mazuri kwa wawili wanaopendana kwenye ndoa kuwa pamoja kupata ushauri au kuhudhuria semina na kujifunza.
Naamini siku moja itawezekana kuwa na semina na kubadilishana mawazo kwa wanandoa, tuommbeane.

Ubarikiwe sana na Bwana kwa hekima uliyonayo ya kuhakikisha unampenda mwenzi wako zaidi na naamini kwa upendo wako ulionao kwake ndoa yako siku moja itakuwa ya tofauti na mfano kwani unachofanya ni kitu sahihi ambacho kila mwanandoa anatakiwa kufanya au kufuata, Hongera sana.

Kuhusu watu kutoa maoni haina tatizo kwani mimi ni kama mtangazaji wa kituo cha TV unatangaza huku umetabasamu kwa watu wa kufikirika(usiowaona) ingawa unaamini kuna watu wanakutazama.

Naomba nitumie email kwa lazarusmbilinyi@gmail.com kuna kitu nataka kukushauri zaidi.

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima