"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 17, 2009

Mwambie "Switch me on"

Kuna Swali ambalo liliulizwa na dada yetu kuhusu mume wake na dada GBennett amechangia kujibu swali kwa kumshauri kufanya mambo mbali mbali kama unavyoweza kusoma hapo chini

Swali lilikuwa:
Mimi ni dada nimeolewa nina kama 12 yrs ya ndoa na nina motto, mume wangu mzito sana kimapenzi kwanza huwa haonyeshi kuwa anataka tendo la ndo.
Ni mimi tu huwa najitahidi kuhitaji ninapojisikia hamu na pia yeye ni mzito kuniandaa hivyo hunipasa kumuandaa yeye na huwa anajilaza tu hafanyi kitu mpaka naamua kujishughulikia na ninamshukuru Mungu nafika kileleni kwa staili ambayo nikiitumia inanifikisha.

Je, nifanyeje ili nifurahie penzi la mume wangu no kises na kukumbatiwa yaani sijui ana tatizo gani?

Jibu
Shalom dada muuliza swali!
Napenda kukupongeza sana kwa kuuliza swali zuri na pia ili wengi tujifunze jinsi ya kuridhishana katika ndoa zetu.
Pia tujifunze kamba tukishirikiana mume na mke huku tukimuomba Mungu aonekane katika eneo au katika hii idara ya kuridhishana chumbani basi ndoa zetu zitakuwa rah asana.
Mimi ninachotaka kukushauri ni kwamba uwe mtu wa maombi sana, kwa maana kwamba ndoa inahitaji maombi mno na Mungu hujibu na unaweza kuhamisha kila mlima unaojitokeza katika ndoa.

Amka hata usiku wa manane omba kwa ajili yako na mumeo pia, mwambie Mungu amfungue na ampe ubunifu kwenye tendo la ndoa kwani Mungu ndiye ambaye alibuni sex katika ndoa na anajua kwa kupitia tendo la ndoa mke na mume huwa na wakati mzuri kujenga bond ambayo itawawezesha kuwa wazuri katika mahusiano ya mwili na roho.

Mimi huwa naomba ulimi wa mume wangu Yesu aufanye uwe mtamu na wa maneno matamu zaidi ya asali, tembea ya mume wangu ionyeshe utukufu, imani yake iwe kwa kristo, tamaa yake iwe kwangu tu, Mungu ampe ubunifu kwenye tunapokuwa mwili mmoja, anifanye nijisikie nipo paradiso, Mungu anifanye nitosheke nae, naomba Mungu anifanye niwe mtamu sana kwa Mume wangu, Niwe namvutia nay eye ananivutia, amfanye atosheke na mimi mkewe na kwamba kila siku niwe mpya kwake.

Dada lazima ufanye maombi ya namna hii, kabla ya tendo ombeni Mungu katika jina ya Yesu Kristo tendo la ndoa liwe tamu sana na kila mmoja aridhike, na baada ya hekaheka za kujiburudisha mshukuru Bwana kwa kuwafanya mjisikie raha.
Pia siku unayotaka tendo la ndoa uwe unapenda sana kuzungumza masuala ya mapenzi na mumeo mara kwa mara mkiwa wawili, weka utani utani kwa mumeo (hakikisha unatoa utani ambao hauwezi kumkwaza maana kuna watu wamelelewa tofauti).

Mfano mimi huwa namtania mume wangu na yeye anapenda sana na naamini huwa inampa matayarisho kwenye ubongo wake, kuna wakati namwambia leo nataka unitafune, hahahahah! Au leo namwambia typwritter haina red ribbon vipi utafanya typing?

Ni muhimu kuwa mbunifu dada, mnaweza mkawa mnaangalia TV halafu ukazima kusudi na ukamnong'oneza “switch me on” au unazima TV UNAENDA CHUMBANI HUKU UNAKUWA UMEANDIKA KIKARATASI KINASEMA “SWITCH ME ON” UNAMPA MKONONI AU UNAWEKA PEMBENI YAKE MAHALI ANAWEZA KUONA, utashangaa smile atakalotoa na lazima mtakuwa na wakati mzuri sana.

Pia waweza andika ka-note na kusema “Umebeba funguo, furaha ya maisha yangu yote” au “nakupenda sana I am proud of you” halafu unaweka kwenye mfuko wa shati lake analovaa asubuhib akienda kazini, au kama mmebarikiwa usafiri unaweka kwenye gari kwa siri kiti anachokalia kabla hajaenda kuendesha gari,au kwenye suite case yake, msifie mwambie yeye ni lulu ktk viumbe amezidi wote, kumbushaneni wakati mnaapa kanisani, rudieni viapo vya harusi yenu tena unaigiza sauti kama ni nzito igiza kuapa kwa kutumia sauti yake atacheka sana hapo hayo ni ktk kuwekana sawa ili aanze kukuchokoza yeye mfikie lengo la kuingia paradise.

Mwambie nakupenda wakati wotena asubuhi akienda kazini mwambie nakupenda na mpige busu usisubiri yeye kukupigia busu kila siku, akipiga simu baada mchana mwambie nakupenda akirudi home mwambie nakupenda yani nakupenda ni wakati wote pia unaweza kumtumia Text message muda wowote ukimkumbuka kwa njia hii itakuwa rahisi wewe na yeye kuweza kuongea mambo ya faragha kwa urahisi kwani mtakuwa mmevunja ukuta unaowafanya msiongee issue za chumbani.

Samahani nashindwa kutafsiri kwa kiswahili baadhi ya maneno hata hivyo naamini ujumbe kamili au wazo kamili umelipata.

Nakutakia mafanikio katika yale unahitaji kwa mume na nina imani kubwa Mungu atafanya na zaidi utafurahia ndoa yako kwani hakuna kitu kitamu duniani kama ndoa au mume na mke ambao wanatoshelezana idara zote.

Ukweli ni kwamba tofauti zilizopo kati ya mume na mke husaidia kutuweka karibu na kuwa kitu kimoja.

Ubarikiwe sana na Bwana
MS GBennett

3 comments:

fikirikwanza said...

Hallo thank you so much kwa somo zuri,nimetamani kama all woma wanegkuwa wana hii mind na akili uliyonayo. Maana wanaume tungeota vitambi si kwa sababu ya misosi ila by the way women treat them.
Hili somo nimedownload japo bila permission naomba mnisamehe.
Thanks .

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli,
Hapo somo limekubali kila mwanamke akifanya installation za hizi skills na mawasiliano mazuri ya namna hii ndoa nyingi zitaponywa, hata kama kila ndoa ina aina yake somo limegusa aina yoyote ya ndoa na Mungu akubariki sana dada GBunnett.
Kwa kuwa hapa tunajifunza na lengo ni kuhakikisha kila mmoja anakuwa na maisha mazuri na yule anayempenda basi unaruhusiwa ku-download chochote kwa faida ya ndoa yako ili tumuinue Kristo katika ndoa zetu.

Upendo daima.

Anonymous said...

shalom!
kaka ubarikiwe sana na wote walisoma hapa nawaombea Mungu aendelee kuponya ndoa zetu wakati wote amen
Ms GBennett