"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 17, 2009

Mwenzenu Mara Moja Kwa Wiki Mbili!

Akifurahi Hawezi Kulalamika! Mimi ni mwanaume mwenye miaka 32 najisikia kupenda sana tendo la ndoa niwe nifanya mara kwa mara, lakini mke wangu amekuwa hapendi kabisa.
Je, nitafanya nini ili kubadilisha hii hali kwani kwa wiki mbili tunafanya mara moja na hiyo moja ni kwa kulazimishana?

Kwanza asante kwa swali suri ambalo linasumbua wanaume wengi duniani ndani ya kuta nne za vyumba vyao.
Pili lazima ufanye analysis je, unampenda au unamtumia tu huyo mke wako?
Why?
Uzoefu unaonesha kwamba hata mwanamke asipofika kileleni bado huweza kufurahia tendo la ndoa (kuwa mwili mmoja) ikiwa tu mwanaume atakuwa mwororo (tenderness), ukaribu (closeness), anayeonesha upendo, anaye jali na mwenye mawasiliano mazuri na mke wake na mwanamke kujisikia anapata real love.

Ukweli ni kwamba mwanaume ambaye ni mbinafsi (selfish) na hajifunzi sanaa ya mapenzi ndani ya ndoa na anamtumia mke wake kutimiza mahitaji yake ya tendo la ndoa (sex) tu hawezi kujenga hamu ya mwanamke kuhitaji huduma ya kuwa mwili mmoja.

Labda kuwa na medical problems au matitazo ya ndani ya emotions zake (deep rooted) hasa kutokana na maisha yake ya nyuma (past life hata kabla hujamuoa) kama vile kubakwa au kudhalilishwa na mwanaume au ndugu wa karibu katika familia, hivyo kisaikolojia ameathirika.

Bottom-line ni kwamba maisha ya kimapenzi ya wanawake wengi katika ndoa huelezea (reflect) jinsi wanaume wanavyo wahudumia katika mzunguko mzima wa maisha yao ya kila siku ya wawili waliooana.

Ni mara chache sana kukutana na wanandoa wanaohitaji ushauri wa masuala ya tendo la ndoa, kama mwanaume anampa mke wake upendo wa kweli ambao mwanamke huhitaji hata kabla ya kuingia chumbani.
Mwanaume ambaye anajifunza sana ya mapenzi (kile mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume), ambaye anamjali mwanamke, ambaye anakuwa na muda wa kutosha kumuandaa (foreplay) na anayehakikisha mwanamke anaridhika na raha ya kuwa mwili mmoja (kudumu kwa muda mrefu wakati wa kuwa mwili mmoja) na kuendelea kuwa naye hata baada ya wote kufika kileleni (siyo unaenda ICU bila taarifa) huwezesha mwanamke kuvutiwa na tendo la ndoa na kujikuta anahitaji kila wakati bila kulazimishwa.

“Acha ile mume wangu anafanya kuniandaa kwa muda unaotosha, mimi huwa napenda sana kila kitendo cha yeye kuendelea kunikumbatia na kunishikashika kwa wororo (tenderness) hata baada ya kufika kileleni”
Luciana aliongea kwa wazi kile anakipata kwa mume wake James.

“Waaambie wanaume umuhimu wa mwanaume kumhudumia (maneno, tabia, upendo, mawasiliano) vizuri mwanamke wakati wa mchana kwani huweza kuathiri kwa kiasi kikubwa sex life usiku”
Grace alitoa haya maelezo kujibu swali kwa nini wanawake wengi hujikuta wamepiga password feelings zako kuhusiana na kutamani tendo la ndoa na waume zao

Mengineyo:
Kwanza chunguza ratiba yako ya kazi na ratiba yake ya kazi na analyse mgawanyo wa kazi uliopo na pia angalia kama huwa anachoka sana jioni au usiku kutokana na majukumu au kazi anazofanya.

Chunguza kama kuna aina yoyote ya mgogoro au matatizo ambayo hayajaweza kupewa solutions kwa muda mrefu na limekuwa donge moyoni mwake.

Je, unafahamu vizuri past life yake kimahusiano au kimapenzi na hakuna tatizo lolote la kisaikolojia au tabia ambazo amerithi kutoka kwao, wengine huamini sex ni uchafu hata baada ya kuolewa au kuoa.

Jichunguze kwanza mwenye ni kiasi gani umetengeneza mazingira ya yeye kupenda kuwa mwili moja kwani mwanaume yupo sex oriented wakati mwanamke yupo romance oriented.
Mwanamke romantic life kwanza then sex ingawa mwanaume hutaka sex kwanza.

Mwisho n muhimu kuliko yote, muombe Mungu akupe hekima na busara uongee naye kwa upendo wa hali ya juu na kwa uwazi kabisa, ukielezea ndoto yako katika suala la kuwa mwili mmoja na nini unapenda na nini unakosa, kwa kuwa ni mke wako ni wewe tu ndiye unaweza kuongea naye kwa urahisi kuliko mtu wa nje.
Naamini wengine wenye uzoefu wanaweza kukushauri zaidi!
Mungu akubariki sana!
+++++++++++++++++++++

2 comments:

Anonymous said...

This msg has touched me so deeply. Mawasiliano ya mchana jamani laiti wanaume wangejua. Sio mchana umtukane mkeo, jioni unavizia wakati anasinzia bila hata kusema neno unaanza kumshikashika. Kabla hajaloa vya kutosha wewe tayari unakimbilia kukandamiza. Dakika tano mchezo umeisha unanyanyuka unajisafisha unarudi kitandani usingizi mzito. Hutaki tena kuguswa ati "tumechoka tulale" au kesho nina ratiba muhimu asubuhi. Hapa inaonesha kuna matatizo mchana/kabla na wakati wa tendo lenyewe. Hivi unadhani mkeo amekuwa muhudumu wa 5 star hotel asiyeruhusiwa kuonja chakula cha mteja? Angalia mama ntilie anavyoonesha ukaribu na chakula na mteja wake. Kama ambavyo mama lishe hukopesha hata siku mteja hana hela na hutoa ofa pia, mwanaume akitaka kupata mapenzi kila mara kwa mkewe hata kama mkewe amechoka hoi, basi awe "consistent" katika tabia yake. Mkewe atamkopesha hata kama yuko hai na anajua kabisa siku hiyo hatafurahia sana, atafanya kwa
ajili ya mumewe. Sio ati unakuta missed calls za mkeo ukiwa kazini hupigi au msg hujibu, ukirudi ukiulizwa unasema ati ulikuwa kwenye mkutano na ulipotoka ulisahau kupiga. Tena ungoje kuulizwa ndo ujibu hivyo. Kisha wakati anasinzia we ndo unatokea kama kibaka kwenye kona ya manzese uzuri anayetaka kupiga "roba" maarufu "ngeta" (kule nairobi). Huo ni wizi, ni kukosa upendo, kumtumia mkeo na unyanyasaji. Kumbuka CONSISTENCE.

Thanks so much Mbilinyi! Keep it up!
By HO
Dar es Salaam

Lazarus Mbilinyi said...

Dada HO,

Hongera sana kwa comments ambazo zinaonesha ni kweli wanandoa tunahitaji mawasiliano mazuri tangu asubuhi, mchana na wakati wote ili kuandaa usiku na zaidi mume ana nafasi kubwa sana kuandaa mkewe kwa ajili ya usiku uliyo na baraka na si kukurupuka tu.

Upendo daima