"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, July 5, 2009

Mwingine akipewa zawadi hujiona anapendwa, mwingine hudhani unapoteza pesa! Mwanaume na mwanamke hutofautiana katika mambo mengi na hufanana katika mambo mengi pia.

Unapokuwa kwenye mahusiano ni jambo la msingi kufahamu kwamba hata kama kuna
tofauti bado kwa kuzikubali tofauti zilizopo na kumfurahia mwenzi wako ndoa huwa kitu cha kuridhisha zaidi kuliko kuendelea kujitahidi kumbadilisha mwenzi afuate misimamo na misingi uliyotoka nayo kwenu.

Baadhi ya tofauti na kufanana ni kama ifuatavyo:
Wanaume ni wajenzi na creators, huchukua risk na majaribio mara kwa mara wakati wanawake huchagua knowledge ambayo ni ya thamani na kuitumia generations to generations.
Wanaume huwa huru katika mawazo yao na utendaji wakati wanawake hupenda kufuata mawazo yanayopendekezwa na wengine.

Wanawake hupenda ku-criticize wao kwa wao wanaume huridhika na wenzao na utendaji wao.
Mwanaume na mwanamke wote huwa na chanzo cha kuridhika wakati mwanaume ni kazi na kipato kwa mwanamke ni familia na watoto.

Wanaume hujikuta katika kutekeleza malengo yao na kuwa kitu muhimu kwao wakati wanawake suala la mahusiano ya wengine huwa muhimu na msingi zaidi.
Wanaume huugua mara mbili zaidi ya wanawake ingawa wanawake huwa concerned na afya zao kuliko wanaume.

Wanawake huweza kuvumilia maumivu na kazi zenye usumbufu kuliko wanaume.
Wote mwanaume na mwanamke ndani yao kuna aina ya ubinafsi (selfish) na kukiwa na issue kila mmoja huwa na njia yake hivyo Usipoteze muda kwa kujaribu kumbadilisha kwa kuingiza sheria zako mpya na misimamo yako uliyotoka nayo kwenu kwa mke au mume au mpenzi wako badala yake furahia tofauti zilizopo na ndoa itakuwa na raha zaidi.

Wote mwanaume na mwanamke huwa na tabia ya kujitolea kuji-sacrifice vitu anapenda, au misingi yake ili kumfurahisha mpenzi wake mwanzoni mwa uchumba au dating.
Hata hivyo kwa kadri relationship inavyozidi kwenda huanza kujilinda mwenyewe na kuwa selfish tena.

Ndani ya kila mwanaume na mwanamke kuna sehemu inahitaji upendo (love) hata jitu katili kama Hitler alikuwa anayeyuka mbele ya love kutoka kwa mwanamke, wote tunahitaji caring, support, msaada na kutiwa moyo tukiwa wagonjwa au kujisikia tupo low emotionally au tunapofanya makosa, ingawa ni kweli mwanamke huhitaji company zaidi na caring zaidi kuhusiana na feelings zake wakati mwanaume huhitaji zaidi caring kwa tabia zake za nje kama usafi.

Wanaume hupenda kuwalinganisha wanawake na wanawake hupenda kuwalinganisha wanaume, wanaume huwapanga (rate) wanawake kwa appearance zao wakati wanawake huwapanga (rate) wanaume kwa wallet ilivyojaa (wealth), status katika jamii, mwonekano na sehemu ambazo watu wote wana magari basi mwanaume huwa rated kwa aina ya gari analoendesha.

Wote mwanaume na mwanamke huwa na mzunguko wa mood na kwamba baadhi ya siku katika mwezi kila mmoja huwa emotional.
Kwa wanawake hii ni kutokana na kiwango tofauti cha liquid kwenye mwili na utendaji wa ubongo siku wakiwa mwezini, hata kama wanaume hawapati siku moods zao zina mzunguko pia na kama mwanamke anamjua vizuri mume wake anaweza kujifunza na kufahamu signal na zaidi jinsi ya kumkubali.

Wote mwanaume na mwanamke wana wivu (jealous), ndani kabisa ya mwanaume na mwanamke kuna kiasi sawa na wivu wa mambo ya mapenzi tofauti ni kwamba wanaume huweza kuficha vizuri zaidi ya wanawake.
Wote mwanaume na mwanamke hutilia mashaka mahusiano (suspicious) tofauti ni kwamba mwanamke huwa mwepesi kuhisi mwanamke mwingine anaingilia mahusiano yake ni mume wake kwa kuangalia kubadilika kwa mumewe wakati mwanaume hupuuza au huchukua muda mrefu kujua mwanaume mwingine anaingilia mke wake.

No comments: