"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 27, 2009

Ni mtazamo wako tu!

Walikatakata wakaondoa hivi lakini bado wakawa na furaha ajabu!Mithali 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.

Pia kuna msemo wa kingereza usemao
‘ A person never rises above his expectations”
Kwa maana kwamba ukitegemea kushindwa, kufanikiwa ni kitu kisichowezekana.
Pia ukitegemea kufanikiwa unaweza kufanikiwa kiwango chochote unachotaka, kwani upo hivyo kutokana na unavyowaza na kuweka mtazamo wako.

Tunapokuja kwenye suala la mahusiano (kufanya mapenzi katika ndoa au kuwa mwili mmoja au tendo la ndoa kwa mwanamke kuwa na IQ kubwa au vipaji (talents) au umri mzuri katika ndoa havina maana sana ukilinganisha na mental attitude uliyonayo kuhusiana na suala la kufanya mapenzi.

Wapo wanawake walioolewa (si wote) ambao ni warembo, wamesoma, ni portable, matiti katika size inayong’ang’aniwa na wanaume, wana vipaji vya ajabu na umri sahihi wa kuwa kwenye ndoa na sifa zingine kedekede zinazofanya aonekane mwanamke wa nguvu, lakini linapokuja suala la mapenzi (sex) au kuwa mwili mmoja wamekuwa si lolote na aibu tupu kama si kukatisha tamaa kwa waume zao.

Kwa upange mwingine wapo wanawake (si wote) kwenye wapo wapo tu na sura zao, wajasoma, IQ ni ndogo, wapo overweight, vifua flat kama wanaume, hawana hata uwezo wowote katika jamii; hata hivyo linapokuja suala la mapenzi au kitandani ni moto wa kuotea mbali na wanawapa waume zao vitu vya uhakika kitandani.

Na wapo ambao anaweza kuwa kwenye kundi lolote hapo juu na akawa zero kitandani au akawa moto kitandani.

Je, ni nini siri ya mwanamke kuwa moto kitandani na mume wake?
Ukweli si size wala shape wala appearance ya mwanamke ndiyo inayo dhihirisha ufundi wake kitandani bali mtazamo (attitude) kuhusu tendo la ndoa (sex) ndio msingi unaoweza kuelezea mafanikio na kushindwa kitandani.

Kama mwanamke anaamini kufanya mapenzi ni uchafu au ni kitu kibaya au mtazamo wowote potofu katika ndoa hataweza kuleta furaha ya kweli.
Kama anaamini mapenzi katika ndoa ni legalize rape basi hata siku moja hataweza kufurahia mapenzi atakuwa anajiona anabakwa kila siku.

Kama anaamini matiti yake ni madogo sana au makubwa kupita kiasi ambacho hawezi kufurahia kufanya mapenzi ni kweli hataweza kufurahia na anaweza kukosa feelings za kweli kuhusu mapenzi ndani ya ndoa.
Kama anaamini skills zake katika kufanya mapenzi ni pungufu basi hataweza kufurahia raha ya kuwa mwili mmoja.
Kama anaamini mwili wake upo ovyo kiasi kwamba hawezi kuwa uchi mbele ya mume wake basi ni dhahiri faragha na mumewe imeingiliwa.

Katika utafiti ambao ulihusisha wanaume ambao sehemu zao za siri ziliondolewa testicles (mapumbu) na wanawake ambao waliondolewa visimi (clitoris) na kuwachunguza wanavyofanya (enjoy) mapenzi na partners wao; ilikuja kujulikana kwamba walifurahia kufanya mapenzi sawa na wengine ambao wapo salama.
Hii ni kudhihirisha kwamba organs (kisimi na pumbu) hazikuwa msingi wa wanandoa kufurahia mapenzi bali jinsi wanavyofikiria au mtazamo wao kuhusu tendo la ndoa.

Hii ina maana unaweza kuwa na size, shape na appearance tofauti au yenye hitilafu kwa mtazamo wa jamii lakini ukiwa na mtazamo (binafsi) mzuri kuhusu mapenzi unaweza kufurahia tendo la ndoa kwa njia ya ajabu sana na unaweza kuwa moto kitandani na mumeo kukufurahia.

2 comments:

Anonymous said...

Shalom!Yaani ulichongea ni ukweli mtupu hii nafananisha ulishawahi kuongea swala kuwa ukiwa na mchumba muonyeshe ulivyo akupende ulivyo na si kuficha yaani akigundua kuwa alikuwa na sanamu ndio mwisho wako kama sijakosea.Hii ina maana sana kwenye mahusiano pia wengi wetu tunajisahau sana ktk hili.Wengi wetu tunajiremba sana mpaka tunakuwa si wenyewe ukikutana na mtu anakusahau kabisa, jirembe kiasi nikiwa na maana Mungu amekufanya mfano wake bado wewe ni mzuri tuu.kuhusu viungo vya mwili ni kujiamini tu kuwa mimi ni mwanamke ambaye nimekamilika.Ni kweli ulivosema kujiremba si kukufanya upate mume tena kwa mwanamume anaetaka mke mh anaangalia vituvingi ndio maana unakuta siku hizi ndoa nyingi zinavunjika kwa kumuangalia mtu urembo wake bila kujua ana tabia gani? kama hujikubali kimaumbile ndio matokeo yake unasikia dawa kwa kuongeza makalio na matiti hii yote kwa kumvutia mwanaume tu kumbe tunajimaliza wenyewe.
Bila kusahau mke mwema hutoka kwa bwana jamani!Tumsifie Mungu kwa kazi yake ya uumbaji.

mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P.

Asante sana kwa comments nzuri ni kweli kila mmoja angejijua kwamba kama alivyo amekamilika na kwamba mwanaume haangalii urembo tu ili mambo yote yaende vizuri na zaidi kujiamini ndiyo msingi wa mahusiano yoyote.
Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima