"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 3, 2009

Ni tabia!

Usafi ni tabia si uwezo kifedha!Hata kama mwonekano wako wa nje si kila kitu bado ni kitu muhimu sana katika mahusiano na mwenzi wako.
Binadamu hunagalia kwa nje na Mungu huangalia moyo (1Samweli 16:7) hii ina maana kwamba mume au mke wako anaangalia nje na si moyo.

Wanawake wengi hujisahau baada ya kuolewa na kuwa na wedding certificate mkononi na wengine akishazaa inakuwa rough hadi inashangaza.
Hivyo si vizuri kutumia wedding certificta au kwamba nimeshaolewa kuwa excuse ili u-relax na kupunguza standard za mwonekano wako.

Unashangaa kwa mume wako kutovutiwa na wewe, au unashangaa mume wako anapokula jiwe kukutambulisha kwa rafiki zake, au unataka anapokutambulisha kwa rafiki zako aanze kibarua cha kujilezea kuwaomba msamaha kwa jinsi ulivyo rough.

Wewe ni mwanaume kabla ya kuoa na muda kidogo baada ya kuoa ulikuwa unanyoa ndevu vizuri kabisa sasa imekuwa ngumu kunyoa as is umeanzisha timu ya bush stars.
Mke umekuwa nyumbani muda wote siku nzima, mume anakuja kutoka kazini jioni anakutana na mwanamke rough na amejiisahau then unalalamika hupati busu na mume amekuwa siyo romantic and gentle?

Fikiria kwa makini na jiulize hivi ulivyo leo baada ya kuolewa ni sawa na ilivyokuwa wakati wa uchumba au umepunguza standard zako na umeanza kujisahau.
Mwanaume huvutiwa kwa kuona hivyo mwanamke anayejua mume wake anahitaji kitu gani hawezi kuzembea kwenye hilo eneo.

Maintain your attractiveness to your partner!

No comments: