"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 13, 2009

Nimepata swali lifuatalo ni nimeruhusiwa kulirusha na kila mmoja aweze kusoma na kama inawezekana kutoa maoni.
Swali:
Je, Ni kweli kwamba kisimi, kinembe (clitoris) ni kiungo pekee ambacho mume ni lazima aguse (chezea) ili mke asisimke na kuwa tayari kuwa mwili mmoja?

Jibu:
Si kweli.
Mwanamke si Channel za radio kwa maana kwamba ukibonyeza kitufe pale station inapatikana basi utapata frequency na kuanza kufaidi matangazo yake (muziki au bahari).
Mwanamke ni kiumbe ni kiumbe cha tofauti ambacho hutawalaliwa na hisia (emotions, mood na feelings).
Pia wanawake wote hutofautiana na hata huyo mmoja huweza kuwa tofauti kila siku hii ina maana kwamba kama jana alisisimka sana ulipomchezea kisimi si kanuni kwamba na leo atasisimka kwani inaweza kuwa katika mzunguko wake basi matiti ndiyo yanasisimka zaidi au G-Spot ndo anasisimka zaidi nk.
Ni jukumu la wewe mwanaume kuwa sensitive na smart kujua hitaji lake au ni kiungo gani kwa huo anasisimka zaidi.

Kuchezea kisimi chake si kanuni au sheria au utaratibu ambao umewekwa na kwamba usipofanya basi hakuna kusisimka, ingawa ni kweli mwanamke huweza kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi zaidi wakati mwingine kuliko kutwanga na kupepeta kwenye kinu.
Mwanamke anahitaji maandalizi kwanza, anahitaji busu, caring, anahitaji mwanaume mwororo, gentle, loving, anayebembeleza, mwanaume mwenye mikono slow na mwenye mwendo wa kube kuzunguka (kumtembelea) kiwanja kizima cha mwili wake kabla ya kufika huko kwenye kisimi.

Ni muhimu kwenda sehemu zingine za mwili kwanza kama matiti (chuchu) na sehemu zingine kuanzia zile ambazo zinasisimka kidogo hadi zile ambazo ukimgusa mwili wake unapata joto kiasi cha yeye kutoa ukelele ambao utajua kweli tumeanza kupanda mlima na kileleni tutafika.
Wanawake wengi (siyo wote) hulalamikia kitendo cha mwanaume kuwa na full speed kwenda kwenye kisimi bila kupita maeneo mengine kiasi ambacho huwa ni kuumia au kuumizana kwani kisimi huwa hakijawa tayari kupokea msisimko.

Kumbuka hili eneo lina zaidi ya nerves 8,000 hivyo ni muhimu kuguswa wakati ambao eneo lipo tayari na evidence kwamba kupo tayari ni eneo zima la south pole kuwa wet.
Kupeleka vidole vyako vikavu na bado kukavu huweza kuumiza badala ya kutoa raha.

Unataka kujifunza zaidi kumpa mpenzi wako kitu cha tofauti soma hapa

4 comments:

Anonymous said...

Bwana Yesu asifiwe! jamani huwa unanigusa sana na mada zako nakufurahia sana Mungu akubariki sana natumai utakuwa mume mwema kwa huyo wifi yetu.
Mimi ni dada nimeolewa nina kama 12 yrs ya ndoa na nina mtoto 1 nahisi mume wangu mzito sana kimapenzi kwanza huwa haonyeshi kuwa anataka tendo la ndoa bali ni mimi tu huwa najitahidi kuhitaji ninapojisikia hamu na mzito kwa kuniandaa ni mimi tu huwa namuandaa yeye anakuwa kajilaza tu hafanyi kitu mpaka naamua kujishuhulikia na ninamshukuru Mungu nafika kileleni kwa staili ambayo nikiitumia inanifikisha. Msaada ninaouhitaji kwako ni ushauri nifanyeje ili nifurahie penzi la mume wangu no kises na kukumbatiwa yaani sijui ana tatizo gani?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada mwenye swali,
Kwanza hongera sana kwa kuuliza swali na zaidi jinsi ulivyo lovable kwa mume wako kwani angekuwa mwingine badala ya kutafuta solution angeanza kutafuta jibu nje.
Pili hongera kwa kupita hapa kwani tunajifunza kuwa wazuri kwa wale tunawapenda bila kujali wao wapoje kwani lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na ndoa au mahusiano ambayo yanatufanya turidhike pamoja na tofauti zilizopo.

Hakuna tatizo lisilo na jibu kwani Mungu anaweza yote.

Issue yako inalenga zaidi katika suala zima la mawasiliano kati yenu wawili.
Hatua ya kwanza Omba Mungu kwamba (kwa kufunga na kuomba) ili uweze kuongea naye kwa hekima ya juu sana nini unapenda wewe na yeye mnahitaji katika mahusiano.
Ongea naye kwa upendo na kwa hekima itokayo juu (usimfundishe) bali mwambie tuzungumze kwamba kila mmoja apendekeze nini anapenda katika mahusiano yenu hasa suala la kuwa mwili mmoja.
Kawaida mwanaume yeyote linapokuja suala la kuwa mwili mmoja huwa genius sasa kama wako yupo passive kiasi hicho basi kuna umuhimu wa kukaa pamoja ninyi wawili kama wadau wa ndoa yenu na kujadili kwa undani kwamba ungependa awe hivi na hivi.
Njia nyingine ni kutafuta vitabu au mafundisho ya ndoa au mpe tumia ujuzi wako wote kuhakikisha anapata information zinazohusu (tendo la ndoa na nafasi ya mwanaume)
Ukweli suala la sex linajulikana sana duniani kwa kila mtu lakini ni gumu sana kuliongelea chumbani kwa wawili wapendanao.

Je, kuna njia yoyote naweza ongea naye? kama hakuna basi jitahidi kuomba Mungu kwani Roho mtakatifu ni mwalimu anaweza kuwapa aina ya lugha ambayo utawasaidia kuwa na furaha ya kweli katika ndoa yako.
Ukiwa na swali usisite kuuliza naamini hata wengine wanaweza kukupa ushauri maana wapo watu wenye busara na hekima hupita hapa na kujifunza na wanaweza kukushauri pia kwenye hili suala

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima

fikirikwanza said...

Sasa nimegundua ndoa nyingi ni matatizo sana, na si kosa lao, hasa nikifikria jinsi tulivyo tofauti na malengo tofauti ya kuoa na kuolewa, kweli kasheshe zina haki ya kutawala ndoa nyingi.
Lakini sasa ukimpya uliopo na aibu zilitawala ndoa wapi tutazungumza na kuelimishana. Pia watu hawapo tayari kusikia na inawezekana watu wengi wanafanya mapenzi lakini hata siku moja hawawezi kuongea au kutaja kile wanacho kifanya eti ni aibu.
swali langu ni hili, hivi mkikamatwa na mtoto mwenye miaka mitano au umri wowote mnafanya mapenzi je, nini kifanyike kwa huyo mtoto? je mmwambie kuwa hicho nini nini au mmdanganye kuwa mlikuwa mnacheza uchi au mbakie tuu kimpya atajijua mwenyewe??

Lazarus Mbilinyi said...

Ukweli ndoa kama instituion haina ubaya wowote na haina matatizo, tatizo kubwa na shida kubwa ni kwa wale candidates wa ndoa ambao ni mimi na wewe. Tunapokurupuka kupata mchumba ambaye tunategemea tukiingia naye kwenye ndoa atabadilika ni dhahili kwamba kutotegemea mgongano kwenye ndoa haitawezekana.

Ndoa ni nzuri sana na haina tatizo lolote kwani Mungu ndivyo alipanga ili kupata familia na taifa.

Kuhusu mtoto wa miaka 5 kuwakamata mpo katika tendo takatifu la kuwa mwili mmoja.
Kwanza inatokana na mazingira au huyo mtoto yupo nchi gani kwani tamaduni zinatofautiana sana kuna nchi ambazo mama, baba na mtoto kuwa nchi si tatizo kubwa kama nchi zingine ambazo hadi mtoto unakuwa form four hujawahi ona baba na mama wakilala kitanda kimoja maana kila mmoja anachake na kukutwa wanafanya mapenzi itakuwa shughuli.

Pia watoto wa siku hizi wanajua mambo kuliko tunavyoamini hata hivyo inatokana na akili ya mtoto na uelewa kama anaelewa inabidi umweleze kwa hekima kwamba baba na mama tulikuwa tunalala ingawa ameondoka na picha ambayo hakustahili na ni vyema baba na mama kuwa makini kuhakikisha watoto wadogo hawaoni vitu kama hivi kuliko kufikiria ni jinsi gani tutawasaidia kuwaaambia.
Kumdanganya haitasaidia sana na kumweleza A to Z katika white and black itampeleka mbali muhimu tumia hekima na lugha ambayo itafnaya ajue baba na mama wanapendana na wanatakiwa kulala pamoja.

Naamini wengine wanaweza kutoa ushauri zaidi