"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 9, 2009

Usijidanganye!

Fikiria wewe ni mkulima na unataka kutumia jembe la kukokotwa na ng’ombe kwa ajili ya kulima shamba.
Kwa kuwa una Ng’ombe mmoja (dume) na Mbuzi mmoja (beberu) unaamua kuwafunganisha nira (yoke) ili uwatumie kukokota jembe na shamba lilimwe.

Ukweli huu ni uvivu wa kufikiri na ni kutaka kusababisha maafa.
Anyway mtu yeyote mwenye akili timamu atajua ubongo wako una matatizo kwani haijawahi tokea mbuzi na ng’ombe wakafungwa nira pamoja na shamba likalimwa.

Linapokuja suala la ndoa au mahusiano wapo watu ambao huamini kufungwa nira pamoja na mtu wa imani tofauti haina tatizo kama kwa ng’ombe na mbuzi kufungiwa nira moja na tayari kwa kulimba shamba.

Kama hujaunganishwa na mwenzi wako katika suala la kiroho basi mahusiano yako yanaelekea kwenye maafa.
Jinsi unavyoamini kuhusu Mungu, jinsi unavyoomba, jinsi unavyosherehekea holidays, kitabu gani unaamini ni kitakatifu, kuamini katika ubatizo upi ni moja ya components zinaweka mfumo wa kiroho wa maisha yako.

Kama hamuwezi kutazamana jicho kwa jicho kwenye maeneo haya basi unachukulia juu juu kile ambacho ni msingi moyoni mwako na umepofushwa na fall in love ila siku ukianza kuona you will be too late to catch the bus.

Kiroho chako na jinsi unavyoji-express ni kitu cha undani katika maisha yako na maumivu ya kichwa au kukatishwa tama kutajitokeza iwapo wawili watashindwa kuwa connect kwenye eneo muhimu kama hili.
2 Corinthians 6:14

No comments: