"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 24, 2009

Vizuizi vya kufika kileleni!

Wanawake wengi huolewa wakiwa na uhakika kwamba mwanaume anayeoana naye anajua misingi ya masuala ya tendo la ndoa, ukweli ni kwamba wanaume wengi bado huwa hawajui chochote kuhusiana na masuala haya. Kutokuwa na ufahamu wa kutosha huwa kikwazo kikubwa na hukatisha tamaa wanandoa wote na kuna wakati wanaweza kujikuta wapo njia panda.

Tendo la ndoa au kuwa mwili mmoja ni muhimu kwa ajili ya kuijaza dunia pia ni muhimu sana kwa ajili ya mwanamke kupata raha kutoka kwa mume wake kupitia tendo takatifu la ndoa hasa anapofika kileleni wakati wa kuwa mwili mmoja.

Hata hivyo kuna asilimia kubwa sana ya wanawake hawajui kufika kileleni ni kitu gani na pia hata kama amewahi kufika basi ni mara chache na kubwa zaidi hajui kwa nini hawezi kufika kileleni akiwa na mume wake.

Sababu Zifuatazo ni moja ya mambo yanayochangia kwa kiwango kikubwa mwanamke kushindwa kufika kileleni (orgasm)

UJINGA
Kuna wanawake wanajua au wanafahamu baadhi ya mashine kama vyerehani lakini ukiuliza kuhusu viungo vyake vya uzazi hajui. Hali huwa mbaya zaidi pale mume na mke wote hawajui chochote kuhusu utendaji wa kazi wa viungo vyao za uzazi na hasa vile vinahusika na kuwa mwili mmoja.

Ni kweli katka zama za giza suala la mwanamke kufika kileleni lilikuwa halijulikani na mwanaume alikuwa anamtumia mke wake kwa raha zake na kujibinafsisha.
Hivyo ni muhimu mume na mke kufahamu utendaji wa viungo kuhusiana na suala zima la kuwa mwili mmoja. Kama hujui kisimi kipo wapi na kina kazi gani itakuwa ngumu sana kukufanyia kazi ili kitoe raha inayotakiwa au kusudiwa.

UNENE
Wanawake wengi ambao wana unene wa kupindukia pia hushindwa kujiamini au kuwa huru (self image) matokeo yake wakati wa kuwa mwili mmoja huhisi mume wake atachukia umbo jipya ambalo bibie kajiongezea hivyo anaweza kuanza tabia za kuogopa kuwa uchi mbele ya mume wake na matokeo ni kuwa disconnected kwenye feelings na tendo la ndoa na hata kama wakifanya anafanya kwa kujificha kwa mume wake (anaogopa kuonesha nyama zembe).
Na asilimia kubwa na overweight ni tamaa yao ya kufukia chakula bila utaratibu.
Anyway, kwanza hakuna uhusiano wa wewe kuwa fat na kuenjoy kuwa mwili mmoja na mume wake tatizo ni wewe tu hujiamini.

KUZUBAA
Wapo wanawake ni wazubavu wa hali ya juu wakati wa kuwa mwili mmoja. Wakati wa kuwa mwili mmoja analala tu kama gogo na kuacha mwanaume mchoyo na mbinafsi anajishughulishe na kumaliza hamu yake na kujiondokea kama vile hakuwa na kiumbe chenye uhai.
Tendo la ndoa ni contact sport (mchezo wa kugusana) ambao huhitaji watu wawili ambao wote wanashambulia kiwanja kwa juhudi zao zote.
Mwanamke anavyokuwa active ndivyo ataweza kutoa mwitikio wa wapi anajisikia utamu na kufurahia na hatimaye kufika kileleni. Wanaume ndiyo hufika kileleni haraka kwa sababu huwa active (ni genius) huwa hawazubai mke akishakuwa naked. Na mwanamke naye akichangamka urahisi wa kufika kileleni huwa mkubwa.

HATIA
Kuwa na hatia ya jambo lolote husababisha kufunga kwa hisia za ndani na kuzuia kuweka kufika kileleni.
Inawezekana unatembea na hatia ya mambo fulani uliyoyatenda katika maisha yako na yanakupa wakati mgumu kuwa free katika moyo wako.
Wakati mtu anakuwa amesamehewa dhambi zake, ufahamu wake (conscience) huwa huru na matokeo yake anakuwa ameondoa vizuizi vya kutofika kileleni.

MUDA
Kitu chochote cha kinachoridhisha huhitaji muda na tendo la ndoa halina msamaha. Zamani za kale (giza) kazi ya mwanamke ilikuwa ni kuzaa watoto tu linapokuwa suala la kuwa mwili mmoja na sex kati ya mke na mume ilikuwa sekunde 30 hadi dakika 3, lakini leo wanawake wamekuwa na uwezo wa kufurahia kuwa mwili mmoja na kupata raha at maximum.
Mke anahitaji zaidi ya dakika 10 hadi 15 kufikia kileleni na pia mwanaume anatakiwa kutoa movement za in and out kwenye uke angalau mara 75.

KUCHOKA
Ili kuwa na tendo zuri la kuwa mwili mmoja kiasi ambacho mke afike kileleni bila tatizo kitu cha msingi ni mume na mke kuwa na muda wa kutosha baada ya kupumzika.
Mke ambaye amechoka kwa kazi na majukumu hawezi kutoa cheche kitandani kwani amechoka.
Ni muhimu kuwa mwili mmoja baada ya wanandoa wote kuwa huru bila uchomvu wa aina yoyote.

MISULI DHAIFU
Inajulikana kwamba 2/3 ya wanawake ambao hawawezi kufika kileleni wana tatizo ya ulegevu au udhaifu wa misuli kwenye uke na ni rahisi sana kuondoa hili tatizo bila gharama kwa kufanya mazoezi ya kegel.

UBABE
Kumetokea wanawake ambao sasa nao wanakuwa kama wanaume hataki ku-surrender kwa mume wake, wanapenda kuwa viongozi wa kila kitu, wanapenda kutoa maamuzi, wana dominate kila kitu katika ndoa matokeo yake hata likija suala la kuwa mwili mmoja hataki kujikabidhi kwa mume wake kikamilifu ili amshughulikie kwa kusaidiana kupeana raha ya kuwa mwili mmoja.
Hawajikubali kama wao ni wanawake wanaohitaji mwanaume kumpa raha ya mwili mmoja matokeo yake feelings zao zipo disconnected na hata wakiguswa hakuna kitu.

Zipo sababu nyingi sana (click hapa) ambazo huweza kuzuia mwanamke asifike kileleni wakati wa kuwa mwili mmoja.
Je, wewe unadhani nyingine ni zipi?

No comments: