"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 4, 2009

Wanatuma Signal!

Ni hufanya mwanaume kuvutiwa na mwanamke?
Ukweli kila mwanamke hutuma signal kwa mwanaume na wanaume wengi huweza kufanya detection ya hizo signal kwa sekunde tu na signal za kwanza ambazo mwanamke huzituma na kupokelewa na mwanaume ni mwonekano na lugha ya mwili (body language)

Ni rahisi mno kwa mwanamke kumvutia mwanaume kwani wanaume huvutiwa sana kwa kile wanaona, hata hivyo jambo la msingi kwa mwanamke ni kufahamu kwamba ni aina gani ya attention anahitaji kutoka kwa mwanaume kwani wavuvi huamini kinachodhihirisha aina ya samaki utakayemkamata ni aina ya chambo unayotumia.

Je, unahitaji mwanaume kuvutiwa na wewe kama mwanamke (person) au kama chombo cha starehe (an object) hivyo basi ni muhimu kuzingatia mambo ya msingi ili kupata kile unahitaji.

Mwanamke kujiamini ni jambo la kwanza na msingi kabisa kwa kumvutia mwanaume, kujiamini wewe mwenyewe na mazingira yanayokuzunguka huweza kumvutia mtu anayefanana na wewe, pia utajisikia na kuona watu wanavutiwa na wewe pia.

Mwonekano wako (appearance) ni jambo la msingi sana, mwonekano wako na jinsi unavyotumia mwili wako kuongea huvutia sana hata hivyo ili uliyemvutia abaki na wewe unahitaji personality na uchangamfu.

Pia Kumbuka kwamba jinsi unavyoonekana na kufanya pale mnakutana kwa mara ya kwanza ni muhimu sana kwani akikutana na wewe wakati upo ovyo kuliko wakati wote hawezi nkupoteza muda kuwa na wewe tena (first impression)

Pia hakikisha unampa mwanaume sababu ya msingi ya yeye kukufikiria wewe, hapo inabidi uwe mbunifu kuhakikisha milango yake ya fahamu itafanya akukumbuke, mwanamke hupendeza akivaa nguo soft, pia kuvaa smile usoni kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa yeye kukuondoa kwenye mind yake.

Jitahidi kuhakikisha anajisikia yeye ni very important, elekeza akili yako kumsikiliza na pia respond kwa kile anaongea na ku-respect mawazo yake. Cheka anatoa jokes zake hata kama jokes zake hazina kichwa wala miguu hapa ni kuwa na interest kwenye interest zake.

Na mwisho usithubutu kuwa kitu kingine na ukasababisha yeye ku-fall in love na sanamu kwani siku akikugundua wewe halisi (real you) hapatatosha. Onyesha originarity yako na kwamba ni wewe kamili na si mwingine katika haiba, akili na tabia.

No comments: