"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 7, 2009

Ya kwako ni Ipi!

Ni vizuri kufahamu kwamba ili mahusiano yadumu kuna umuhimu wa wapendanao kuwa na asilimia kubwa ya kufanana kwa tabia kuliko kuwa tofauti.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za mahusiano ambayo baada ya muda mwanandoa huweza kujikuta ndoto zinayeyuka.

Mahusiano ya hasira.
Hapa mtu anaenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye ni tofauti kabisa na familia yake kwa kila kitu na lengo ni kuikomoa familia yake (wazazi na ndugu) kwa sababu una hasira nao.
Kuna njia za kupamba na hasira lakini si katika kuoa au kuolewa kwani mwenye kuumia ni wewe.
Pambana na hasira zako kwa njia zingine pia jifahamu na uwe na moyo wa kusamehe ndo kuonesha maturity lakini si hasira na kwenda kuoa au kuolewa na mwenzi ambaye yupo tofauti na wewe mwenyewe kwa lengo la kuwakomoa wazazi.

Mahusiano ya kimishenari
Haya ni mahusiano ambayo mmoja hujaribu kubadilisha dini ya mwenzake ili aoe au kuolewa “Usipobadilisha dini sikuoi au huwezi kunioa”,
Je, akikubali kubadilisha dini then akakuoa na baada ya kukuoa akaacha dini yako itakuwaje? Utajuta!
Ukweli ni kwamba mahusiano ya aina hii hayawezi kuwa na afya mbele ya safari kwani mmoja huwa na agenda ya siri (anaweza kusema ndiyo nimekubali kumbe moyoni hajakubali kabisa anakutaka wewe tu siyo dini yako) na bahati mbaya zaidi ukishaingiza mambo ya dini kwenye ndoa ni ngumu sana kuvunjika.
Unachanganya emotions za mapenzi na dini?
Romance na dini?
Atakukubali kubadilisha ila mbele ya safari (siyo mwisho) mmoja huangukia pua.

Mahusiano ya kutoa sadaka
Wengi hasa wanawake (si wote) huamua kujitoa sadaka kumpenda mwanaume ambaye hapendeki kwa malengo kwamba siku moja atanipenda asilimia 100.
Huu ni uhusiano kama wa mgonjwa na nesi kwa maana kwamba hujitoa kupenda, kufariji, hata kumtunza mpenzi wake kimavazi, chakula, pesa akitegemea atakuja kupendwa zaidi au kuolewa wakati huohuo anayefanyiwa wala hana mpango (wajinga waliwao).
Mahusiano ya ana hii huwa so exciting mwanzoni hata hivyo mwisho wa safari anayejitoa sadaka huona amedanganywa na kutumiwa.

Mahusiano Exotic
Haya ni mahusiano ya watu ambao kunatofauti kubwa sana ya utamaduni na mila.
Ni kweli mahusiano ya aina hii huwa exciting na adventurous.
Hata hivyo kuna wakati hukosa ladha, hivyo jambo la msingi kabla ya kuwekeza muda wako, nguvu zako, pesa zako kwenye haya mahusiano ambayo unaenda nchi za mbali kubeba exotic species hakikisha umefikiria miaka 50 ijayo.

Mahusiano ya tofauti ya umri uliokithiri
Hapa kunakuwa na tofauti kubwa sana ya umri wa wahusika, ni kweli age is just a number hata hivyo haiko hivyo wakati wote.
Kupishana miaka zaidi ya 20 kuna matatizo yake.

Hata kama unataka kuishi na mama au baba si suala la mke au mume kwani kuna wakati wanandoa huhitaji kuwa na fun ambazo kwa umri kupishana sana ni ngumu.
Hata tukiacha sababu ya kisaikolojia za tofauti kubwa ya umri suala la kupishana sana umri ni moja ya mahusiano yenye tofauti kubwa kuliko kufanana.

Mwanzoni inaweza kuwa raha kwani mwenye umri mkubwa anaweza kuwa amejijenga hata hivyo baada ya muda anaweza kukugeuka kwa hivyo vitu vyake, zaidi anakuwa hana energy kwa baadhi ya shughuli pia kuna kupishana sana katika interest kwani mwingine anakuwa wa miaka ya 47 iliyopita na mwingine kizazi kipya au unaweza kuona mwenzako ni kama mtoto au ana IQ ya kitoto kila siku.

No comments: