"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 29, 2009

"Many waters cannot quench love, neither can the floods drown it."
-The Bible, Song of Solomon 8:7

Ni kama mkulima!

Je, umewahi kusikia kwamba mwanaume hutazama maisha kimakenika (mechanics) na mwanawake hutazama maisha kwa mfano wa mkulima?

Kukiwa na matatizo katika ndoa au mahusiano au na Yule anampenda mwanaume mara moja huwa na wazo kwamba hapa kuna tatizo na anachofanya ni kutafuta spare part mpya na kuiweka na maisha kuendelea kama kawaida.

Kwa upande mwingine mwanamke, kukiwa na tatizo katika mahusiano au ndoa yeye huona hilo tatizo ni mfano ya bustani (garden) inayokua na inayohitaji matunzo na efforts kuhakikisha kila kitu kinakuwa kizuri zaidi.
Huamini mahaba na mapenzi mazuri ni wakati garden imechanua maua vizuri na kukiwa na tatizo ni magugu yanayotakiwa kuondolewa.

"Love is like a mountain, hard to climb,
but once you get to the top the view is beautiful."

-Daniel Monroe Tuttle

Wa Kufanana naye - chumbani

Tofauti ya kiumbo kati ya mke na mume ni asilimia ndogo sana ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa ujumla.
Bila kufahamu tofauti zilizopo tunaweza kujikuta katika shida na matatizo au confusion ya uhakiuka chumbani.
Ukiacha tofauti zingine zote zilizopo kati ya mke na mume linapokuja suala la sex mwanaume sex ni hitaji la kimwili kwanza (physical) na baadae emotions wakati mwanamke ni hitaji la emotions kwanza then kimwili.
Hii ina maana kwa mwanamke sex ni upendo kwanza, kujisikia vizuri kwanza, kupata caring kwanza kwa mwanamume ni kuwasha tu na bus linaondoka.

Linapokuja suala la kila anakiona mwanaume anavutiwa kwa nguvu ya ajabu (hasa anapomuona mwanamke, wakati huohuo mwanamke naye anauwezo na nguvu ya ajabu ya hamu ya upendo, ukaribu, mapenzi na kusikilizwa na mwanaume.

Mwanaume huwaza ni mara ngapi anahitaji sex wakati mwanamke anawaza ni namna gani sex itakuwa.

Wa kufanana naye - Migogoro!

Kukiwa na mgogoro kati ya mume na mke, kawaida mke hujitahidi kufanya bonding na mumewe kwa kuongea (talk, relate) na kuhakikisha emotions zinakuwa wazi kwa kuwa hajui tofauti ya mwanaume huamini na mume wake naye atakuwa mwepesi kuongelea kama yeye na matokeo yake mwanamke huishia kuwa na hasira na frustrated.
Jambo la msingi ni kwamba mume anatakiwa kufahamu kwamba kunapotokea mgogoro au kupishana lugha ni jambo la maana sana kumsikiliza mke au kuhakikisha mnaongea na unampa mke muda na wakati wa kutosha kuongea yote aliyonayo (kutoa emotions zake hata kama atalia machozi ila hakikisha analia akiwa mwilini mwako) na kwa njia hiyo anajiona unamjali kuliko kumwambia tusiongee sasa au tutaongea baadae au kukwepa au ku-ignore maana hapo ataumia zaidi na kuona humjali, hapendwi na upo harsh.
Pia mke naye asikasirike pale anaona mume anakwepa kuongelea tatizo au mgogoro uliopo kwani wanaume ndivyo walivyo (tofauti zilizopo kwani wanaume huamini kwa kuacha kuongelea ndiyo njia nzuri ya kumaliza mgogoro) hivyo wewe mke mpe muda na akitulia (akitoka kwenye cave) mnaweza kuongea zaidi.
When men and women agree, it is only in their conclusions; their reasons are always different.
- George Santayana.

Friday, August 28, 2009

Wa kufanana naye - Kuomba msamaha!

Wanawake wengi akisema samahani ( I am sorry) ni njia mojawapo ya kujiunganisha (connect) na Mume au mtu mwingine kama kuna mgogoro au tatizo au kitu chochote anaona hakipo sawa, inaweza kusema samahani hata upande mwingine unavyijisikia vibaya.

Kwa mwanaume kusema samahani ina maana anakubali kwamba amekosa na anatakiwa kuomba msamaha.
Mwanaume anaamini kwamba kwa kusema hivyo inamuweka chini zaidi na hujiona si mwanaume wa uhakika (unmasculine) na kwake haikubaliki haikubaliki kabisa.
Kama mume wako huwa anatoa samahani waziwazi basi umebarikiwa kwani mwingine badala ya kusema samahani yupo tayari akanunue zawadi kubwa ujue anaomba msamaha, hata hivyo kama wewe ni mwanaume kumbuka kwamba ni muhimu sana kutamka neno samahani nimekosa kwa mkeo bila kuzunguka wala kuzungusha sentensi.

Na kukitokea conflict yoyote wanawake hujisikia wana wajibu wa kuhakikisha wanafanya kitu kuondoa hiyo conflict ndiyo maana wanawake wengi wapo tayari kwenda hata kwa mtu mwingine anayemwamini kuomba ushauri.
Wakati wanaume hukwepa (withdraw) na anaweza kutumia muda mwingine kufanya vitu na rafiki zake na kukwepa familia ambayo huko mke wake anamsuguano naye.
Kama ni mwanaume ni vizuri kufikiri na kujiuliza upya kipi muhimu?
Familia au rafiki zako?
Familia ilikuwepo hata kabla ya kanisa na familia ni mahali ambapo kanisa huanzia hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unamaliza conflict yoyote na kurudi nyumbani (kuwa na familia).
Ukipoteza familia umepoteza vyote!

Wakufanana naye

Wanaume kila kitu kina folder lake! Wanaume hufikiria kitu kimoja kimoja (ndani kiboksi) au kingereza (COMPARTMENT) wakati mwanamke hifikiria vitu vingi kwa wakati mmoja (GLOBAL).
Pia jinsi tunavyotunza information kwenye ubongo mwanamke na mwanaume ni tofauti kabisa.
Wanaume tunaweza kuhifadhi information kwa kuzitenganisha kila information na folder lake kama vile kazi, hobbies, mke, sex, nk pia hili folder linakuwa limo ndani ya drawer kwa maana kwamba hufungua na kufunga kitu kimoja kwanza ndipo aje kingine.
Hii ina maana kwamba mwanaume atawaza kuhusu kazi, then hobbies, then mke, then sex tofauti tofauti.
Kwa upande wa wanawake wao ni opposite kwani vitu vyote kwao ni munganiko na wanayaona maisha globally.
Hii ina maana kwamba mwanamke huwaza kuhusu kazi, hobbies, mume, sex vyote kwa wakati mmoja.

MFANO
Fikiria mume wako yupo kazini na unampigia simu kwamba anaporudi kazini apitia dukani anunue maziwa na unashangaa anafika nyumbani mikono mitupu.
Hii ni kwa sababu wakati unampigia simu alikuwa anahusika na kazi, analikuwa ana folder la kazi alikuwa kazini (kwenye kiboksi cha kazi) kwake focus ilikuwa ni kazi ifanyike.

Je, umewahi kuwa unaongea kitu na mume wako let say yeye anaangalia mechi ya soka huwa unajisikiaje, si unamuona anaipa attention kubwa hiyo mechi anaangalia kuliko wewe mke wake na unamshangaa hadi unatamani TV iharibike.

Kama wewe ni mwanaume naamini umewahi kuwa na kamzozo kadogo na mkeo siku moja, hata hivyo cha ajabu zaidi ukajikuta mke anakumbushia na mizozo mingine au vitu vingine ambavyo ulifanya miezi mitatu au sita iliyopita.
Wewe unashangaa kwani kuna uhusiano gani na hayo yalifanyika miezi sita iliyopita na hili tunaongelea sasa (zozana).

Kama kumewakua na disagreement kati ya mke na mume asubuhi ni rahisi kusikia mke anasema kichwa bado kinamuuna jioni ya hiyo siku kwani siku nzima atakuwa ana global meetig kwenye ubongo wake kuwaza hiyo disagreement ya asubuhi.

Kinachotokea kwa mume ni kwamba baada ya hiyo disagreement asubuhi kabla ya kuondoka, disagreement ni kama file au folder hivyo anapoondoka kwenda kazini anafungua drawer yake anafunga na kuondoka na akifika kazini anafungua drwer ya file la kazi na kuendelea kufanya kazi, lakini kwa mke kwake siku nzima atashinda anawaza kuhusu hyo disagreement hadi jioni mume akirudi.

Pia inawezekana wakati mnaingia chumbani hamkufunga mlango na kwa kuwa mliingia huku mnaharaka na mahaba basi mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa.
Hii ina maana kwamba mke atakuwa anafanya sex huku anawaza mlango haujafungwa wakati mume hata kama mlango anajua haujafungwa yeye atahusika na kiboksi kimoja cha kufanya sex tu.

Ni vizuri kujua tofauti ili pale kukiwa na tofauti badala ya kukasirika na kuchukia unafurahi na kushukuru Mungu kwa hizo tofauti kama si kumwombea mwenzako kwa Mungu.

Thursday, August 27, 2009

Wa kufanana naye!

Uwezo wa kuwasiliana kati ya mke na mume ni moja ya precious commodities muhimu sana katika ndoa au mahusiano yoyote.

Wanandoa wenye uwezo mzuri wa kusiliana huwa na ndoa/mahusiano bora na zaidi huweza kuwa na watoto ambao nao huwa wazuri katika kuwasiliana na hatimaye kuwa candidates wazuri wa ndoa baadae.
Pia kuwa na mawasiliano mazuri husaidia mtu kuwasiliana na watu wengine na kuwa na mvuto zaidi.

Kuna usemi wa kingereza usemao
"Great communicators are people who change their approach based upon the person they are talking to"

Hii ina maana kwamba kama wewe ni mwanaume huwezi ongea the same style kwa mwanaume mwenzako na mwanamke.
Kuongea na mwanamke au mke ni tofauti na mwanaume au mume.
Hivyo kujua au kufahamu jinsi ya kuongea au kuwasiliana na mke wako au mume wako ni jambo la msingi sana ili kuwa na mahusiano mazuri.


Kumbuka mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana kwani;
Huwaza na kufikiri tofauti,
Huongea tofauti,
Huamua tofauti na zaidi
linapokuja suala la hisia kuna tofauti kubwa sana.


Inawezekana wewe ukiwa na mume wako au mke wako huwa mnajikuta ni bubu, au ni kubishana tu au kila mmoja hamwelewi mwenzake au mwenzako akiongea unahisi haeleweki kwani anazunguka wakati anatakiwa kuwa direct to the point.


Unataka kujua kwa nini?


Tutaendelea kesho.
Monday, August 24, 2009

Style ipi inasisimua?

Kama vijiko ina raha yake! Swali
Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 32 nipo kwenye ndoa miaka 5 na nimejaribu milalo mbalimbali ya kuweza kunisisimua kimapenzi hadi kunifikisha kileleni kirahisi na imeshindikana.
Je, ni mlalo upi (sexual position/love making position) unaweza kupendekeza ili nisisimke na kufika kileleni?

Jibu
Kwanza asante kwa swali zuri na si wewe peke yako mwenye kukumbana na tatizo la aina hii, kwani wanandoa wengi hata kama hawaridhishwi inavyotakiwa katika ndoa zao kimapenzi bado wamekuwa wagumu kuzungumzia suala la sex kati ya mke na mume au kuomba ushauri.
Pia suala la sex ni muhimu sana katika ndoa kwani ukiridhika katika sex na ndoa utaiona inakuridhisha.

Pili aina ya mlalo (sexual, love making psotion) si dawa ya kukusisimua ingawa ni moja ya vionjo ambavyo vinaweza kukufanya uwe na tendo takatifu la ndoa linakuridhisha.
Hata hivyo kutokana na uzoefu pamoja na tafiti nyingi na medical reports nyingi dhahiri kwamba mlalo wa Rear Entry au Doggie Style ni moja ya mlalo unaoridhisha mwanamke na kumhakikishia kufika kileleni (orgasm) bila shaka.

Why?
Kitendo cha uume kukuingia kwa nyuma husaidia kumpa uwezo mwanaume kuweza kukupa thrusting inayokupa raha pia uume huweza kusugua G-spot na kuweza kukumfikisha mwanamke katika utamu na raha isiyotamkika.
Ili uume kufikia G spot (deliecious hidden joy button) lazima uume uingie huku uke ukiwa angled na hii doggie style ndiyo mlalo perfect.
Pia ukifika kileleni kwa kwa kuguswa G spot utataka zaidi na utaingizwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa raha ya mapenzi.

Zaidi pia ni kwamba mwanaume anakuwa na uwezo wa kuwa huru kuendelea kuchezea (rub) kisimi, kuchezea matiti (chuchu) hasa kama hivi vyote vinakusisimua na kama mpo portable mnaweza kuendelea kupeana kisses huku kila kitu kikiwa kinapaa kwenda hewani.

Hii ni deep penetrative sex ambayo mwanaume huwa dominant na mwanamke huwa submissive hivyo ni mlalo natural (primitive)

Pia muungano wa miili miwili kugusana kimahaba husaidia mwanaume kuona (visual) mwili wa mwanamke kwa nyuma na kama mwanaume ni mgonjwa wa kuona matako ya mke wake (fahari ya mwanamke wa Afrika) basi itakuwa dawa sahihi kwake kukupeleka mwendo wa mbali zaidi kwa yeye mwenyewe kusisimka kwa kuona vitu au kitu (ila isiwe giza nene).

Zaidi pia shaft ya uume wa mume huweza kutoa sensation ya ajabu kwenye vulva kiasi cha mke kupata raha ya ajabu.

Kawaida mwanamke huweza kufika kileleni kwa njia ya kisimi, G-spot na uke wenyewe, hivyo hii style inaweza kukupa vyote kwa wakati mmoja. Kutofika kileleni kwa sytle ya aina hii ni kweli hapo kutakuwa kuna tatizo kubwa.

Pia wakati wa kupeana mahaba mwanaume hujikuta balls zake zinagusa uke au kisimi na hii inaweza kukupa raha kama si kukufanya uwe wet zaidi na zaidi hahaha over and over!
Je kuna mlalo mwingine zaidi?
Ni kweli tendl la ndoa ni sanaa hivyo ubunifu ni kitu cha msingi kabisa, mlalo mwingine ni ule wa front to back/spoons (mke na mume kulala kama vijiko vinavyopangwa kwa maana kwamba wote mnalala (kiupande)kuelekea upande mmoja kwa mume kulala nyuma ya mke na kumwingia kiubavu kwa nyuma).
Hii pia huweza kuleta matokeo sawa na ile ya doggie style au rear entry.
NB:
Jambo la msingi ni kwamba ili kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha kwa na maandalizi ya kutosha ndiyo jambo la msingi (foreplay) si suala la kukimbilia haraka doggie style wakati hamjasisimuana vya kutosha.
Na mawasiliano ni jambo la msingi kabisa.

"'Marriage is not mind reading, so ask your spouse what he/she wants and believe what he/she says.'"
— Clare Graca

Kukubali kutokukubaliana!

Kabla hatujaoana, mchungaji aliyefungisha ndoa alituambia
You are two imperfect people making an imperfect union and that is wondwerful”
huu ushauri ulinifanya nishangae kwani naamini ndoa bora wanandoa hukubaliana kila kitu.

.Hata hivyo baada ya kuishi kwenye ndoa miaka 5 tumejifunza kukubaliana na tofauti na mawazo ya kila mmoja wetu na tumegundua kwamba tofauti zilizopo baina yetu zinatufanya kila mmoja wetu kuwa special
Beth Swanson

Sunday, August 23, 2009

Siku mbili au nne kabla

Awe baby girl au baby boy wote wanathamani sawa! Ili kupata mimba timing ni kitu cha msingi sana.
Na kutaka kupata jinsia ya mtoto unayotaka hapo unahitaji timing ambayo ni strategic lini mke na mume wakutane kimwili.

Kuna njia inayojulikana kwa jina la Shettles ambayo imeendelezwa na Daktari Landrum Shettles ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Vitro fertilization pia ametoa kitabukinachoitwa “How to Choose the Sex of Your Baby, 1996), kinatoa ratiba kamili ya lini tendo la ndoa lifanyike ili kupata mtoto wa kiume au wa kike kirahisi.

Hii ni kutokana na uhakika kwamba mbegu za mtoto wa kiume husafiri haraka (speed) kuliko mbegu za mtoto wa kike na hufa haraka wakati huohuo mbegu za mtoto wa kike huwa na speed ndogo na huishi kwa muda mrefu bila kufa.
Hii ina maana gani kama utataka kuwa na rangi za pink na blue (mtoto wa kike au kiume)?

Wanandoa wanaotegemea kupata mtoto wa kiume njia ya Shettles inashauri mke na mume kukutana kimwili siku moja kabla ua siku hiyohiyo ambayo mke anakuwa fertile au ana ovulate.
Hii huongeza uwezekano kwamba ile mbegu yenye speed (kiume) itakutana na yai (kwani kurutubishwa hutokea katika fallopian tubes na mbegu moja yenye bahati huweza kulipenya yai lililotolewa kutoka kwenye ovary).

Wanandoa wanaotegemea kupata mtoto wa kike wanashauriwa kukutana kimwili siku mbili au nne kabla ya ovulation na hakuna kukutana kimwili tena baada ya hizo siku.
Hapa ni kumaanisha kwamba mbegu za mtoto wa kiume pamoja na speed zake zote zitawahi kufika na kufa kabla ya yai kufika na mbegu za mtoto wa kike zinakuwa zipo zinasubiri yai (yai litazikuta zinasubiri na mbegu moja yenye bahati itapenya na kuingia kwenye yai kulirutubisha kwani zinaweza kuishi kwa muda mrefu kwenye reproductive tract.

Njia hii ya Shettles ina uhakika wa asilimia 80% kwa wanandoa kufanikiwa kile wanahitaji hata hivyo wazazi wengi au wanandoa wengi wanakubaliana kwamba mtoto mwenye afya ndiye jambo la maana bila kujalisha ni baby girl au baby boy.

Kubwa kuliko yote ni kwamba haya ni masuala ya kibinadamu tu kwani Mungu ndiye mwenye uwezo wote linapokuja suala la kupata mtoto au baby boy au baby girl.

Saturday, August 22, 2009

Kuridhika

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba kuridhika na ndoa (marital satisfaction) huendana na kuridhika kimapenzi (sexual satisfaction) hata hivyo suala la kuridhika katika ndoa na kimapenzi ni kama swali ya yai na kuku kujiuliza kipi kilitangulia.
Je, kuridhika na ndoa huweza kusaidia kuridhika kimapenzi?
Je, si kuridhika kimapenzi ndiko husababisha kuridhika na ndoa uliyonayo?

Kama mwanandoa mmoja haridhiki kimapenzi (sex) katika ndoa hupelekea kujisikia haridhiki na ndoa yenyewe pia kama mwanandoa mmoja haridhiki na ndoa aliyonayo hupelekea kujiona haridhiki na mapenzi katika ndoa.
Hii ina maana kwamba huwezi kuwa na kimoja bila kingine kuwepo.

Mungu ametuamuru kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kumridhisha mke au mume wake kimapenzi na Sayansi nayo inatoa ushahidi kwamba kuna faida kubwa ikiwa wanandoa wataishi maisha ya kuridhishana kimapenzi na hatimaye ndoa yenyewe.

Kama kanisa linaamini talaka ni kitu kibaya na kukaa katika ndoa ni jambo jema basi halina budi kufundisha na kusisitiza kwa nguvu zote au uwezo wote wanandoa kuridhishana kimapenzi kunakopelekea kuridhika katika ndoa zao.

Ni mara ngapi kwa wiki huweza kusababisha kuridhishana katika hisia za mapenzi (sex)?
Mwili wa mwanaume huweza kuzalisha sperms kila baada ya masaa 72 (siku tatu) ndivyo Mungu aliumba.
Mathematically ina maana kwamba tendo la ndoa ni muhimu sana siku 2 au 3 kwa wiki kuweza kufanya connection ya feelings za wanandoa kiroho na kimwili.
Kukiwa na kuridhishana kimapenzi katika ndoa ni ukweli kwamba hata wanandoa wataridhika na ndoa yao kwa ujumla.

Friday, August 21, 2009

Jaribu hizi tatu!

Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena!
Hawezi kushirikisha kitu chochote (emotions/feelings) ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja.
Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu.
Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo.

Tembea katika Roho:Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu.
Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume.
Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kwamba huwezi ukampenda Mungu usiyemuona ukashindwa kumpenda partner wako ambaye unamuona.
Ukiguswa na Mungu lazima na ndoa yako itakuwa ya tofauti.
Kumbuka kutembea katika Roho (Roho Mtakatifu) ni kitu tofauti na kujiita Mkristo

Achana na kukaa kwenye lawama, maumivu, uchungu, kuangalia udhaifu wa partner wako:Yeyote ambaye analalamika kwamba ndani ya ndoa yake hakuna upendo ukichunguza kwa makini utakuta amebeba fulushi zito sana la orodha ya mambo mabaya ambayo partner wake anamfanyia au udhaifu wa partner wake.
Anaongelea huo udhaifu wa partner wake, anasimulia rafiki zake, anauamini, anauwaza, anaukiri kutembea nao kama sala.


Kumbuka!
“You are by want you think”Biblia pia inasema
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo
(Mithali 23:7)

Hisia mbaya (negative thoughts) hata kama ni kweli huwa na matokeo mabaya kwenye feelings.

Orodhesha vitu 10 vizuri kuhusu mke/mume wako na kiri mara mbili kwa siku kwa siku 21
Shukuru kwa kila jambo.
Kulalamika kila siku huweza kuharibu emotions zako bila kujua hata kama mume wako au mke wako hafai kabisa bado unaweza kutumia mambo mazuri aliyonayo kuirudisha ndoa yako kwenye mstari.

Huwezi ukawa na mawazo tele ya udhaifu wa mke wako au mume wako na wakati huohuo ukamfurahia na kumpenda na kuwa na feelings za upendo wa juu.
Vita ya upendo huweza kushinda au kushindwa kwa mawazo yako kwani moyo ni mtumishi wa mawazo yako.

Moyo huamini kile mawazo yako yanakitunza.
Mtu mmoja (jina limewekewa password) alikiri kwamba hampendi tena mke wake na kwamba ilikuwa ni miezi mitatu kila mmoja alikuwa analala chumba chake, nilipomwambia aandike mambo kumi mazuri kuhusu mke wake kwenye karatasi.
Tukakubaliana kila siku asubuhi anapoenda kazini kuyatafakari hayo mambo mazuri 10 kuhusu mke wake na pia kuyatafakati tena jioni akirudi kazini anapoendesha gari lake.
Baada ya siku kumi akakiri kwamba sasa mambo yameiva kwani tumerudiana, zaidi kulala chumba kimoja sasa tunalala kitanda kimoja.

Na baada ya wiki tatu akakiri kwamba anampenda mke wake kuliko wakati wowote katika maisha yao ya ndoa tangu waoane.
Alipoulizwa je, umeyashika (memorize) yale mambo 1o mazuri kuhusu mke wako akasema kwamba yale aliyashika siku ya tatu na siku ya nne akaamue kuongeza hadi yakawa 15 na kwa kuwa yalikuwa mtindo wa Cards hivyo alikuwa anayapitia moja baada ya lingine na kuyachanganya na kuyakiri over and over.

Hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa na orodha ya mambo 10 mazuri kuhusu mke au mume wake na akayatamka na kumshukuru Mungu twice a day na kusiwe na kufufuka kwa upendo mpya (compassionate love)

Kumsifu na kumshukuru mke wako au mume wako mbele za Mungu kwa mambo mazuri aliyonayo ni silaha ya nguvu kubwa ili kuwasha upendo na mapenzi mapya katika ndoa.
Ubarikiwe na Bwana!

Thursday, August 20, 2009

Ukaribu kimapenzi

Haina haja kuogopa kuelezea hisia zako kwa yule unampendaUtafiti wa hivi karibuni Umetoa ushahidi ambao unafurahisha na kuleta matumaini mapya kuhusu ndoa.
Kutokana na huu utafiti ni dhahiri kwamba wanandoa pamoja na washauri wa mambo ya ndoa watakuwa na mtazamo mpya kuhusu ndoa na zaidi kuzifanya ziwe za kudumu na kuwa na afya.

Utafiti huu wa miaka 13 ambao ulianza mwaka 1981 ambapo kiongozi wa huo utafiti Ted Huston alianza kufuatilia maisha ya wanandoa wapya 168.
Alipomaliza utafiti wake mwaka 1994 ni ndoa 56 kati ya 168 zilikuwa tayari zimeshavunjika (divorce).

Huston alijifunza mambo makubwa matatu
Ukaribu wa wapenzi, faragha kwa wapenzi (intimacy)
- Kinachosababisha migogoro (conflicts)
- Jinsi ya kuwezesha ndoa kudumu na kuwa na furaha.

Mara nyingi washauri wengi wa mambo ya ndoa wanaamini kwamba migogoro, kuzozana, kuzipiga, kutofautiana, kutoana ngeu, kutoheshimiana tofauti zilizopo kati ya mke na mume na kuvurugana katika ndoa ndiyo sababu za wanandoa kutalikiana.

Hata hivyo utafiti wa Huston Umetoa mtazamo mpya kwamba kukosekana kwa faragha ya wanandoa (intimacy) na upendo ndiyo sababu kubwa na ya msingi wa mahusiano mengi kujizungusha mshale wa mwanaume wa kigogo akiwa nyikani kuelekea kwenye talaka.
Kuzipiga na migogoro katika ndoa ni matokeo (results) si kitu kinachosababisha (cause) ya kukosekana kwa intimacy.

Hii ina maana kwamba ni jambo la maana sana kwa wanandoa na washauri kutumia muda wao kuhakikisha wanandoa wanatunza hisia chanya (positive feelings) kati yao na siyo kuhangaika waache kugombana.

Zifuatazo ni njia mojawapo ambazo zinaweza kukuhakikishia unatunza feelings zako na ukaribu na mpenzi wako.
Elezea au onesha mapenzi yako (affections) mara kwa mara kwa mume au mke wako kama vile kukumbatiana, kubusiana, kushikana (cuddling), zawadi ndogo ndogo, na kitu chochote ambacho unajisikia kufanya kwa ajili ya mpenzi wako.
Wasiliana vizuri, shirikisha feelings zako, ongea mambo yanayohusu mahusiano yenu au ndoa yenu, mambo mazuri na ndoto mbalimbali kuhusu ndoa yenu au mahusiano yenu na uwe mkweli (siyo kufungana kamba, maana wanaume wengine kwa kupiga fix hawajambo, na kuna wanawake pia bila kufungwa kamba hujamfurahisha)

Hakikisha mke/mume anakuwa update na kile kinaendelea kila eneo la maisha yako au yenu, hata kama ni vitu vidogo ambavyo unaona vidogo sana.
Kuwa supportive na mwenye kutia moyo (encouraging) ili mwenzi wako ajisikie safe kujishirikisha kutoa mawazo, hisia na emotions kwako.

Pia tafuta project ambayo wote itawapa wakati mzuri kuifanya pamoja.
Panga maisha ya baadae pamoja huku ukiweka msisitizo kwenye malengo ambayo mnaweza kufanya pamoja kwa msisimko.

NB:
To protect and preserve your marriage, focus on maintaining intimacy and closeness with your partner.

Wednesday, August 19, 2009

Kuchukuliana!

Tukioa na kuolewa tunazama kwenye udhaifu na kwenye uchumba tunaona uzuri tu!Kabla ya ndoa au wakati wa uchumba wengi hujikuta wakiwa makini sana katika kuangalia uimara wa wapenzi wao na baada ya ndoa hujikuta wakijikita katika kuangalia udhaifu (weakness) za mwenzi wao.
Hii ni kwa sababu wakati wa uchumba wawili wanaopendana hujihusisha katika kuburudishana kwa maana kwamba wakati mwingi hutumia kuwa na social activities na kila mmoja huwa na romantic interest.

Wakiingia kwenye ndoa mambo huwa tofauti (waliooa na kuolewa anafahamu na kama hujaolewa au kuoa huwezi elewa kwani hujafika hii hatua) kwani hapa ni uwajibikaji (task oriented maana wawili hawa sasa wanatakiwa ku-share skills zako in reality.

Kuwa na udhaifu fulani ambao mwenzako inabidi akuchukulie ni hitaji la kila mmoja na halikwepeki kwani ni kitu ambacho kipo kwa ajili ya kutuwezesha kufanya marekebisho ya kujuana kupitia tofauti zilizopo ili kuwa na ndoa iliyo imara zaidi.

Jambo la msingi hapa ni kujifunza tofauti zilizopo na udhaifu uliopo na kuchukuliana, na pia ni jambo lililowazi kwamba huwezi kumpata mtu hapa duniani ambaye hana udhaifu au hana kasoro au amekamilika kila eneo la maisha, it is next to impossible.
Kama unaota kwamba siku moja unataka umpate partner ambaye hataumiza moyo wako unakosea sana kwani kila kwenye upendo kuumia moyo kupo.

Pia ni vizuri kufahamu kwamba kuna mambo duniani bila kujalisha umesoma kiasi gani, una akili kiasi gani, au una uwezo kiasi gani au jamii inakuamini kiasi gani bila Mungu inakuwa bado ni zero kubwa.

Mwanandoa analiye na hofu ya Mungu (ameokoka siyo mwenye dini) na ambaye amejazwa Roho mtakatifu yupo tofauti na mwanandoa yeyote duniani hasa linapokuja suala la kuchukuliana udhaifu na mwenzi wake.
Je tofauti hiyo ipoje?

Binadamua tunatabia ya kuona mabaya kwa wengine hata mke au mume badala ya mazuri.
Hivyo ili kukubali udhaifu wa partner wako unahitaji sifa 9 ambazo zinapatikana Galatia 5: 22-23
Mwanandoa wa aina hii huweza kufurahia ndoa kwa sababu anaweza kushinda kumchukulia mwenzake udhaifu wote kwa kuwezeshwa na Roho mtakatifu.
Kutembea katika roho huweza kufanya udhaifu wa partner wako kuwa si kitu.

Tofauti ya wanandoa haitakiwa kuwa janga kwani kile ambacho wanandoa wanafanya wakati wa mgogoro au tofauti huelezea success au failure ya ndoa.

Ndoa nyingi ambazo leo tunaona nzuri zilipitia conflicts hata hivyo kupitia conflict (siyo zote) zilisaidia wahusika kujuana na kufahamiana vizuri na kupendana zaidi.

NB:
Marriage is one of the most gratifying and difficult of all human relationships.
Preparing well for it is a great gift to give your future spouse and the children who will join your sacred union.

Tuesday, August 18, 2009

Kutunza Moto chumbani! usirudie haya....

Kuwa na utaratibu uleule miaka nenda rudi.
Kwa kuwa unajua nini hufanyika ukiingia chumbani na mke/mume wako, hivyo unavua nguo zako na zake, unamvuta ( kwani anajua ukimvuta kwa mtindo huo nini unataka naye anakuacha uendelee, nawe unachukua kiungo A na kuiingiza kwenye kiungo B, unafanya kile unachokijua, baada ya dakika 5 zoezi limeisha, unageuka unalala, hoi folilo!
Unaonaje hapo?

Hapa haijalishi hili tendo ni tamu kiasi gani, nunaburudika kwa raha kiasi gani, unapiga kelele za raha kiasi gani, ni dhahiri ya miaka kadhaa hili zoezi litakuwa nadra sana kufanyika na ikifanyika lazima mmoja atajisikia it is boring.

Kuwa na utaratibu unaofanana kila siku kila mwezi na kila mwaka huhatarisha mahusiano ya kimapenzi kwa mke na mume.
Njia nzuri ya kulinda upendo na connection ya thamani kati ya mke na mume katika mapenzi ni kuwa na kitu kipya baada ya muda fulani hata kubadilisha mazingira tu acha skills.
Ukweli kukiwa na new tips na techniques mtafurahia sana kuwa mwili mmoja kwani mtakuwa hot, na mtahitajiana mara kwa mara na zaidi.

Kuogopa kuongelea au kujaribu vitu vipya wakati wa kuwa mwili mmmoja.
Je, umewahi kuwa na wazo zuri au jipya la kutaka kuongeza ladha mpya chumbani ukiwa na mke au mume wako na unashindwa uanze vipi au hujui mwenzi wako ata-respond vipi?
Au unaogopa atakuuliza ulijifunza wapi? Au akaenda mbali zaidi kwa kukuuliza nani amekufundisha?

Ukweli ni kwamba kuna asilimia 90 mpenzi wako atapenda kusikia na pia atashirikiana na wewe kujifunza hizo new skills muhimu tumia hekima na busara kuwakilisha mawazo yako na kila kitu kitakuwa shwari huko chumbani.
Pia ni dalili kwamba mnaogopana na zaid hampo wazi sana kuongea mambo yenu ya ndani ambayo ni muhimu na yanaweza kuwaweka karibu zaidi.
Jiamini na ongea kile unapenda kwa nini ujinyime raha?
Kalaghe bhaho!

Kujaribu kumlazimisha mume/mke wako tendo la ndoa.
Kama mke au mume amechoka au hana mood haina haja kuanza kumlazimisha afanye; for sure it will not work.
Wakati mke au mume anasisimka mwili humwaga kemikali za adrenaline ambazo husaidia kuupa mwili energy ya tendo zima la ndoa hivyo kama amechoka anaweza asisisimke vya kutosha na maana yake atakuwa hana nguvu za kujirusha sawasawa at the maximum ili kuleta matokeo mazuri.

Ikiwezekana kama wewe ni mwanamke na mume usiku amegoma kwa kwua amechoka (kwani huwezi kuisimamisha stick hadi ubongo wake uamue) usijali subiri hadi asubuhi kabla hajaamka kwani kiwango cha testosterone huwa juu kuliko wakati wote hivyo utamfaidi tu na hana ujanja stick itakuwa imesimama na ipo tayaritayari, usifanye kosa tumia busara.

Kama wewe ni mwanaume na mke anasema amechoka kitu cha kwanza ni kutengeneza mood yake ili awe katika hali ya kuwa relaxed, maneno matamu, ongea kile huwa anapenda kusikia, ni vizuri mwanaume kujua nini humfanya ajisikie kunyegeka na kuwa excited hata kama utatumia nusu saa kwani si una mission?
Tumia skills zako zote.
Itafika mahali atajieleza mwenyewe kwa jinsi unavyomwona ila ukishindwa kamwe usimlazimisha na pia usifanye kwa kuwa amesema yupo tayari ni muhimu kufahamu kwamba kukubali kwake ni ni sababu anapenda na siyo ili yaishe utaishia kuulizwa “hujamaliza?”

Kuacha au kukwepa/kuruka kipengele cha kuandaana kabla ya tendo la ndoa
Wanandoa wengi (hasa wanaume) hupenda kukwepa kumuandaa mke (foreplay) ili kuwahi kufaidi kitu chenyewe hata hivyo kumuandaa mke humpa faida hata mume mwenyewe.
Kwa kubusu, kumshikashika (touching) na mengine yote huweza kusababisha mke kujisikia ameridhika na atajisikia humtumii kwa tamaa zako.
Hivyo slow down, take time!
Lazima mwanaume uwe playful na usiwe na mikono mwepesi bali mikono slow.

Kutumia mikanda ya video za X kuimarisha utendajie wa mpenzi.
Wakati maisha ya ndoa yamefikia hali mbaya wapo wanandoa ambao huamua kutumia video (mikanda ya X) kujifunza wakidhania maisha yao ya mapenzi yanaweza kuwa kiwango cha juu kiasi cha kufika kwenye roof.

Ni kosa kubwa and it is Wrong! Dangerous.
Hawa akina XX video wapo ukoo mmoja na wale jamaa wa Sodoma na Gomora!

Kutumia outside source huweza haraka sana kuharibu kuliko kutengeneza au kusaidia.
Ndoa ni mke na Mume pamoja na Mungu mwenye kupokea utukufu unaotokana na uumbaji wake kwa hao wawili.
(Naamini kuna critics watasema hapa nimeongea upuuzi hata hivyo mtu wa rohoni atafahamu naongea kitu gani)

Monday, August 17, 2009

......Itakosa ladha!

Ukifanya haya ndoa itakosa ladha:
1. Kumzoea mwenzi wako kiasi kwamba huoni yupo special
2. Kukosa interest kwa kile mwenzi wako anajihusisha kufanya
3. Kuwa mlevi.
4. Kutoshughulikia ndugu wanapoingilia ndoa (in laws)
5. Kukosa muda kuwa na mwenzi wako hasa baada ya watoto kuzaliwa.

6. Kujisikia huna kitu common na mwenzako
7. Kukosa kula chakula pamoja angalau mara 3 kwa wiki.
8. Kukosa kulala pamoja
9. Kutojua matokeo ya kuvaa nguo nzuri, usafi, kupendeza kwa mwonekano.
10. Kutosafiri pamoja hasa safari za ghafla na dhalula kwa lengo la kuwa wawili tu.

11. Kuishi pamoja kwa sababu ya watoto tu, na si upendo wa kweli.
12. Kushindwa Kukukubaliana kutokubaliana.
13. Kushindwa kujitunza mwenyewe kimwili, kiroho na kijamii.
14. Kushindwa kuchunga afya yako.
15. Kutumia muda mwingi na jamii badala ya mwenzi wako na familia yako.

16. Kushindwa kuwa na muda wa kuburudika pamoja.
17. Kutokuwa na interest zinazofanana.
18. Kutokubaliana katika pesa.
19. Kutotumia angalau saa moja kwa wiki wewe tu na mwenzi wako kuongea pamoja.
20. Kushindwa kujadili vitu unavyopenda au kutopenda likija suala la mapenzi.

21. Kushindwa kushikana mikono au kukumbatiana huku kila mmoja akiongea na mwenzake au kupeana ndoto za maisha.
22. Kuwa mwema zaidi kwa walio nje ya familia wakati suala hilo hilo unashindwa kufanya ndani ya familia au kwa mwenzi wako.
23. Kukosa kubusu asubuhi unapoondoka kwenda kazini au Unaporudi kutoka kazini.
24. Kukosa kufarijiana.
25. Kushindwa kuuteka moyo wa mwenzi wako.

26. Kufikiri na kuamini kwamba mwenzi wako kila siku yeye tu ndiye anakosea
27. Kukosa tendo la ndoa kwa siku 21 wakati mnaishi pamoja na kulala nyumba moja na hakuna tatizo la kimatibabu.
28. Kuwa na hisia kwamba mwenzi wako ni adui yako na humpendi.
29. Kukosa muda wa kucheka pamoja na mwenzi wako.
30. Kushindwa kwenda kanisani pamoja
31. Kutokujali kuongelea moja ya hayo hapo juu kuonesha kwamba unataka mabadiliko.

Sunday, August 16, 2009

Laughter is the shortest distance between two people.
Victor Borge

Saturday, August 15, 2009

Tusibebeshane!

Wakati mwingine huwa tunajikuta tumebeba maboksi ambayo tunadhani ndani yake kuna vitu ambavyo tulitegemea vitatupa furaha na ridhiko katika mioyo na maisha.
Kitu cha ajabu ni kwamba tunapofika na haya maboksi majumbani mwetu tukifungua ndani tunajikuta kuna vitu ambavyo hatukutegemea kabisa na mbaya zaidi hatuwezi kuyarudisha kule tumeyabeba.

Maisha ya mahusiano nayo wakati mwingine ni kama kubebeshana maboksi, mwenzako akijua wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa na kujuta kwa nini umeamua kuwa naye katika safari moja ya maisha kwani siku zote imekuwa ni wajibu wako kubeba maboksi yake ya hasira, ukari, manyanyaso ya kila aina, uchoyo, kiburi, ubishi, uchafu, ukatili, ubinafsi, na kila aina ya takataka ambazo zinaweza kukufanya uone maisha ya mahusiano na yeye hayana maana.

Je, hujakutana na watu ambao katika mahusiano yao mmoja huwajibika kumpendezesha mwenzake kumfanya awe na furaha au ajisikie vizuri huku yeye mwenyewe akiishi kwa hofu na mashaka na utumwa wa hali ya juu, anajitoa maisha yake zaidi ya binadamu kile anaweza huku akiongozwa na hofu na mashaka na woga wa hali ya juu, hana hata uwezo wa kujadili au kuongea na mwenzi wake kuhusu mwenendo wa mahusiano yao maana anaogopa kunaweza kuzuka mgogoro au zogo?

Na huyo anayefanyiwa wema wote hana shukurani ingawa anajua mwenzake anateseka, badala ya kuwa mapenzi umekuwa utumwa.

Kuna kitu kinaitwa “Narcissism” hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving).
Hili Neno linaendana na story ya kijana wa Kigiriki ambaye alivutiwa na taswira yake mwenyewe kwenye bwawa kiasi cha kushindwa kuondoka hadi akafia hapo.
Hili tatizo huanzia wakati mtu bado mtoto mdogo hasa baada ya Kukosa upendo na huruma, ukweli ni kwamba yeye mwenye hajipendi na matokeo yake hawezi kujua kumpenda mtu yeyote.

Utafiti unaonesha ni asilimia 75 ya wanaume ni narcissists.
Na Adolph Hitler alikuwa kinara wa hizi tabia ingawa huyu alikuwa hatari hata hivyo tunao akina Hitler wengi sana kwenye mahusiano yetu ya kila siku kama vile ndoa, uchumba nk na haijalishi ni mwanaume au mwanamke.

Hawa akina Hitler wanachofanya ni kukubebesha kibox cha wewe Kujiona una hatia, hofu, woga, mashaka, kutojiamini ili wakupelekesha wanavyotaka wao.
Hawa wanaweza kukudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na piawanaweza kuzira kuongea na wewe (silence) na wanachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zao.

Hata unapoishi nao unakuwa unaishi maisha ya mateso na kunyimwa uhuru.
Hii aina ya mahusiano ni hatari tupu na huhitaji msaada wa ushauri kwa wataalamu wa maswala ya ndoa na mahusiano.
Wengine ni watu wenye status kubwa katika jamii zetu anaweza kuwa manager, lecturer, tajiri, mbunge au waziri na hawa watu huonekana watu wa heshima kubwa sana mbele ya jamii kwani ni wapole, wema, watii, ni marafiki, wastaarabu, wamevaa ngozi ya kondoo huku ndani ni mbwa mwitu wakali hata hivyo katika maisha yao ya ndani na familia zao ni hatari kabisa (lethal)
Kama ni mume wako au mke wako ukifanya kosa moja tu yeye huona unastahili kupewa adhabu ambayo hutaisahau badala ya kusamehe na kusahau na kuendelea na maisha kwa raha na furaha.
Hawa wanaume au wanawake hufurahia sana kutesa wenzi wao hawana huruma hata chembe na hawafai katika mahusiano ingawa mbele ya jamii wanaonekana ni watu wazuri.

"Remember, you married her, you didn't hire her!"
Dr Phil

Friday, August 14, 2009

The Reverend Billy Graham and his wife Ruth When asked his secret of love,
being married fifty-four years to the same person,
he said,
"Ruth and I are happily incompatible."
Billy Graham

Kubadilika kwa stick!

Hakuna ubishi kwamba utendaji kimapenzi kwa mwanaume hupungua kufuatana umri unavyoongezeka.

Umri unavyoongezeaka hata kiwango cha homoni za testosterone hupungua na jinsi kiwango cha homoni kinavyopungua mwanaume huchukua muda mrefu kuweza kusisimka na baada ya kusisimka hutumia muda mrefu kusimamisha au kudindisha na si hivyo tu bali hutumia muda mrefu kufika kileleni na kubwa kuliko yote ni kwamba akisha fika kileleni huchukua muda mrefu zaidi kusimamisha tena ili kufika kileleni kwa mara nyingine.
Pia umri huweza kupunguza kiwango cha mbegu anazotoa pamoja na ubora wake.

Pia mwanaume anapozeeka huweza kupunguza uwezo wa utendaji wa kibofu chake cha mkojo, tafiti zinaonesha kwamba mrija wa mkojo huwa dhaifu kadri mwanaume anavyoongezeka umri pia misuli ya kibofu hupunguza uwezo.

Kubwa kuliko zote ni suala la mabadiliko ya uume kadri miaka inavyongezeka na kawaida huwa na mabadiiko makubwa mawili hii ni kwa mujibu wa madaktari wawili kwanza Profesa Ira Sharlip wa chuo kikuu cha California, San Francisco na wa pili ni Ronald Tamler, (MD, PhD), wa mpango wa huduma za afya kwa wanaume hospitali ya Mount Sinai New York City huko Marekani.

Mwonekano (Appearance)
Kichwa cha stick hubadilika rangi yake kutokana na kupungua kwa mtiririko wa damu kwenda huko south pole.

Pia nywele (pubic hair) huweza kuanza kupotea hii ni kutokana na homoni ya testosterone kupungua.
Kwa hiyo ukifika umri huo usishangae kuwa na massive deforestation au kuota kipara ukaanza kutafuta mchawi nani.

Kimo (size)
Kuongezeka uzito au kujazia eneo la kiuno au chini ya tumbo ni njambo la kawaida kwa mwanaume anapoongezeka umri kwa sababu mafuta (fat) hujaa maeneo ya chini ya tumbo (abdomen).
Kadri fat inavyojaa maeneo ya tumbo kwenda chini husabaisha shaft ya stick kujaza fat ambako husababisha urefu wa stick kupungua.

Pia mwanaume mwenye kitambi (obesity) huweza kuizika stick yake kwa fat inayokuwa deposited kwenye tumbo lake na anaweza kuongeza urefu wa stick hadi inch moja kama ataamua kupunguza uzito.

Kwa ufupi ni kwamba kama mwanaume mwenye miaka 30 huweza kusimamisha stick yake na kuwa na urefu wa inches 6 basi akifikisha miaka 60 au 70 stick yake inaweza kupungua na kuwa na uredu wa inches 5 ikisimama.

Thursday, August 13, 2009

When there is love in a marriage, there is harmony in the home;
When there is harmony in the home, there is contentment in the community;
When there is contentment in the community, there is prosperity in the nation;
When there is prosperity in the nation, there is peace in the world.
Chinese proverb

16 Words

In the beginning of our relationships, we send cards describing our love and send flowers when we are sorry.
Over time, not only do we forget to give our partners small gifts of affection, but sometimes, we forget to say how we feel.
There are sixteen essential words that we must make an effort to say to our loved ones every day or whenever appropriate.
These words are:-

I love you
I am sorry
I understand
You are beautiful
I need you
Thank you

Kulea kipaji cha Mtoto

Anaweza kuwa ni comedian wa kimataifa!SWALI
Hivi ukutaka kujua kipaji cha mwanao akiwa bado mdogo ni vigezo vipi utumie au nyenzo tunakuwa tunakosa kwa kujua hilo maana napenda kweli kujua karama za mwanangu akiwa bado mtoto ili nikuze pamoja nitampa elimu.

JIBU
Kipaji au talent ni uwezo wa aina ya pekee ambao mtu anakuwa nao hapa duniani. Kila mtu ameletwa duniani kufanya kitu fulani special kupitia talents alizonazo.
Hata hivyo kutokana na kushindwa kujua talents zetu tangu watoto, wengi huishia kufanya kazi ambazo hawazipendi katika maisha yao. Ambao wamejua talents zao wengi wanafurahia kazi zao na kuendelea kupata mafanikio makubwa.

Kazi ya mzazi ni kuhakikisha anamsaidia mtoto kumuwezesha kutambua kipaji chake kwani mtoto huwa anafika umri ambao lazima atoe maamuzi ya future yake hasa baada ya kumaliza kidato cha sita au umri wa kuanzia miaka 15.
Pia hii ina maana kwamba anapogundua mapema talents zake ndipo anafanikiwa mapema kuwa na maisha anayomridhika na kumfanya kupata mafanikio.

JE, NINI KINAHITAJI MZAZI KUJUA KIPAJI AU KARAMA ZA MTOTO?
Kwanza hakikisha unamuwekea mazingira ya kukutana au kuwa na vitu vingi iwezekanavyo ili kumuwezesha kuvumbua kitu ambacho atapenda kufanya kuliko vyote katika hivi vifuatavyo:-
Viti vinavyohusika na mahesabu kama vile cards, checkers, kuhesabu na kukokotoa Hesabu kwa kichwa.
Vitu vinavyohusiha yeye kujifunza lugha kama hii ni pamoja na yeye kujifunza kujua kujieleza mwenyewe, kuwashawishi wenzake na masimulizi ya hadithi tofauti
Vitu vinavyohusisha muziki kama vile vyombo vya muziki, kuimba na pia kwenda naye sehemu wanaimba au tamasha la muziki.

Vitu vinavyohusisha mazoezi ya mwili kama vile kuchezesha viungo, kucheza mpira, kuogelea, kuendesha baiskeli nk.
Kujifunza kuhusu mwengine ili aweze kujua jinsi ya kujjichanganya na wengine nk
Vitu vinavyohusisha mazingira kama vile mimea, wanyama na nature.
Baada ya hapo mtoto atajua nini kinakuja chenyewe naturally, kipi kinamfanya ajikisie vizuri na kuridhika.

MAMBO YA KUZINGATIA
Usimlazimishe kufanya kile wewe unataka afanye au awe unavyotaka wewe, kwani kumlazimisha mtoto kufanya kitu ambacho haridhiki nacho humzuia kugundua talents zake na hatimaye kuishia kuishi maisha ambayo hayampi ridhiko.
Uwe msaada wa kumtia moyo kile anafanya hata kama kwako hakina maana na mjengee kujiamini na kile anafanya.

MFANO:
Anaweza kuja na kukwambia “mama ona nimechora chura!” jitahidi kumpa credit kwa kazi kubwa aliyofanya hata kama huyo chura aliyechorwa anaonekana kama ni tembo, ukimtia moyo na kumsifia kesho anaweza kuchora vizuri zaidi na miaka 10 ijayo akawa ni cartoonist wa kimataifa.

Usiogope anapofanya kitu na kushindwa kama anakipenda jambo la msingi ni wewe kuhakikisha unamtia moyo ajiamini zaidi.
Usiwe critical na mtu mwenye kudharau vile anafanya kwani akiona anafanikiwa mwenyewe then atajitahidi kufanya zaidi.

DALILI MOJAWAWAPO KWAMBA MTOTO ANA KIPAJI NI KAMA HIZI
Kiongozi:
Anafurahia kuwa kiongozi wa wenzake (kuongoza) kuanzia kazi za shule hadi katika maongezi na wenzake, anataka watoto wenzake wafanye kile anafanya yeye. Pia anaweza kuwakusanya watoto wenzake kwa ajili ya kitu fulani. Pia watoto wenzake wanapenda sana kumfuta yeye.

Mfanyabiashara/business owner/ entrepreneur
Hapendi homework hadi kuwe na kitu kinachomfurahisha, ana mawazo mazuri jinsi shule zinavyoendeshwa na anaweza kuanza kuuza vitu kwa kwenzake ili kupata pesa na kukuuliza umtunzie fedha zake.

Genius:
Huvutiwa kufanya vitu ambavyow engine huona ni too complicated, wakati mwingine hata mzazi unaweza kununua kitu au toy kwa ajili yake ukawa hujui kinavyofanya kazi ile yeye akikabidhiwa anagundua kinavyotakiwa kufanya kazi, akiwa shuleni anajulikana kwa uwezo wake wa kupata majibu ya maswali magumu au mambo magumu.
Anaweza kuwa mvivu kusoma ingawa anajua kila kila wanachojifunza na anaweza kujifunza mwenyewe vitu vipya kiasi cha kuweza kurushwa darasa.

Pop star:
Ana nguvu nyingi na mbunifu, hawezi kukaa chini dakika moja na huonesha energy kila mahali kwani anajiona yupo huru na anaweza kufanya anachotaka. Anavyopenda nywele ziwe, anavyopamba chumba, anavyopeleka kazi zake kwa mwali shule huwa tofauti na akifikisha miaka 10 anauwezo wa kutoa wimbo kwenye album.

Mwana siasa na msherekeshaji:
Muda wote anaongelea habari za rafiki zake na walimu wake shule, anapenda sana kusoma vitabu na akisoma anapenda kukwambia kila kitu alichosoma, huwa na ufahamu mkubwa zaidi wenzake wa rika moja, anafurahia maongezi na watoto walio wakubwa kuliko yeye au hata watu wazima.
Mkiingia kwenye debate kuhusu kitu chochote lazima atashinda.

JE, NITAJUAJE MTOTO WANGU ANA KIPAJI MAALUMU?
Watoto wenye vipaji maalumu wapo tofauti kabisa na watoto wengine, na watoto wa aina hii huwa na tabia mojawapo ya hizi zifuatazo.
Hulala kwa muda mfupi sana tangu wachanga.
Wakiwa wachanga ukimlaza upande mmoja kwa muda mrefu huonesha dalili ya kutoridhika (annoyed)

Anaweza kuongea au kutembea zaidi ya kawaida ya watoto wengine.
Anaweza kuchelewa kuongea hata hivyo akianza huongea maneno na sentensi nzima nzima
Anakuwa na uwezo mkubwa wa kugundua vitu na kuyajua mazingira tofauti na watoto wa umri wake, atafungua kabati, au kuharibu vitu na kutaka kuvirtudisha kwenye hali yake ya kawaida
Anapenda kujua kila kitu kuhusu kila kitu, kila wazo, kila hali au tukio
Ukimnunulia toy anachezea hadi anachanachana kabisa

Anakuwa active kwa malengo siyo kuruka ruka tu ovyo.
Anaweza kujua kitu halisi na kitu ambacho si hali mapema sana.
Anajifunza haraka bila kurudirudia na kurudia kitu kilekile ni usumbufu.
Anakuwa na kumbukumbu kubwa sana ya topic tofauti na anaweza kukumbuka haraka
Anaweza kujieleza na uwezo wa kupata majibu kwa vitu vigumu kuliko watoto wa umri mmoja.
Hufurahia kujifunza vitu vipya, na huchoshwa sana na maelezo yanayojirudia
Ni rahisi kujua right and wrong.
Mambo anayofanya akiwa na miaka 6 huwa sawa na mtoto wa miaka 10 au 11

Wednesday, August 12, 2009

Ni lini?

Baada ya muda katika ndoa kila kitu kinaweza kuwa katika ratiba isiyobadirika, huwa vilevile, routine, predictable, uniform, sare jana juzi, leo na kesho maongezi ni yaleyale, ratiba ya kuwa mwili mmoja ni vilevile hakuna kipya na hakuna raha.

Inawezekana hawa wewe msomaji kile kinachotokea kwenye ndoa yako kinakupa wakati mgumu na unajiuliza hivi nitaishi bila kuridhika kiasi hiki hadi lini.

Hata hivyo kabla hujaanza kumlaumu partner wako ni vizuri ukajiuliza maswali yafuatayo huku ukitafakari kwa undani wewe mwenyewe bila kumnyoshea mwingine kidole

Hivi wakati mnachumbiana (let say dating) ni vitu gani ulikuwa unavifanya ili huyu partner wao aonekane yeye ni special kwako?

Je, hapa karibuni au wiki hii umefanya kitu gani kwa partner wako aonekane yeye ni special?

Je, unakumbuka ni kitu gani na lini mmekuwa pamoja na mmefanya kitu special na mkawa na wakati mzuri nje ya hapo nyumbani mnapoishi?

Je, ni mara ngapi mnakuwa wote kufanya kile kila mmoja anakifurahia kufanya?

Ukiulizwa utaje vitu vitano ambavyo partner wako anavipenda au anaviona vya maana sana katika maisha yake na kujisikia vizuri katika maisha unaweza kutaja? Na je umehusika vipi kuhakikisha anavipata?

Je, mume wako au mke wako yupo namba ngapi kwenye list yako ya vitu vya thamani duniani?
Haya maswali yakipata majibu yake inaweza kuwa njia sahihi kwako kuanza kutengeneza mahusiano yenye direction mpya kuelekea furaha na amani.
Najua mtu yeyote akikuuliza je, unampenda huyo partner wako jibu utakalo toa ni “ndiyo nampenda” hata hivyo ulivyo busy na kazi na watoto na kazi zingine ni dhahiri kwamba humpendi na kama unampenda basi hujaweka efforts zinazotakiwa.
Ni kweli hivyo vitu ni muhimu sana hata hivyo ndoa ni zaidi ya vyote, hata kama umekuwa unasema nitafanya hivyo karibuni hata hivyo karibuni yako sasa ni mwaka hakuna kitu.

Wakati uliokubalika ni sasa, sasa ni wakati wa kuwekeza kiasi cha kutosha kwa partner wako, na utatakiwa kurekebisha ratiba yako ili partner wako aingizwe kiuhakika katika ratiba yako ngumu.

Ukweli ni kwamba hata watoto hufurahia kuwa na wazazi wanaopendana kuliko wao kufurahia kuchezea gitaa linalotoa sauti nzuri au kufunga goli anapopelekwa na mzazi kucheza soka kuliko wazazi ambao hawapendani ndani ya nyumba.

Ndoa yako ni muhimu sana, na mke wako au mume wako ni muhimu sana kumbuka Mungu aliumba ndoa kabla ya kanisa, kabla ya kazi na kabla ya watoto.

"New love is the brightest and long love is the greatest, but revived love is the tenderest thing known on earth"
Thomas Hardy

Any fool can have a trophy wife.
It takes a real man to have a trophy marriage.
Diane Sollee,

Ni mtazamo wako tu!

Wengine hata katika giza nene la shida bado huwa na furaha!Moja ya tatizo la kawaida kwa ndoa za sasa ni mtazamo wa wanandoa kuamini kwamba ndoa yao haitafika popote au siku moja itashindikana au mmoja wa wanandoa kuwa na wazo kwamba siku moja ataondoka zake au wote kuwa na mtazamo kwamba siku moja nitaondoka na kuanza kivyangu upya.

Ukiwa na wazo la kushindwa ni hakika utashindwa vizuri sana kwani muda wote utakuwa unaangalia matatizo yote (negatives) ambayo yanakuwa alama kwamba sasa kushindikana kumeanza.
Yaani kwa kuwa una mawazo kwamba siku moja ndoa itashindwa basi akili yako hujipanga kusubiri dalili za kushindikana hata wewe mwenyewe kujua.

Wapo wanandoa wanaweza kusimama juu ya paa na kukiri kwamba ndoa zao ni za furaha hata hivyo ukichunguza kwa makini siri ya furaha yao si kwa sababu hawakutani na matatizo au shida au mambo magumu bali ni kwa sababu ya mtazamo wao kwamba wao ni mke na mume hadi kifo kitakapowatenganisha na zaidi sana wanajua sanaa (art) ya kusuluhisha matatizo katika ndoa yao kwa kuanza na wao wenyewe kila mmoja kuamini kwamba anaweza kubadilika kwanza na kuleta mabadiliko na siyo kunyosheana vidole au kila mmoja kujiona yupo right all the time.

Inawezekana wewe unayesoma hapa sasa hivi ni mmoja ya wale ambao likitokea tatizo nyumbani na mumeo/mkeo basi ni kununa tu eti kwa kuwa siku moja utaondoka zako! Au kwa sababu una mipango yako kabambe na murua kabisa ya kumuacha mwenzio kwenye mataa hata hujafikiria watoto na huo uamuzi wako ambao ni kujifaraji tu kwani kuondoka si jibu la mambo yote bali ni njia nzuri ya kwenda kuanza kukutana na tatizo jipya na kubwa zaidi.

Kwani wewe ndo mtu wa kwanza kukutana na tatizo kama hilo kwenye ndoa?
Si kweli, badala ya kuchangamka na kupenda kwa moyo wako wote wewe unafikiria kuondoka au kudhani sasa mwisho wa ndoa umefika.

Eti oooh tupo tofauti sana hatuwezi kuishi pamoja tena! Kwani ni nini kilikuvutia hadi ukakubali kuoana naye? Ulilogwa? Eti siku hizi simpendi kabisa! Lini umeanza kutompenda? Si umeamua mwenyewe kutompenda kwani love is a choice, wewe mwenyewe umeamua kutompenda na kweli humpendi ukichagua kumpenda utampenda.

Eti mke wangu ni mchafu sana! Unataka kumuacha kwa sababu ni mchafu? Mbona wakati wa uchumba alikuwa mchafu na ulikuwa una ignore! Nani mchafu kama si wewe uliyechumbia mwanamke mchafu, leo badala ya kutunza kilicho chako king’ae unataka kukimbia?

Unapoingia kwenye ndoa huku ukiwa na ufahamu au mtazamo kwamba ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha hapo tayari umepiga hatua kubwa sana na mbali kukuhakikishia ndoa yako inadumu na kuwa ya furaha kwa sababu unakuwa tayari kukubali kurekebisha kila tofauti zinazojitokeza kwani unajua huyu ni mwenzi wangu na kuna umuhimu wa kuishi kwa furaha kila wakati.

Ukiingia kwenye ndoa huku unategemea kushindwa ni kweli utashindwa vizuri sana na ukitegemea kufanikiwa na kuwa na ndoa ya furaha ni kweli utakuwa na furaha na zaidi utajifunza njia ya kuwa na furaha na utakuwa moja ya wanandoa wenye furaha duniani.

Quote:
“If you treat the wrong person like the right person, you could well end upthinking you have married the right person after all.
On the other hand, if you marry the right person, and treat that person wrong, you certainly will have endedup thinking you have married the wrong person”
Zig Ziglar

Tuesday, August 11, 2009

Ni wewe kwanza!

Wakati mwingine hata ndoa ambazo huonekana nzuri huweza kushindwa na zile zinazoonekana mbaya hudumu.

Zipo ndoa ambazo wawili huishi kwa mipaka hadi unashangaa sasa kwa nini inaitwa ndoa, kwa mfano mume au mke anatakiwa kuongea kwa mahesabu kwani akikosea neno anaweza kumkasirisha mwenzake na nyumba ikawa haikaliki na hakuna ladha kabisa kuongea na partner wake matokeo yake hata wakiwa wawili hakuna cha maana cha kuongea na kila mmoja hujibakia bubu kwani hujiona ni bora kuwa bubu kuliko ukaongea na ukawasha moto usioweza kuuzima.

Na mwingine hataniwi hata akifika nyumbani kutoka kazini si mama si mume au watoto wanajua kwamba baba amerudi au mama amerudi kila kitu sasa ni moto.
Swali la kujiuliza je, kwa nini uwe hivyo na unapata faida gani kuwa hivyo? kwa nini familia iwe na nyoka mtu?
Pia wapo wanandoa ambao huwa hawakubali kushindwa hasa pale kukiwa na tofauti ya mawazo au kutoelewana kati yako.
Kila siku wewe ndiye upo sahihi na kila siku mwenzako ndiye anakosea, haiwezekani binadamu wawili wakaishi pamoja na kila siku mara zote mmoja ndo anayekosea, huo si ustaarabu na ni ubabe tu.

"Ijulikane kwamba ndoa hurekebishwa kwa kuanza na wanandoa wenyewe, wanaweza kwenda kwa wazazi au marafiki au majirani au mchungaji, au padre au washauri maarufu wa ndoa au mtu yeyote mwenye utaalamu wa kushauri masuala ya ndoa, kama wanandoa wenyewe hawataki kujirekebisha na kuweka mambo sawa tangu chumbani mwao, mawazo au ushauri wa wengine hauwezi kupenya kwenye maisha yao ya ndoa na kuleta mabadiliko".

Nothing can penetrate in any marital problem when partners do not choose to change.

Umri na kukomaa

Kuna usemi kwamba wanawake hukomaa mapema kuliko wanaume hata kama wana umri unaofanana.
Binti wa miaka 17 anaweza kufanya mambo kama mtu mzima (adult) wakati kijana wa kiume wa miaka 17 anaweza kuwa bado anacheza na kuonekana mtoto (ingawa siyo wote)

Je ni kweli wanawake hukomaa (pevuka, iva) haraka kuliko wanaume?

Kuna tofauti kubwa kati ya umri na kukomaa.
Wakati umri ni miaka ambayo mtu anakuwa ameishi kwenye sayari ya dunia tangu azaliwe, kukomaa huonesha upo umbali kiasi gani katika kufikiria na mtazamo wa maisha.

Kukomaa huhusisha (tukuko) emotions, hisia (feelings), saikolojia na kiroho, wakati umri ni kitu ambacho ni umbo la nje.Baadhi ya tafiti zinaeleza sababu zinazofanya wanawake kukomaa haraka kuwa ni malezi jamii inawapa wanawake ambayo huwafanya kuwa wawajibikaji mapema katika jamii kuliko wanaume.

Kwa asili wanaume ni viumbe ambao huwa na hitaji la kutunzwa (nurtured) matokeo yake muda mwingi huhitaji mtu wa kuwalea na kuwatunza, hii ni namna ambayo vitu vipo na vipo hivyo ili kufanya balance.
Ukweli ni kwamba tofauti zilizopo baina ya mwanamke na mwanaume ndizo huwafanya kuwa na partner mzuri.
Kwa mfano mwanamke amefundishwa kulea na mwanaume amefundishwa kulelewa kitendo cha kuishi pamoja huwafanya kila mmoja kutimiza hitaji la mwenzake.

Ndiyo maana kwa asili mwanamke hujikuta akiwa anavutiwa (attracted) na mwanaume ambaye umri wake upo juu kuliko yeye, hii humpa mwanamke hisia kwamba mwanaume ambaye wapo umri unaofanana anaweza kuwa hajakomaa( kiakili na kimawazo) kama yeye na matokeo yake huvutiwa na mwanaume mwenye umri mkubwa ili kuleta mlingano katika hisia na mahitaji ya kimaisha.
Ndiyo maana wanawake wengi (siyo wote) wamejikuta wakiolewa na wanaume ambao umri wao ni mkuwa kuliko wanawake wenyewe.

Pia ieleweke kwamba kukomaa ni tofauti na umri kwa sababu kukomaa wakati mwingine ni kutokana na matokeo ya kushinda shida, majaribu, matatizo, mikasa na misukosuko ambayo mtu anapitia katika maisha na jinsi anavyokabiliana uso kwa uso na kushinda au kupata jawabu hata kwa machozi au kudhaurliwa au kuchekwa au kukataliwa au kufukuzwa na kupuuzwa.

Hizi shida na matatizo au majaribu au kupitia mambo magumu ni ni mwalimu mzuri anayeweza kumfanya binadamu yeyote kuwa strong na mkomavu.

Monday, August 10, 2009

Injini Haina Mafuta!

Injini inahitaji mafuta kufanya kazi vizuriSwali:
Mimi na mume wangu wote ni wakristo wazuri kabisa, napenda sana maombi na nina hamu sana sisi kama mume na mke kuomba hata kwa dakika 5 pamoja kwa ajili ya kuombeana sisi wenyewe au watoto na kujiweka tayari kuwa mwili mmoja usiku kabla ya kulala.
Kwa sasa nimekuwa na shauku kubwa sana kuomba pamoja na mume wangu na kitendo cha mume wangu kukataa au kukosa muda wa kuomba na mimi nimeona inaniathiri kiroho, kiakili, kihisia na kimapenzi pia hujiona sina support.

Wakati huohuo mume wangu anapenda sana sex na anapenda tuwe na sex angalau mara 3 kwa wiki, wakati mwingine ananivamia tu usiku wa manane apate sex na inakuwa ngumu kwangu kukubali kwani injini yangu inakuwa haina mafuta (not connected sexually)

Kitendo hiki huumiza sana hisia zangu na zaidi hunifanya kukosa uzingizi the rest of the night ingawa mwenzangu bada ya kujipendelea (sex) hulala fofofo kama yupo ICU.
Na siku inayofuata huwa nakuwa nimechoka, nimeumizwa hisia na sina nguvu tena.
Nimekuwa namwambia ni kweli tendo la ndoa (sex) ni muhimu sana ktk ndoa, hata hivyo kwangu kuomba pamoja kabla ya tendo la ndoa ni muhimu ziadi kuliko tendo lenyewe.

Hiki kitu kimekuwa ni kidonda na kinaniumiza sana je, nifanyeje?

Majibu:
Ukweli swali lako si swali jipya kuulizwa, wanawake wengi hujisikia kutolindwa au wanaume hawawajali na wanawake wengi hukasirika sana suala la kukosa ukaribu wa kihisia (emotional intimacy) ambao huonekana kama ni hitaji kubwa la kimapenzi kutoka kwa waume zao.

Pamojna na kuwa maombi ni njia inayotufanya kuwasiliana na uwezo uliojuu (Mungu) pia maombi ni moja ya njia muhimu sana ya kuwaunganisha mke na mume kuwa na muunganiko wa hisia kiroho ambao hupelekea kuwa na muunganiko unaoshangza wa kimapenzi kimwili.

Mwanandoa yeyote ambaye ameokoka anajua hii ni secret weapon kwa kujihakikishia kunakuwa na connection ya kiroho na kimwili wa wanandoa ili kuwa na faragha.

Hata hivyo kwa upande wa mume wako inawezekana hajui kwamba anakuumiza na kuchukua faida ya kujipendelea kwa kuacha kutimiza hitaji lako la maombi kwanza ili kuwa na wakati mzuri wa kuwa mwili mmoja. Na inawezekana anashangaa sana why hupendi tendo zuri ambayo ni haki yako katika ndoa.

Ukweli ni kwamba mwanaume na mwanamke ni tofauti katika mwitikio wa mapenzi na tunatakiwa kuzikubali hizo tofauti na kila upande kufanya kile kinatakiwa ama sivyo mahusiano yetu yanaweza kuzolewa na kimbunga na kujikuta ndani ya shimo ambalo kutoka ni ndoto.
Kama wanaume tutafahamu na kuwa na maalifa ya kutosha kujua jinsi mwanamke alivyoumbwa na jinsi mwili wake pamoja na hisia zake vinavyofanya kazi basi tunaweza kumsikiliza na kufanya sawa na wanavyohitaji.

Wanaume hatuhitaji kujiona tunaadhibiwa kwa wake zetu kuhitaji kutimiziwa mahitaji ya kihisia kwanza kabla ya kuwa mwili mmoja.
Wanaume tunahitaji kufahamu kwamba mke huweza kutoa response kubwa na kwa kufurahia pale tu mahusiano yanapkuwa yanapata kile yanastahili yaani kumuandaa mke kimapenzi kwa kufanya connection kihisia kwanza (najua kwa baadhi ya wanaume huu ni utumwa usiokubalika hata hivyo tumekubali kuwapenda wake zetu zaidi ya tunavyojipenda wenyewe, yaani kama Kristo alivyolipenda kanisa – sacrificial love)

Mke anatakiwa kufahamu kwamba mume hawezi kusoma mawazo yake hadi aambiwe kwa kukaa pamoja tena kwa hekima na upendo au lugha ya upendo siyo kuwa critical.
Kuna usemi kwamba “men can read newspaper not minds” hivyo usithubutu kukaa kimya eti atajua au alitakiwa kujua.

Pia wanaume tunahitaji kukumbushwa kwamba mke unahitaji emotional intimacy (injini kujazwa mafuta) over and over and over.

Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo
(Ephesians 5: 21)

Sunday, August 9, 2009

Hamu inatofautiana!

Kama una hamu basi msaidie kazi!Katika mahusiano mengi mmoja ya wanandoa huwa na hamu (drive) ya sex na kutaka sex mara nyingi zaidi kuliko mwenzake kwa sababu binadamu tunatofautiana levels za drive ya sex.

Kama wewe na mwenzi wako mna kiwango kinachofanana cha kuhitaji sex basi ninyi mmebarikiwa na you are luck ones.

Ukweli ni kwamba suala la sex (sexuality) ni moja ya eneo ambalo ni tete sana katika ndoa, ndiyo maana kukataliwa sex na mwenzi wako huwa ni jambo linaloumiza sana (hasa wanaume) ingawa wapo wanawake wana drive kubwa ya sex kuliko mwanaume ambaye siku zote anaonekana anahitaji sex 24/7.

Hata hivyo kuna sababu za msingi za kibaolojia zinazopelekea mmoja wa wanandoa kuhitaji sex zaidi ya mwenzake.

Nini husababisha hamu ya sex?
Hamu ya kutaka sex husababishwa na homoni ambayo kitaalamu huitwa testosterone.
Wote wanaume na wanawake wanayo hii homoni kwenye miili yao.
Wanaume wanayo nyingi zaidi kuliko wanawake kwa sababu wanawake wanayo homoni nyingine inayojulikana kama estrogen.

Msingi ni kwamba kiwango cha testosterone ulichonacho mwilini huweza kuelezea ni kiasi gani au hamu ya sex itakuwaje.
Ukiwa na kiwango kikubwa unakuwa na sex drive kubwa na ukiwa na kiwango kidogo unakuwa na sex drive ndogo.

Mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanaume wana kiwango kikubwa sana cha testosterone na hii husababisha wao kuwa na hitaji kubwa la sex (stronge sex desire).
Moja ya tatu ya wanaume wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na low sex drive.

Kwa upande mwingine mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanawake wote wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na kiwango cha kawaida cha drive ya sex na moja ya tatu (theluthi moja) tu ndiyo wenye kiwango kikubwa cha testosterone na hawa huwa na sex drive kubwa.

Hii ina maana kwamba mbili ya tatu ya wanaume wenye strong sex drive huishia kuishi (kuoana) na wanawake ambao wana sex drive kidogo na wapo wanaume hujikuta wapo ndani ya nyumba na wanaume (theluthi moja) ambayo sex drive ni ndogo sana.

Je, ni homoni peke yake husababisha kutokuwa na hamu ya sex?
Siyo homoni peke yake ndiyo inayosababisha mwanamke au mwanamke kuwa na sex drive ndogo kuna vitu vingine vingi huweza kufanya sex drive kuwa ndogo kama vile kuchoka na kazi, kulea mtoto, migogoro katika ndoa, nk.

Pia ni jambo la msingi kutambua kwamba kwa mwanamke suala la maisha huchukuliwa kwa pamoja kwa maana kwamba yupo connected na kila eneo la maisha yake kama vile familia, kazi, sex nk.

Kama mwanamke amekuwa na siku mbaya kazini au amekuwa na wakati mgumu na watoto wake ni ngumu sana kujisikia ana hamu na sex.

Wanawake huhitaji muda wa kuondoa masumbufu au kusafisha mawazo yao kabla ya kujihusisha na sex na hii hufanywa na mwanaume ambaye kwake ni mtu wa karibu.
Mwanamke huhitaji kuwa connected na mume kabla hajawa tayari kujiingiza kwenye masuala ya kuwa mwili mmoja.

Saturday, August 8, 2009

Wana hamu hawa!

Kuna gari mwanaume analijua ambalo hata usiku wa manane akikumbuka anapenda kuliendesha!Hivi kwa nini wanaume huwa hawahangaikii upendo (romance) kama wanawake?

Jibu limelalia zaidi kutokana na walivyoumbwa wiring yao ipo tofauti.
Wanawake huanzia kwenye romance, mawasiliano mazuri na hatimaye sex (spiritual to physical) wakati wanaume husafiri kwa opposite direction (physical to spiritual)

Ukichunguza kwa undani zaidi utagundua kwamba mwanaume anapokuwa na uhitaji mkubwa au hamu kubwa ya sex huwa anakuwa anataka kujiunghanisha emotionally na mwanamke, ndiyo maana kwa mwanaume sex ni mhimu sana wakati kwa mwanamke romance ni muhimu sana.

Kuwa na uelewa mdogo kuhusu hii tofauti hufika mahali wanawake waka –underestimate umuhimu wa sex kwa mwanaume na wakati mwingine wamewahukumu kwamba mwanaume anachotaka ni kitu kimoja tu nacho ni sex.

Hata hivyo mwanaume kusisimka kimapenzi na kuhitaji sex ni njia ya kujiunganisha na mwanamke kihisia na ili ajifahamu kihisia kwamba anakupenda.
Ni kupitia sex moyo wa mwanaume hufunguka na kumruhusu kupata hisia za upendo (love) kwa mke wake.

Ni kupitia sex mwanaume hupata feeling za kupenda ingawa kwa mwanamke sex huja baada ya kutoa na kupokea upendo (romance)
Wanawake huhitaji mawasiliano mazuri na kujisikia wanapendwa ili kufungua moyo kwa ajili ya sex wakati huohuo mwanaume huguswa na upendo wa mwanamke kupitia sex.
Kama mwanamke anavyohitaji mawasiliano mazuri na mwanaume (partner) ili ajisikia anapendwa, mwanaume huhitaji sex ili ajisikie anapendwa.

Sex drive ya mwanaume mara nyingi si rahisi kuweza kuifanya iwe turned off, yupo designed kuwaza kuhusu sex na kuhitaji sex muda mwingi na ni mara chache sana mwanaume hujikuta amechoka au yupo stressed kuhitaji sex.

Hii haina maana kwamba mwanaume huwa anaoa ili kupata sex tu na haina maana pia kwamba anaoa ili asipate sex, Bali sex ni moja ya sababu muhimu za yeye kuoa na jambo la msingi ni kwake kuwa na mwanamke special ambaye yeye kama mwanaume atakuwa anapata hitaji lake la sex maisha yake yote.

Wanaume wengi (siyo wote) likija suala la sex ni 24/7!

Friday, August 7, 2009

Kuwasha na Kuzima!

Kama kuzima, kuwasha nako ni simple!Turn off kwa mke kutoka kwa mume:

Mwanaume ambaye hana ufahamu wa kimapenzi.
Hajui ni nini na wapi kipi kinapatikana na kinafanywa vipi.
Kwa mfano hajui kisimi nini, kipo wapi na kina manufaa gani na hana mpango wa kujua au kujifunza lolote kuhusu mapenzi.

Mume ambaye hana hamu ya kujifunza jinsi ya kumridhisha mke zaidi.
Kutokuwa na hamu (interest) ya kutaka kujua skills na mambo mapya inaweza kuwa ni turn off kwa mke kwani kila mwanamke ni tofauti na katika mapenzi (kuwa mwili mmoja) huwezi kukoma (stop) kujifunza haijalishi unajua kiasi gani bado kuwa vitu vingi sana vya kujifunza .

Mume ambaye ni mbinafsi kujipa raha yeye mwenyewe.
Kama unahitaji kujua maana ya tendo la ndoa linalowaridhisha wote basi jifunze kutangulia mwenzako na kumridhisha kwamba yeye (pleasing)

Mwanaume asiyeuliza hata swali wakiwa kitandani.
Mke huhitaji mume ambaye ni initiator anayejua kuutumia uwanja (mwili wa mke wake) na kuuliza anajisikiaje kila sehemu anayogusa au kukanyaga.

Mambo ambayo huwa ni turn on kwa mke kutoka kwa mume wake:

Mume ambaye amejaa ufahamu kuhusu mwili wa mkewe.
Kwa mfano mume ananua kisimi kipo wapi, kipoje, kina sifa gani, kina respond vipi, kinafanywa vipi kitoe raha na anajua ni namna gani mke atakuwa amepata raha anayohitaji kupitia hapo nk hapo ni kila kiungo ambacho mke anaweza kusisimka na kupata raha ya mwili kutoka kwa mume wake na kuridhika.

Mume ambaye focus kubwa ni kumpa raha mke na si kutimiza wajibu.
Hana haraka na kufanya na kumaliza na kutimiza wajibu bali ana mikono slow kiasi cha kufamfanya mke ajione ni mke anayeridhishwa na mume kuliko mwanamke yeyote duniani.
Ni mume ambaye mke akikumbuka jinsi wanavyofanya huko faragha basi kama mume amesafiri anaanza kutamani mume arudi haraka maana hakuna muda mzuri kwake duniani kama kuwa na mume faragha na kufaidiana.

Mume anayemfanya mke kujiona ni beautiful chumbani na nje ya chumbani.

Anampa sifa na kumfanya mke akione ni kweli ni mzuri na anapendeza chumbani na nje ya chumbani.

Mwanaume anayejali kuridhika au kutoridhika kwa mke katika sex.
Mwanamke yeyote hupenda kujua au kuona mume wake anakuwa completely involved kuhakikisha anampa raha ya kimahaba na mume anakuwa na mtazamo au anajitahidi kuongeza ujuzi ili kuhakikisha mke anapata raha zaidi kila wakiwa pamoja chumbani.
Siyo mwanaume ambaye haweza hata kujua hali ya zoezi zima la tendo la ndoa lipoje zuri, kawaida au wanaelekea kwenye cliff.
Anapenda mwanaume anayetaka kujua ni kitu gani kinampa raha live, siyo kuwa selfish na baada ya kumaliza mke anaendea kuugua na kujiona ametumiwa tu.

Mume anayemfanya mke kujiona yeye ni namba moja kwake kwa kila kitu.
Mke hapendi tu kujiona yeye ni factor kwa mume bali anapenda kuona ni very important factor kwa maisha ya mume wake.
Mke lazima ajisikia salama na huru katika kile anatenda katika ndoa na mume wake.
Mume anahitaji kuwa creative jinsi ya kufanya mke vipi ajisikia.
Ni kweli sex ni kitu kizuri sana (wonderful) na huweza kumpa raha mume na mke hata hivyo Mungu amempa mume uwezo wa kufanya kazi apate pesa hata aweze kumnunulia mke vitu vidogo vidogo kama massage oil ili wakiwa wawili wapeane raha katika miili yao.
HITIMISHO:
Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe.
Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.
1Wakorintho 7: 3-5