"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 10, 2009

Injini Haina Mafuta!

Injini inahitaji mafuta kufanya kazi vizuriSwali:
Mimi na mume wangu wote ni wakristo wazuri kabisa, napenda sana maombi na nina hamu sana sisi kama mume na mke kuomba hata kwa dakika 5 pamoja kwa ajili ya kuombeana sisi wenyewe au watoto na kujiweka tayari kuwa mwili mmoja usiku kabla ya kulala.
Kwa sasa nimekuwa na shauku kubwa sana kuomba pamoja na mume wangu na kitendo cha mume wangu kukataa au kukosa muda wa kuomba na mimi nimeona inaniathiri kiroho, kiakili, kihisia na kimapenzi pia hujiona sina support.

Wakati huohuo mume wangu anapenda sana sex na anapenda tuwe na sex angalau mara 3 kwa wiki, wakati mwingine ananivamia tu usiku wa manane apate sex na inakuwa ngumu kwangu kukubali kwani injini yangu inakuwa haina mafuta (not connected sexually)

Kitendo hiki huumiza sana hisia zangu na zaidi hunifanya kukosa uzingizi the rest of the night ingawa mwenzangu bada ya kujipendelea (sex) hulala fofofo kama yupo ICU.
Na siku inayofuata huwa nakuwa nimechoka, nimeumizwa hisia na sina nguvu tena.
Nimekuwa namwambia ni kweli tendo la ndoa (sex) ni muhimu sana ktk ndoa, hata hivyo kwangu kuomba pamoja kabla ya tendo la ndoa ni muhimu ziadi kuliko tendo lenyewe.

Hiki kitu kimekuwa ni kidonda na kinaniumiza sana je, nifanyeje?

Majibu:
Ukweli swali lako si swali jipya kuulizwa, wanawake wengi hujisikia kutolindwa au wanaume hawawajali na wanawake wengi hukasirika sana suala la kukosa ukaribu wa kihisia (emotional intimacy) ambao huonekana kama ni hitaji kubwa la kimapenzi kutoka kwa waume zao.

Pamojna na kuwa maombi ni njia inayotufanya kuwasiliana na uwezo uliojuu (Mungu) pia maombi ni moja ya njia muhimu sana ya kuwaunganisha mke na mume kuwa na muunganiko wa hisia kiroho ambao hupelekea kuwa na muunganiko unaoshangza wa kimapenzi kimwili.

Mwanandoa yeyote ambaye ameokoka anajua hii ni secret weapon kwa kujihakikishia kunakuwa na connection ya kiroho na kimwili wa wanandoa ili kuwa na faragha.

Hata hivyo kwa upande wa mume wako inawezekana hajui kwamba anakuumiza na kuchukua faida ya kujipendelea kwa kuacha kutimiza hitaji lako la maombi kwanza ili kuwa na wakati mzuri wa kuwa mwili mmoja. Na inawezekana anashangaa sana why hupendi tendo zuri ambayo ni haki yako katika ndoa.

Ukweli ni kwamba mwanaume na mwanamke ni tofauti katika mwitikio wa mapenzi na tunatakiwa kuzikubali hizo tofauti na kila upande kufanya kile kinatakiwa ama sivyo mahusiano yetu yanaweza kuzolewa na kimbunga na kujikuta ndani ya shimo ambalo kutoka ni ndoto.
Kama wanaume tutafahamu na kuwa na maalifa ya kutosha kujua jinsi mwanamke alivyoumbwa na jinsi mwili wake pamoja na hisia zake vinavyofanya kazi basi tunaweza kumsikiliza na kufanya sawa na wanavyohitaji.

Wanaume hatuhitaji kujiona tunaadhibiwa kwa wake zetu kuhitaji kutimiziwa mahitaji ya kihisia kwanza kabla ya kuwa mwili mmoja.
Wanaume tunahitaji kufahamu kwamba mke huweza kutoa response kubwa na kwa kufurahia pale tu mahusiano yanapkuwa yanapata kile yanastahili yaani kumuandaa mke kimapenzi kwa kufanya connection kihisia kwanza (najua kwa baadhi ya wanaume huu ni utumwa usiokubalika hata hivyo tumekubali kuwapenda wake zetu zaidi ya tunavyojipenda wenyewe, yaani kama Kristo alivyolipenda kanisa – sacrificial love)

Mke anatakiwa kufahamu kwamba mume hawezi kusoma mawazo yake hadi aambiwe kwa kukaa pamoja tena kwa hekima na upendo au lugha ya upendo siyo kuwa critical.
Kuna usemi kwamba “men can read newspaper not minds” hivyo usithubutu kukaa kimya eti atajua au alitakiwa kujua.

Pia wanaume tunahitaji kukumbushwa kwamba mke unahitaji emotional intimacy (injini kujazwa mafuta) over and over and over.

Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo
(Ephesians 5: 21)

3 comments:

Anonymous said...

Wanandoa wenzangu!
Ni kweli suala la wanandoa kuomba pamoja kabla ya kuwa mwili mmoja au maombi ya pamoja kama mke na mume ni jambo muhimu sana.
Baada ya kuolewa nilikuwa naamini tukiomba kwanza na mume wangu itanifanya nisifurahia sex hiyo ni kutokana na nilivyolelewa kwamba sex ni kitu kibaya (kumbe kwenye ndoa sex ni tendo takatifu na kitu kizuri nimejua sasa)
Hata hivyo kila mara mume wangu aliponishika mikono na kuomba pamoja tukiwa wawili chumbani ilinifanya kijisikia tupo karibu zaidi na tukiingiwa kwenye tendo takatifu la kuwa mwili mmoja nilikuwa najisikia raha tofauti na siku ambazo hakutuwa tunaomba pamoja kwanza.
Hivyo naamiini maombi ni Muhimu sana kwa ajili ya connection ya kimwili.

Mbarikiwe na Bwana

Anonymous said...

Hii mada muhimu sana!
Kuhusu suala la mume kuamka na kuhitaji sex usiku wa manane bila taarifa, ni kweli mbele ya jicho la kawaida inaonekana mume huwa haridhiki na sex inavyotakiwa ndiyo maana hulala na usiku akawa na maruweruwe na kusubiri mke alale usingizi then mke akiwa amelala fofofo hujiona hana jinsi na kuamua kujipendelea kitu ambacho wkangu mimi kama mwanammke ni kama amenibaka.
Hivyo kama wanandoa ni vizuri kuongea wazi na waume zetu kuhusu sex na kupanga iweje kwani ukiwa na watoto pamoja na kazi mtu unakuwa busy (mwanamke) na hapo ndipo wanaume zetu huanza kutuvamia kwani nao wana hormones ambazo after 72 hrs wanazidiwa.
Maoni yangu tu!

Anonymous said...

Kuwa na faragha kiroho kwa njia ya maombi ya pamoja kwa kushikana mikono, kukumbatiana au vinginevyo ni njia nzuri ambayo huweza kupelekea kuwa na ukaribu wa kuunganishwa emotionally mume na mke na hatimaye kuwa sex inayoridhisha.
Pia kama wanandoa tunaweza kusaidiana kujua nini mke anahitaji na nini mume anahitaji.
Ni hayo tu.
RM - Dar