"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 17, 2009

......Itakosa ladha!

Ukifanya haya ndoa itakosa ladha:
1. Kumzoea mwenzi wako kiasi kwamba huoni yupo special
2. Kukosa interest kwa kile mwenzi wako anajihusisha kufanya
3. Kuwa mlevi.
4. Kutoshughulikia ndugu wanapoingilia ndoa (in laws)
5. Kukosa muda kuwa na mwenzi wako hasa baada ya watoto kuzaliwa.

6. Kujisikia huna kitu common na mwenzako
7. Kukosa kula chakula pamoja angalau mara 3 kwa wiki.
8. Kukosa kulala pamoja
9. Kutojua matokeo ya kuvaa nguo nzuri, usafi, kupendeza kwa mwonekano.
10. Kutosafiri pamoja hasa safari za ghafla na dhalula kwa lengo la kuwa wawili tu.

11. Kuishi pamoja kwa sababu ya watoto tu, na si upendo wa kweli.
12. Kushindwa Kukukubaliana kutokubaliana.
13. Kushindwa kujitunza mwenyewe kimwili, kiroho na kijamii.
14. Kushindwa kuchunga afya yako.
15. Kutumia muda mwingi na jamii badala ya mwenzi wako na familia yako.

16. Kushindwa kuwa na muda wa kuburudika pamoja.
17. Kutokuwa na interest zinazofanana.
18. Kutokubaliana katika pesa.
19. Kutotumia angalau saa moja kwa wiki wewe tu na mwenzi wako kuongea pamoja.
20. Kushindwa kujadili vitu unavyopenda au kutopenda likija suala la mapenzi.

21. Kushindwa kushikana mikono au kukumbatiana huku kila mmoja akiongea na mwenzake au kupeana ndoto za maisha.
22. Kuwa mwema zaidi kwa walio nje ya familia wakati suala hilo hilo unashindwa kufanya ndani ya familia au kwa mwenzi wako.
23. Kukosa kubusu asubuhi unapoondoka kwenda kazini au Unaporudi kutoka kazini.
24. Kukosa kufarijiana.
25. Kushindwa kuuteka moyo wa mwenzi wako.

26. Kufikiri na kuamini kwamba mwenzi wako kila siku yeye tu ndiye anakosea
27. Kukosa tendo la ndoa kwa siku 21 wakati mnaishi pamoja na kulala nyumba moja na hakuna tatizo la kimatibabu.
28. Kuwa na hisia kwamba mwenzi wako ni adui yako na humpendi.
29. Kukosa muda wa kucheka pamoja na mwenzi wako.
30. Kushindwa kwenda kanisani pamoja
31. Kutokujali kuongelea moja ya hayo hapo juu kuonesha kwamba unataka mabadiliko.

2 comments:

Anonymous said...

Habari!

Umenena yaliyo kweli na tutayafanyia kazi.
Ila na mimi naongeza:
-kushukuru endapo umekula chakula alichopika mkeo

-kusali pamoja faragha japo mara moja kwa wiki hasa saa 8 usiku.

halafu kaka Mbilinyi naomba kuuliza ulishawahi kuongelea swala la tendo la ndoa kuwa uhitaji unatofautiana sasa kama mmoja kati yetu kaumbwa hivo kuwa hamu ya tendo la ndoa lipo mbali anaweza kubalika au utambadilishaje huyo?

mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Hongera sana kwa kuongeza mengine na inapendeza sana.

Kuhusu kutofautiana hamu ya tendo la ndoa kati ya wanandoa ni kweli hili suala la gumu kidogo.
mwanaume kawaida ndiye yupo focused kwenye sex hadi wakati mwingine mke hudhani anatumiwa tu. Na mwanamke yupo focused kwenye upendo na romance hadi mume hushangaa vipi mbona mwenzangu hataki sex.
Kubwa zaidi ni pale mke anakuwa na hamu kubwa ya sex kuliko mume na hiyo huenda mbali zaidi kwani mke hudhani havutii, au ana kasoro na nk.
Ukwei tunatofautiana katika hamu ya sex kati ya mke na mume na kama ukiona wewe na mume au mke wako mambo ni sawa basi mmebarikiwa sana otherwise kwa wengine inabidi kila mmoja kujitahidi kumtanguliza mwenzake bila kunyimana. Kwani mwanaume huweza kuwa attracted kwa mke kupitia sex kihisia na mke huvutiwa kwa upendo wa mume kihisia hivyo kila mmoja ajue nafasi yake na kumpa mwenzake kile anahitaji, si kweli kwamba wanaume tunapenda sex tu bila upendo wa wake zetu ila ndivyo tumeumbwa na kwa sex tunajiona tupo karibu zaidi emotinally na mke na muhimu kwetu ni kuwapa upendo ili mfunguke katika hisia za mapenzi nk.

Tutajadili zaidi!

Ubarikiwe

Upendo daima