"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 13, 2009

Kulea kipaji cha Mtoto

Anaweza kuwa ni comedian wa kimataifa!SWALI
Hivi ukutaka kujua kipaji cha mwanao akiwa bado mdogo ni vigezo vipi utumie au nyenzo tunakuwa tunakosa kwa kujua hilo maana napenda kweli kujua karama za mwanangu akiwa bado mtoto ili nikuze pamoja nitampa elimu.

JIBU
Kipaji au talent ni uwezo wa aina ya pekee ambao mtu anakuwa nao hapa duniani. Kila mtu ameletwa duniani kufanya kitu fulani special kupitia talents alizonazo.
Hata hivyo kutokana na kushindwa kujua talents zetu tangu watoto, wengi huishia kufanya kazi ambazo hawazipendi katika maisha yao. Ambao wamejua talents zao wengi wanafurahia kazi zao na kuendelea kupata mafanikio makubwa.

Kazi ya mzazi ni kuhakikisha anamsaidia mtoto kumuwezesha kutambua kipaji chake kwani mtoto huwa anafika umri ambao lazima atoe maamuzi ya future yake hasa baada ya kumaliza kidato cha sita au umri wa kuanzia miaka 15.
Pia hii ina maana kwamba anapogundua mapema talents zake ndipo anafanikiwa mapema kuwa na maisha anayomridhika na kumfanya kupata mafanikio.

JE, NINI KINAHITAJI MZAZI KUJUA KIPAJI AU KARAMA ZA MTOTO?
Kwanza hakikisha unamuwekea mazingira ya kukutana au kuwa na vitu vingi iwezekanavyo ili kumuwezesha kuvumbua kitu ambacho atapenda kufanya kuliko vyote katika hivi vifuatavyo:-
Viti vinavyohusika na mahesabu kama vile cards, checkers, kuhesabu na kukokotoa Hesabu kwa kichwa.
Vitu vinavyohusiha yeye kujifunza lugha kama hii ni pamoja na yeye kujifunza kujua kujieleza mwenyewe, kuwashawishi wenzake na masimulizi ya hadithi tofauti
Vitu vinavyohusisha muziki kama vile vyombo vya muziki, kuimba na pia kwenda naye sehemu wanaimba au tamasha la muziki.

Vitu vinavyohusisha mazoezi ya mwili kama vile kuchezesha viungo, kucheza mpira, kuogelea, kuendesha baiskeli nk.
Kujifunza kuhusu mwengine ili aweze kujua jinsi ya kujjichanganya na wengine nk
Vitu vinavyohusisha mazingira kama vile mimea, wanyama na nature.
Baada ya hapo mtoto atajua nini kinakuja chenyewe naturally, kipi kinamfanya ajikisie vizuri na kuridhika.

MAMBO YA KUZINGATIA
Usimlazimishe kufanya kile wewe unataka afanye au awe unavyotaka wewe, kwani kumlazimisha mtoto kufanya kitu ambacho haridhiki nacho humzuia kugundua talents zake na hatimaye kuishia kuishi maisha ambayo hayampi ridhiko.
Uwe msaada wa kumtia moyo kile anafanya hata kama kwako hakina maana na mjengee kujiamini na kile anafanya.

MFANO:
Anaweza kuja na kukwambia “mama ona nimechora chura!” jitahidi kumpa credit kwa kazi kubwa aliyofanya hata kama huyo chura aliyechorwa anaonekana kama ni tembo, ukimtia moyo na kumsifia kesho anaweza kuchora vizuri zaidi na miaka 10 ijayo akawa ni cartoonist wa kimataifa.

Usiogope anapofanya kitu na kushindwa kama anakipenda jambo la msingi ni wewe kuhakikisha unamtia moyo ajiamini zaidi.
Usiwe critical na mtu mwenye kudharau vile anafanya kwani akiona anafanikiwa mwenyewe then atajitahidi kufanya zaidi.

DALILI MOJAWAWAPO KWAMBA MTOTO ANA KIPAJI NI KAMA HIZI
Kiongozi:
Anafurahia kuwa kiongozi wa wenzake (kuongoza) kuanzia kazi za shule hadi katika maongezi na wenzake, anataka watoto wenzake wafanye kile anafanya yeye. Pia anaweza kuwakusanya watoto wenzake kwa ajili ya kitu fulani. Pia watoto wenzake wanapenda sana kumfuta yeye.

Mfanyabiashara/business owner/ entrepreneur
Hapendi homework hadi kuwe na kitu kinachomfurahisha, ana mawazo mazuri jinsi shule zinavyoendeshwa na anaweza kuanza kuuza vitu kwa kwenzake ili kupata pesa na kukuuliza umtunzie fedha zake.

Genius:
Huvutiwa kufanya vitu ambavyow engine huona ni too complicated, wakati mwingine hata mzazi unaweza kununua kitu au toy kwa ajili yake ukawa hujui kinavyofanya kazi ile yeye akikabidhiwa anagundua kinavyotakiwa kufanya kazi, akiwa shuleni anajulikana kwa uwezo wake wa kupata majibu ya maswali magumu au mambo magumu.
Anaweza kuwa mvivu kusoma ingawa anajua kila kila wanachojifunza na anaweza kujifunza mwenyewe vitu vipya kiasi cha kuweza kurushwa darasa.

Pop star:
Ana nguvu nyingi na mbunifu, hawezi kukaa chini dakika moja na huonesha energy kila mahali kwani anajiona yupo huru na anaweza kufanya anachotaka. Anavyopenda nywele ziwe, anavyopamba chumba, anavyopeleka kazi zake kwa mwali shule huwa tofauti na akifikisha miaka 10 anauwezo wa kutoa wimbo kwenye album.

Mwana siasa na msherekeshaji:
Muda wote anaongelea habari za rafiki zake na walimu wake shule, anapenda sana kusoma vitabu na akisoma anapenda kukwambia kila kitu alichosoma, huwa na ufahamu mkubwa zaidi wenzake wa rika moja, anafurahia maongezi na watoto walio wakubwa kuliko yeye au hata watu wazima.
Mkiingia kwenye debate kuhusu kitu chochote lazima atashinda.

JE, NITAJUAJE MTOTO WANGU ANA KIPAJI MAALUMU?
Watoto wenye vipaji maalumu wapo tofauti kabisa na watoto wengine, na watoto wa aina hii huwa na tabia mojawapo ya hizi zifuatazo.
Hulala kwa muda mfupi sana tangu wachanga.
Wakiwa wachanga ukimlaza upande mmoja kwa muda mrefu huonesha dalili ya kutoridhika (annoyed)

Anaweza kuongea au kutembea zaidi ya kawaida ya watoto wengine.
Anaweza kuchelewa kuongea hata hivyo akianza huongea maneno na sentensi nzima nzima
Anakuwa na uwezo mkubwa wa kugundua vitu na kuyajua mazingira tofauti na watoto wa umri wake, atafungua kabati, au kuharibu vitu na kutaka kuvirtudisha kwenye hali yake ya kawaida
Anapenda kujua kila kitu kuhusu kila kitu, kila wazo, kila hali au tukio
Ukimnunulia toy anachezea hadi anachanachana kabisa

Anakuwa active kwa malengo siyo kuruka ruka tu ovyo.
Anaweza kujua kitu halisi na kitu ambacho si hali mapema sana.
Anajifunza haraka bila kurudirudia na kurudia kitu kilekile ni usumbufu.
Anakuwa na kumbukumbu kubwa sana ya topic tofauti na anaweza kukumbuka haraka
Anaweza kujieleza na uwezo wa kupata majibu kwa vitu vigumu kuliko watoto wa umri mmoja.
Hufurahia kujifunza vitu vipya, na huchoshwa sana na maelezo yanayojirudia
Ni rahisi kujua right and wrong.
Mambo anayofanya akiwa na miaka 6 huwa sawa na mtoto wa miaka 10 au 11

5 comments:

Anonymous said...

Wow!
Leo kaka Mbilinyi umenifurahisha sana unajua nini jana nilivunjika moyo uliposema hutaifanya kwa sasa kazi hii niliokuomba ya kujua kipaji cha mwanangu.
Mungu azidi kukubariki jamani yaani asilimia 60 ulichoandika naviona kwa mwanangu 40 aliobaki natekeleza vile ulivoagiza asante sana coz nampenda sana mwanangu niliemsubiria miaka mingi iliopita na napenda akawe mtu fulani katika taifa letu.
Tunataka kulea mtoto katika njia impasayo!
Kumbuka yale mambo 16 bado hujamalizia.
Pole sana na shule, msalimie mama mzaa chema mwenzangu.

Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Nimefurahi sana na pia najisikia huru maana ahadi ni deni na ukikopa kumbuka kulipa, pia nimefurahi zaidi kwa kuwa unapenda kuhakikisha mwanao anajua telents zake mapema na hivyo kumwezesha kwenda direction inayotakiwa mapema na hatimaye kuwa na maisha ambayo anaishi kwa kufanya kazi anaipenda na anaifurahia na matokeo yake atakuwa very successfull kwa familia na taifa.

Kuhusu yale maneno 16 nakiri kwamba nilichanganya kidogo ila ukweli ni kwamba kuna maneno kumi na sita na si mambo kumi na sita so nitakupakulia hayo maneno kumi na sita ambayo yakiwa moyoni mwako na uwe unayaongea kila mara kwa mpenzi wako basi yatajenga kitu cha tofauti katika ndoa yako.

Pia nashukuru sana kwa maombi yako mitihani ilikuwa mizuri na salama

Ubarikiwe sana na bwana!

Upendo daima

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli "kulea kipaji cha mtoto" Na kupeni hongera. Maana naona Shangazi yangu hapo mambo si mabaya.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana dada Yasinta,

Ni kweli shangazi yako ni kiboko, najitahidi kumpa vitu na kumpeleka katika mazingira tofauti ili kujua nini talents zake hata hivyo hadi sasa nimeshajua kitu gani kinafaa na anakipenda na atapenda kufanya akiwa mkubwa.

Tuendeleze vipaji vya watoto wetu

Upendo daima!

fikirikwanza said...

Mie kwa ushauri wangu naona huyu anaonekana kuwa fundi mzuri wa viswiswi,na kwa coaching staff unaweza mwona mwang'ande!!
msalime fundi wangu!!
baba mdogo.