"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 18, 2009

Kutunza Moto chumbani! usirudie haya....

Kuwa na utaratibu uleule miaka nenda rudi.
Kwa kuwa unajua nini hufanyika ukiingia chumbani na mke/mume wako, hivyo unavua nguo zako na zake, unamvuta ( kwani anajua ukimvuta kwa mtindo huo nini unataka naye anakuacha uendelee, nawe unachukua kiungo A na kuiingiza kwenye kiungo B, unafanya kile unachokijua, baada ya dakika 5 zoezi limeisha, unageuka unalala, hoi folilo!
Unaonaje hapo?

Hapa haijalishi hili tendo ni tamu kiasi gani, nunaburudika kwa raha kiasi gani, unapiga kelele za raha kiasi gani, ni dhahiri ya miaka kadhaa hili zoezi litakuwa nadra sana kufanyika na ikifanyika lazima mmoja atajisikia it is boring.

Kuwa na utaratibu unaofanana kila siku kila mwezi na kila mwaka huhatarisha mahusiano ya kimapenzi kwa mke na mume.
Njia nzuri ya kulinda upendo na connection ya thamani kati ya mke na mume katika mapenzi ni kuwa na kitu kipya baada ya muda fulani hata kubadilisha mazingira tu acha skills.
Ukweli kukiwa na new tips na techniques mtafurahia sana kuwa mwili mmoja kwani mtakuwa hot, na mtahitajiana mara kwa mara na zaidi.

Kuogopa kuongelea au kujaribu vitu vipya wakati wa kuwa mwili mmmoja.
Je, umewahi kuwa na wazo zuri au jipya la kutaka kuongeza ladha mpya chumbani ukiwa na mke au mume wako na unashindwa uanze vipi au hujui mwenzi wako ata-respond vipi?
Au unaogopa atakuuliza ulijifunza wapi? Au akaenda mbali zaidi kwa kukuuliza nani amekufundisha?

Ukweli ni kwamba kuna asilimia 90 mpenzi wako atapenda kusikia na pia atashirikiana na wewe kujifunza hizo new skills muhimu tumia hekima na busara kuwakilisha mawazo yako na kila kitu kitakuwa shwari huko chumbani.
Pia ni dalili kwamba mnaogopana na zaid hampo wazi sana kuongea mambo yenu ya ndani ambayo ni muhimu na yanaweza kuwaweka karibu zaidi.
Jiamini na ongea kile unapenda kwa nini ujinyime raha?
Kalaghe bhaho!

Kujaribu kumlazimisha mume/mke wako tendo la ndoa.
Kama mke au mume amechoka au hana mood haina haja kuanza kumlazimisha afanye; for sure it will not work.
Wakati mke au mume anasisimka mwili humwaga kemikali za adrenaline ambazo husaidia kuupa mwili energy ya tendo zima la ndoa hivyo kama amechoka anaweza asisisimke vya kutosha na maana yake atakuwa hana nguvu za kujirusha sawasawa at the maximum ili kuleta matokeo mazuri.

Ikiwezekana kama wewe ni mwanamke na mume usiku amegoma kwa kwua amechoka (kwani huwezi kuisimamisha stick hadi ubongo wake uamue) usijali subiri hadi asubuhi kabla hajaamka kwani kiwango cha testosterone huwa juu kuliko wakati wote hivyo utamfaidi tu na hana ujanja stick itakuwa imesimama na ipo tayaritayari, usifanye kosa tumia busara.

Kama wewe ni mwanaume na mke anasema amechoka kitu cha kwanza ni kutengeneza mood yake ili awe katika hali ya kuwa relaxed, maneno matamu, ongea kile huwa anapenda kusikia, ni vizuri mwanaume kujua nini humfanya ajisikie kunyegeka na kuwa excited hata kama utatumia nusu saa kwani si una mission?
Tumia skills zako zote.
Itafika mahali atajieleza mwenyewe kwa jinsi unavyomwona ila ukishindwa kamwe usimlazimisha na pia usifanye kwa kuwa amesema yupo tayari ni muhimu kufahamu kwamba kukubali kwake ni ni sababu anapenda na siyo ili yaishe utaishia kuulizwa “hujamaliza?”

Kuacha au kukwepa/kuruka kipengele cha kuandaana kabla ya tendo la ndoa
Wanandoa wengi (hasa wanaume) hupenda kukwepa kumuandaa mke (foreplay) ili kuwahi kufaidi kitu chenyewe hata hivyo kumuandaa mke humpa faida hata mume mwenyewe.
Kwa kubusu, kumshikashika (touching) na mengine yote huweza kusababisha mke kujisikia ameridhika na atajisikia humtumii kwa tamaa zako.
Hivyo slow down, take time!
Lazima mwanaume uwe playful na usiwe na mikono mwepesi bali mikono slow.

Kutumia mikanda ya video za X kuimarisha utendajie wa mpenzi.
Wakati maisha ya ndoa yamefikia hali mbaya wapo wanandoa ambao huamua kutumia video (mikanda ya X) kujifunza wakidhania maisha yao ya mapenzi yanaweza kuwa kiwango cha juu kiasi cha kufika kwenye roof.

Ni kosa kubwa and it is Wrong! Dangerous.
Hawa akina XX video wapo ukoo mmoja na wale jamaa wa Sodoma na Gomora!

Kutumia outside source huweza haraka sana kuharibu kuliko kutengeneza au kusaidia.
Ndoa ni mke na Mume pamoja na Mungu mwenye kupokea utukufu unaotokana na uumbaji wake kwa hao wawili.
(Naamini kuna critics watasema hapa nimeongea upuuzi hata hivyo mtu wa rohoni atafahamu naongea kitu gani)

12 comments:

Anonymous said...

Bwana Yesu asifiwe kaka Lazarus,
naomba niende nje ya topic kabisa naomba msaada wako wa kimawazo kwan nawaza sipati jibu nahisi kama nachanganyikiwa, ni hivi mm niliolewa mwaka 2005,wakati huo nilikuwa ndo namaliza chuo na nilifahamiana na mume wangu kwa dada mmoja tulikuwa tunasoma nae chuo ila yy alikuwa ameshaolewa alikuwa kajifungua nikaenda kumpa pongezi na kumuona baby wake ndo nilipokutana na huyu mume wangu kumbe yeye mume wangu alikuwa ni rafiki wa mume wa huyu dada mwanachuo mwenzangu. aliponiona akanipenda haikuchukua hata miezi mitatu akawa ananisisitiza twende nyumban akajitambulishe then kweli akanioa, nilijitahidi kumuuliza kwa nn anataka tuoane haraka hivyo akasema yy anahitaj kuoa kwan anaona umri unamtupa mkono na nilikuwa na ham ya kuolewa nikaona bora niolewe ingawa simjui vizuri tabia huyu mwanaume lakini nilipojaribu kumuuliza yule dada mwanachuo mwenzangu kuhusu huyu mwanaume akawa anamsifia sana kuwa ni mtaratibu na hajawah kumuona anahangaika na wanawake kwan alishawah kushare na compaund kwenye nyumba moja aliyopanga na kwa vile ni rafiki wamume wake wote wakawa wanamsifia nikaamua bora tu nikubali tuoane yy alikuw ana umri kama wa miaka 35 mie 26. tukaoana tukaishi vizuri nikabahatika kupata mimba lakin bahati mbaya ikaharibika ndan ya miez 3, tumeishi vizuri na mume wangu lakini kuna kitu kilikuwa kinanipa waswas mume wangu alikuwa hataki nishike cm yake na hapendi pia akawa ananiambia sijiamini nikaamua kuacha.mwez wa 3 mwaka huu nikazibamba mesej kwenye cm ya mume wangu yaan roho imeniuma sana kugundua mume wangu ana mwanamke nje mbaya zaidi huyo msichana anae tembea nae nimekuja kugundua ni mdogo wake na yule dada aliyeniunganisha mm na mume wangu aliyekuwa mwanachuo mwenzangu, nimechanganyikiwa sijui nifanyaje kaka nikimuuliza mume wangu ananijibu vibaya sana nimejaribu kumkataza huyo msichana asiendelee na mume wangu wote wananijibu vibaya najuta kuolewa jaman nawaza mume wangu anahangaika nn lakini sijui kwa vile sina mtoto ndo anatafuta nje nimejaribu kuongea na huyo dada kumueleza jinsi mdogo wake anavyoniharibia ndoa nae ananijibu ujeuri mpaka nahisi kama vile yy ndo aliewaunganisha mume wangu na mdogo wake. ngoja nikuandikie baadhi ya msg ambazo mume wangu anatumiwa na huyo msichana UTANIKUMBATIA NIKIFIKA STEND? MIE NAOMBA TUKUMBATIANE CHUMBANI TUKIFIKA,HAPA NTAONA AIBU ISITOSHE NDO MARA YA KWANZA KUWA NA UHUSIANO KAMA HUU,hii msg huyu dada alikuwaanamtumia mume wangu alipokuwa morogoro kikazi lastweek. nyingine hii MM BINAFSI NIMEFURAHI SANA! NA JINSI UNAVYONIJALI ULIVYOKUJA SAME YAAN UNANIDHIHIRISHIA UPENDO WAKO KWANGU NI WADAIMA, NAMI SITOKUACHA,WW NIMUME WANGU SASA. hii msh ametuma huyo msichana kwenda kwa mume wangu jaman, naomba unisaidie japo kwa mawazo nifanye nn ningekuwa napafaham nyumban kwa huyo binti ningekwenda sipafaham ndoa imekuwa chungu pls nijibu leoleo sababu hata kazi nashindwa kufanya nataman hata kunywa sumu kaka EE MUNGU NISAIDIE

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana na Mungu akutie nguvu sana.

Hata hivyo haina haja kunywa sumu au kutaka kujiua kwa sababu ya message na mwenendo mzima wa cheating za mume wako.

Jambo la msingi umeshajua nini kinaendelea na hilo ndo jambo la msingi na upo hatua kubwa zaidi.

Usijaribu wala kuthubutu kunywa sumu au kujiua kuna matumaini baaada ya hayo na Mungu atafanya kitu cha tofauti katika ndoa yako.

Nitumie email kwa lazarusmbilinyi@gmail.com haraka sana kwani hapa tutaandika hapata tosha.

Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

Upendo daima

Anonymous said...

Am just a Tanzanian, a final year university student outside Tanzania its has been about four months been read your post,they are very nice and they give good advise to me and other people who read these post.
GOOD BLESS YOU,YOU AND YOUR WIFE AND YOUR CHILD.MAY GOD BE WITH YOU AND BE BLESSED.

Lazarus Mbilinyi said...

Thank you indeed!
God bless you too, you are welcome to share anything that can make a difference to others.

Love always

Anonymous said...

Kwanza nampa pole huyo dada,

Mambo ya ndoa ni kitu cha ajabu kwani ni tofauti kabisa na uhusiano wowote katika hii sura ya nchi, na ndio maana katika suala hili zima la kuoa au kuolewa si vizuri kushinikizwa na ndugu au marafiki kwani inapotokea issue kama hiyo mara nyingi tunaishia kuwalaumu wale waliotuhamasisha tuoane, suala zima la kuoa au kuolewa linatakiwa liwe ni uwamuzi wa mtu binafsi kwamba ni kweli namkubali na kumpenda huyo ambaye atakuwa mwenza wa maisha.

Ingawa mara nyingi sisi akina dada tunaishia kwenye kushauriwa na ndugu au marafiki katika suala la kupata mwenza, hasa pale dada unapoona kama vile umri umekwenda na kweli unataka mtu wa kukuoa, huwa tunakubali kwa haraka kile ambacho mwanaume anataka hata kama atasema anataka ndoa ndani ya mwezi mmoja, na katika mazingira kama haya inakuwa ngumu kufahamu hata vitu vichache kuhusu huyo atakayekuwa mume wako wa maisha kwa mfano kufahamu kwamba labda huyo bwana siyo mwaminifu, tapeli, ana hasira sana ila kwa sababu mimi kama binti ninachoangalia sana ni kutaka kuolewa na nina hamu ya kuolewa basi haya mengine tunakuwa hatuna muda sana wa kuyafuatilia au kuchunguza.

Mimi ningependa kumwomba huyo dada asichukue maamuzi ya haraka huku akiwa na hasira ni kweli anaweza kufanya kitu kibaya. Nadhani huu si wakati wa kuanza kumwangalia yule rafiki aliyemuunganishia maana huyo alishafanikisha kazi yake mpaka wakawa wanandoa, hapo sana ni yeye na huyo mume wake. Ingawa nafahamu ni ngumu kwetu wanawake kwa hatua aliyofikia mumuwe kwani sisi wanawake huwa tunaathirika sana kiasi kwamba nyingi unasikia mtu kajiua au ameamua kuachana na mume, lakini hakuna njia nyingine ya kuponya hiyo ndoa yake isipokuwa ni yeye na mume wake kuanza upya mazungumzo kwa yeye kuonyesha upendo, unyenyekevu na kuwa karibu na mume wake kuliko wakati wote wote.

Huu ndio wakati wako wa kuonyesha kumpenda mumeo kuliko wakati wowote ili uweze kuongea naye kuhusu huyo nyoka aliyevamia ndoa yako, na ukimuomba Mungu akupe hekima katika kuongea naye kwani kwa sasa najua hilo ni jeraha kubwa mno ndani ya moyo wako. Huna haja ya kumfuaata huyo rafiki yako kwa sasa njia sahihi ni wewe na mumeo kuanza mazungumzo ya amani.

Mungu akubariki na kukutia nguvu katika hatua unayoindea.

Nesige P.

Anonymous said...

shalom, dada muomba msaada, nimetingwa kidogo hapa ila kama unaweza niandikie email kwa ufupi kupitia grace.bennett11@yahoo.com kwa ushauri unahitaji darasa mpenzi wangu kama alivyosema kaka lazarus hapa.
Mungu akutie nguvu na kuponya ndoa yako ubarikiwe sana

MS GBENNETT

fikirikwanza said...

Pole dada yetu, lakini sumu hata usiiwaze, tatizo si kubwa kiasi cha kukosa matumaini kiasi hiki.
Kila jaribu linamlango wa kutokea.
Nafikiri kwanza ni wakati wa kumpenda huyo mume wake bila preconditions,strategie ya pili ni kuwa rafiki wa huyo dada anaye toka na mume wako na huyo dada aliyekuelekeza kwa huyo jamaa na mpende bila preconditions. Na ongea nao bila kuweka kwanza jambo hilo ila ukiona wakati muafaka wa kulionglea basi liongelea kwa makini bila kutanguliza hasiza wala jaziba.
Ukitaka kuongea na mume wako kuhusu hiyo ishu , hakikisha kunauwezekano atakuelewa na ataongea na wewe. Wanaume ni wepesi kufanya makosa lakini ni wepesi vilevile kujirudi.
Mumeo anajua anacho kifanya na kuwa si sahihi. Kwa kuwa wewe ndoo unaishi naye ,basi ishi naye kwa upendo kana kwamba hujajua chochote na hiyo ni mali yako .
Mungu akusaidie.

Lazarus Mbilinyi said...

Wapendwa wote!
Ni kweli huyu dada anahitaji msaada wetu sote kuhakikisha ndoa yake inarudi kwenye mstari,tumkumbuke katika maombi kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana na zaidi ya yote hata katika giza nene bado Mungu wetu hutenda miujiza.

Asante sana dada Grace ni muhimu sana tukampa resources zote tulizonazo kuhakikisha ndoa yake inarudi na kuwa ya furaha.

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima

angel said...

Helow dada pole sana kwa yaliyokupata lakini sumu si suluhisho,kumbuka yupo yesu aliekufa kwa ajili yetu na amukubali kupokea magumu yetu yote kwa hiyo wewe mpigie goti tu mumeo kwa mungu,tena ukiweza muombee na huyo mwizi wako yeye mungu atakuonyesha njia,wapo wadada wengi wamepitia kama yako wakamtumainia mungu zaid wakashinda sasa iweje wewe unywe sumu???!!
kwa mungu hakuna linaloshindikana kamwe,wezi kama hao hua hawafiki mbali my dia,wapo wengi wameiba waume za watu lakini hua hawafiki mbali maana mungu anasikia vilio vya hao wanaoibiwa,mifano mingi tu ipo dadangu kweli hua hawafiki mbali.
nakuombea mungu akutie nguvu uyashinde yote!
Angel

Anonymous said...

Shalom wapendwa,
Mimi naona msaada mkubwa tutakao mpatia ni maombi,ikiwezekana tuchukue jukumu la kufunga na kuomba rehema kwa ajili yake na mume wake kwani Bwana aliyeko ndani yetu ni Mkuu sana na hakuna analoshindwa. Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Wapendwa wote.

Sisi sote ni kiungo kimoja katika Kristo hivyo basi kuombeana n jambo la msingi kabisa na tunaamini maombi hufanya kile Mungu anaweza kufanya.

Tutatangaza siku rasmi ya kufunga na kuomba kwa ajii ya wote wenye mahitaji katika mahusiano na ndoa.

Upendo daima

Anonymous said...

shalom dada,
kwanza kabisa mi nakushauri chunguza chanzo cha tatizo ni nini na nani kati yako na mumeo yupi ni tatizo, kama utagundua wewe ndo tatizo basi omba Mungu akusamehe na akufanye akufundishe kuwa mke mwema mwenye hekima na busara kama vile kitabu cha mithali kinavyoeleza mke mwema anavyopaswa awe. pili ungama kwa kosa la kutaka kujiua.

chunguza dada maombi yako unaombaje mpenzi, maana syle ya maombi ya ndoa sio kama maombi ya kuomba kutaka kula ugali au juice.

ndoa huwa ina maombi ya pekee kabisa, unatakiwa uombe maombi ya kumiliki ndoa yako kumteka mumeo kwa jina la Yesu. sijui kama unafanya hivyo. na kama dada unafanya maombi na namna hii ninayozungumzia basi mumeo asingetoka kamwe nakuhakikishia kwa jina la Yesu kristo wa nazareth. vinginevyo umejisahau kwenye majukumu flani flani ambayo lazma uombe Mungu akufanye kuwa mke mwema unaeng'aa kwa mumeo.

haijalishi ulikutana na mumeo kwa namana gani bali ca msingi ni kulia na Mungu tu mpendwa na hakaika utauona mkono wa bwana.

pia napenda kukushauri ondoa kinyongo kwa mumeo na huyo kimada na jamaa yake. omba Mungu akupe moyo wa kusamehe na uwasamehe alafu nimwambie usionyeshe chuki kwa mumeo we ndo ongeza upendo, mpikie mfulie usi thubutu kumsusa, maana kama unataka muujiza wa ndoa yako jifunze tabia ya MUNGU YA KUSAMEHE NA KUSAHAU.

we jisemee moyoni tu mume wangu humjui mwokozi wangu, nena mema kwa ajili ya mumeo wala usisambaze habari kwa watu, tena njia nzuri ni kwenda kanisani ibada ya maombi upate faraja ya bwana Yesu au sikiliza radio kama praise power kama upo mahali hii radio inashika kuna vipindi vizuri vya kutiwa moyo.

endelea na maombi ya kulia na Mungu, omba maombi ya ndoa ya kumiliki na kumfunga mumeo asiwake tamaa tena kwa mwanamke yeyote yule kwa jina la Yesu.

nikupe tu mfano jinsi ya kuomba haya maombi.
1:mshukuru Mungu kwa kukupa mume mzuri tena mwema na kukupa ndoa njema tena tamu.

2:fanya toba kwa ajili yako na yake.
3:teka macho yake na yafunge kwa super glue ya damu ya Yesu yasione mwanamke yeyote yule.bali wewe uonekane queen,mrembo kuliko wote duniani, princess kwake kwa jina la YESU.
4: TEKA NYARA NA FUNGA UFAHAMU NA MOYO WAKE PIA KWA DAMU YA YESU, USITAMANI KWINGINE BALI WEWE UKUBALIKE SANA MOYONI MWAKE KW3A JINA LA YESU.
5: TEKA LIPS ZAKE, MIKONO NA HAZINA YAKE HAPA NAMAANISHA UUME WAKE NI WAKO, MWAMBIE YESU NAUFUNGA UUME WA MUME WANGU KWA DAMU YA YESU USIWAKE WALA USISIMAME KWA MWANAMKE AWAYE YEYOTE YULE ISIPOKUWA UUME WA MUME WANGU UWAKE TAMAA KUNIINGIA MIMI TU NA KUFURAHIA UKE WANGU TU KWA JINA LA YESU

DADA MWAMBIE MUNGU LIPS NA MIDOMO YA MUME WAKO IWAKE TAMAA NA KULAMBA MWILI WAKO TU,PIA USISAHAU KUUNENEA MEMA MWILI WAKO KTK MAOMBI.OMBA MUNGU AUFANYE UKE WAKO UWE MTAMU SANA KWA MUMEO KWA JINA LA YESU YANI MUMEO AKIINGIA AKUTANE NA UTAMU ZAIDI YA ASALI KWA JILA LA YESU. VIVYO HIYO KWA CHUCHU ZAKO NA G SPOT PIA MWAMBIE YESU MUMEO AKIKUGUSA TU AKUTANE NA UTAMU ULIOPITILIZA KTK KRISTO YESU. OMBA NAYEYE MWILI WAKE UWE MTAMU SANA KWAKO AKIKUINGIA TU UPATE UTAMU KWELI KWELI.

NINA MENGI MPENZI YA KUKWAMBIA ILA MDA UMEBANA HAYA BUT NAJUA HAYA MACHACHE YATAKUPA MWANGA PIA

NAKUOMBEA YESU APONYE NDOA YAKO.

UBARIKIWE SANA


MS GBENNETT