"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, August 5, 2009

Mahitaji yake!

Kama ni mwanandoa ambaye unataka kuwa na ndoa yenye furaha, inaweza kuwa ndiyo kwanza unaanza maisha ya ndoa, au unaweza kuwa upo kwenye ndoa kwa muda mrefu na ndoa ipo hali mbaya kiasi kwamba unajuta kwa nini upo kwenye ndoa au inawezekana wewe ni mmoja ya wandoa ambao wanafurahia kuwa kwenye ndoa na unapenda kujifunza zaidi na kuwa na ndoa yenye kumpa Mungu utukufu zaidi.

Jambo la msingi ni kwamba unaweza kuijenga ndoa imara kama tujifunze kufahamu mahitaji ya mwenzako na kuyatumia.

Bila kutimizwa kwa haya mahitaji muhimu wanandoa wengi hujikuta katika matatizo makubwa baina yao.
Mahitaji ya mwanaume na mwanamke ni tofauti hivyo basi kila mmoja anahitaji kuwa makini kujua upande mwingine unahitaji kitu gani na si kuhitaji tu bali kutimiza.

Mahitaji matano muhimu ya mwanaume katika ndoa
Kuridhishwa kimapenzi (sex)
Mtu wa kuandamana naye
Mke anayevutia
Msaada nyumbani (domestic)
Kuwa na mwanamke anayemuhitaji (depend on him)

Mahitaji muhimu ya mwanamke katika ndoa
Upendo (affection & romance)
Mtu wa kuongea naye
Uwazi na ukweli
Kutimiziwa hitaji la fedha
Mwanaume anayejali familia
Kwa mwanandoa kukosa moja ya hayo mahitaji muhimu huweza kutengeneza kiu ambayo lazima ipate maji.
Baada ya mwanandoa kukosa mahitaji hayo muhimu anaweza kushawishika kuanza kutafuta kutimizwa nje ya ndoa yake.

NB:
Hata kama mwanandoa mmoja anashindwa kutimiza mahitaji muhimu kwa mwenzake kutoka nje ya ndoa bado si jibu au jawabu kwenda kukipata kile unakosa.
Njia sahihi ni kukaa pamoja na kuelezana kwa upendo kila mmoja kueleza kile anakosa na kuendelea kuijenga ndoa kwa pamoja kwani huko nje kuna foxes ambao kama si kuweza kukutafuna mzima mzima basi unaweza kuangamiza familia nzima.
Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Efeso 4:32

1 comment:

Anonymous said...

WHOOOOOOOOOW GUYS WHAAAAAAAAAAAAT? LOOOOOOOKIN GOOOOOOOOOOD MAMAAAAAAAAA.

USA