"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 3, 2009

Mwanaume ni Box

Hapo ana "fix' tatizo usimsumbue! Kama umekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu ni dhahiri kwamba umetambua kwamba kuna tofauti zipo kati yako na mwenzi wako, na hizo tofauti ndizo zinawafanya kuwa karibu zaidi au kukorofishana zaidi.Wanaume ni mfano wa box katika utendaji wao katika maisha.

Kivipi?
Hii ni kutokana na anavyo process maisha na kukabiliana nayo.
Kukabiliana huko ni mfano wa box kwa maana kwamba lazima aingie kwenye kibox kimoja na kumaliza kukufanyia kazi then anaanza kibox kingine na kukufanyia kazi na hawezi kwenda ndani ya kibox kingine kabla ya kumaliza kibox cha kwanza.

Kila issue au shughuli mwanaume anafanya ni mfano wa box ambalo linakuwa limemtenga na jambo lingine kwa kuta za box hadi amalize jambo la kwanza ndipo anaweza kuona box lingine na kuhamia humo.

Kwa asili mwanaume ni problem solver, anachofanya ni kuingia kwenye box moja, anahakikisha amepata solution, then anaanza issue nyingine hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Kama anahisi kwenye box la kwanza hakuna tija anaacha na kuhamia lingine ambalo linampa uwezo wa kuonekana mzuri na si failure

Hii ina maana kwamba kama kuna mgogoro na mke na katika kuongea mke haelekei, basi mara moja ata-ignore na kuhamia box lingine hata kama itakuwa kuwa kimya tu na kurelax.

Hii ina maana kwamba mwanaume akiwa anatazama TV (yupo kwenye box la kwanza) hawezi au huwa hayupo tayari kumsikiliza mke wake anayeongea kitu tofauti na program anayotazama kwenye TV (kibox kingine).
Pia kwa kuwa yupo kwenye box (anaangalia TV) inaweza kuwa ngumu kujua mke anafanya nini au kuna kitu kingine anatakiwa kufanya kwani yupo katika kishughulikia TV (program anayoipenda)

Ndiyo maana mke anaweza kuwa bored na mumewe kwani mume hawezi kumsikiliza mke anaongea na wakati huohuo yeye mwanaume anatazama Tv. Yaani mke anapenda mume awe kwenye vibox viwili kwa wakati mmoja kitu ambacho si asili ya mwanaume.

Pia mke anaweza kulalamika kwamba kwa nini mume anashindwa kumwangalia mtoto huku anatazama Tv yake, hata hivyo kwa mwanaume kumwangalia mtoto na kuangalia TV ni vibox viwili tofauti na hawezi kufanya mambo mawili katika vibox viwili si asili yake.

Mwanamke anaweza kuwa anafanya tendo la ndoa huku anawaza kama mlango haujafungwa na akaenjoy sex hata hivyo kwa mwanamke tendo la ndoa ni box lingine na kusahau kwamba mlango umefungwa au la ni box lingine na hivyo hawezi kujali atakachojali ni kufurahia sex ambalo ni box yumo na anajitahidi ku-fix.

Bottom-line ni kwamba mke na mume huweza kukatishana tamaa sana kutokana mmoja kufanya katika mtazamo tofauti na mwingine.
Mbaya zaidi tunaamini kwamba upande mwingine unafanya makusudi hata hivyo si kweli bali tofauti zilizopo na kujua tofauti zilizopo hutufanya kuwa na mahusiano mazuri.
Akiingia kwenye box usimsemeshe kwani unavyozidi kumsemesha ndivyo atakavyotumia muda mwingine kuchelewa kutoka. Kwake kuingia kwenye box ni njia ya ku-relax, mwache!

No comments: