"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 29, 2009

Ni kama mkulima!

Je, umewahi kusikia kwamba mwanaume hutazama maisha kimakenika (mechanics) na mwanawake hutazama maisha kwa mfano wa mkulima?

Kukiwa na matatizo katika ndoa au mahusiano au na Yule anampenda mwanaume mara moja huwa na wazo kwamba hapa kuna tatizo na anachofanya ni kutafuta spare part mpya na kuiweka na maisha kuendelea kama kawaida.

Kwa upande mwingine mwanamke, kukiwa na tatizo katika mahusiano au ndoa yeye huona hilo tatizo ni mfano ya bustani (garden) inayokua na inayohitaji matunzo na efforts kuhakikisha kila kitu kinakuwa kizuri zaidi.
Huamini mahaba na mapenzi mazuri ni wakati garden imechanua maua vizuri na kukiwa na tatizo ni magugu yanayotakiwa kuondolewa.

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Basi ntaomba kuwa NADOKOA UELIMISHAJI HUU kuwapa wengine wasioujua.
Blessings

Lazarus Mbilinyi said...

Mzee wa Changamoto!

Unakaribishwa sana kuhakikisha na wengine wanajua kile wewe unajua.

Upendo daima