"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 15, 2009

Tusibebeshane!

Wakati mwingine huwa tunajikuta tumebeba maboksi ambayo tunadhani ndani yake kuna vitu ambavyo tulitegemea vitatupa furaha na ridhiko katika mioyo na maisha.
Kitu cha ajabu ni kwamba tunapofika na haya maboksi majumbani mwetu tukifungua ndani tunajikuta kuna vitu ambavyo hatukutegemea kabisa na mbaya zaidi hatuwezi kuyarudisha kule tumeyabeba.

Maisha ya mahusiano nayo wakati mwingine ni kama kubebeshana maboksi, mwenzako akijua wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa na kujuta kwa nini umeamua kuwa naye katika safari moja ya maisha kwani siku zote imekuwa ni wajibu wako kubeba maboksi yake ya hasira, ukari, manyanyaso ya kila aina, uchoyo, kiburi, ubishi, uchafu, ukatili, ubinafsi, na kila aina ya takataka ambazo zinaweza kukufanya uone maisha ya mahusiano na yeye hayana maana.

Je, hujakutana na watu ambao katika mahusiano yao mmoja huwajibika kumpendezesha mwenzake kumfanya awe na furaha au ajisikie vizuri huku yeye mwenyewe akiishi kwa hofu na mashaka na utumwa wa hali ya juu, anajitoa maisha yake zaidi ya binadamu kile anaweza huku akiongozwa na hofu na mashaka na woga wa hali ya juu, hana hata uwezo wa kujadili au kuongea na mwenzi wake kuhusu mwenendo wa mahusiano yao maana anaogopa kunaweza kuzuka mgogoro au zogo?

Na huyo anayefanyiwa wema wote hana shukurani ingawa anajua mwenzake anateseka, badala ya kuwa mapenzi umekuwa utumwa.

Kuna kitu kinaitwa “Narcissism” hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving).
Hili Neno linaendana na story ya kijana wa Kigiriki ambaye alivutiwa na taswira yake mwenyewe kwenye bwawa kiasi cha kushindwa kuondoka hadi akafia hapo.
Hili tatizo huanzia wakati mtu bado mtoto mdogo hasa baada ya Kukosa upendo na huruma, ukweli ni kwamba yeye mwenye hajipendi na matokeo yake hawezi kujua kumpenda mtu yeyote.

Utafiti unaonesha ni asilimia 75 ya wanaume ni narcissists.
Na Adolph Hitler alikuwa kinara wa hizi tabia ingawa huyu alikuwa hatari hata hivyo tunao akina Hitler wengi sana kwenye mahusiano yetu ya kila siku kama vile ndoa, uchumba nk na haijalishi ni mwanaume au mwanamke.

Hawa akina Hitler wanachofanya ni kukubebesha kibox cha wewe Kujiona una hatia, hofu, woga, mashaka, kutojiamini ili wakupelekesha wanavyotaka wao.
Hawa wanaweza kukudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na piawanaweza kuzira kuongea na wewe (silence) na wanachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zao.

Hata unapoishi nao unakuwa unaishi maisha ya mateso na kunyimwa uhuru.
Hii aina ya mahusiano ni hatari tupu na huhitaji msaada wa ushauri kwa wataalamu wa maswala ya ndoa na mahusiano.
Wengine ni watu wenye status kubwa katika jamii zetu anaweza kuwa manager, lecturer, tajiri, mbunge au waziri na hawa watu huonekana watu wa heshima kubwa sana mbele ya jamii kwani ni wapole, wema, watii, ni marafiki, wastaarabu, wamevaa ngozi ya kondoo huku ndani ni mbwa mwitu wakali hata hivyo katika maisha yao ya ndani na familia zao ni hatari kabisa (lethal)
Kama ni mume wako au mke wako ukifanya kosa moja tu yeye huona unastahili kupewa adhabu ambayo hutaisahau badala ya kusamehe na kusahau na kuendelea na maisha kwa raha na furaha.
Hawa wanaume au wanawake hufurahia sana kutesa wenzi wao hawana huruma hata chembe na hawafai katika mahusiano ingawa mbele ya jamii wanaonekana ni watu wazuri.

"Remember, you married her, you didn't hire her!"
Dr Phil

No comments: