"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 11, 2009

Umri na kukomaa

Kuna usemi kwamba wanawake hukomaa mapema kuliko wanaume hata kama wana umri unaofanana.
Binti wa miaka 17 anaweza kufanya mambo kama mtu mzima (adult) wakati kijana wa kiume wa miaka 17 anaweza kuwa bado anacheza na kuonekana mtoto (ingawa siyo wote)

Je ni kweli wanawake hukomaa (pevuka, iva) haraka kuliko wanaume?

Kuna tofauti kubwa kati ya umri na kukomaa.
Wakati umri ni miaka ambayo mtu anakuwa ameishi kwenye sayari ya dunia tangu azaliwe, kukomaa huonesha upo umbali kiasi gani katika kufikiria na mtazamo wa maisha.

Kukomaa huhusisha (tukuko) emotions, hisia (feelings), saikolojia na kiroho, wakati umri ni kitu ambacho ni umbo la nje.Baadhi ya tafiti zinaeleza sababu zinazofanya wanawake kukomaa haraka kuwa ni malezi jamii inawapa wanawake ambayo huwafanya kuwa wawajibikaji mapema katika jamii kuliko wanaume.

Kwa asili wanaume ni viumbe ambao huwa na hitaji la kutunzwa (nurtured) matokeo yake muda mwingi huhitaji mtu wa kuwalea na kuwatunza, hii ni namna ambayo vitu vipo na vipo hivyo ili kufanya balance.
Ukweli ni kwamba tofauti zilizopo baina ya mwanamke na mwanaume ndizo huwafanya kuwa na partner mzuri.
Kwa mfano mwanamke amefundishwa kulea na mwanaume amefundishwa kulelewa kitendo cha kuishi pamoja huwafanya kila mmoja kutimiza hitaji la mwenzake.

Ndiyo maana kwa asili mwanamke hujikuta akiwa anavutiwa (attracted) na mwanaume ambaye umri wake upo juu kuliko yeye, hii humpa mwanamke hisia kwamba mwanaume ambaye wapo umri unaofanana anaweza kuwa hajakomaa( kiakili na kimawazo) kama yeye na matokeo yake huvutiwa na mwanaume mwenye umri mkubwa ili kuleta mlingano katika hisia na mahitaji ya kimaisha.
Ndiyo maana wanawake wengi (siyo wote) wamejikuta wakiolewa na wanaume ambao umri wao ni mkuwa kuliko wanawake wenyewe.

Pia ieleweke kwamba kukomaa ni tofauti na umri kwa sababu kukomaa wakati mwingine ni kutokana na matokeo ya kushinda shida, majaribu, matatizo, mikasa na misukosuko ambayo mtu anapitia katika maisha na jinsi anavyokabiliana uso kwa uso na kushinda au kupata jawabu hata kwa machozi au kudhaurliwa au kuchekwa au kukataliwa au kufukuzwa na kupuuzwa.

Hizi shida na matatizo au majaribu au kupitia mambo magumu ni ni mwalimu mzuri anayeweza kumfanya binadamu yeyote kuwa strong na mkomavu.

6 comments:

Anonymous said...

Hapo nakubaliana na mada
Na nyongeza yangu ni kwamba mazingira, jinsi unavyolelewa na wazazi na mambo unayopitia katika maisha huweza kukufanya kukomaa haraka kiakili hata kama una umri mdogo.
Ndiyo maana unaweza kukutana na watu wazima (adults) ambao wamepitwa mbali na vijana katika kuonesha ukomavu wa akili na mtazamo wa maisha.
Hivyo umri na kukomaa (maturity) ni vitu viwili tofauti

RM - Dar

Anonymous said...

Ni kweli,
Wanawake huwa ahead miaka 2-4 zaidi ya wanaume kukomaa kiakili hahaha!

Anonymous said...

Hivyo ndiyo sababu wakati mwingine wanaume hupenda kuolewa na wanawake waliowazidi umri ili wawe wanalelewa, basi hiyo ni janja yao!

Hata hivyo age is just a number!

Anonymous said...

mmmhh jaman naomba kaka lazarus nieleweshe kidogo mm nina boyfriend ambae nimemzidi umri kama miaka 3, mm nafanya kazi na yy yupo chuo anatarajia kuingia mwaka wa 2 mwaka huu, ina maana hafai kuja kuwa mume?? na tuna malengo mazuri ila kwa upande wa kifedha mie ndo namsaidia sana ukizingatia yy bado hana kazi ji mwanafunzi. pls advice me

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana na jinsi mada ilivyokuchanganya! Usihofu!

Hata hivyo si kweli kwamba mara zote mwanaume akiwa na umri mdogo kuliko mwanamke hafai kuwa mume, zipo ndoa ambazo mimi mwenyewe ni shahidi mke ana umri mkubwa kuliko mume na mambo yapo shwari kabisa.
Na si kweli kwamba ndoa zote ambazo mume ana umri mkubwa kuliko mke huwa ni zenye furaha na kumridhisha, jambo la msingi ni kukumbuka kwamba kila partners wana namna yao na kawaida hutengeneza bond yao na msingi mkubwa wa mahusiano yao au ndoa yao ni nguzo zilizotumika kujenga hayo mahusiano.

Jambo la msingi ni kwamba wewe ndiye unamfahamu vizuri huyo mpenzi wako na je unaona nini miaka 10 ijayo au ndo kweli unambeba kwa kila kitu na hana jipya na upo naye ili na wewe uonekana una rafiki wa kiume?
Kuachana miaka 3 haina effect kubwa sana kama huyo mpenzi wako wa kiume amekomaa kiakili na unajua malengo ya urafiki wenu ni ndoa ambayo kila mmoja ataridhika kuanzia sasa.
Kuhusu umri soma hii link http://mbilinyi.blogspot.com/2008/07/umri-katika-kuoana.html

Pia ni vizuri kujua je ni kweli huyu ni muoaji au ndo walewale kusubiri umtunze then aje akupige chini na aoe mwanamke mpya mwenye umri mdogo kuliko yeye? Isikupe homa sana jiamini na chunguza misingi ya urafiki wenu kwanza kwani mapenzi ni upofu na siku ukiachwa ndo utaaanza kuona na hakuna kitu huumiza namna hii kwa mwanamke na dada kama wewe.
Hivyo uwe makini ingawa naamini hakuna tatizo suala la umri halina nguvu sana, jambo la msingi ni upendo wa kweli na mnapendana sawasawa au geresha tu? Kama kuna upendo wa kweli basi umri hauna nguvu kwani upendo ni jibu la mambo yote.

Nitajuaje ni yeye? Soma kwenye hii link http://mbilinyi.blogspot.com/2009/04/nitajuaje-ni-yeye.html
Naamini wengine wanaweza kukushauri pia
Ubarikiwe na Bwana
Upendo daima

Anonymous said...

kaka lazarus nakuunga mkono wa asilimia zote,umenena vema

MS GBENNETT