"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 29, 2009

Wa Kufanana naye - chumbani

Tofauti ya kiumbo kati ya mke na mume ni asilimia ndogo sana ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa ujumla.
Bila kufahamu tofauti zilizopo tunaweza kujikuta katika shida na matatizo au confusion ya uhakiuka chumbani.
Ukiacha tofauti zingine zote zilizopo kati ya mke na mume linapokuja suala la sex mwanaume sex ni hitaji la kimwili kwanza (physical) na baadae emotions wakati mwanamke ni hitaji la emotions kwanza then kimwili.
Hii ina maana kwa mwanamke sex ni upendo kwanza, kujisikia vizuri kwanza, kupata caring kwanza kwa mwanamume ni kuwasha tu na bus linaondoka.

Linapokuja suala la kila anakiona mwanaume anavutiwa kwa nguvu ya ajabu (hasa anapomuona mwanamke, wakati huohuo mwanamke naye anauwezo na nguvu ya ajabu ya hamu ya upendo, ukaribu, mapenzi na kusikilizwa na mwanaume.

Mwanaume huwaza ni mara ngapi anahitaji sex wakati mwanamke anawaza ni namna gani sex itakuwa.

2 comments:

Anonymous said...

kaka lazarus naomba nikuulize kitu kimoja mm boyfriend wangu yupo mbeya mie nipo arusha kwa ukweli hakuna kitu kinachoniudhi kama nimpigie cm halafu asipokee, unaweza ukapiga cm 3 times haipokelewi then akikupigia anakupa excuse kwamba cm ilikuwa mfukon haina vibration hivyo sijaisikia yaan kiukweli naudhika kupita maelezo leo asubuhi nampigia cm haipatikan nataman nami nizime cm yangu ili akinitafuta asinipate hewan jaman nimfanyaje? nimeshamlalamikia yya anasema im sorry namwambia kwa hiyo unafanya makosa u know sorry is there for u

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana dadangu,

Unajua hakuna simu muhimu kama ya mchumba au mpenzi na wengine hutamani kulala na simu on ili mpenzi akipiga ijibiwe haraka iwezekanavyo kwani mawasiliano ni muhimu sana na matamu.

Ukiona unapiga simu kwa mpenzi na hapokei na sababu kibao inabidi ukaze moyo kwani hiyo ni dalili kwamba kuna kitu kingine zaidi ya hapo na kwamba kutopokea simu ni matokeo.
Mpenzi anayekujali hasa mwanaume yeye siku zote mara nyingi anakuwa mstari we mbele kuhakikisha anawasiliana na ww full speed.
Kawaida ukiona uantuma message na unajibiwa kwa mkato ujue kuna sababu na ukipiga simu ikawa haipokelewi pia kuna sababu.

Hivyo jambo la msingi ongea naye vizuri kwa upendo na uwazi kwamba hujisikii vizuri yeye kama mpenzi wako kukupa homa kiasi hicho kama hana mwingine.
Haina haja akudanganye kwamba anakupenda wakati hana time na wewe kiasi cha kutopokea simu.

Pia chunguza sijajua unaweza kuchunguza vipi ila chunguza unavyoweza inawezekana ni kweli simu yake ina matatizo ingawa hapo kuna tatizo.
Sijajua kiroho una uwezo kiasi gani ila kama una uwezo na masafa marefu basi MAOMBI ndiyo mzizi wa uhakika maana hata kama ana cheat itafika siku mambo yote yatakuwa on the table.

Zaidi jiamini, usilazimishe kwani maisha bila mwanaume bado yanawezekana kwani ukiamini someone is better than No one ipo siku utaumia au kuangukia pua. Hakikisha unampenda mwanaume ambaye unaona future ipo hata miaka 20 ijayo si kwamba watu wajue na wewe una mwanaume.

Mungu akubariki sana naamini mpenzi wako atabadilika kama kweli anakupenda na ataacha sababu hizo zisizo na msingi.

Tenda wema na usilipe ubaya kwa ubaya jitahidi kuwa mwanamke mwema ambaye ni kazi kumpata na mwanaume ukipata unamtunza.

Upendo daima!