"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 27, 2009

Wa kufanana naye!

Uwezo wa kuwasiliana kati ya mke na mume ni moja ya precious commodities muhimu sana katika ndoa au mahusiano yoyote.

Wanandoa wenye uwezo mzuri wa kusiliana huwa na ndoa/mahusiano bora na zaidi huweza kuwa na watoto ambao nao huwa wazuri katika kuwasiliana na hatimaye kuwa candidates wazuri wa ndoa baadae.
Pia kuwa na mawasiliano mazuri husaidia mtu kuwasiliana na watu wengine na kuwa na mvuto zaidi.

Kuna usemi wa kingereza usemao
"Great communicators are people who change their approach based upon the person they are talking to"

Hii ina maana kwamba kama wewe ni mwanaume huwezi ongea the same style kwa mwanaume mwenzako na mwanamke.
Kuongea na mwanamke au mke ni tofauti na mwanaume au mume.
Hivyo kujua au kufahamu jinsi ya kuongea au kuwasiliana na mke wako au mume wako ni jambo la msingi sana ili kuwa na mahusiano mazuri.


Kumbuka mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana kwani;
Huwaza na kufikiri tofauti,
Huongea tofauti,
Huamua tofauti na zaidi
linapokuja suala la hisia kuna tofauti kubwa sana.


Inawezekana wewe ukiwa na mume wako au mke wako huwa mnajikuta ni bubu, au ni kubishana tu au kila mmoja hamwelewi mwenzake au mwenzako akiongea unahisi haeleweki kwani anazunguka wakati anatakiwa kuwa direct to the point.


Unataka kujua kwa nini?


Tutaendelea kesho.
2 comments:

Anonymous said...

Hi!
kaka mbona ulikuwa kimya najua utakuwa ulibanwa na majukumu flaniflani hivi ukiwa kama baba.
Lakini asante kwa kurejea ukiwa mzima natumai.

Hivi kaka Mbilinyi kuna haja wanandoa kuweka ratiba ya tendo la ndoa au unaona imekaaje hiyo?
Maana kwa mtazamo wangu mtu ambaye ni mvivu katika hili ukiweka ratiba na ikafuatwa itakuwa ni vema.

Halafu unaelewa chochote kuhusu kupatikana watoto mapacha? Napenda sana nipate mapacha maana nina mishono 5 na nimebarikiwa mtoto mmoja na ningependa kupata tena mtoto sasa ningepata wawili duuu!


Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Ni kweli kuna siku mbili nzima nilikuwa nje kabisa ya mtandao kuna boss kuna project nilikuwa nafanya si unajua wengine ni forester so muda mwingine tunakuwa mbali kabisa hata hivyo nimerudi salama.

Kuhusu swali lako la ratiba ya tendo la ndoa kuna faida na hasara labda ili nikujibu vizuri au nitoe vizuri faida zake na hasara zake nikaiandae vizuri ili tuone kipi zaidi kati ya hasara na faida.

Kuhusu mtoto au watoto mapacha, sidhani kama unaweza kupanga ninavyojua mimi ni kitu ambacho kinatokea bila kupanga. Labda nikamuone daktari nimuulize scientifically hii ipoje bahati nzuri naishi jirani na daktari wa mambo ya uzazi so usijali give me time nitakuja na jibu makini kabisa.

Nakutakia siku njema na kama una swali unaweza kuuliza.

Upendo daima.