"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, August 28, 2009

Wakufanana naye

Wanaume kila kitu kina folder lake! Wanaume hufikiria kitu kimoja kimoja (ndani kiboksi) au kingereza (COMPARTMENT) wakati mwanamke hifikiria vitu vingi kwa wakati mmoja (GLOBAL).
Pia jinsi tunavyotunza information kwenye ubongo mwanamke na mwanaume ni tofauti kabisa.
Wanaume tunaweza kuhifadhi information kwa kuzitenganisha kila information na folder lake kama vile kazi, hobbies, mke, sex, nk pia hili folder linakuwa limo ndani ya drawer kwa maana kwamba hufungua na kufunga kitu kimoja kwanza ndipo aje kingine.
Hii ina maana kwamba mwanaume atawaza kuhusu kazi, then hobbies, then mke, then sex tofauti tofauti.
Kwa upande wa wanawake wao ni opposite kwani vitu vyote kwao ni munganiko na wanayaona maisha globally.
Hii ina maana kwamba mwanamke huwaza kuhusu kazi, hobbies, mume, sex vyote kwa wakati mmoja.

MFANO
Fikiria mume wako yupo kazini na unampigia simu kwamba anaporudi kazini apitia dukani anunue maziwa na unashangaa anafika nyumbani mikono mitupu.
Hii ni kwa sababu wakati unampigia simu alikuwa anahusika na kazi, analikuwa ana folder la kazi alikuwa kazini (kwenye kiboksi cha kazi) kwake focus ilikuwa ni kazi ifanyike.

Je, umewahi kuwa unaongea kitu na mume wako let say yeye anaangalia mechi ya soka huwa unajisikiaje, si unamuona anaipa attention kubwa hiyo mechi anaangalia kuliko wewe mke wake na unamshangaa hadi unatamani TV iharibike.

Kama wewe ni mwanaume naamini umewahi kuwa na kamzozo kadogo na mkeo siku moja, hata hivyo cha ajabu zaidi ukajikuta mke anakumbushia na mizozo mingine au vitu vingine ambavyo ulifanya miezi mitatu au sita iliyopita.
Wewe unashangaa kwani kuna uhusiano gani na hayo yalifanyika miezi sita iliyopita na hili tunaongelea sasa (zozana).

Kama kumewakua na disagreement kati ya mke na mume asubuhi ni rahisi kusikia mke anasema kichwa bado kinamuuna jioni ya hiyo siku kwani siku nzima atakuwa ana global meetig kwenye ubongo wake kuwaza hiyo disagreement ya asubuhi.

Kinachotokea kwa mume ni kwamba baada ya hiyo disagreement asubuhi kabla ya kuondoka, disagreement ni kama file au folder hivyo anapoondoka kwenda kazini anafungua drawer yake anafunga na kuondoka na akifika kazini anafungua drwer ya file la kazi na kuendelea kufanya kazi, lakini kwa mke kwake siku nzima atashinda anawaza kuhusu hyo disagreement hadi jioni mume akirudi.

Pia inawezekana wakati mnaingia chumbani hamkufunga mlango na kwa kuwa mliingia huku mnaharaka na mahaba basi mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa.
Hii ina maana kwamba mke atakuwa anafanya sex huku anawaza mlango haujafungwa wakati mume hata kama mlango anajua haujafungwa yeye atahusika na kiboksi kimoja cha kufanya sex tu.

Ni vizuri kujua tofauti ili pale kukiwa na tofauti badala ya kukasirika na kuchukia unafurahi na kushukuru Mungu kwa hizo tofauti kama si kumwombea mwenzako kwa Mungu.

4 comments:

Anonymous said...

NI KWELI HUJAKOSEA JINSI TULIVYOUMBWA SISI WANAWAKE ILA ITAPENDEZA KAMA MUMEO ATAYAJUA TOFAUTI ZATU!NAHISI MKEO ANAPATA RAHA ZA AJABU KWANI UNAMJUA HIVYO NI RAHISI KUMUHENDO.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli upo sahihi,
Kujua au kufahamu tofauti zilizopo kati ya mke na mume maeneo yote (kihisia, kisaikolojia, kiroho na kimwili) ni jambo la msingi sana na linasaidia ndoa kuwa ya furaha sana.
Tangu nimefahamu kwamba kuna tofauti kubwa kati yangu na mke wangu kwa kweli imenisaidia sana kufanikisha furaha ya ndoa yangu kwani kuna wakati huwa naishia kucheka na kufurahai tu jinsi Mungu alivyowaumba ninyi viumbe wanawake na ni kweli kujua tofauti zilizopo ndo kufanana hasaa kwani ni raha sana na huwezi kukwazika wala kujilaumu zaidi jambo la msingi ni kuombeana kati ya mke na mume kwani shetani hapendi kabisa ndoa zenye furaha.

Upendo daima!

Anonymous said...

In the end, for all our differences and conflicts, most women and men share the same food, work, shelter, bed, life, joy, anguish, and fate. We need each other.

Anonymous said...

There will always be a battle between the sexes because men and women want different things. Men want women and women want men.