"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 4, 2009

Wanawake ni spaghetti

Tofauti na wanaume ambao ni mfano wa box katka utendaji wao wanawake wao ni mfano wa sahani ya pasta (spaghetti)

Kama ukitazama vizuri sahani ya spaghetti utagundua kwamba kuna nyuzi binafsi nyingi zilizounganishwa na kuchanganyana (noodles).
Kama utaamua kuchunguza uzi mmoja (noodle) utagundua kwamba huo uzi mmoja una intersect na mwingine na unaweza kujikuta umeufuata mwingine.

Hivi ndivyo ilivyo kwa mwanamke kwamba kila wazo na jambo limeunganishwa na wazo na jambo lingine.
Mwanaume hufikiria kitu kimoja tu kwa wakati mmoja wakati mwanamke huweza kufikiria vitu vingi kwa wakati mmoja. Na hii haifanyi mwanamke kuwa bora kuliko mwanaume bali ni ndivyo tulivyo tofauti.

Maisha kwa mwanamke ni process kubwa zaidi kuliko mwanaume
Kwa mwanamke kila kitu kimefunganishwa pamoja kama sahani ya spaghetti noodles.
Ndiyo maana hawawezi kuachana na issue yoyote na emotions zao na wanaweza kuona vizuri big picture na kuiunganisha na kuona vizuri kuliko mwanaume.

Ndiyo maana kwa wastani wanawake huwa wazuri kwenye masuala ya mahusiano na mawasiliano wakati wanaume huwa wazuri kwenye masuala ya sayansi na hesabu
Pia hii ni nkuthibitisha kwa nini wanawake huweza kufanya vitu vingi (multitasking) kwa wakati mmoja bila kukosea.
Anaweza kuwa anafanya kazi inayohusisha akili na wakati huohuo anakufikiria mpenzi wake, au mwanamke anaweza kuwa anawandaa watoto kwenda shule wakati huohuo anaanda list ya vitu vya kununua store (groceries).
Pia anaweza kuwa anaongea na simu huku anapika chakula au anaweza kuwa anaongea na simu huku anaendelea kufanya typing bila kukosea.Anaweza kufanya processing ya information nyingi huku akitunza track ya vyote anafanya kwa wakati mmoja.
Kwa mwanamke kuongelea issue ni moja ya approach ya kupata solution kwani anaweza kujiunganisha logically, emotionally, relationally na spiritually kwenye hiyo issue anayoongelea.
Wanawake huweza kutatua matatizo ila kwa approach tofauti na wanaume na kuacha kuongea naye hujiona kama kukataliwa kiana au kudharauliwa.

Ndiyo maana kuna wakati huleta msuguano akiwa na mwanaume kwani ili kutatua tatizo mwanamke hupenda kuongea na mume ambaye kwako ni mtu anayemwambia na wa karibu wakati huohuo mume naye ili kupata solution hujiona ni vizuri kukaa mbali kwenye kibox chake bila kusemeshwa.

Bottom line ni kwamba Mungu aliumba mwanamke na mwanaume wakiwa na tofauti kwani mke na mume hufikiria tofauti, huhusisha emotions tofauti, hutoa maamuzi tofauti na hujifunza vitu vipya tofauti hata hivyo mwanaume na mwanamke huweza kuunganishwa vizuri sana na kuweza kutengeneza mahusiano yenye afya na kuweza kusababisha hawa wawili kuwa kitu kimoja kilicho kamili.

Hii ni issue ya kiroho zaidi kwani kuumbwa katika utofauti huu huwa tunamtukuza Mungu na tofauti huanzia tangu kuwa na jinsi tofauti, kuwa na historia tofauti, kutoka familia tofauti, kuwa na haiba tofauti na zaidi alikuumba wewe na kukuweka katika agano na mwenzako kitu ambacho ni zaidi kubwa katika maisha yetu.

Unapomkana mwenzi wako kwa sababu ya tofauti zilizopo maana yake unaukana mpango halisi wa Mungu kwako.

Ukishajifunza jinsi mwanamke na mwanaume wanafikiria na kujisikia kuhusu kitu chochote unaweza kubadilisha jinsi unavyomchukulia mambo hasa kama unahitaji kuwa na ndoa yenye afya.

No comments: