"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 30, 2009

Usijisahau!

Wengine kupiga mswaki tu huwa vita! kazi kweli kweli!Ili ufurahi kuwa mwili mmoja maandalizi hayaanzii chumbani bali huanza tangu asubuhi unavyoamka na yote unafanya siku nzima (communication) na mume wako au mke wako huweza kuongeza hamu na pia kujikuta mpo connected na hatimaye kuwa na usiku wenye raha.
Mbusu (romantically) wakati unaondoka asubuhi au mnaagana kila mmoja kwenda na kupambana na shughuli za maisha na familia.
Mpigie simu au text au email mchana kwamba una mkumbuka na mwambie kitu chochote kizuri kuhusu yeye.

Hata hivyo kuna mambo madogo lakini muhimu sana ambayo kila mwanandoa ni muhimu kukumbuka ili kuhakikisha akitaka kuwa mwili mmoja na mwenzake mambo yanakuwa motomoto,

Kwanza, kama mke wako (kama wewe ni mwanaume) umeona analalamika kwamba huwa unamshika/mpapasa/gusa/chezea (touch), busu pale tu ukitaka kuwa mwili mmoja na sivinginevyo basi wewe unafanya makosa makubwa sana na unamnyima haki yake ya kuzaliwa ya kupewa non sexual touch.

Pili, kumbuka kukiwa na non sexual touch nyingi zinafumfanya mwili wako kujisikia vizuri na hupeleka feelings hadi moyoni mwake kwamba kuna mtu anamjali na kumbuka pia kuna wanawake touching ndiyo ugonjwa wao so ukimpatia kwako itakuwa paradise kila siku.
Jitahidi angalau gusa bega lake, mshike mikono, mkumbatie nk.

Tatu, watu 100 waliambiwa waandike vitu ambavyo husababisha kuwa turned off na wake zai au waume zao, asilimia 99 waliandika kwamba mwonekano mbaya ni sababu mojawapo.
Usijidanganye eti hata nikivaa ovyo kama ananipenda atanipenda tu, Pole sana anaweza kukupenda lakini asitamani kuwa mwili mmoja na wewe kwani upo rough, mchafu, unanuka, huvutii na mzembe na hufai kabisa.

Nne, kunukia vizuri ni moja ya sifa za kwamba upo sexy.
Ukinukia vizuri mume wako au mke wako anatamani kuwa karibu na wewe na kunuka ni kinyume chake, hata ulalamike na ukajitahidi kumpeleka kisimani kunywa maji hanywi.
Ukiwa na majasho na hujaoga unafunika homoni za pheromones ambazo huvutia na kuwafanya wanaopendana kuwa na bond imara.
Hivyo smell good!

Tano, uwe mzuri na maridadi kwenye mawasiliano hasa kama wewe ni mwanaume, mke wako anaporudi kazini au jioni anapoongea kuhusu yale amekutana nayo siku nzima msikilize na uwe pamoja naye kuhakikisha anaongea maneno yako yote huku ukimsikiliza na ajue unamsikiliza na upo makini na unapenda kumsikiliza kwa njia hiyo unafungua hisia zake na anakuwa open kukuruhusu baada ya mda ufurahia mwili wake.

Tutaendelea…………………….

Tuesday, September 29, 2009

Kwa nini rahisi nje na si ndani?


Je, unajitahidi kuhakikisha mume au mke wako awe anakusikiliza?
Je, unahisi hakusikilizi na hana response kwa kila kile unataka kuongea naye?
Je, ukitaka kuwasiliana naye unajikuta hana muda na wewe au ndoa imekuwa kimya kizito kinachotisha na umefika mahali unajiuliza hivi kwa nini tunaishi watu wawili tofauti kiasi hiki.

Je, unajua kwamba sasa tunaishi kwenye ulimwengu unaoshangaza sana, just one click unaweza kuwasiliana na mtu yeyote duniani bila kujali yupo bara gani, nchi gani, mkoa gani au wilaya gani huduma nyingi ni bure na pia unaweza kuwa na options kama hutaki ku-click unaweza kupiga simu, unaweza ku-beep, unaweza kutumia FEDEX au DHL kuhakikisha unawasiliana na mtu yeyote mahali popote.

Kitu kinachoshangaza zaidi ni kwamba katika ulimwengu wa sasa suala la mawasiliano kati ya mke na mume yanazidi kuwa magumu kuliko mke au mume kuwasiliana na ulimwengu wa nje.

Hata hivyo tunafahamu kwamba ulimwengu wa sasa haupo kwenye industrial age bali information and technology age ambapo information huweza kusambaa kila pande bila tatizo hata hivyo lazima tufahamu kwamba mawasiliano kwa ajili ya information ni tofauti na mawasiliano ambayo ni PERSONAL
Kuwasiliana na partner wako ni mawasiliano ambayo ni personal yaani two souls together wakati mawasiliano na wengine nje ya mke wako au mume wako ni kwa information.

Mawasiliano ni indicator ya failure au success ya ndoa hivyo ni vizuri kujiuliza je unawasiliana vipi na mke wako au mume wako ukilinganisha na wengine zaidi yake.

Kuna wanandoa wawili bila kujua walikuwa wanamtindo wa kutumiana email kwanza kwa kawaida baadae wakaja kufikia hatua ya kuwa closer zaidi na kuamua kufanya mpango wakutane ili waweze kufahamiana zaidi, wakakubaliana wakutane kituo cha train usiku na kweli wakakutana na kwa kuwa kila mmoja alikuwa very excited hawakuwa makini sana kuchunguzana sana sura hata hivyo baada ya maongezi wote wakajikuta wanaelekea mtaa mmoja katika hilo jiji na baadae block moja apartment moja, nyumba mmoja, mtoto wao mmoja na zaidi kumbe ni mke na mume bila kujua.

Kumbe aliyekuwa haongei naye nyumbani ndiye yule aliyekuwa anaongea naye kwa love and romantic wote wakifika kazini.
Jambo la msingi huwezi kuwasiliana na mke au mume kwa email kama ndiyo njia pekee ya kujenga mawasiliano, unahitaji kusikia sauti yake na pia kumuona anapoongea hata kwa machozi uweze kumfuta au mpangusa, unahitaji kusikia kile anaongea kwa sauti nna kile haongei pia unahitaji kumsikiliza kila anaongea kwa moyo kitu ambacho email au technolojia zingine haziwezi isipokuwa kuwa live na mke au mume kwa furaha, upendo na kicheko.

Jiulize kwa nini wakati wa uchumba au mwanzo wa ndoa ukiwa na mume wako au mke wako ile akichezesha jicho tu ulikuwa unaweza kufahamu anataka kuongea kitu gani na sasa mkiwa wawili ni kimya hadi aje mgeni na akiondoka anawaacha mabubu.

Kumbuka mmeamua kuishi pamoja kwa hiari yenu hakuna aliyewalazimisha hivyo anza kuwasiliana kama pale mwanzo ili ndoa yenu iwe ya kuridhisha .
NB:
Wise men talk because they have something to say; fools, because they have to say something.

Sunday, September 27, 2009

Usikate tamaa!

Usikate tamaa tumia uwezo wako!Moja ya siri kubwa ya mahusiano ya binadamu ni jinsi Mungu anavyo weza kufanya miujiza kwa mwanaume na mwanamke ambao wanaamua kufuata njia za kimungu ili ndoa yao iwe ya kuridhisha na mpya kila siku.

Ni pale tu tunapotii mpango wa Mungu na kumtegemea yeye (kitu ambacho wengi huona kigumu) huweza kupata maana halisi ya upendo wa kweli (intimacy, love and affections) kati ya mke na mume.

Mungu ameweka hamu ya kupendwa ndani yetu kwa sababu maalumu na Mungu hana mpango wa kutufanya tuishi katika ndoa ambazo zinatufanya kuwa frustrated na disappointed bali furaha na kicheko katika familia ingawa siri kubwa ya kwanza ni kumpenda Mungu kwanza.

"The love of God is direct proportional to the love of people”
Hii ina maana unampompenda Mungu kwanza ndipo utampenda mke au mume pia kwani upendo wa Mungu kwetu hufanya reflection kuwapenda wale wanaotuzunguka akiwepo partner wako.

Mpango wa Mungu ni kwamba ule upendo unaowafikisha wanandoa wapya madhabahuni kufunga ndoa huwa ni upendo kichanga kabisa (infant) siyo upendo uliokomaa kwani upendo wa kweli (real love) kati ya mke na mume huweza kuzaliwa baada ya mke na mume kuishi pamoja kwa muda mrefu kwa kupitia shida, majaribu, conflicts, storms, tofauti, furaha, amani na kila mmoja kuwa commited kwa mwenzake kwa kuzikubali tofauti na kila mmoja kuondoa uchoyo binafsi na kujenga kitu kimoja kinachofanana.

Bahati mbaya kubwa ni kwamba wanandoa wapya wengi baada ya kukutana na disappointments au frustrations huhisi ni dalili kwamba ndoa imefika mwisho kumbe huo ndiyo mwanzo wa kujenga upendo mpya.

“The fairly tale must end for the potentials of true intimacy to begin”

Ndoa huhitaji kazi na jitihada ya wawili walioamua kuishi pamoja haitokei naturally kama watu wawili wanapopendana kwa mara ya kwanza (fall in love) na kwamba inakuwa tambalale kila iitwapo leo.

Ndoa ni kuvumiliana na kujitoa ili kujenga upendo wa kweli kwa muda na si wka usiku mmoja tu. Unahitaji kuwekeza jitihada zako, uaminifu (trust), imani na matumaini.

Mke kuwa na hitaji la upendo wa ndani (intimacy) kutoka kwa mume wake tofauti na mwanaume ni hitaji ambalo hufanya kazi kama injini kwa wanandoa kuhitaji kuridhishana hata hivyo mke akiamua kuchukua njia nyingine ya kuwa mkali na mchungukwa mume anaweza kuifanya ndoa ijae uchungu na upweke na hatimaye kusambaratika.

Mungu ameweka siri kubwa sana kwa watu wawili imperfect kutengeneza kitu kimoja (mwili mmoja) hii ni kazi inayohitaji kazi ili kuwe na bond strong.

Tukumbuke kwamba wanandoa wapya wawili ambao hukubaliana kwenda mbele za Mungu kutoa viapo vya kuishi pamoja kama mke na mume ni binadamu wa kawaida ambao ni dhaifu (vulnerable & insecure) haijalishi wanajitahidi kiasi gani kuficha mapungufu yao kila mmoja kwa mwenzake hata hivyo baada ya kuoana na kuanza maisha kila mmoja hujifunza kwamba ni kitu kisichokwepeka kuficha mapungufu na kwamba upungufu ni sehemu ya binadamua na jambo la msingi ni kila mmoja kumkubali mwenzake kama alivyo.

“A woman never marries the man of her dreams, she helps the man she marries to become the man of her dreams”

Ukiwaona wachumba ambao wanategemea kuoana macho yao huwa hayaoni chochote isipokuwa uimara na ahadi kamili ya upendo uliondani ya mioyo yao.
Ikitokea ukamuuliza binti (wachumba) je, unaona kasoro yoyote kwa mchumba wako (kijana wa kiume) bila shaka atakwambia Mungu amenibariki sana kunipa mume mtarajiwa ambaye hana kasoro wala tatizo lolote.

Hata hivyo hizo ni illusions, ni maluweluwe ni fantasy ni kitu ambacho hakitadumu kwa muda mrefu kwani akishaolewa tu hatahitaji kufikiri sana kuorodhesha kasoro za mume wake na wakati mwingine atalalamika kwamba nilikuwa sijui kwamba tupo tofauti kiasi hiki.
"Wachumba huishi kwenye ikulu na wanandoa huishi kwenye nyumba halisi"

Kabla ya kuolewa mwanamke huona matumaini yanayong’aa kwa mume wake mtarajiwa, anaona ulinzi, uimara, matumaini na upendo usio mfano na mwingine huringa na kutembea kwa madaha hata hivyo baada ya kuolewa anaanza kuona udhaifu na ndoto zote zinaanza kuyeyuka na kusinyaa kama au maridadi kwenye jua kali la ikweta, hukatishwa tamaa na yote huja ghafla kama kimbunga na anaanza kuumia na kujuta kwa kuwa mahitaji yake hayajatimizwa kama alivyokuwa anaona mwanzoni.
Haamini jinsi mume asivyomjali na kumsikiliza na kumpenda.

Hadi hapo mke anaweza kuamua kuitikia kwa:-
(i) Kwa hasira kutokana na hayo mume wake amemuonesha]
(ii) Kwa Kuwekeza kwa upendo, imani katika uwezo/uimara (strength zile anaziona kwa mume wake na kuanza kuijenga ndoa upya

Ili mambo yaenda vizuri au upendo wa kweli uzaliwa mke anatakiwa kuamini uwezo wa ndani wa mume wake alionao ( streghth siyo weakness).
Anaweza kuwekeza kwa mume halisi aliyejificha kwa mume wa nje mwenye kutojali kutimiza ndoto zake za uchumba na honeymoon.

"The secret in marriage is not finding a hero to be your husband, but finding the hero in your husband”
Mungu amempa kila mwanamke uwezo wa ajabu wa kumsaidia mume wake kukua na baada ya muda mume kuwa mcha Mungu sawa na anavyotakiwa.
Bahati mbaya ni kwamba wanawake wengi wamekatishwa tamaa sana kiasi kwamba huyu mwanaume aliyenaye leo hawezi kuwekeza chochote kwa ajili ya mume huyu atakavyokuwa kesho.

Una Uwezo wa kushangaza!

Mtu mwenye nguvu kuliko watu wote katika historia ya dunia alikuwa Samson, kama ingekuwa leo basi Samson angeitwa Mr. Universe au Mr. Israel.
Kama ni masumbwi basi Samson angebeba mikanda yote ya World Boxing Association (WBA) au World Boxing Council (WBC) au World Boxing Federation (WBF) au World Boxing Organization (WBO).
Hakuna cha akina Tyson wala Evander Holyfield au Wladimir Klitschko wote wangedundwa sekunde chache tu baada ya pambano kuanza.

Samson alikuwa shujaa (hero) kwa taifa la Israel, aliweza kuua simba kwa mikono mitupu, maelfu ya watu mikono mitupu pia na hata mageti ya vyuma yalishindwa kumfungia kwani aliyavunja bila huruma.

Samson alikuwa na ugonjwa na mabinti wa kifilisti (aliwapenda sana ingawa alionywa na kwake ikawa sikio lisiosikia...)
Mara ya kwanza alioana binti ambaye Biblia haimtaji jina na wengi huhisi hii ilikuwa ni Sababu tosha kwa Samsoni kuanzisha vita na wafilisti, ndoa haikudumu ilivurugika siku ya harusi hata hivyo Samson akampata mrembo mwingine kutoka kwa wafilisti, Delila ambaye hata hivyo wafilisti walimrubuni atafute siri ya nguvu za Samson.
Hata hivyo mke wa Samson yaani Delila alikuwa na nguvu kuliko Samson kama huamini subiri!

Huyu mwanamke alimaliza historia ya Samson na Samson akatoboa siri ya nguvu zake baada ya kuwekwa kufuani kwa Delila na matokeo yake akatobolewa macho na jina la Mungu wake likatukanwa.
Delila alitumia uwezo wake kama mwanamke kumshawishi Samson atoboe siri ya nguvu zake ambayo ilikuwa ni nywele zake kutonyolewa tangu utoto wake.
Baada ya kutoboa siri tu wafilisti wakamshika, wakamtoboa macho, wakamtesa na kumchezea kama mdoli na kumpa kazi ngumu.

Heading za magazeti ya KASHESHE, HABARI LEO, DAILY NEWS, THE GURDIAN, TANZANIA DAIMA, TAIFA LEO, MWANANCHI NA MENGINEYO YA WAKATI HUO HUKO ISRAEL yalipambwa na vichwa vya habari kuhusu Delila kummaliza Shujaa na Mbabe Samson, sipati picha!
(Kwa habari kamili kuhusu Samsoni soma Biblia kitabu acha waamuzi sura 13- 16)

Habari hii inatuelimisha au kutukumbusha kwamba uwezo alionao mwanamke kwa mume wake ni mkubwa ajabu na anaweza kufanya lolote anataka akijua jinsi ya kuchezesha kalata zake hasa kwa kujua mume wake udhaifu wake upo wapi.

Wanawake wote wanauwezo mkubwa sana juu ya wanaume tatizo kubwa wanawake wengi wameshindwa kutumia uwezo wao, ushawishi wao kuhakikisha mume anamuweka sawa au kufanya vile anapenda kwa sababu hawajajifahamu.
Hapa ninazungumzia kufanya yale ambayo mwanaume anaamini mume wake anazembea kama vile kuiweka ndoa katika mstari sahihi.

Ni kawaida kuwa na Generals, au Governors au Rais au mawaziri wanaume hata hivyo wengi wao hujikuta wake zao wakiwa chimbuko la uongozi wao na kwamba huwa wanawasaidia kutoa maamuzi ya mambo mengi.

Kuna usemi kwamba:
“A man’s wife has more power over him than the state”

Hata binadamu wa kwanza pale katika Bustani ya Eden alianguka baada ya shetani kumtumia Eva (mwanamke) kwa kumdanganya kula matunda na hatimaye amshawishi mume wake naye ale kwani alijua angemtumia mume ingekuwa ngumu sana mume kumshawishi mke akubali badala yake aliona mwanamke ni rahisi kumshawishi mume na akakubali.

Bottom line ni kwamba mwanamke anao uwezo mkubwa sana katika kuvumbua kile kilichomo ndani ya mume wake na kwamba mwanamke akitumia uwezo wake ambao Mungu amempa kuhusu mume basi anaweza kujenga mahusiano na ndoa imara na inayoridhisha.
Wapo wanawake kila kukicha ni kulalamika tu kwamba mume wangu mume wangu, acha kulalamika tumia uwezo wako wa kuwa mwanamke kumsaidia mume kuwa mume bora katika ndoa kwani Mungu amekupa uwezo wa ajabu ndani yako kiasi kwamba mume yeyote anaweza kumkubali kile mke anasema pale mke akitumia uwezo wake sawa na Mungu alivyompa.

Friday, September 25, 2009

Kumaliza haraka!

JE MAANA YA KUMALIZA MAPEMA NI NINI?
Kumaliza mapema ni kitendo cha mwanaume kushindwa kuthibiti kukojoa (Ejaculation) kwa muda unaotakiwa hadi mke kuridhika wakati wa tendo la ndoa au ni kitendo cha uume wa mume kushindwa kusimama (dinda) kwa muda wa kutosha hadi mke kuridhika na tendo la ndoa au kufika kileleni.

Kudumu muda mrefu wakati wa sex maana yake ni kuweza kuthibiti kukojoa mapema (premature ejaculation).
Kukojoa mapema kwa mwanaume kabla ya mwanamke kuridhika ni tatizo sugu la wanaume wengi duniani.
Watu huelezea aina hii ya udhaifu kwa kutumia muda kwa maana kwamba wengine huchukua sekunde chache tu katika dakika na anakuwa amemaliza, wengine ni strokes chache tu in and out anakuwa ameshamaliza hoi na hawezi kuendelea tena huku mke bado hamu imemjaa.

Jambo la msingi hapa ni kwa nini inashindikana kuzuia kumaliza mapema na kwa nini inatokea bila kupenda (involuntary control or reflex)?.

JE, HILI TATIZO NI KUBWA KIASI GANI DUNIANI?
Kwa mfano kwa Marekani peke yake robo tatu ya wanaume wote hujikuta timing inawashinda kuweza kuthibiti kukojoa mapema wakiwa na wapenzi wao.
Habari njema ni kwamba huu udhaifu hupungua jinsi mwanaume anavyoongezeka umri hivyo akikua ataacha.

JE, UNAWEZA KUTHIBITI VIPI HII HALI?
Njia kubwa ya kuthibiti tatizo la kukojoa mapema ni mwanaume mwenyewe kujijua jinsi anavyosisimka (sexual excitement level) hasa wakati wa tendo la ndoa.
Kufahamu kiwango cha kusisimka anachokuwa nacho kwa vipindi tofauti wakati wa tendo la ndoa na muhimu zaidi kujua ule wakati ambao anakaribia mahali ambapo hawezi kujizuia tena (inevitable ejaculation).

Kuwa na ujuzi (skills) za kubaki amesisimka kwa muda mrefu hadi mke wake kuridhika ndilo jambo la msingi hapa.
Hili suala linahitaji uvumilivu, ugunduzi, kujitoa na ujuzi kwani matokeo huwa mazuri sana.
Kama watu wanavyojifunza kuogelea wakaweza basi hata hili mwanaume anaweza kujifunza.
Pia ili kushinda hili tatizo mume na mke wanahitaji kushirikiana hasa kwa mke kumtias moyo mzee kwamba anaweza na kuhakikisha kila mmoja hasa mume anakuwa free kutokana na kila distractions, tensions, anxiety na hofu.
Wote kwa pamoja ni muhimu kujihusisha na maandalizi ya tendo la ndoa (foreplay) na kufurahia kila sensation ambazo kila mmoja anapata.

JE, HATUA ZAKE NI ZIPI?
Mume asiharakishe kuingie (penetrate) haraka kwa mke na hata akiingia asianze thrusting haraka baada ya kumwingia mke, chukua muda kuingia polepole na kwa hatua.
Wakati uume ukiingia kwenye uke kutakuwa na sensation tofauti na jotojoto ambalo litapelekea mume kujikuta anataka kumaliza kama aliingia kwa fujo hivyo dawa yake ni
Kuingiza uume kidogo kidogo (inch kwa inch huku una relax kwa sekunde chache kwani kila msukumo mmoja unakupa control ya kumaliza haraka.

Na baada ya kuingia mume asianze thrusting hapohapo ni vizuri kusubiri kwa sekunde chache hadi ule msisimko wa kutaka kumaliza ushuke chini katika kiwango cha kuweza kuhimili (manageable level)
Kama ikitokea wakati una penetrate au umemaliza penetration ukajikuta unataka kumaliza (ejaculate) haraka anza kupumua (breath) kupitia mdomo na pua ili kuondoa hewa kwenye mapafu kwani kuondoa hewa deep na polepole husaidia kuondoa nguvu ya kutaka kumaliza haraka.

Ukishaanza kujisikia vizuri ndani ya uke unaweza kuanza kufanya thrusting kawaida kama 4 – 5 hivi (in and out) kwa polepole na za kuvuta (long) na pumzika kwa sekunde kadhaa. Mwanaume ndiyo dereva so unatakiwa kujua hali ya hewa kwenye stick inaendaje kwa ukijisahau kwa muda mrefu stick inaweza kupoteza erection so inabidi uwe mzuri kucheza na hiyo hardware yako pia kusugua kwa break ambazo haziridhishi mke anaweza kujikuta kazi unayofanya haina maana.
Hivyo hapa suala la msingi ni unapumzika kusugua kwa sababu unapunguza excitement inayotaka kusababisha mume kumaliza mapema na wakati huohuo unaelekeza uwezo wako kuhakikisha uume unasimama kiasi cha kutosha kuendelea kumpa raha mke.
Umeelewa?

Baada ya hako ka gap sasa unaweza kusugua zaidi kama mara 6 hadi 10 hivi na kupumzika na unaweza kuendelea na kupumzika kidogo kidogo na hatimaye baadae unaweza kuendelea full gear hadi mwisho.
Ni vizuri pia kumsoma mke wako mambo yapoje ana yupo hatua gani kama na yeye amekolea basi unaweza kuamua kufika kileleni kwa wewe kwenda haraka strokes zako.

Huu utaratibu utakusaidia kuweza kupata uzoefu wa kuwa na control ya kujijua wakati gani unakuwa unakaribia point ambayo hwezi kujizuia kuamaliza.

KWA UFUPI NI KWAMBA:
Kuingia kwenye uke na kuanza kusugua (thrusting) moja kwa moja huweza kusababisha kumaliza haraka kwani uume unakuwa bado una tension kubwa.
Kusugua haraka haraka na kwa ufupi hupelekea kumaliza haraka wakati kusgua polepole na kwa urefu husababisha kuwa na control ya kumaliza mapema.
Kusugua moja kwa moja (Continuous/nonstop) iwe haraka au polepole, fupifupi au ndefu hii husababisha kumaliza mapema hivyo kusugua kwa mapozi (timing) husaidia kuwa na control.

Kufahamu point ambayo mume huweza kuwa na msisimko wa kutaka kumaliza ni muhimu sana kwa kujifunza kujua jinsi ya kuthibiti kumaliza mapema.

Ukihisi unakaribia mahali ambapo huwezi kufunga break basi pumua kwa uwezo wako wote hiyo inaweza kusababisha kupunguza sensation ya kutaka kumaliza mapema.

JAMBO LA MSINGI NI KWAMBA!
Ufanisi ya hii njia ni kwa wanandoa kujihusisha huku wakiwa huru hakuna uadui wala mgogoro wowote na kila mmoja lazima awe pleasing kwa mwenzake.
Pia ni muhimu sana kwa mke kuwa na ushirikiano kwa mume hadi atakapojua jinsi ya kuwa na control ya kutaka kumaliza mapema, anyway program nzima ni kwa faidi ya mke.

Mke anaweza kujikuta hakuna utamu wowote wa hili zoezi kwani kitendo cha mume kuwa na break mara kwa mara kinamnyima raha yake hata hivyo hii ni learning process akishajua in and out kuhusu kuwa na control kila kitu kitaenda vizuri.
Zipo njia nyingi na hiyo ni mojwapo tu!


Uchumba/Honeymoon ni mtoto!

Uchumba/honeymoon ni kitoto kichanga cha upendo wa kweli katika ndoa.Kizuizi cha faragha ya mapenzi (intimacy) kwa wanandoa.
Kukiwa na disappointment kwenye ndoa hasa mwanamke baada ya kuhisi yale alitegemea hakuna, huweza kuwa kizuizi kikubwa sana cha kujenga faragha ya mapenzi katika ndoa.
Kawaida ufahamu wetu kuhusu mapenzi (love) na ndoa kabla ya kuolewa au kuoa huwa unrealistic na si sahihi sana kwa kuwa tunakuwa bado tunakuwa hatujafika kwenye maisha ya kweli ya ndoa.
Kumbuka uchumba ni social activity ambayo unakuwa na interest kubwa ya kuwa na focus ya romantic yaani kila mmoja kumfurahisha mwenzake kiasi cha mwenzake kushindwa kuona hitilafu, kwa upande mwingine Ndoa ni task oriented work ambayo inahusisha kushirikiana katika uhalisi wa maisha ya kweli ya watu wawili imperfect.
Ikiingia kwenye ndoa unakutana na maisha halisi pande zote yaani positive na negative kama vile kuelewana na kuitoelewana, kupatana na migogoro, furaha na huzuni, kufurahishana na kuzozana, kufaulu na kushindwa.

Tatizo kubwa ni kwamba wengi huwa wanaingia kwenye ndoa na expectation za aina moja tu na akikosa vile alitegemea anakuwa frustrated na kujiona ameolewa au ameoa wrong partner, SI KWELI NI MTAZAMO WAKO TU UKIKUA UTAACHA NA UTAKUWA NA NDOA NZURI SANA.
Pia dunia ya sasa (modern society & information society/culture) imeathiri kwa kiasi kikubwa sana uelewa wetu kuhusu ndoa tofauti na wazazi wetu.
Chunguza jinsi media zinavyotudanganya kwa matangazo kuhusu wanawake, vijana na jamii kwa ujumla pia movie, TV, cartoons na romance novel vyote vinatupa hadithi za alinacha na kutudanganya kwamba sasa tunajua kuhusu ndoa.
Zinatudanganya kwamba mwanamke akimpata mfalme na yeye atakuwa malkia na atahudumiwa kama malkia na kwamba ameahidiwa kupata upendo wa kweli milele.

Fikiria kungekuwa na ndoa ambayo ziku zote ndani ya maisha mke na mume ni vilevile, si juu wa chini, hakuna disagreement kwa kuwa hakuna kitu cha kujadili na kutofautiana, hakuna mgogoro kewani wanaogopa kujieleza ukweli kwani mwenzake atakwazika.
Ukweli ni kwamba maisha yao yatakuwa shallow sana, hao ni wanandoa mfu, huwezi kupenda bila kukubali kwamba kawaida katika mahusiano kuna disappointment na conflict na pia ni mtazamo wako tu.
Wapo wanawake ambao kimtazamo wapo mbali kwa maana kwamba pamoja na disappointments, kuyeyuka kwa ndoto za yale aliahidiwa kabla ya ndoa bado huamua kuishi maisha ya furaha na kuendelea kutembea katika makusudi ya Mungu katika ndoa yake.
Wamefahamu kwamba masimulizi ya ukiolewa utakuwa princes ndani ya castle ya prince ni illusions ni vitu ambavyo vinaweza kuwa vipo au visiwepo.
Wanafahamu kwamba watu wazima wanaishi kwenye real world na kwamba upendo wa uchumba na honeymoon ni kitoto kichanga (infant) cha upendo wa kweli na kwamba kitahitaji kujifunza kutambaa, kutembea na kujigonda, kudondoka na hata kuumia ili siku moja hicho kichanga kiwe mtu mzima yaani TRUE LOVE
Wale wanaopingana na huu mtazamo hujikuta wakiruka toka mume mmoja hadi mwingine na kukutana na mambo yaleyale na walichofanya ni kubadilisha shape, size au rangi ya mwanaume ila matatizo yamekuwa mapya na makubwa zaidi.

Ni muhimu sana kuamini kwamba Mungu anao uwezo wa kufanya maajabu au miujiza katika magumu yote unapitia katika ndoa yako na anaweza kuiwezesha ndoa yako kuwa na upendo wa kweli.

Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa
ya mumewe.
Mithali 12:4

Thursday, September 24, 2009

Sikutegemea kabisa!

Nimechoka sana kuendelea nkujitahidi kuhakikisha ndoa yetu inakuwa nzuri na inanifanya kuridhika, miaka nenda rudi tumekuwa tunabishana the same thing.
Sasa tumefika mahali hata hatuwezi kuongelea tatizo lolote katika ndoa yetu, ni kama vile kila mmoja amaona haitawezekana ingawa ndani ya moyo wa kila mmoja kuna vita ya chini chini inaendelea (cold war) ndiyo maana kitu kidogo tu huweza kusababisha moto kuwaka.
Hakuna raha, hakuna msisimko, hakuna upendo, hakuna kuvumiliana na hakuna ukaribu wa mapenzi ni kama watu wawili tofauti tulioamua kuishi kama kaka na dada wanaogombana katika nyumba.
Nafahamu hakuna ndoa ambayo ni perfect, hata hivyo nilitegemea hii ndoa yetu iwe ya kuridhisha kwa kiasi fulani.

Mume wangu hanijali tena, anakuwa excited na natokeo ya mechi ya soka (Asernal huko UK) kuliko mahusiano yetu, hukasirika sana hiyo timu yake ikifungwa huko UK wakati yeye yupo Tanzania na hakasiriki kuumiza feelings zangu mimi mke wake ambaye tunalala akitanda kimoja.
Hata akifanya kitu kizuri ni kama bahati mbaya katika wajibu wake ila si kwa kupenda au kuamua nimfurahishe mke wangu au kuonesha ananipenda na kunijali.
Naamini hii si maana ya ndoa ilivyo au inavyotakiwa kuwa , najuta kuolewa na huyu mwanaume pia sijafahamu kama nisingeolewa ningejua ndoa ina mambo magumu kama haya.
Swali linaloniumiza kichwa ni hivi kwa nini hawezi kutamabua mahitaji yangu kama ilivyokuwa mwanzo? Kwa nini hathamini ndoa yetu kama mimi ninavyothamini?
Je, nilifanya makosa kuoana nay eye?
Na je, bado kuna matumaini?
Ni mimi Jema (si jina la kweli ) miaka 7 kwenye ndoa.
UFAFANUZI ZAIDI:
Wanawake wengi hujikuta feelings zako zimaumizwa kama Jema, wao hutegemea baada ya kjuolewa wamepata mwanaume ambaye angempa TRUE LOVE matokeo yake anapewa TRUE FRUSTRATIONS.
Badala ya maisha ya furaha wamejikuta ni ndanin ya TOTAL DISAPOINTMENT, wamejikuta ndoto zimayeyuka na matarajio au mahitaji yao yakiwa ni ndoto za mchana.

Tukumbuke kwamba kila mwanamke huwa na ndoto kwamba siku moja atapata MR RIGHT, atampata Prince na yeye kuwa princes, na huyu mwanaume atajitahidi kufanikisha ndoto zake na mapenzi yatakuwa motomoto siku zote za maisha yao na ndoa yao.
Wakati wa uchumba hufika na binti hujikuta kweli amempata mwanaume wa ndoto zake kwani hakuna tatizo wala kitu unachoona hafai kwani kama ni matching basi imefanywa mbinguni.
Wanafanana kwani streght za mwanaume zina match weakness za mwanamke.
Ni mwanaume anayemsikiliza na kumpa mahitaji yote na anaahidi kwamba atajitahidi kuhakikisha ndoa yako unakuwa mfano.
Macho ya mwanamke hujawa na HOPES na ameamini kwamba amempata wa kumpa TRUE LOVE.
Kila anayewaona mitaani anawapa mkono wa kheri kwa kuwa siku moja watakuwa mke na mume kwa ndoa safi na kuingie honeymoon kwa madaha na mbwembwe.

Baada ya kumaliza honeymoon, maisha yanaanza, siku zinaenda, miezi inaenda na miaka inaenda, conflict zinaanza kujitokeza kwani kila mmoja alizawali sehemu tofauti, malezi tofauti na zaidi ni mwanamke na mwanaume wapo tofauti.
Mume anaanza kupuuza kumsikiliza mke wake tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuoana. Mume anaanza kutumia muda mwingi kufanya mambo yake au kuwa na rafiki zake.
Weekend zikifika anaenda na rafiki zake kutazama sports na kuongea mambo ya business na anarudi nyumbani usiku saa sita bila taarifa kwamba atachelewa.
Mke amesubiri amechoka na ameamua kulala huku hajala maana anaamini kula na mume ndo raha ya ndoa.
Mke anaanza kupata shock na kuwa disappointed jinsi prince wake anavyoanza kufanya mambo yake tofauti na matarajio.
Mke anaanza kujihisi upweke unaanza na hofu kutanda kwenye mawazo yake nini kimetokea kwa mume wake.
Anajikuta yupoo kwenye njia panda. Maswali yanaanza kujaa kichwani (kumbuka mwanamke ana 8 lanes za kupitisha atraffic za emotions kwenye mind yake).
Je, nifanyeje nisimkasirishe na wakati huohuo nimwambie anavyofanya ni vibaya na ajirekebishe?
Je, nilioana na mwanaume sahihi?

MUHIMU SANA KUELEWA HAYA:
Hapo juu tunaona contrast kati ya matarajio ya mwanamke na reality ya maisha ya ndoa.
Matarajio mengi ya wanawake wengi kuhusu ndoa ni UNREALISTIC, si matarajio sahihi, ni vitu ambavyo katika maisha ya kweli kwenye ndoa huwezi kuvipata, ni illusions kama vile movie.

Wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawana matarajio kwamba kwenye ndoa kuna conflict, kuna kuumizwa, kuna hasira, kuna majaribu, kuna shida, dhiki, tabu na kwamba hivyo vyote ni sehemu ya ndoa kwani ndoa ni mwanaume na mwanamke ambao kila mmoja ni NOT PERFECT ana matatizo yake si malaika.

Kujiandaa na kuwa tayari kwa ndoa ni pamoja na kufahamu kwamba kwenye ndoa kutakuwa na CHALLENGES ambazo kwa kushirikiana mke na mume wataweza kuzishinda na zaidi kuwa na ndoa sawa na NDOTO ZAO.
Kuamini kwamba umejiandaa vizuri kwa ndoa na kwamba ukikutana na HUGE DISAPPOINTMENT na kudhani kwamba si sahihi hii ina maana bado hukujiandaa kwa ndoa kwani ulikuwa na upande mmoja tu kwamba ndoa ni tambarare kama mawindoni.

Kuna msema kwamba:
“Marriage is a Romance in which the Hero dies in the fuirst chapter”
Hivyo badi kumbuka kwamba upendo wa mwanzo (honeymoon) ni fantasy ni siku halisi ni illusions upendo wa kweli hujengwa baada ya wawili kuvunjwa vunjwa na shida na matatizo na kushinda pamoja na kukiri wenyewe kwamba kweli mimi na mwenzangu tumetoka mbali.

Ukikutana na disappointment kwa mara ya kwanza katika ndoa yako usiinue macho kuangalia wanaume wengine kwenye ndoa zingine na ukajiona wewe ulikosea kumpata huyo mume wako bali shukuru Mungu kwa hayo unapitia na jambo la msingi kwa hazina kubwa ua upendo uliyonayo huku ukimuomba Mungu anza kuchimbua hazina ya ushujaa wa mume wako na kuijenga ndoa upya ili iwe na upendo wa kweli.

UJUMBE MUHIMU:
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
Mithali 14:1


Wednesday, September 23, 2009

Kumwelewa Mke!

Ndivyo walivyo!Kumuelewa mwanamke kwenye mahusiano.
Wanaume wengi hulalamika kwamba wanawake huwa hawaeleweki linapokuja suala la mahusiano (mapenzi).
Kama wewe ni mwanaume habari njema ni kwamba kumwelewa mwanamke au mke wako au mpenzi wako ni rahisi mno na ukishafahamu siri yake basi inakuwa rahisi kumpa kile anahitaji katika mahusiano yenu (ndoa).

Kwanza mwanaume na mwanamke ni tofauti as if wanatoka sayari tofauti.
Kawaida paka hufukuza panya na mbwa hukufuza paka sababu kubwa ni kwamba naturally panya, paka na mbwa wapo wired tofauti.

Kubali na fahamu kwamba mke wako yupo tofauti na wewe wala usilalamike au utake awe vile unataka wewe.
Zikubali tofauti zilizopo na zifurahie na endelea kumpenda.
Viva la difference!

Mimi mwenyewe ni shahidi katika zamani za ujinga wangu kutaka mke wangu awe kama ninavyotaka mimi.
Nilichojifunza ni kwamba tofauti zilizopo zilikuwa designed na Mungu mwenyewe ili ndoa au mahusiano kuwa imara na kuridhisha kwa maana kwamba kila mmoja aweze kutimiza hitaji la mwenzake (kukamilishana).

Yale mwanaume anahitaji na kuyapenda naturally ni tofauti na mwanamke na ndoa ndiyo mahusiano ya pekee duniani (on the planet) ya kuwaunganisha mwanaume na mwanamke ili kila mmoja aridhike pale design ya kimungu inapofuatwa.
Pili, kumuelewa mwanamke katika ndoa ina maana mwanaume lazima afahamu jinsi mwanamke na mwanaume wanavyokuwa motivated.
Nini huwavuta kufanya kile wanafanya?
Wanawake huvutwa na
Kuthibitishiwa (approval, security)
Mahusiano yanayoridhisha
Mawasiliano mazuri.
Kwa mfano mwanamke anahamu ya kusikia kutoka kinywani kwa mume wake kwamba nakupenda haijalishi jana au juzi au siku ya harusi ulisema nakupenda, neno Nakupenda analihitaji masikioni mwake mara kwa mara tena uwe una maanisha.
Pia anahitaji kusikia unamwambia amepeza au amepika chakula kitamu au kitu chochote anafanya anahitahi approval.

Tatu wanaume na wanawake wana mahitaji tofauti.
Kumuelewa mke wako katika ndoa ina maana ya kufahamu kwamba kile wewe unahitaji inawezekana siyo kile yeye anahitaji.

Ikitokea kwamba mwanamke na mwanaume wote waandike orodha ya vitu 3 ambavyo anahitaji katika ndoa, ukweli ni kwamba vitatofautiana sana.
Wanawake wengi suala la mawasiliano huwekwa juu kwenye orodha, kwa upande mwingine, wanaume wengi huweka sex juu katika orodha kama hitaji lao kubwa katika ndoa.
Utafiti mwingi unaonesha kwamba mambo matatu ambayo huwa juu kwenye orodha ya wanaume na wanawake ni kama ifuatavyo:
Mahitaji 3 muhimu ya mwanamke katika ndoa;
Mawasiliano (conversation)
Kugusswa (Non-sexual touch)
Kujisikia anapendwa na anahusudiwa (cherished, adored)

Mahitaji 3 muhimu ya mwanaume katika ndoa ni
Mapenzi (sex)
Kuheshimiwa (respect)
Hewa (
kwenda pangoni)

Je unadhani mahitaji yako kama mwanamke ni tofauti au mwanaume ni tofauti?

Tuesday, September 22, 2009

Anachoka sana!

Kaka Mbilinyi,
Asante sana kwa jinsi unavyotuelimisha kuhusu masuala ya ndoa na nyumba zetu, naomba msaada wa swali lifuatalo;

Ni kawaida mume wangu kulala usingizi wa kufa mtu mara tu baada ya kuwa mwili mmoja (sex) pia nimegundua kwamba nikisubiri au kupitisha siku kama 4 au 5 hivi angalau huwa ana pata nguvu (hachoki sana) ingawa baada ya kumaliza tu analala fofofo.
Je, anatatizo gani?

Dada asante kwa swali zuri na naamini inawezekana kushoka kwake nikutokana na sababu zifuatazo:
Kwanza huwa anakuwa amechoka na sex inasaidia kumfanya ajisikie relaxed na hatimaye usingizi mtamu (figuratively and literally).
Pili homoni zinazozalishwa baada ya kufika kileleni humwezesha kujisikia raha na amani ambayo hupelekea kulala usingizi wa uhakika, hii ina maana sex ni dawa ya kupata usingizi.

Tatu kitendo cha kutoa sperms huhitaji tension kubwa au hutengeneza mvutano mkubwa sana kwenye mwili ambao huhitaji nguvu nyingi kujipinda ili kutoa hizo risasi, na mwanaume hujikuta amechoka sana baada ya kutoa hizo risasi na hatimaye kulala usingizi.

Nne wapo wanaume (hata wanawake) muda wote wa kuwa mwili mmoja (harakati zote au shughuli nzima) hushika au hubana pumzi (hold), hiki kitendo husababisha kutopumua vizuri na husababisha kukosa oxygen (oxygen debt) mwilini kutokana na zoezi zima hivyo baada ya kumaliza hujikuta kiusingizi kinakuja chenyewe (sleepness)

Tano inawezekana huwa anakuwa amechoka sana na kazi anazofanya (fatigue) kabla ya sex hivyo kitendo cha kushiriki kuwa mwili mmoja hummaliza nguvu kabisa na mwili wake huwa unalia kilio cha kutaka kupumzika hivyo akimaliza tu analala fofofo, wataalamu wanasema tendo zima la sex moja ambalo wahusika hufika kileleni ni sawa na kukimbia kilomita 8, sasa kama kazini alikuwa amechoka, ukiongeza na hizo kilomita 8 si atachoka?

Sita wapo ambao wanaumwa na jambo la msingi ni kuchunguza na ukihisi kweli anaumwa mwone dakatari kwani anaweza kufia kifuani siku moja.

Jambo la ziada pia kama unaweza kabla ya kuwa mwili mmoja na mumeo hakikisha anapata kinywaji (siyo kilevi) ambacho kitaweza kumsisimua (stimulant) na kuwa tayari kwa sex kama vile Kahawa ambayo ina caffeine ambayo husababisha kuwa macho na hai na kuweza kushiriki tendo takatifu bila tatizo, jambo la msingi uwe mbunifu kuhakikisha kabla ya kuwa mwili mmoja anajua hajachoka na kama hajachoka basi ni kweli ataweza kukupeleke kwenye nchi ya ahadi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hapa

Sunday, September 20, 2009

HAZINA ILIYOFICHIKA

Je, unafahamu kwamba kisimi ni kiungo pekee katika mwili wa mwanamke (binadamu) ambacho kipo kwa ajili ya kumpa raha ya mapenzi (pleasure)?

Pia dunia imejigawa katika makundi matatu ya wanaume: wale wanaofahamu clitoris (kisimi, kinembe) kipo sehemu gani katika mwili wa mwanamke, wale wanaoendelea kutafuta kisimi kipo wapi katika mwili wa mwanamke na wale ambao hata hawajui ni kitu gani (hapa tunazungumzia wanaume ambao wapo kwenye ndoa na sivinginevyo).

Dunia inashangaza! Wewe mwambie mwanaume kuna hazina (gold) imegunduliwa chini ya bahari, atatumia mamilioni kuhakikisha anaifikia na kuipata. Mwambia kuna maji katika sayari ya Mars atafanya kila analoweza kwa kutumia technolojia kuhakikisha anafika huko kuyaona hayo maji.
Lakini mwanaume huyohuyo akiambiwa kwamba between the legs katika mwili wa mke wake kuna button ambayo ikibonyezwa (rubbed or licked) mwanamke anaweza kuijikuta yupo International Space Station linapokuja suala la kuwa mwili mmoja.

Kama mwanaume anashindwa kujua hii hazina iliyofichika na jinsi ya kuitumia kumpa raha mke wake, basi aelezwe kwani hapo ni mahali maalumu ambapo mwanaume lazima au awe na skills na uzoefu ambao utafanya mke wake ajisikie kweli ana mume ambaye anajua mahitaji yake ya mwili na ndoa pia.

Kufanya mapenzi kati ya mke na mume bila mke kusisimuliwa kisimi ni sawa na kuwapigia viziwi muziki wa ala nzuri.

Wanaume wengi wamakuwa ovyo linapokuja suala la kuwa mwili mmoja na mke wake kwa sababu wanashindwa ku-hit the right button akiwa na hardware ya mke wake hata kama anatumia software sahihi.

Mwaka 1976 Kuna ripoti iliyojulikana kama Kinsey; ilithibitisha kwamba mahali ambapo panaweza kumsaidia mwanamke kufika kileleni ni kuchezea clitoris hata hivyo mwaka 1976 Mwanamama Shere Hite aliwafannyia interview wanaume wengi kuwauliza Clitoris ni kitu gani majibu yalikuwa yanashangaza kwani wanaume wengi walikuwa hawajui ni kitu gani acha kwamba ni organ kwenye mwili wa mwanamke na mwingine alimjibu kwamba clitoris ni kitambaa cha kupigia deki.

Si wanaume tu ambao hawajui vizuri kuhusu hazina iliyofichika bali hata wanawake wenyewe hawajui uzuri wa hiyo hazina ni kama wanahazina ila hawajui na wanalalamika kwamba hawafurahii mapenzi na waume zao kumbe hata miili yao hawaijui inahazina kiasi gani na zinapatikana wapi.
Na kama wanawake wenyewe hawajui hazina iliyofichika ipo wapi, je wataweza vipi kumuelekeza mwingine kuichunguza na kuitumia?
Kama ni mwanamke basi zingatia yafuatayo:
Kila jambo huanza kwa kujifahamu kwanza hivyo kama hujajijua una hazina ya aina gani unaweza kujichunguza kwanza na kuipenda kwa kuwa hapo ndipo iliyohazina ya furaha ya mapenzi na mume wako.
Chukua kioo then jiangalia, feel it!
Uwe na mazoea ya kuweza kutamka neno kisimi, kinembe au clitoris kwa uwazi na usiwe na aibu kwani kuwa na aibu ndiyo kunafanya hata ukiwa na mume wako usimwambie kwamba furaha yako inaanzia kwenye hazina iliyofichika.
Acha kudanganya kwamba umefika kileleni (faking orgasm) kumbe unamfunga kamba mume wakona pia ni kutokuwa na adabu kwa kisimi chako.

Muulize mume wako kama atafurahia mahaba bila wewe kugusa stick (uume) wake, ukweli atasema hapana na wewe mwambia bila yeye kwenda kwenye hazina iliyofichika basi hutaridhika na kama anashindwa kukipata usimruhusu kwenda sehemu yoyote ya mwili wako hadi afanikiwe hahahah!

Au kwa maelezo zaidi kuhusu hii hazina iliyofichika soma hapa na ukiwa na time soma hapa tena

Saturday, September 19, 2009

Inaamua yenyewe!

Kaka Mbilinyi,
Asante kwa jinsi unavyojitahidi kutuelimisha kuhusiana na masuala ya ndoa. Mapenzi, uchumba, familia na mahusiano kwa ujumla, katika kupitia baadhi ya majibu ya maswali yameulizwa hapa nami nikaona niulize swali langu.
Nina tatizo la kuwahi kumaliza (ejaculation) au kukojoa mapema nikiwa na wife wangu, yaani ile kugusa na kuingiza hata kabla sijafika popote najikuta nimemaliza bila kupenda, pia nahisi mke wangu haridhiki inavyotakiwa na nimejitahidi kuhakikisha nakuwa na romance au foreplay ya uhakika lakini likija suala la stick kuiingiza pale mahali, inanizidi ujanja na kufanya yale sijaituma!
Nifanyeje?

Asante sana kwa swali zuri ambalo wanaume wengi duniani wanakumbana nalo na wanawake wengi wamejikuta wanakatishwa tamaa na kujiona matarajio yao yanayeyuka kama barafu wakati wa jua kali pale Buguruni.

Kwa maelezo zaidi soma kwanza hapa pia ukipata muda zaidi soma hapa na kwa nyongeza malizia kwa kusoma hapa kwani nilishajadili kwa undani kabisa.
Weekend Njema!

Friday, September 18, 2009

"A happy marriage has in it all the pleasures of friendships, all the enjoyment of sense and reason - and indeed all the sweets of life".
- Joseph Addison

Thursday, September 17, 2009

Kipi bora?

Hello kaka Mbilinyi,
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 25 naishi Dar es Salaam, Kumetokea ubishi mzito kijiweni kwetu kutaka kujua kama kuna kimoja ni muhimu kuliko kingine kati ya SEX au USINGIZI?

Kaka nashukuru kwa swali ambalo naamini bado ni kitendawili kwani linahusu watu wote na watu tunatofautiana kile tunapenda.
suala la sex na usingizi ni preference ya mtu kwani mwingine sex ni muhimu kuliko kulala usingizi na mwingine kulala usingizi ni muhimu zaidi kuliko sex na mwingine hajali iwe usingizi twende au sex twende hana shida.

Kuna baadhi ya watu hawawezi kufurahia sex kama wamechoka au kama hawajalala usingizi, hii ina maana kulala usingizi kwao ni jambo la msingi kwanza, wapo wengine (hasa wanaume siyo wote) hata kama amechoka na ana usingizi kwake sex kwanza na baadae kulala usingizi, kwanza hata kama amelala anaota sex na kuwaza sex kama huamini tafuta au uliza wanawake 5 tu walioolewa kama kuna siku walikubaliana na mume wake walale kwani mwanamke anajisikia amechoka lakini usiku wa maneno mwanaume akamng’ang’ania kuwa mwili mmoja.

Na kuna kundi la watu wengine hufanya sex huku wapo usingizini iwe usiku wa manane au asubuhi kwani ndoto zao huwafanya kuwa active na kuenjoy sex as if wapo macho.
Na kuna documentation nyingi zinaonesha wapo ambao hufanya sex huku wapo usingizini na kwa utendaji wa hali ya juu na skills za uhakika ingawa wakiulizwa asubuhi ilikuwaje usiku wanaruka mita mia.

Ni vizuri kuwa na muda mzuri wa kupumzika (kulala usingizi) kwani usingizi hupunguza stress, kubalance uzito, magonjwa ya moyo, depression nk.
Hata hivyo faidi za sex wengi wanaziruka kuna articles nyingi tu na research paper nyingi zinaelezea faida za sex kama vile kupunguza maumivu ya kichwa, kuwaweka wanandoa emotionally closer ingawa kulala usingizi ndiko kunapewa headlines nyingi sana kwenye media kwa sababu usingizi ni muhimu kwa survival ya binadamu.

Naamini furaha, na healthy sex ni kitu cha msingi sana kwa personal satisfaction ya mwanandoa hata hivyo pata usingizi wa kutosha ili uwe na energy ya kupata sex ambayo itakufanya uridhike.

Ukitaka kusoma zaidi kuhusu faida za tendo la ndoa bonyeza hapa
Siku njema!

Wednesday, September 16, 2009

Sipendi kabisa sasa hivi......

Nina jipya lakini sipendi kuendesha!SWALI:
Kaka samahani kwa usumbufu naomba unisaidie swali langu:
Mimi mwanamke ambaye ni mwanandoa mpya kabisa na ndoa yetu ina miezi saba sasa.
Nampenda sana mume wangu hata hivyo nachukia sana kufanya sex kwani sijisikii chochote mume wangu akiwa ndani yangu.

Wote tulikuwa mabikira kabla ya kuoana hivyo naamini tatizo ni jinsi anavyofanya (move) ndani yangu (uke) kwani akiwa ndani yangu husugua polepole (so slow) na kusimama mara kwa mara bila kunisugua kwa uhakika.
Akinigusa clitoris yangu huwa najisikia kusisimka na raha zaidi lakini hafanyi chochote.
Nikiwauliza rafiki zangu wananiambia mume wangu ni bad lover kitu ambacho sikubaliana nacho kwani ukiacha sex mambo mengine ni shwari kabisa.

Nahisi kupoteza mood kabisa kwa hili tendo takatifu.
Je, nifanyeje ili mume wangu awe ananifanya ninavyotaka na kutamani na pia nitapataje mood na kuweza kufurahia ndoa yangu (sex)?

JIBU:
Dada inaonekana tangu mwanzo wa mahusiano yenu (uchumba) mlikuwa hamuongei masuala muhimu kama matarajio yako kuhusu sex na inawezekana ulidhani ukiolewa utaweza kuongea bila shida, hata hivyo umejikuta unaona ni ngumu kuongea masuala ya sex na mume wako.

Njia bora ni wewe kukaa na mume wako na kuongea wazi na kwa upendo bila kukefyakefya wala kulalamika.
Mwambie kile unapenda akufanyie na kinakufanya ujisikia raha na hatimaye kufurahia tendo la ndoa.
Inawezekana huwa anakuwa slow na haendi kwa speed kwa kuogopa kumaliza mapema hivyo mwambie wewe hutajali kama atafanya unavyotoka hata kama atamaliza mapema, wewe mhakikishie kwamba unamfurahia na unapenda iwe hivyo.
Sasa hapo hapo ulipo kabla hujamalizia kusoma hadi mwisho, chukua simu yako ya mkononi mwandikie message (sms) kwamba baadae una kitu kizuri unataka kumwambia hivyo mkifika nyumbani akukumbushe.

Huruhusiwi kuendelea kusoma kama hujatuma hivyo message au kumpigia simu kwani kutofanya hivyo ni kiburi na dhambi kama dhambi zingine, sitanii!

Pia njia nyingine ni wewe kuwa mjanja kumuomba mtumie milalo tofauti ambayo wewe ndo Utakuwa rubani wa airbus na kujihakikishia inapaa apende asipende.
Kwa mfano wewe mwanamke kuwa juu na yeye chini, kwa mlalo huu wewe mwanamke ndiye Utakuwa una control thrusting (speed, depth, angle nk) na masuala ya kuwahi kumaliza atajijua mwenyewe.
Pia kwa wewe kuwa juu anaweza kuendelea kuhudumia clitoris yako kwa kuipa stimulation kwa kutumia vidole au kidole huku wewe ukiendelea na rock and roll mbele na nyumba juu na chini.
Kwa njia hii unaweza kuimarisha excitement kwenye suala la mapenzi na kukuwezesha kufika kileleni haraka na kukupa mood zaidi ili kesho uhitaji zaidi.

Pia si vizuri kuombe ushauri kwa kila anayeitwa rafiki kwani rafiki ni wachache ila wanafiki ndo wengi na wengine wanamtaka huyo mumeo hivyo mlinde na mtunze na zaidi fanya kila mnaloweza kuhakikisha maisha yenu ya sex yanakuwa ya kuridhisha kwani kwa njia hiyo utajisikia ndoa yako inaridhisha.

Usikubali shetani aje kulala kitandani kwenu, mfukuze kwa maombi na pia kwa wewe kujifunza na kuongeza efforts kuwa innovative na creative idara zote hapo nyumbani.

Naamini kwa tips hizo unaweza kutatua tatizo lako, unaweza kuniuliza tena
Kama unaweza pitia posts za huko nyumba ambazo naamini zinaweza kukusaidia zaidi kuhakikisha maisha yako ya ndoa yanakupa kuridhika.
Ubarikiwe na Bwana!

Kila mmoja ni tofauti

Mimi ni mwanaume ambaye nimeoa na nina miaka 3 kwenye ndoa, nimegundua kwamba mke wangu sehemu zake za siri zina umbo tofauti kwa maana kwamba mashavu ya ndani ya uke (kingereza wanaita labia minora) zimejitokeza na zina hang nje kwa urefu wa zaidi ya kama sentimita 2 kiasi cha kuzidi vulva na pia clitoris ni kubwa na hujitokeza na kuoneka wazi hata kabla ya kusisimka.
Jambo kubwa zaidi ni kwamba anapokuwa anaoga sehemu zake za siri hufanya vibration kama vile kumeshikwa na shock ya umeme.

Je, kwa nini hizi genitals zake hufanya vibration wakati hata hazijasisimuliwa mfano wakati anaoga?

Je, hii ni kawaida kwa mwanamke?
Nimekuwa naogopa kumuuliza uso kwa uso na pia inanichanganya sana,
nisaidie.

Asante sana kwa swali zuri ambalo ni mara ya kwanza kuulizwa hapa The Hill of Wealth.

Wanawake wote hutofautiana sana katika size, shape, rangi na texture ya maumbo ya miili yao kama vile matiti, makalio, miguu, nywele, vitovu, na sehemu za siri.
Linapokuja suala la sehemu za siri jinsi kunavyoonekana kwa nje anaweza kuwa vulva au labia zilizojitokeza zaidi au kuwa flat.
Jambo la msingi ni kwamba ni jambo la kawaida kuwa hivyo na si ugonjwa bali ni fahari ya mwanamke kuwa na ladha tofauti katika mwonekano wa natural spring water yake ili mume ukinjwa maji uridhike.

Pia clitoris hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine ukianza na wale ambao hakionekani kabisa hadi wale ambao huweza kuonekana.
Na kama mwanamke ananyanyua vyuma na kutumia madawa ya testosterone ukiona kisimi chake unaweza kukimbia ukadhani ni mwanaume mwenzako kwani hukua na kujitokeza kama stick ya mwanaume.

Kama wanaume walivyo na sticks tofauti zingine zimepinda na zingine zimenyoka na zingine ni fupi na zingine ni ndefu wakati zingine ni nyembamba na zingine ni nene, wanawake nao wanatofautiana.

Pia suala la sehemu za siri kutetemeka kwa kushtuka kama shock ya umeme ni jambo la kawaida kwani hiyo ni involuntary action jinsi ngozi yake inavyofanya response katika mazingira tofauti (kumbuka biology ya form two).
Ni kawaida ngozi kutetemeka hata sehemu zingine za mwili.

Kuna kitabu kimoja kimeandika na Paul Joannides chenye title “Guide to getting it on” kama unaweza kukipata kwani kinaelezea vizuri masuala au shape na size za vulva na clitoris kwa wanawake na ukisoma basi utajua mke wako hana tatizo lolote.

Kama mke wakoo analalamika kutokana na hayo maumbile unaweza kuongea naye na kwenda kumuona daktari aliyekaribu na wewe otherwise haina haja kuogopa na kuchanganyikiwa na badala yake endelea kujienjoy na wife kwani hakuna tatizo lolote.
Ubarikiwe!

Je, naweza kuongeza size?

Unaweza kuongeza size ya nyumba si ........... Kaka Mbilinyi naomba kujua hivi ninawezaje kuongeza size ya uume wangu ili nimfurahishe vizuri mke wangu kwani uume wangu naamini ni mfupi sana na haumfikishi mke wangu pale anahitaji kufika.

Asante kwa swali zuri hata hivyo hili swali limeshaulizwa mara nyingi hapa na kwa ufupi huwezi kuongeza urefu wa stick yako kwenda size yoyote, size na shape ya uume wako ni kitu ambacho kimeamuriwa genetically.

Pia kumbuka kama tunazungumzia sanaa ya mapenzi (sex) kuwa na stick ndefu au kubwa hakuwezi kumfanya mke wako kuwa happy bali jinsi na namna unavyotumia kwa ujuzi wako hiyo stick mkiwa kitandani ndicho kina make the difference.

Hivyo kama unataka kumfurahisha mke wako kitandani focus kwenye love techniques siyo size ya stick yako.

Pia kama kuna binadamu angegundua dawa halisi ya kuongeza urefu basi hata Bill Gates asingeona ndani kiutajiri maana wanaume wengi tu wangehitaji hiyo software ili warekebishe hardware zao.
Usidanganywe na media!
Linapokuja suala la sex kinachotakiwa ni skills & techniques siyo tool

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Ni nyuzi 45, nifanyeje?

Kaka Mbilinyi Shaloam!
Mimi ni kijana wa kiume wa miaka 20 na napenda kujua kwani tangu nimebarehe nimejikuta uume wangu umepinda nyuzi 45.
Je, hii inaweza kuniletea matatizo wakati wa tendo la ndoa kwa mke wangu nitakapooa?
Je, kuna matatizo yoyote nitakutana nayo wakati wa kuwa mwili mmoja na mwenzi wangu?
Please nisaidie!

Mdogo wangu,
Asante sana kwa kuuliza swali ambalo naamini si wewe peke yako umejikuta stick inayumba nyuzi kadhaa ingawa yako kweli inabidi ujiulize maana nyuzi 45 si haba.

Uume kupinda kwa angle fulani ni jambo la kawaida na haiwezi kuleta madhara yoyote wakati wa kuwa mwili mmoja na mwenzi wako.

Hata hivyo Siwezi kutoa uamuzi wa jumla kwako kwamba stick yako ipo shwari kwani kupinda nyuzi 45 ni angle kali kidogo na kwa kuwa hakuna vipimo vimefanyika sitaweza kukupa uhakika asilimia mia kwamba kila kitu kipo sahihi.
Kama unaweza nenda kwa daktari anayehusika na masuala ya urology ambaye anaweza kupima hiyo angle wakati umesisimka na kawaida ili aweza kupima kama kuna condition yoyote ya tofauti na anaweza kukushauri kitaalamu zaidi na mapema kabla hujamwingiza bibie ndani ya nyuma ukaanza kushiriki mwili mmoja huku unaficha stick au kung’ang’ania iwe giza kila wakati mkiwa faragha na yeye anataka kuiona siyo kupapasa.
Je, hujisikii maumivu hasa uume ukisimama? kwani kupinda kwa uume kama hiyo angle 45 ni moja ya dalili ya penile fracture.
Hivyo mwone daktari haraka iwezekanavyo!

Tuesday, September 15, 2009

Unadanganya hadi kisimani kunywa maji!

SWALI:
Mimi ni mwanamke na nipo kwenye ndoa kwa miaka 4 sasa na nimekuwa bingwa wa kudanganya kwamba nimefika kileleni (fake orgasm).
Tadhari napenda kujua hivi ni kitu gani huweza kusababisha mwanamke kufika kileleni, Ukiacha oral sex?
Je, uume unatakiwa kugusa spot au angle gani kwenye uke ili mwanamke kufika kileleni?
Au niseme nini kitaweza kunisisimua ili nifike kileleni?

JIBU:
Kwanza asante kwa kuulizwa swali la msingi ambalo wanawake wengi hupitia kwa maana kwamba huwa wanawafunga kamba waume zao kwamba wamefika kileleni kumbe ni hakuna lolote.

Tukirudi kwenye swali lako, ukweli ni kwamba kinachomfanya mwanamke mmoja afike kileleni kinaweza kuwa tofauti na mwanamke mwingine kwani kila mwanamke yupo tofauti katika mwitikio wa mapenzi (sex) na hata mwanamke mmoja huwa na tofauti ya mwitikio wa mapenzi kwa siku tofauti katika mwezi mmoja.

Wanawake wote ni tofauti kimwitikio linapokuja suala la kusisimka hadi kufika kileleni, kuna mwingine ukigusa chuchu tu anasisimka, mwingine atakwambia anaumia na kuna mwingine akichezewa vizuri kisimi husisimka mwingine hapana nk.

Ku-fake kufika kileleni huonekana kama wazo zuri katika kumfanya mume wako ajione amefanya kazi ya uhakika, hata hivyo haina maana yoyote katika kuwahakikishia mnakuwa na great sex maana mwisho wa siku wewe ndo unapunjwa.

Ni kama huwa unajenga matarajio hewa ndo maana hujajua nini kinaweza kukufanya ufike kileleni kiukweli.

Jambo la kwanza ambalo unaweza kufanya ni kwanza kuutambua mwili wako au kujua nini kinakusisimua au ni wapi unasisimuka na kunakupa raha ambayo inaweza kukupelekea kufika kileleni ukiwa na mume wako.
Hii ni pamoja na kumsaidia mume wako ajue kitu gani akikufanyia wewe kinakufikisha na kukupa raha ya kukufikisha kileleni au ndege kupaa hewani.

Ukiwa na mume wako akufanyie experiments nyingi sana kwa kuanza na milalo tofauti (sexual position), kukugusa sehemu zote unazosisimka kama clitoris, vulva, nje ya uke, ndani ya uke na mwili mzima tena kwa ujuzi wa kila aina huku ukiwa wazi kwa upendo na kutiana moyo.

pia inaonekana unaamini kwamba oral sex ndiyo ticket pekee ya mwanamke kufika kileleni, hii si kweli kwani kuna wanawake wanapenda sana na kuna wengine huona ni kitu kigumu kama kulipa kodi, kama kwako is fine, it is ok.

Jambo la msingi ni wewe kupenda kufanya kile unapenda na si kile unasikia wengine wanafanya kwani kila mtu ana ladha yake linapokuja suala la mapenzi hasa kutokana na background na tamaduni na malezi.
Tutaendelea.......................

Saturday, September 12, 2009

When a man opens the car door for his wife, it's either a new car or a new wife.
~Prince Philip

Friday, September 11, 2009

Maswali ya kujiuliza kabla ya kuoa au kuolewa - 2

Kabla hujaanza kujenga mnara, fikiria gharama kwanza......... Swali la nne:
Je, unajua mtazamo wa mwenzako kuhusu sex?
Je,anapenda na kujiona atafurahia sex?
Je, mnaweza kuongelea kwa uwazi na uhuru kuhusu sex kwa pamoja wawili bila kuogopa au kukiri kwamba tuache tutaongea tukiwa tumeoana?
Je, unategemea sex iweje au unahitaji kiasi gani?
Kila siku au mara moja kwa mwezi inatosha?
Je, ni vitu gani unategemea kufanya kuhusiana na sex?
Je, ni vitu gani vinavyohusu sex unaamini unatajisikia uncomfortable?
Kama ndiyo je, ni vitu gani? Be specific!
Je, partner wangu ananivutia kimapenzi kwa kadri ninavyotegemea?

Wanawake mara nyingi hujikuta wanakuwa waoga sana kujadili topic ya sex, au maandalizi ya kufanya mapenzi (forepaly) au sex position n.k hata hivyo kuruka hiki Kipengele kuna matatizo yake kwa future ya wanandoa.
Kama mnashindwa kuongea kuhusu sex sasa kitu gani kitawafanya muweze kuongea mkioana.
Kutegemea mke au mume kusoma your mind inaweza kupelekea kwenye maluweluwe ya kutisha.

Swali la tano:
Je, linapokuja suala la pesa wewe ni mtumiaji au mtunzaji pesa?
Je, nini malengo yako kifedha?
Je, mkioana mtakuwa na joint account au kila mtu yake?
Na nani atakuwa na jukumu la kuhakikisha kila bills zinalipwa?
Na je kila mmoja anaingia kwenye ndoa akiwa na deni kiasi gani huko Bank?
Matatizo kuhusu pesa ni moja na migogoro sugu katika ndoa na kuna umuhimu sana kujua au kuwasiliana vizuri masuala la pesa kabla ya kuoana na kuanza kuzozana kila kukicha.

Swali la sita :
Je, kuna tatizo lolote kwenye mahusiano yenu ambalo kila mmoja anahisi ni vizuri kulimaliza kabla ya kuoana.
Je, umeshamweleza mwenzako vitu ambavyo hutavivumilia kabisa katika ndoa yenu au vitu ambavyo utavikubali?
Kwanza unatakiwa kujua kwamba tofauti katika ndoa haziwezi kukwepeka hivyo jinsi ninyi wawili mnavyohusika kupambana na tofauti kwa upendo na kuheshimiana tangu mwanzo inaonesha ndoa yenu itakuwa na furaha au karaha.

Swali la saba :
Je, unahitaji watoto?
Lini na wangapi?
Je, partner wako anahitaji watoto na kama ndiyo lini na wangapi?
Na je, wote mnakubaliana na njia za kulea watoto?
Isije mwingine anataka watoto na mwingine hataki au mwingine anataka watoto wawili na mwingine anataka timu zima ya soka.

Swali la nane:
Je. Mume wako mtarajiwa au mke wako mtarajiwa yupo upande wako kuhusiana na tatizo lolote kutoka kwa ndugu zake?
Au mama yake akiongea au baba yake akiongea kitu chochote anafyata mkia na anawasilikiza hata kama hicho kitu hapendi na wewe hupendi?
Je, wazazi wana uwezo gani kuamua kuhusu mambo yenu?
Suala la wakwe, marafiki na ndugu lina umuhimu wake katika ndoa.
Usiingie ukiamini kwamba ukioa au kuolewa ndo utajitahidi kubadilisha mtazamo ili kila kitu kiwe kama wewe unavyotoka.

Swali la tisa:
Je, dini au suala la imani ni muhimu sana katika maisha yako?
Je, mpenzi wako yeye anaaamini nini au yupo dini gani na nini matarajio yenu baada ya kuoana?
Unahitaji kufikiria mbaliza zaidi kwani itakuwa ngumu sana kuwa na watoto wenye wazazi wenye mitazamo tofauti ya dini zao.

Swali la kumi :
Je, linapokuja suala la mahusiano na mpenzi wako unajisikiaje?
Je, wewe ni mzuri kuongea au kusikiliza, na je wewe na mpezi wako kila mmoja anajisikiaje kuhusu maneno mwenzake anatumia kuongea, iwe utani au ukali?
Je, wewe huwa unajieleza vipi ukikasirika au kukatishwa tamaa? Na yeye je?
Je, huwa unapenda kukaa kimya ukiona kunaweza kuzuka mgogoro au huwa anaamua kuongea kwa sauti na matusi juu? Na yeye je?
Au una tabia na kubabiza milango au kuvunja vitu kama kutupa simu ya mkononi ukikasirika na yeye je?
Jinsi mnavyowasiliana kuna matokeo makubwa sana kuhusu ndoa mnaenda kuitengeneza.
Kuwa na communication skills nzuri au kujenga tabia ya kuwa na mawasiliano mazuri ni jambo la msingi sana.

Bottom line ni kwamba jinsi wewe na partner wako mnavyojihusisha wakati wa good times na bad times huweza kuelezea ndoa yenu na ni muhimu sana kuwa tayari kujibu baadhi ya maswali muhimu kama hayo nimeyaweka hapo juu kabla ya kukubali kuoana hadi kifo kitakapowatenganisha.
Kumbuka ndoa ni shimo ambalo ukiingia hakuna kutoka hadi kifo!

Maswali Muhimu kabla ya kuoa na kuolewa

Kabla ya kukiri “Hadi kifo kitakapotutengenisha” au hata kabla ya kukubali kuvishwa pete ya engagement kuna maswali muhimu sana (hard questions) ambayo unahitaji kujiuliza na kwa njia hiyo unaweza kujua success au failure ya mahusiano ya ndoa pengine hata kabla ndoa haijafika popote.

Kujiuliza mwenyewe na kumuuliza yule unategemea kuoana naye maswali ya msingi kabla ya kuoa au kuinvest upendo wako itasaidia wewe kufahamu kama umempata mtu sahihi na pia kuweza kuondoa matatizo ya kawaida ambayo wengi hupelekea kuachana.

Chukua muda (honestly) kufanya evaluation jinsi unavyojisikia (feelings) na motivations kwa ajili ya wewe kuoa au kuolewa.
Ni vizuri kupata majibu ya maswali kabla hujaoana naye ili kuweza kushughulikia matatizo hayo kabla ya ndoa kuanza.

Kuna maeneo muhimu sana katika ndoa ambayo bila kuyafahamu na kuingia kichwa kichwa hakuna wa kumlilia isipokuwa wewe mwenyewe na suala la ndoa ni suala sensitive sana ukishindwa (achana) utapata label ambayo utaibeba maisha yako yote hapa duniani na pia unaweza kuathiri maisha ya wengine.

Swali la kwanza
Je, ni kweli tunapendana?
Je, ni kweli ninampenda Mwenzangu hata miaka 30 ijayo?
Ni kitu gani au sifa zipi zinanifanya nimpende?
Uwe mkweli.
Unahitaji kufahamu na kujisikia ni kweli unampenda mwenzako isije kuwa ni tamaa tu.
Upendo huanza kidogokidogo na hutokea kwa kumpenda mtu mzima kama alivyo awe ana pesa au hana pesa pia siyo kumpendakama wewe unavyotaka awe.
Kumbuka mke au mume si kipande cha udongo wa mfinyanzi kwamba utamefinyanga kwa kadri unavyotaka wewe.

Swali la pili:
Kwa nini tunaoana?
Kwa nini namhitaji huyu mtu kuoana naye?
Je, ni kwa sababu ninataka mtoto?
Kwa sababu ninataka hela zake au najisikia upweke upweke, au nataka sex au nataka kuondokana na kero za mama au wazazi?
Au naona nachelewa kuolewa/kuoa au rafiki zangu wananisema sana au na mimi nionekane nimeoa au kuolewa?
Kuoa au kuolewa kwa sababu za ajabu ajabu huweza kukufikisha mahali ambapo utajikuta upo disappointed, frustrated na hatimaye kuachana.
Oa au olewa kwa sababu ni wakati wake.

Swali la tatu:
Je, ni nini matarajio ya ndoa yangu?
Je, umeshajiandaa na kila kitu kuhusu ndoa?
Matarajio mtu anaingia nayo kwenye ndoa huweza kujenga au kuharibu ndoa.
Kuna baadhi ya imani potofu kuhusu ndoa unatakiwa kuzifahamu hata kabla hujaingia kwenye ndoa.
Kuamini kwamba ukiolewa basi mwenzako anatakiwa kukufanya happy si kweli, furaha unayo wewe kwanza.
Kufikiria kwamba eti mume/mke ataweza kusoma mind yako si kweli unahitaji kueleza kile unataka siyo kubaki kimya eti anajua.
Kuamini kwamba ukioa au kuolewa basi kila kitu mtafanya pamoja si kweli kila mtu ana interest zake.
Na kutaka kuwa na ndoa unayotaka wewe badala ya wote kwa pamoja unaweza kujikuta kwenye total disappointment.

"Truly loving another means letting go of all expectations.
It means full acceptance, even celebration of another's personhood."
-Karen Casey

Tutaendelea kesho….

Thursday, September 10, 2009

Usichafue loo!

Kama nyundo, kuzozana mara kwa mara ni kugongagonga, hutikisika na siku hudondoka chini!
Jinsi ya kuzuia kuzozana kusichafue (contaminate) ndoa yako
Kuzozana mara kwa mara katika ndoa huweza kusababisha contamination ya mahusiano hasa ndoa.

Kama wewe na mwenzi wako mmejikuta mara kwa mara mnakuwa na mzozo wa maneno, vita ya maneno, kubishana kusikoisha kwa kila kitu, kila mmoja kumfokea mwenzake, kuzozana pengine siku mbili mfululizo au wiki basi inabidi mfahamu kwamba hicho kitendo hakileti afya yoyote katika mahusiano yenu na bila kubadilika basi mnaweza kujikuta mmechimba shimo ambalo kutoka itakuwa ngumu sana.

Kuzozana hujitokeza pale mtu anakuwa frustrated na kile alikuwa anategemea mwenzake afanye, pia kuna wengine wamezaliwa mazingira ambayo bila kipigishana kelele za mizozo bado maisha kwao hayana ladha, inawezekana wapo sahihi kwamba kukisema kile kipo moyoni (gubu au donge) ni muhimu hata hivyo kutoa donge lako moyoni kwa sauti ya juu (kelele) kwa kulaumu na kimashtaka ni kuonesha something is wrong in you.

Tunaweza kuwa frustrated mara kwa mara katika mahusiano lakini hakuna sababu kwa nini tunashindwa kuwasiliana vizuri na kwa kila mmoja kuwa na respect kwa mwenzake.

Kuna msemo kwamba “It takes two to tango, and it takes two to argue”.
Ikiwezekana hakikisha unawasiliana vizuri na kumpa heshima partner wako wakati unatoa lile unahisi linaumiza moyo wako kama ifuatavyo:
Unapoongea usiongee kwa sauti kubwa (kelele hadi majirani wanaanza “kusema hao wameenza!”).
Wala usimlaumu mwenzako (shambulia tatizo usimshambulie partner wako).
Usimnyoshee vidole au kutoa mashitaka (tumia hekima kuelezea kile kinakuumiza kumbuka ndoa ni sisi siyo wewe au mimi).
Usiape (swear) au kumbandika tabia ya kudumu (kila siku upo hivyo!).
Usiingize irrelevant issues ambazo hazihusiki na mzozo uliopo.

Kama wote mtakuwa makini kuhakikisha unafanyia kazi hizo rules hata kama mmoja wenu atakumbuka itasaidia kuwa na solution ya kutengeneza ndoa yenye afya.

Ni vibaya sana kuwa na mtazamo negative kwa partner wako hasa kunapotokea tofauti yoyote, hakuna wakati muhimu kama kutumia maneno sahihi na kuwa makini na namna unawakilisha kitu ambacho hujapendezwa na mwenzi wako kwani kwa maneno tunabariki na kwa maneno tunalaani na kuna maneno yakitamkwa basi huingia kwenye moyo wa mwenzi wako na kuweza kubadilisha mwelekeo wa ndoa vizuri au vibaya.

Kumbuka kumpenda mpenzi wako hata wakati wa mzozo ni jambo la maana kuliko sadaka.

"Truly loving another means letting go of all expectations.
It means full acceptance, even celebration of another's personhood."
-Karen Casey

Wednesday, September 9, 2009

Ni Binti

Karen-Jody Mbilinyi Wapendwa wasomaji wa blog hii, kwanza napenda kuomba msamaha kwa kutokuwa hewani kwa muda wa wiki mbili.

Pia napenda kuwashukuru kwa maombi yenu na pia wale wambao waliweza hata kutuma ujumbe kuulizia imekuwaje hata hivyo nimerudi tena baada ya kumaliza jukumu kubwa la kuhakikisha mke wangu mpenzi anajifungua mtoto na tunashukuru Mungu kila kitu kilienda salama kabisa.

Hata kama alipitisha wiki mbili kutokana na tarehe ambayo alitakiwa kujifungua bado Mungu alikuwa mwema kwani Jumatano tarehe 2 mwezi Septemba saa kumi na mbili na dakika hamsini na mbili katika hospitali ya Mkoa (Pembroke) Ontario – Canada Mungu alitupa zawadi ya mtoto wa kike aitwaye Karen-Jody (Greek-Hebrew name – pure praise of God).


Hata baada ya siku 5 ukuaji wako unaridhisha

Ufanisi wa kazi yako kama nesi wa zamu ulitufanya kujisikia tupo mahali salama.

Kama baba ilikuwa furaha na kumshukuru Mungu kushika mtoto dakika chache baada ya kuzaliwa

Dada Jody; jinsi ulivyohusika tangu siku ya kwanza kuhakikisha tunapata daktari anayefaa kwetu ni furaha na heshima kwako.
Dada Jennifer; maombi yako na maneno yako ya kumtia moyo Gloria ilikuwa kazi njema hadi anajifungua salama,
Emmanuel; hongera kwa kupata dada!
Gloria; nakupongeza sana kwa jinsi ulivyo mvumilivu na imara hasa kuvumilia uchungu wa masaa zaidi ya sita. Ilikuwa na mara yangu ya kwanza kuwepo uso kwa uso wodini kusaidiana na manesi na marafiki na ndugu kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Jambo kubwa nililojifunza kwa kuwepo kwangu wakati mtoto anazaliwa ni jinsi Mungu alivyowabariki wanawake huu uwezo na kuvumilia maumivu na uchungu wa kazaa acha ile ya kubeba mimba kwa miezi 9.

Napenda kuwapongeza wanawake mahali popote uwe umezaa au bado kwa kweli kuwa mwanamke ni heshima na wanaume tunahitahi kuwajali, kuwapenda na kuwalinda na adui wa aina yoyote na zaidi kuwapa kile mnahitaji katika mahusiano yetu kwani ninyi ni viumbe wa thamani sana kutokana na nguvu ya uumbaji ambayo Mungu amewapo ndani yenu.
Sasa nimerudi ninayo mambo mengi sana ya kujadiliana pamoja na kujifunza na wewe kuhusu ndoa, mahusiano na maisha kwa ujumla hivyo karibu sana
Tunawashukuru wote kwa maombi yenu na Mungu awabariki sana!

Saturday, September 5, 2009

Dawa ya Mama Mkwe!

Hapo zamani za kale huko China, Binti aitwaye Li-Li aliolewa, yeye na mume wake wakaenda kuishi kwa mama wa mume wake yaani mama mkwe.
Kwa muda mfupi tu walioishi Li-Li aligundua kwamba yeye na mama mkwe hawaendani kabisa, walitofautiana kwa kila kitu na Li-Li alikasirishwa sana na tabia za mama mkwe wake kwani mama mkwe alikuwa anamlaumu (criticize) muda wote.

Siku zilipitia, wiki zikapita na miezi ikapita kila siku Li-Li na mama mkwe ni kuzozana na kushambuliana, kibaya zaidi ni kwamba kutokana na traditions za Uchina ilimpasa Li-Li kumpigia goti kila lile ambalo mama mkwe alihitaji afanye na ukweli hali mbaya ya mahusiano kati ya Li-Li na mama mkwe ilimfanya hata mume wake Li-Li kujisikia vibaya sana.

Mwisho Li-Li hakuweza tena kuvumilia tabia mbaya na utawala wa imla wa mama mkwe hivyo akaamue kufanya kitu, hivyo akafunga safari kwa rafiki wa baba yake ambaye alikuwa anaitwa Mzee Huang ambaye alikuwa anauza dawa za kienyeji (herbs).
Alipofika kwa mzee Huang akamweleza yote anayokutana nayo na kwamba anaomba msaada kama anaweza kumpa sumu ili aweze kumuua yule mama mkwe na kuondokana na lile tatizo milele (once and for all)

Mzee Huang akafikiria kwa muda na mwisho akamwambia Li-Li atamsaidia kulimaliza tatizo lake ingawa Li-Li alitakiwa kusikiliza kwa makini na kutii kile ataambiwa akafanye.

Na Li-Li naye kwa furaha akajibu kwamba nitafanya chochote utaniambia nifanye.
Ndipo Mzee Huang akaingia ndani na kutoka na mfuko uliosheheni dawa (herbs) na akaanza kumpa maelezo Li-Li:
"Huwezi kutumia sumu ya haraka kumuua mama mkwe wako kwani kila mmoja atakutilia mashaka (suspicious) wewe hivyo nimekupa kiasi cha kutosha cha dawa (herbs) ambayo itatumika kidogo kidogo na kujenga sumu ya kutosha na hatimaye kumaliza.
Hivyo kila siku tengeneza mlo safi na weka dawa kidogo kwenye hicho chakula.
Sasa, ili kila mtu asikutilie mashaka wewe hasa akifa lazima uwe makini sana kujifanya rafiki kwake, usibishane naye na kubali chochote anakwambia na umuhudumie kama vile ni malkia, si unajua ipo siku atapotea kabisa”.

Li-Li alikuwa na furaha ya ajabu, akamshukuru mzee Huang na akaenda nyumbani kuanza shughuli ya kumuua mama mkwe wake.

Miezi ikapita, wiki zikapita na siku zikapita, Li-Li aliendelea kumpa mama mkwe chakula chenye ile sumu na alikuwa anakumbuka sana jinsi Mzee Huang alivyokuwa amemweleza jinsi ya kuepuka kutiliwa mashaka, hivyo aliweza kujizua hasira zake na alimtii mama mkwe kwa kila kitu na alimhudumia kama mama yake mzazi (malkia)

Baada ya miezi sita, nyumba nzima ilibadilika baada ya Li-Li kuweza kizishinda hasira zake kwa mama mkwe na kumtii na wakajikuta hawagombani tena na hawakuweza kuzozana au kubishana kwa miezi sita mfululizo na wakajikuta wanaelewana na kuishi vizuri.
Pia mtazamo wa mama mkwe nao ulibadilika na alianza kumpenda Li-Li kama binti yake mwenyewe na akawa anawasilimua rafiki zake mwenyewe kwamba Li-Li alikuwa ni binti mzuri mwenye tabia njema ambaye hakuna mama mkwe duniani anaweza kumpata. Li-Li na mama mkwe wakawa ni kama mama na binti yake.

Pia mume wa Li-Li alikuwa na furaha ya ajabu alipoona kile kinatokea katika familia.
Ndipo Li-Li akarudi kwa mzee Huang kuomba masaada tena, akamwambia mzee Huang;
Tafadhari nisaidie jinsi ya kuiondoa ile sumu isimuue mama mkwe kwani amebadilika na amekuwa mwanamke mwema sana kwangu na ninampenda kama mama yangu mzazi na sitapenda afe kwa sababu ya sumu niliyompa”.

Mzee Huang akawa anatabasamu huku anatikisa kichwa.
Li-Li huna haja kuwa na mashaka au kuogopa, sikukupa sumu yoyote, dawa niliyokupa ilikuwa ni vitamins kwa ajili ya kuimarisha afya. Sumu kubwa iliyokuwepo ilikuwa kichwani mwako (mind) na mtazamo wako kuhusu mama mkwe na hiyo sumu yote imesafishwa na upendo ambayo umeutoa kwake”.

Je, msomaji wangu umegundua kwamba jinsi unavyowahudumia wengine ndivyo na wao watakavyokuhudumia wewe.

Kuna msemo wa kichina ambao unasema:
"The person who loves others will also be loved in return."

Inawezekana ni kweli unasuguana sana na mama mkwe au mume wako au mke wako au mpenzi wako na tatizo kubwa ni mtazamo wako kuhusu yeye na ungeamua kumpenda na kumhudumia kama malkia au mfalme mambo yangebadilika.

Wednesday, September 2, 2009

Kupanga siku je?

Swali:
Je ni vizuri kupanga siku kwa ajili ya tendo la ndoa.

Jibu:
Ni vizuri au vibaya.

Mahaba ya kushitukiza yana raha yake na pia kuwa na utaratibu kuna raha yake pia kwani maisha ya sasa ni kuendeshana kwa kasi ya ajabu hadi wanandoa wanajisahau au wanajikutahawana muda wa kuwa mwili mmoja.
Kila mmoja anarudi home amechoka na anaishia kulala na kukoroma.
Kama huamini kuwa watu wako busy ngoja nikuulize wewe unayesoma hapa je, leo ni tarehe ngapi?

Kupanga siku kwa ajili ya tendo la ndoa huweza kuwa vibaya kama wahusika hawatakuwa efforts zozote kuhakikisha hiyo siku wamepanga ipo exciting.
Vinginvevyo kupanga siku maalumu kuna raha yake kama kila mmoja atahusikua kuhakikisha hiyo siku inakuwa siku ya raha tangu asubuhi wakiamka.

Kwanza jambo la msingi ni kwamba bila kuweka muda au kutenga muda kwa ajili wa wanandoa wawili kukutana kimahaba kila wiki kwa muda Fulani kunaweza kutokea hatari ya kuweka mambo mengine kipaumbele na sex kuwekwa pembeni na matokeo yake kuwa na disconnection kati ya wawili.

Pia inawezekana mwanandoa mmoja huwa anachoka sana na amekuwa kila mara anajitetea kwamba amechoka na jawabu kwa mwandoa wa aina hii ni kupanga siku ili hiyo siku na yeye ajitoe kwa ajili ya mke au mume wake kumpa haki yake (birth right and marriage right) kwani yule anayekosa hujiona anapuuzwa na kujiona mwenzake hamjali.

Kumbuka pia tupo katika kipindi ambacho sasa mume na mke wanapoenda kazini wanakutana na wengine au wanashinda na waume za watu au wake za watu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia, hivyo basi asipopata (feelings) anazohitahitaji nyumbani anaweza kujikuta anavutiwa na mke wa mtu au mume wa mtu au mwanaume au mwanamke anashinda naye kazini ambako anatumia muda mwingi kuliko hapo nyummbani.

Kama umepanga siku maalumu basi hints zifuatazo zinaweza kukusaidia.
Husisha mawazo yako kuitegemea vizuri hiyo siku na tarehe ambayo mmepanga ili kuwa na usiku wa kuburudishana ambao kila mmoja anaridhika.
Tabasamu kila ukikumbuka jinsi utakavyoutumia huo usiku na mke au mume wako.
Unaweza kumpigia simu, mtumie sms, email mke au mume kumkumbushia yale unategemea huo usiku na jinsi itakavyokuwa raha kuwa na mahaba.
Kama unaweza (mwenye nafasi) tengeneza chumba katika sura ya kuvutia hadi ujisikia ni kweli leo something great and sweet is going to happen.

Pia hakikisha miili inaandaliwa vizuri kwa kuwa safi na appearance kimavazi. Kama ni mwanamke vaa sexy.
Maandalizi ni muhimu kuliko tendo lenyewe.
Mwenye kuweza kuja na zawadi hasa mwanaume ni muhimu sana ukifika nyumbani mpe mke zawadi yoyote na kumpa maneno matamu hata kama amechoka atapata nguvu za ajabu na atajisikia special.
Pia kama unaweza mtumie hiyo zawadi mchana pamoja na message kwamba unategemea kuonana naye jioni kwa usiku maalumu.

Inawezekana kuwa na sex yenye kuridhisha hata kama imekuwa ya kupangwa.

Wewe una maoni gani?