"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 22, 2009

Anachoka sana!

Kaka Mbilinyi,
Asante sana kwa jinsi unavyotuelimisha kuhusu masuala ya ndoa na nyumba zetu, naomba msaada wa swali lifuatalo;

Ni kawaida mume wangu kulala usingizi wa kufa mtu mara tu baada ya kuwa mwili mmoja (sex) pia nimegundua kwamba nikisubiri au kupitisha siku kama 4 au 5 hivi angalau huwa ana pata nguvu (hachoki sana) ingawa baada ya kumaliza tu analala fofofo.
Je, anatatizo gani?

Dada asante kwa swali zuri na naamini inawezekana kushoka kwake nikutokana na sababu zifuatazo:
Kwanza huwa anakuwa amechoka na sex inasaidia kumfanya ajisikie relaxed na hatimaye usingizi mtamu (figuratively and literally).
Pili homoni zinazozalishwa baada ya kufika kileleni humwezesha kujisikia raha na amani ambayo hupelekea kulala usingizi wa uhakika, hii ina maana sex ni dawa ya kupata usingizi.

Tatu kitendo cha kutoa sperms huhitaji tension kubwa au hutengeneza mvutano mkubwa sana kwenye mwili ambao huhitaji nguvu nyingi kujipinda ili kutoa hizo risasi, na mwanaume hujikuta amechoka sana baada ya kutoa hizo risasi na hatimaye kulala usingizi.

Nne wapo wanaume (hata wanawake) muda wote wa kuwa mwili mmoja (harakati zote au shughuli nzima) hushika au hubana pumzi (hold), hiki kitendo husababisha kutopumua vizuri na husababisha kukosa oxygen (oxygen debt) mwilini kutokana na zoezi zima hivyo baada ya kumaliza hujikuta kiusingizi kinakuja chenyewe (sleepness)

Tano inawezekana huwa anakuwa amechoka sana na kazi anazofanya (fatigue) kabla ya sex hivyo kitendo cha kushiriki kuwa mwili mmoja hummaliza nguvu kabisa na mwili wake huwa unalia kilio cha kutaka kupumzika hivyo akimaliza tu analala fofofo, wataalamu wanasema tendo zima la sex moja ambalo wahusika hufika kileleni ni sawa na kukimbia kilomita 8, sasa kama kazini alikuwa amechoka, ukiongeza na hizo kilomita 8 si atachoka?

Sita wapo ambao wanaumwa na jambo la msingi ni kuchunguza na ukihisi kweli anaumwa mwone dakatari kwani anaweza kufia kifuani siku moja.

Jambo la ziada pia kama unaweza kabla ya kuwa mwili mmoja na mumeo hakikisha anapata kinywaji (siyo kilevi) ambacho kitaweza kumsisimua (stimulant) na kuwa tayari kwa sex kama vile Kahawa ambayo ina caffeine ambayo husababisha kuwa macho na hai na kuweza kushiriki tendo takatifu bila tatizo, jambo la msingi uwe mbunifu kuhakikisha kabla ya kuwa mwili mmoja anajua hajachoka na kama hajachoka basi ni kweli ataweza kukupeleke kwenye nchi ya ahadi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hapa

No comments: