"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 16, 2009

Kila mmoja ni tofauti

Mimi ni mwanaume ambaye nimeoa na nina miaka 3 kwenye ndoa, nimegundua kwamba mke wangu sehemu zake za siri zina umbo tofauti kwa maana kwamba mashavu ya ndani ya uke (kingereza wanaita labia minora) zimejitokeza na zina hang nje kwa urefu wa zaidi ya kama sentimita 2 kiasi cha kuzidi vulva na pia clitoris ni kubwa na hujitokeza na kuoneka wazi hata kabla ya kusisimka.
Jambo kubwa zaidi ni kwamba anapokuwa anaoga sehemu zake za siri hufanya vibration kama vile kumeshikwa na shock ya umeme.

Je, kwa nini hizi genitals zake hufanya vibration wakati hata hazijasisimuliwa mfano wakati anaoga?

Je, hii ni kawaida kwa mwanamke?
Nimekuwa naogopa kumuuliza uso kwa uso na pia inanichanganya sana,
nisaidie.

Asante sana kwa swali zuri ambalo ni mara ya kwanza kuulizwa hapa The Hill of Wealth.

Wanawake wote hutofautiana sana katika size, shape, rangi na texture ya maumbo ya miili yao kama vile matiti, makalio, miguu, nywele, vitovu, na sehemu za siri.
Linapokuja suala la sehemu za siri jinsi kunavyoonekana kwa nje anaweza kuwa vulva au labia zilizojitokeza zaidi au kuwa flat.
Jambo la msingi ni kwamba ni jambo la kawaida kuwa hivyo na si ugonjwa bali ni fahari ya mwanamke kuwa na ladha tofauti katika mwonekano wa natural spring water yake ili mume ukinjwa maji uridhike.

Pia clitoris hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine ukianza na wale ambao hakionekani kabisa hadi wale ambao huweza kuonekana.
Na kama mwanamke ananyanyua vyuma na kutumia madawa ya testosterone ukiona kisimi chake unaweza kukimbia ukadhani ni mwanaume mwenzako kwani hukua na kujitokeza kama stick ya mwanaume.

Kama wanaume walivyo na sticks tofauti zingine zimepinda na zingine zimenyoka na zingine ni fupi na zingine ni ndefu wakati zingine ni nyembamba na zingine ni nene, wanawake nao wanatofautiana.

Pia suala la sehemu za siri kutetemeka kwa kushtuka kama shock ya umeme ni jambo la kawaida kwani hiyo ni involuntary action jinsi ngozi yake inavyofanya response katika mazingira tofauti (kumbuka biology ya form two).
Ni kawaida ngozi kutetemeka hata sehemu zingine za mwili.

Kuna kitabu kimoja kimeandika na Paul Joannides chenye title “Guide to getting it on” kama unaweza kukipata kwani kinaelezea vizuri masuala au shape na size za vulva na clitoris kwa wanawake na ukisoma basi utajua mke wako hana tatizo lolote.

Kama mke wakoo analalamika kutokana na hayo maumbile unaweza kuongea naye na kwenda kumuona daktari aliyekaribu na wewe otherwise haina haja kuogopa na kuchanganyikiwa na badala yake endelea kujienjoy na wife kwani hakuna tatizo lolote.
Ubarikiwe!

No comments: