"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, September 17, 2009

Kipi bora?

Hello kaka Mbilinyi,
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 25 naishi Dar es Salaam, Kumetokea ubishi mzito kijiweni kwetu kutaka kujua kama kuna kimoja ni muhimu kuliko kingine kati ya SEX au USINGIZI?

Kaka nashukuru kwa swali ambalo naamini bado ni kitendawili kwani linahusu watu wote na watu tunatofautiana kile tunapenda.
suala la sex na usingizi ni preference ya mtu kwani mwingine sex ni muhimu kuliko kulala usingizi na mwingine kulala usingizi ni muhimu zaidi kuliko sex na mwingine hajali iwe usingizi twende au sex twende hana shida.

Kuna baadhi ya watu hawawezi kufurahia sex kama wamechoka au kama hawajalala usingizi, hii ina maana kulala usingizi kwao ni jambo la msingi kwanza, wapo wengine (hasa wanaume siyo wote) hata kama amechoka na ana usingizi kwake sex kwanza na baadae kulala usingizi, kwanza hata kama amelala anaota sex na kuwaza sex kama huamini tafuta au uliza wanawake 5 tu walioolewa kama kuna siku walikubaliana na mume wake walale kwani mwanamke anajisikia amechoka lakini usiku wa maneno mwanaume akamng’ang’ania kuwa mwili mmoja.

Na kuna kundi la watu wengine hufanya sex huku wapo usingizini iwe usiku wa manane au asubuhi kwani ndoto zao huwafanya kuwa active na kuenjoy sex as if wapo macho.
Na kuna documentation nyingi zinaonesha wapo ambao hufanya sex huku wapo usingizini na kwa utendaji wa hali ya juu na skills za uhakika ingawa wakiulizwa asubuhi ilikuwaje usiku wanaruka mita mia.

Ni vizuri kuwa na muda mzuri wa kupumzika (kulala usingizi) kwani usingizi hupunguza stress, kubalance uzito, magonjwa ya moyo, depression nk.
Hata hivyo faidi za sex wengi wanaziruka kuna articles nyingi tu na research paper nyingi zinaelezea faida za sex kama vile kupunguza maumivu ya kichwa, kuwaweka wanandoa emotionally closer ingawa kulala usingizi ndiko kunapewa headlines nyingi sana kwenye media kwa sababu usingizi ni muhimu kwa survival ya binadamu.

Naamini furaha, na healthy sex ni kitu cha msingi sana kwa personal satisfaction ya mwanandoa hata hivyo pata usingizi wa kutosha ili uwe na energy ya kupata sex ambayo itakufanya uridhike.

Ukitaka kusoma zaidi kuhusu faida za tendo la ndoa bonyeza hapa
Siku njema!

No comments: