"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 23, 2009

Kumwelewa Mke!

Ndivyo walivyo!Kumuelewa mwanamke kwenye mahusiano.
Wanaume wengi hulalamika kwamba wanawake huwa hawaeleweki linapokuja suala la mahusiano (mapenzi).
Kama wewe ni mwanaume habari njema ni kwamba kumwelewa mwanamke au mke wako au mpenzi wako ni rahisi mno na ukishafahamu siri yake basi inakuwa rahisi kumpa kile anahitaji katika mahusiano yenu (ndoa).

Kwanza mwanaume na mwanamke ni tofauti as if wanatoka sayari tofauti.
Kawaida paka hufukuza panya na mbwa hukufuza paka sababu kubwa ni kwamba naturally panya, paka na mbwa wapo wired tofauti.

Kubali na fahamu kwamba mke wako yupo tofauti na wewe wala usilalamike au utake awe vile unataka wewe.
Zikubali tofauti zilizopo na zifurahie na endelea kumpenda.
Viva la difference!

Mimi mwenyewe ni shahidi katika zamani za ujinga wangu kutaka mke wangu awe kama ninavyotaka mimi.
Nilichojifunza ni kwamba tofauti zilizopo zilikuwa designed na Mungu mwenyewe ili ndoa au mahusiano kuwa imara na kuridhisha kwa maana kwamba kila mmoja aweze kutimiza hitaji la mwenzake (kukamilishana).

Yale mwanaume anahitaji na kuyapenda naturally ni tofauti na mwanamke na ndoa ndiyo mahusiano ya pekee duniani (on the planet) ya kuwaunganisha mwanaume na mwanamke ili kila mmoja aridhike pale design ya kimungu inapofuatwa.
Pili, kumuelewa mwanamke katika ndoa ina maana mwanaume lazima afahamu jinsi mwanamke na mwanaume wanavyokuwa motivated.
Nini huwavuta kufanya kile wanafanya?
Wanawake huvutwa na
Kuthibitishiwa (approval, security)
Mahusiano yanayoridhisha
Mawasiliano mazuri.
Kwa mfano mwanamke anahamu ya kusikia kutoka kinywani kwa mume wake kwamba nakupenda haijalishi jana au juzi au siku ya harusi ulisema nakupenda, neno Nakupenda analihitaji masikioni mwake mara kwa mara tena uwe una maanisha.
Pia anahitaji kusikia unamwambia amepeza au amepika chakula kitamu au kitu chochote anafanya anahitahi approval.

Tatu wanaume na wanawake wana mahitaji tofauti.
Kumuelewa mke wako katika ndoa ina maana ya kufahamu kwamba kile wewe unahitaji inawezekana siyo kile yeye anahitaji.

Ikitokea kwamba mwanamke na mwanaume wote waandike orodha ya vitu 3 ambavyo anahitaji katika ndoa, ukweli ni kwamba vitatofautiana sana.
Wanawake wengi suala la mawasiliano huwekwa juu kwenye orodha, kwa upande mwingine, wanaume wengi huweka sex juu katika orodha kama hitaji lao kubwa katika ndoa.
Utafiti mwingi unaonesha kwamba mambo matatu ambayo huwa juu kwenye orodha ya wanaume na wanawake ni kama ifuatavyo:
Mahitaji 3 muhimu ya mwanamke katika ndoa;
Mawasiliano (conversation)
Kugusswa (Non-sexual touch)
Kujisikia anapendwa na anahusudiwa (cherished, adored)

Mahitaji 3 muhimu ya mwanaume katika ndoa ni
Mapenzi (sex)
Kuheshimiwa (respect)
Hewa (
kwenda pangoni)

Je unadhani mahitaji yako kama mwanamke ni tofauti au mwanaume ni tofauti?

No comments: