"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 2, 2009

Kupanga siku je?

Swali:
Je ni vizuri kupanga siku kwa ajili ya tendo la ndoa.

Jibu:
Ni vizuri au vibaya.

Mahaba ya kushitukiza yana raha yake na pia kuwa na utaratibu kuna raha yake pia kwani maisha ya sasa ni kuendeshana kwa kasi ya ajabu hadi wanandoa wanajisahau au wanajikutahawana muda wa kuwa mwili mmoja.
Kila mmoja anarudi home amechoka na anaishia kulala na kukoroma.
Kama huamini kuwa watu wako busy ngoja nikuulize wewe unayesoma hapa je, leo ni tarehe ngapi?

Kupanga siku kwa ajili ya tendo la ndoa huweza kuwa vibaya kama wahusika hawatakuwa efforts zozote kuhakikisha hiyo siku wamepanga ipo exciting.
Vinginvevyo kupanga siku maalumu kuna raha yake kama kila mmoja atahusikua kuhakikisha hiyo siku inakuwa siku ya raha tangu asubuhi wakiamka.

Kwanza jambo la msingi ni kwamba bila kuweka muda au kutenga muda kwa ajili wa wanandoa wawili kukutana kimahaba kila wiki kwa muda Fulani kunaweza kutokea hatari ya kuweka mambo mengine kipaumbele na sex kuwekwa pembeni na matokeo yake kuwa na disconnection kati ya wawili.

Pia inawezekana mwanandoa mmoja huwa anachoka sana na amekuwa kila mara anajitetea kwamba amechoka na jawabu kwa mwandoa wa aina hii ni kupanga siku ili hiyo siku na yeye ajitoe kwa ajili ya mke au mume wake kumpa haki yake (birth right and marriage right) kwani yule anayekosa hujiona anapuuzwa na kujiona mwenzake hamjali.

Kumbuka pia tupo katika kipindi ambacho sasa mume na mke wanapoenda kazini wanakutana na wengine au wanashinda na waume za watu au wake za watu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia, hivyo basi asipopata (feelings) anazohitahitaji nyumbani anaweza kujikuta anavutiwa na mke wa mtu au mume wa mtu au mwanaume au mwanamke anashinda naye kazini ambako anatumia muda mwingi kuliko hapo nyummbani.

Kama umepanga siku maalumu basi hints zifuatazo zinaweza kukusaidia.
Husisha mawazo yako kuitegemea vizuri hiyo siku na tarehe ambayo mmepanga ili kuwa na usiku wa kuburudishana ambao kila mmoja anaridhika.
Tabasamu kila ukikumbuka jinsi utakavyoutumia huo usiku na mke au mume wako.
Unaweza kumpigia simu, mtumie sms, email mke au mume kumkumbushia yale unategemea huo usiku na jinsi itakavyokuwa raha kuwa na mahaba.
Kama unaweza (mwenye nafasi) tengeneza chumba katika sura ya kuvutia hadi ujisikia ni kweli leo something great and sweet is going to happen.

Pia hakikisha miili inaandaliwa vizuri kwa kuwa safi na appearance kimavazi. Kama ni mwanamke vaa sexy.
Maandalizi ni muhimu kuliko tendo lenyewe.
Mwenye kuweza kuja na zawadi hasa mwanaume ni muhimu sana ukifika nyumbani mpe mke zawadi yoyote na kumpa maneno matamu hata kama amechoka atapata nguvu za ajabu na atajisikia special.
Pia kama unaweza mtumie hiyo zawadi mchana pamoja na message kwamba unategemea kuonana naye jioni kwa usiku maalumu.

Inawezekana kuwa na sex yenye kuridhisha hata kama imekuwa ya kupangwa.

Wewe una maoni gani?

2 comments:

Anonymous said...

Hi!
kwa maoni yangu kupanga siku ni vizuri kwa sababu mandalizi yatakuwa ya hali ya juu na kila mmoja anakuwa anamtamani mwenzake lakini msipopanga naona mara nyingi sisi wakina mama ndio inakuwa tabu siku una hamu anadai kachoka ila akihitaji yeye aaaah hata usiku wa manane hana displine kwa kweli tena hapo anakuwa tayari bila kujali wewe pia unahitaji maandalizi au kama karudi na mood nzuri kakuta umelala bila kujali u hali gani yeye anahitaji yaani kuna usemi nasikia watu wanasemaga kuwa wanawake tumeubwa kwa ajili ya wanaume huwa naukataa lakini kwa hili unakuwa applicable.

kwa hiyo kupanga siku ni vzr tena hata kwa uzazi unakuwa huna haja ya kinga maana mna ratiba yenu tayari na kama inatokea dharuha siku ya ratiba yenu kwa mfano msiba au kaugomvi kdg basi hilo ni tatizo anaumia kila mmoja.

Tena ikiwa kwa mfano kwa wk mara 2sioni kama mbaya.

Ila naomba kuuliza ni muda gani mzuri kwa tendo la ndoa usiku, mchana au asubuhi? Na hasa ni muda gani mzuri wa kutafuta mtoto kwa mida hiyo niliotaja?

Je ni kwanini wanaume wakitaka kuoa hawafundishwi jinsi ya kuishi na mke? maana hili nalo linachangia mke akishaolewa kutoka nje ya ndoa yake kwa kukosa vitu flani vidogovidogo ambavyo viko ndani ya uwezo wa mumewe.
Asante ni hayo tu.

Mama P !

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Hongera kwa ushauri wako na nimependa mawazo yako kwani jambo la msingi ni wawili mke na mume kukaa pamoja na kujadili kwa upendo kabisa ni namna gani kila mmoja aweze kuridhishwa kiuhakika katika ndoa na njia nzuri ni kukaa pamoja na kuelezeana iwe ratiba au bila ratiba muhimu kila mmoja amtangulize mwenzake.

Upendo daima