"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 11, 2009

Maswali Muhimu kabla ya kuoa na kuolewa

Kabla ya kukiri “Hadi kifo kitakapotutengenisha” au hata kabla ya kukubali kuvishwa pete ya engagement kuna maswali muhimu sana (hard questions) ambayo unahitaji kujiuliza na kwa njia hiyo unaweza kujua success au failure ya mahusiano ya ndoa pengine hata kabla ndoa haijafika popote.

Kujiuliza mwenyewe na kumuuliza yule unategemea kuoana naye maswali ya msingi kabla ya kuoa au kuinvest upendo wako itasaidia wewe kufahamu kama umempata mtu sahihi na pia kuweza kuondoa matatizo ya kawaida ambayo wengi hupelekea kuachana.

Chukua muda (honestly) kufanya evaluation jinsi unavyojisikia (feelings) na motivations kwa ajili ya wewe kuoa au kuolewa.
Ni vizuri kupata majibu ya maswali kabla hujaoana naye ili kuweza kushughulikia matatizo hayo kabla ya ndoa kuanza.

Kuna maeneo muhimu sana katika ndoa ambayo bila kuyafahamu na kuingia kichwa kichwa hakuna wa kumlilia isipokuwa wewe mwenyewe na suala la ndoa ni suala sensitive sana ukishindwa (achana) utapata label ambayo utaibeba maisha yako yote hapa duniani na pia unaweza kuathiri maisha ya wengine.

Swali la kwanza
Je, ni kweli tunapendana?
Je, ni kweli ninampenda Mwenzangu hata miaka 30 ijayo?
Ni kitu gani au sifa zipi zinanifanya nimpende?
Uwe mkweli.
Unahitaji kufahamu na kujisikia ni kweli unampenda mwenzako isije kuwa ni tamaa tu.
Upendo huanza kidogokidogo na hutokea kwa kumpenda mtu mzima kama alivyo awe ana pesa au hana pesa pia siyo kumpendakama wewe unavyotaka awe.
Kumbuka mke au mume si kipande cha udongo wa mfinyanzi kwamba utamefinyanga kwa kadri unavyotaka wewe.

Swali la pili:
Kwa nini tunaoana?
Kwa nini namhitaji huyu mtu kuoana naye?
Je, ni kwa sababu ninataka mtoto?
Kwa sababu ninataka hela zake au najisikia upweke upweke, au nataka sex au nataka kuondokana na kero za mama au wazazi?
Au naona nachelewa kuolewa/kuoa au rafiki zangu wananisema sana au na mimi nionekane nimeoa au kuolewa?
Kuoa au kuolewa kwa sababu za ajabu ajabu huweza kukufikisha mahali ambapo utajikuta upo disappointed, frustrated na hatimaye kuachana.
Oa au olewa kwa sababu ni wakati wake.

Swali la tatu:
Je, ni nini matarajio ya ndoa yangu?
Je, umeshajiandaa na kila kitu kuhusu ndoa?
Matarajio mtu anaingia nayo kwenye ndoa huweza kujenga au kuharibu ndoa.
Kuna baadhi ya imani potofu kuhusu ndoa unatakiwa kuzifahamu hata kabla hujaingia kwenye ndoa.
Kuamini kwamba ukiolewa basi mwenzako anatakiwa kukufanya happy si kweli, furaha unayo wewe kwanza.
Kufikiria kwamba eti mume/mke ataweza kusoma mind yako si kweli unahitaji kueleza kile unataka siyo kubaki kimya eti anajua.
Kuamini kwamba ukioa au kuolewa basi kila kitu mtafanya pamoja si kweli kila mtu ana interest zake.
Na kutaka kuwa na ndoa unayotaka wewe badala ya wote kwa pamoja unaweza kujikuta kwenye total disappointment.

"Truly loving another means letting go of all expectations.
It means full acceptance, even celebration of another's personhood."
-Karen Casey

Tutaendelea kesho….

No comments: