"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 11, 2009

Maswali ya kujiuliza kabla ya kuoa au kuolewa - 2

Kabla hujaanza kujenga mnara, fikiria gharama kwanza......... Swali la nne:
Je, unajua mtazamo wa mwenzako kuhusu sex?
Je,anapenda na kujiona atafurahia sex?
Je, mnaweza kuongelea kwa uwazi na uhuru kuhusu sex kwa pamoja wawili bila kuogopa au kukiri kwamba tuache tutaongea tukiwa tumeoana?
Je, unategemea sex iweje au unahitaji kiasi gani?
Kila siku au mara moja kwa mwezi inatosha?
Je, ni vitu gani unategemea kufanya kuhusiana na sex?
Je, ni vitu gani vinavyohusu sex unaamini unatajisikia uncomfortable?
Kama ndiyo je, ni vitu gani? Be specific!
Je, partner wangu ananivutia kimapenzi kwa kadri ninavyotegemea?

Wanawake mara nyingi hujikuta wanakuwa waoga sana kujadili topic ya sex, au maandalizi ya kufanya mapenzi (forepaly) au sex position n.k hata hivyo kuruka hiki Kipengele kuna matatizo yake kwa future ya wanandoa.
Kama mnashindwa kuongea kuhusu sex sasa kitu gani kitawafanya muweze kuongea mkioana.
Kutegemea mke au mume kusoma your mind inaweza kupelekea kwenye maluweluwe ya kutisha.

Swali la tano:
Je, linapokuja suala la pesa wewe ni mtumiaji au mtunzaji pesa?
Je, nini malengo yako kifedha?
Je, mkioana mtakuwa na joint account au kila mtu yake?
Na nani atakuwa na jukumu la kuhakikisha kila bills zinalipwa?
Na je kila mmoja anaingia kwenye ndoa akiwa na deni kiasi gani huko Bank?
Matatizo kuhusu pesa ni moja na migogoro sugu katika ndoa na kuna umuhimu sana kujua au kuwasiliana vizuri masuala la pesa kabla ya kuoana na kuanza kuzozana kila kukicha.

Swali la sita :
Je, kuna tatizo lolote kwenye mahusiano yenu ambalo kila mmoja anahisi ni vizuri kulimaliza kabla ya kuoana.
Je, umeshamweleza mwenzako vitu ambavyo hutavivumilia kabisa katika ndoa yenu au vitu ambavyo utavikubali?
Kwanza unatakiwa kujua kwamba tofauti katika ndoa haziwezi kukwepeka hivyo jinsi ninyi wawili mnavyohusika kupambana na tofauti kwa upendo na kuheshimiana tangu mwanzo inaonesha ndoa yenu itakuwa na furaha au karaha.

Swali la saba :
Je, unahitaji watoto?
Lini na wangapi?
Je, partner wako anahitaji watoto na kama ndiyo lini na wangapi?
Na je, wote mnakubaliana na njia za kulea watoto?
Isije mwingine anataka watoto na mwingine hataki au mwingine anataka watoto wawili na mwingine anataka timu zima ya soka.

Swali la nane:
Je. Mume wako mtarajiwa au mke wako mtarajiwa yupo upande wako kuhusiana na tatizo lolote kutoka kwa ndugu zake?
Au mama yake akiongea au baba yake akiongea kitu chochote anafyata mkia na anawasilikiza hata kama hicho kitu hapendi na wewe hupendi?
Je, wazazi wana uwezo gani kuamua kuhusu mambo yenu?
Suala la wakwe, marafiki na ndugu lina umuhimu wake katika ndoa.
Usiingie ukiamini kwamba ukioa au kuolewa ndo utajitahidi kubadilisha mtazamo ili kila kitu kiwe kama wewe unavyotoka.

Swali la tisa:
Je, dini au suala la imani ni muhimu sana katika maisha yako?
Je, mpenzi wako yeye anaaamini nini au yupo dini gani na nini matarajio yenu baada ya kuoana?
Unahitaji kufikiria mbaliza zaidi kwani itakuwa ngumu sana kuwa na watoto wenye wazazi wenye mitazamo tofauti ya dini zao.

Swali la kumi :
Je, linapokuja suala la mahusiano na mpenzi wako unajisikiaje?
Je, wewe ni mzuri kuongea au kusikiliza, na je wewe na mpezi wako kila mmoja anajisikiaje kuhusu maneno mwenzake anatumia kuongea, iwe utani au ukali?
Je, wewe huwa unajieleza vipi ukikasirika au kukatishwa tamaa? Na yeye je?
Je, huwa unapenda kukaa kimya ukiona kunaweza kuzuka mgogoro au huwa anaamua kuongea kwa sauti na matusi juu? Na yeye je?
Au una tabia na kubabiza milango au kuvunja vitu kama kutupa simu ya mkononi ukikasirika na yeye je?
Jinsi mnavyowasiliana kuna matokeo makubwa sana kuhusu ndoa mnaenda kuitengeneza.
Kuwa na communication skills nzuri au kujenga tabia ya kuwa na mawasiliano mazuri ni jambo la msingi sana.

Bottom line ni kwamba jinsi wewe na partner wako mnavyojihusisha wakati wa good times na bad times huweza kuelezea ndoa yenu na ni muhimu sana kuwa tayari kujibu baadhi ya maswali muhimu kama hayo nimeyaweka hapo juu kabla ya kukubali kuoana hadi kifo kitakapowatenganisha.
Kumbuka ndoa ni shimo ambalo ukiingia hakuna kutoka hadi kifo!

1 comment:

Anonymous said...

Asante sana kwa somo zuri ambalo limenifanya kujiuliza upya suala la kuolewa.

Nimefurahia sana jinsi ulivyoeleza kwa upana haya maswali ya kujiuliza.

God bless u so much

NN