"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 9, 2009

Ni Binti

Karen-Jody Mbilinyi Wapendwa wasomaji wa blog hii, kwanza napenda kuomba msamaha kwa kutokuwa hewani kwa muda wa wiki mbili.

Pia napenda kuwashukuru kwa maombi yenu na pia wale wambao waliweza hata kutuma ujumbe kuulizia imekuwaje hata hivyo nimerudi tena baada ya kumaliza jukumu kubwa la kuhakikisha mke wangu mpenzi anajifungua mtoto na tunashukuru Mungu kila kitu kilienda salama kabisa.

Hata kama alipitisha wiki mbili kutokana na tarehe ambayo alitakiwa kujifungua bado Mungu alikuwa mwema kwani Jumatano tarehe 2 mwezi Septemba saa kumi na mbili na dakika hamsini na mbili katika hospitali ya Mkoa (Pembroke) Ontario – Canada Mungu alitupa zawadi ya mtoto wa kike aitwaye Karen-Jody (Greek-Hebrew name – pure praise of God).


Hata baada ya siku 5 ukuaji wako unaridhisha

Ufanisi wa kazi yako kama nesi wa zamu ulitufanya kujisikia tupo mahali salama.

Kama baba ilikuwa furaha na kumshukuru Mungu kushika mtoto dakika chache baada ya kuzaliwa

Dada Jody; jinsi ulivyohusika tangu siku ya kwanza kuhakikisha tunapata daktari anayefaa kwetu ni furaha na heshima kwako.
Dada Jennifer; maombi yako na maneno yako ya kumtia moyo Gloria ilikuwa kazi njema hadi anajifungua salama,
Emmanuel; hongera kwa kupata dada!
Gloria; nakupongeza sana kwa jinsi ulivyo mvumilivu na imara hasa kuvumilia uchungu wa masaa zaidi ya sita. Ilikuwa na mara yangu ya kwanza kuwepo uso kwa uso wodini kusaidiana na manesi na marafiki na ndugu kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Jambo kubwa nililojifunza kwa kuwepo kwangu wakati mtoto anazaliwa ni jinsi Mungu alivyowabariki wanawake huu uwezo na kuvumilia maumivu na uchungu wa kazaa acha ile ya kubeba mimba kwa miezi 9.

Napenda kuwapongeza wanawake mahali popote uwe umezaa au bado kwa kweli kuwa mwanamke ni heshima na wanaume tunahitahi kuwajali, kuwapenda na kuwalinda na adui wa aina yoyote na zaidi kuwapa kile mnahitaji katika mahusiano yetu kwani ninyi ni viumbe wa thamani sana kutokana na nguvu ya uumbaji ambayo Mungu amewapo ndani yenu.
Sasa nimerudi ninayo mambo mengi sana ya kujadiliana pamoja na kujifunza na wewe kuhusu ndoa, mahusiano na maisha kwa ujumla hivyo karibu sana
Tunawashukuru wote kwa maombi yenu na Mungu awabariki sana!

28 comments:

Anonymous said...

Wooooow!
Honereni sana kwa kupatiwa zawadi ya aina tofauti(baby gal)kweli huyo ni real angle.
Nampa pole sana mama Emmanuel kwa uchungu alioupata na hatimae kupata zawadi yake.
Kweli Mungu ni mwema na anastahili kuabudiwa kwa fadhili zake.
Namtakia mtoto maisha mema ya upendo na kila aina ya furaha.


Mama P!

angel said...

heey
a baby girl!!!
she is a flower
congratss bro....
mungu awajalie kila la heri katika familia yenu na huyo flower wenu mpya
hongera sana kaka...
Angel

Yasinta Ngonyani said...

Hongereni sana mama, baba na pia kaka na pia ukoo mzima wa akina Mbilinyi. Na pia napenda kuwashukuru wote walioshiriki kumsaidia Grolia maana hii kazi ni ngumu sana: Nawatakieni kila la kheri. Karibu katika Ulimwengu huu Binti Mbilinyi.

Anonymous said...

Wow! What a beautiful baby, Mashallah!
Congratulations sana kaka pamoja na mke wako. Watoto ni furaha kubwa sana kwa wazazi. 4 sure, we women need love and respect sema tu some men take us 4 granted.

Inshallah M/mungu awakuzie mtoto wenu.

Maryam

Anonymous said...

Bwana yesu apewe sifa, Hongera sana Kaka Mbilinyi kwa kupata baby girl Mungu akubariki na kukutia nguvu ili uweze kumpatia mapenzi mema na kile anastahili kupata kutoka kwako kama baba.
Hongera sana, mpe Hongera sana na Wife wako kwa yote.
Msafiri

Anonymous said...

"Hongera kaka she is beautiful"

Anonymous said...

Hongera kwa kupata baby girl!
Enjoy yourself,
GOD BLess Yuo.

Anonymous said...

"congratulation kaka for a new baby. You become more baba by having more kids!!!"

Anonymous said...

"woow woow wow!!mtoto mpya?hongereni sana sana ,inguluvi itange"

Anonymous said...

"Hongera kaka Mungu awatangulie wote bwana asifiwe sana,wape hi wote canada."

Anonymous said...

Hi Lazarus & Gloria

Wow what a blessings! Congratulations for having a Beautiful Baby Girl! By the way, how is Gloria doing?

I wish you all the best and God bless you abundantly.

Anonymous said...

HONGERENI SANA JAMANI
MUNGU WETU NI MWEMAAAAA, SHE IS REALLY HEALTHY BABY GIRL

THANKS FOR INFORMATION!!!

Anonymous said...

Hello Lazaro,
Hongera sana maana anaonekana kwenye picha kama mwenye umri wa miezi miwili hivi kumbe just a week.
Nawatakia malezi mema na mafanikio mema katika shuguli zako.
Mungu awabariki

Anonymous said...

This is very good news! Hongera sana to you and Gloria! The baby looks so cuuuttee...... please give her a big kiss from me.
I can also see Emma being the big and protective brother.
Nice pics, thanks for sharing.
Wishing you and the family all the very best.

Anonymous said...

Hurrayyyyyyyyyyyyyyyyy n hongera sanaaaaaaaaaa...cos umebalance gender..hahhahhah

actually u were in my thoughts...n good u send us a nice surprise:-) mashallah she looks very healthy n big duh!! mamake alimbebea tumbo gani jamaniiiiiiiii...na alikula nini...nataka ku-adopt theory yake.....hahhahha

sasa na hilo jino la kithungu...bibi na babu kule south wataweza kuliitaaaaa...:-)...simo miyeeee

haya kila la kheri kwenye malezi...i guess Emmanuel is thrilled to hv a canadian baby sister.

Cheers, tc n stay blessed.

Anonymous said...

Hey Congratulations my dear. I am sure Gloria and the baby are doing fine with the cold creeping in there in Ontario compared to the sun getting hotter here in Kampala.


Wish you all the best,

Anonymous said...

Congratulations!! Praise the Lord, indeed it is pure praise of God.

Anonymous said...

Wow! Congratulations bro, this is the best news I have received this week. Am sure Emanuel is very happy. Please pass my sincere congrats to Gloria.

God bless you and your family,

Anonymous said...

Dear bro hongera sana sana Mungu na akupiganie,
Tuombee na sisi wengine safari ni ndefu.

Anonymous said...

Dear Lazarus,

A baby is a celebration of Love.

Stay blessed and kisses to the little princess

Regards

Anonymous said...

Wow!!!!!!!!!!!!!!!!!
Congrats. I'm really proud of you.
Cute baby. She looks older than the age.
How comes Emmanuel has grown so fast.
Regards,
Ittica

Anonymous said...

GOD BLESS LAZARUS FAMILY. CUTE BABY WHOOOOW'.
MWAAAA'

Anonymous said...

Sasa haka katoto mbona kanachanganya watu. yaani kameanza na kufungua macho na kunyonya hiyo kitu mdomoni. Mbona mapema mno jamani. Halafu mbona kazuri mnoooooooo. Nipeni siri ya mafanikio yenu lazarus vs gloria......mhhhhhhh too much cute' lo. Naona emma kashikilia mtoto kweli kweli na mkewe pembeni.......congratulaion again and again. luv ya all'
GOD BLESS U

Anonymous said...

Hongereeeniiiiiiii... sana , sifa na utukufu apewe Bwana Yesu aliwawezesha katika yote.

Anonymous said...

Kaka na shemeji Mungu awabariki! Nimesoma maelezo kweli yamenigusa!!
Ni mfano na tunahitaji kujifunza!!
Mungu awalinde nyote!!
Elly Mbilinyi

Mary Damian said...

Hongereni sana familia ya Lazarus Mbilinyi! Mungu na azidi kumtunza mama na mtoto! Neema yake isipunguke kwenu. Amen

Patrick Sanga said...

Hongera sana kaka na familia yako nzima kwa kupata zawadi nzuri ya mtoto wa kike, Bwana Mungu awalinde na kuwapigania siku zote za maisha yenu.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Sanga,

Asante sana, nawe nakutakia baraka njema kwa familia yako.