"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 16, 2009

Ni nyuzi 45, nifanyeje?

Kaka Mbilinyi Shaloam!
Mimi ni kijana wa kiume wa miaka 20 na napenda kujua kwani tangu nimebarehe nimejikuta uume wangu umepinda nyuzi 45.
Je, hii inaweza kuniletea matatizo wakati wa tendo la ndoa kwa mke wangu nitakapooa?
Je, kuna matatizo yoyote nitakutana nayo wakati wa kuwa mwili mmoja na mwenzi wangu?
Please nisaidie!

Mdogo wangu,
Asante sana kwa kuuliza swali ambalo naamini si wewe peke yako umejikuta stick inayumba nyuzi kadhaa ingawa yako kweli inabidi ujiulize maana nyuzi 45 si haba.

Uume kupinda kwa angle fulani ni jambo la kawaida na haiwezi kuleta madhara yoyote wakati wa kuwa mwili mmoja na mwenzi wako.

Hata hivyo Siwezi kutoa uamuzi wa jumla kwako kwamba stick yako ipo shwari kwani kupinda nyuzi 45 ni angle kali kidogo na kwa kuwa hakuna vipimo vimefanyika sitaweza kukupa uhakika asilimia mia kwamba kila kitu kipo sahihi.
Kama unaweza nenda kwa daktari anayehusika na masuala ya urology ambaye anaweza kupima hiyo angle wakati umesisimka na kawaida ili aweza kupima kama kuna condition yoyote ya tofauti na anaweza kukushauri kitaalamu zaidi na mapema kabla hujamwingiza bibie ndani ya nyuma ukaanza kushiriki mwili mmoja huku unaficha stick au kung’ang’ania iwe giza kila wakati mkiwa faragha na yeye anataka kuiona siyo kupapasa.
Je, hujisikii maumivu hasa uume ukisimama? kwani kupinda kwa uume kama hiyo angle 45 ni moja ya dalili ya penile fracture.
Hivyo mwone daktari haraka iwezekanavyo!

No comments: