"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, September 24, 2009

Sikutegemea kabisa!

Nimechoka sana kuendelea nkujitahidi kuhakikisha ndoa yetu inakuwa nzuri na inanifanya kuridhika, miaka nenda rudi tumekuwa tunabishana the same thing.
Sasa tumefika mahali hata hatuwezi kuongelea tatizo lolote katika ndoa yetu, ni kama vile kila mmoja amaona haitawezekana ingawa ndani ya moyo wa kila mmoja kuna vita ya chini chini inaendelea (cold war) ndiyo maana kitu kidogo tu huweza kusababisha moto kuwaka.
Hakuna raha, hakuna msisimko, hakuna upendo, hakuna kuvumiliana na hakuna ukaribu wa mapenzi ni kama watu wawili tofauti tulioamua kuishi kama kaka na dada wanaogombana katika nyumba.
Nafahamu hakuna ndoa ambayo ni perfect, hata hivyo nilitegemea hii ndoa yetu iwe ya kuridhisha kwa kiasi fulani.

Mume wangu hanijali tena, anakuwa excited na natokeo ya mechi ya soka (Asernal huko UK) kuliko mahusiano yetu, hukasirika sana hiyo timu yake ikifungwa huko UK wakati yeye yupo Tanzania na hakasiriki kuumiza feelings zangu mimi mke wake ambaye tunalala akitanda kimoja.
Hata akifanya kitu kizuri ni kama bahati mbaya katika wajibu wake ila si kwa kupenda au kuamua nimfurahishe mke wangu au kuonesha ananipenda na kunijali.
Naamini hii si maana ya ndoa ilivyo au inavyotakiwa kuwa , najuta kuolewa na huyu mwanaume pia sijafahamu kama nisingeolewa ningejua ndoa ina mambo magumu kama haya.
Swali linaloniumiza kichwa ni hivi kwa nini hawezi kutamabua mahitaji yangu kama ilivyokuwa mwanzo? Kwa nini hathamini ndoa yetu kama mimi ninavyothamini?
Je, nilifanya makosa kuoana nay eye?
Na je, bado kuna matumaini?
Ni mimi Jema (si jina la kweli ) miaka 7 kwenye ndoa.
UFAFANUZI ZAIDI:
Wanawake wengi hujikuta feelings zako zimaumizwa kama Jema, wao hutegemea baada ya kjuolewa wamepata mwanaume ambaye angempa TRUE LOVE matokeo yake anapewa TRUE FRUSTRATIONS.
Badala ya maisha ya furaha wamejikuta ni ndanin ya TOTAL DISAPOINTMENT, wamejikuta ndoto zimayeyuka na matarajio au mahitaji yao yakiwa ni ndoto za mchana.

Tukumbuke kwamba kila mwanamke huwa na ndoto kwamba siku moja atapata MR RIGHT, atampata Prince na yeye kuwa princes, na huyu mwanaume atajitahidi kufanikisha ndoto zake na mapenzi yatakuwa motomoto siku zote za maisha yao na ndoa yao.
Wakati wa uchumba hufika na binti hujikuta kweli amempata mwanaume wa ndoto zake kwani hakuna tatizo wala kitu unachoona hafai kwani kama ni matching basi imefanywa mbinguni.
Wanafanana kwani streght za mwanaume zina match weakness za mwanamke.
Ni mwanaume anayemsikiliza na kumpa mahitaji yote na anaahidi kwamba atajitahidi kuhakikisha ndoa yako unakuwa mfano.
Macho ya mwanamke hujawa na HOPES na ameamini kwamba amempata wa kumpa TRUE LOVE.
Kila anayewaona mitaani anawapa mkono wa kheri kwa kuwa siku moja watakuwa mke na mume kwa ndoa safi na kuingie honeymoon kwa madaha na mbwembwe.

Baada ya kumaliza honeymoon, maisha yanaanza, siku zinaenda, miezi inaenda na miaka inaenda, conflict zinaanza kujitokeza kwani kila mmoja alizawali sehemu tofauti, malezi tofauti na zaidi ni mwanamke na mwanaume wapo tofauti.
Mume anaanza kupuuza kumsikiliza mke wake tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuoana. Mume anaanza kutumia muda mwingi kufanya mambo yake au kuwa na rafiki zake.
Weekend zikifika anaenda na rafiki zake kutazama sports na kuongea mambo ya business na anarudi nyumbani usiku saa sita bila taarifa kwamba atachelewa.
Mke amesubiri amechoka na ameamua kulala huku hajala maana anaamini kula na mume ndo raha ya ndoa.
Mke anaanza kupata shock na kuwa disappointed jinsi prince wake anavyoanza kufanya mambo yake tofauti na matarajio.
Mke anaanza kujihisi upweke unaanza na hofu kutanda kwenye mawazo yake nini kimetokea kwa mume wake.
Anajikuta yupoo kwenye njia panda. Maswali yanaanza kujaa kichwani (kumbuka mwanamke ana 8 lanes za kupitisha atraffic za emotions kwenye mind yake).
Je, nifanyeje nisimkasirishe na wakati huohuo nimwambie anavyofanya ni vibaya na ajirekebishe?
Je, nilioana na mwanaume sahihi?

MUHIMU SANA KUELEWA HAYA:
Hapo juu tunaona contrast kati ya matarajio ya mwanamke na reality ya maisha ya ndoa.
Matarajio mengi ya wanawake wengi kuhusu ndoa ni UNREALISTIC, si matarajio sahihi, ni vitu ambavyo katika maisha ya kweli kwenye ndoa huwezi kuvipata, ni illusions kama vile movie.

Wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawana matarajio kwamba kwenye ndoa kuna conflict, kuna kuumizwa, kuna hasira, kuna majaribu, kuna shida, dhiki, tabu na kwamba hivyo vyote ni sehemu ya ndoa kwani ndoa ni mwanaume na mwanamke ambao kila mmoja ni NOT PERFECT ana matatizo yake si malaika.

Kujiandaa na kuwa tayari kwa ndoa ni pamoja na kufahamu kwamba kwenye ndoa kutakuwa na CHALLENGES ambazo kwa kushirikiana mke na mume wataweza kuzishinda na zaidi kuwa na ndoa sawa na NDOTO ZAO.
Kuamini kwamba umejiandaa vizuri kwa ndoa na kwamba ukikutana na HUGE DISAPPOINTMENT na kudhani kwamba si sahihi hii ina maana bado hukujiandaa kwa ndoa kwani ulikuwa na upande mmoja tu kwamba ndoa ni tambarare kama mawindoni.

Kuna msema kwamba:
“Marriage is a Romance in which the Hero dies in the fuirst chapter”
Hivyo badi kumbuka kwamba upendo wa mwanzo (honeymoon) ni fantasy ni siku halisi ni illusions upendo wa kweli hujengwa baada ya wawili kuvunjwa vunjwa na shida na matatizo na kushinda pamoja na kukiri wenyewe kwamba kweli mimi na mwenzangu tumetoka mbali.

Ukikutana na disappointment kwa mara ya kwanza katika ndoa yako usiinue macho kuangalia wanaume wengine kwenye ndoa zingine na ukajiona wewe ulikosea kumpata huyo mume wako bali shukuru Mungu kwa hayo unapitia na jambo la msingi kwa hazina kubwa ua upendo uliyonayo huku ukimuomba Mungu anza kuchimbua hazina ya ushujaa wa mume wako na kuijenga ndoa upya ili iwe na upendo wa kweli.

UJUMBE MUHIMU:
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
Mithali 14:1


4 comments:

Anonymous said...

Kaka asante sana kwa somo zuri na Mungu akubariki sana.

Lazarus Mbilinyi said...

Mpendwa,
Asante kwa comments zako, muhimu ni kwamba nimeanza series ambayo itachukua siku kadhaa kuzungumzia jinsi mwanamke anavyoweza kumfanya mume wake kuwa Hero hata kama mapenzi yameanza kutoweka. Kumbuka Mungu amempa mwanamke uwezo wa tofauti sana kuhusiana na suala la mahusiano ya ndoa.

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima

Anonymous said...

MUNGU ANAPENDA WAKATI WOTE TUWE NA FURAHA ASABABISHAE HAYO NI SHETAN SASA SIMAMA KUPANIA KUMHARIBU IBILISI NA UTAONA, MI NINA USHUHUDA MKUBWA SANA NILIPITIA MAPITO LKN MUNGU ATABAKI KUWA MUNGU MAANA NILIONA STAKI MSHAURI YEYOTE ISIPOKUWA NILIGUNDUA NINA MSHAURI WA AJABU YESU KRISTO WA NAZARETH MTENDA MUUJIZA SHETAN ALIPIGWA KISAWASAWA NA DAMU YA YESU NA NDOA YANGU NI VICHEKO TU SASA WAKAT WOTE.

MAMA D

Lazarus Mbilinyi said...

Mama D,

Hongera sana na Mungu akubariki sana kwa ushuhuda wako.

Huwa inashangaza sana kama hujajua kutumia silaha ya maombi katika jina la Yesu kwani kwake hakuna lisilowezekana.
Amen!

Upendo daima

Lazarus