"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 16, 2009

Sipendi kabisa sasa hivi......

Nina jipya lakini sipendi kuendesha!SWALI:
Kaka samahani kwa usumbufu naomba unisaidie swali langu:
Mimi mwanamke ambaye ni mwanandoa mpya kabisa na ndoa yetu ina miezi saba sasa.
Nampenda sana mume wangu hata hivyo nachukia sana kufanya sex kwani sijisikii chochote mume wangu akiwa ndani yangu.

Wote tulikuwa mabikira kabla ya kuoana hivyo naamini tatizo ni jinsi anavyofanya (move) ndani yangu (uke) kwani akiwa ndani yangu husugua polepole (so slow) na kusimama mara kwa mara bila kunisugua kwa uhakika.
Akinigusa clitoris yangu huwa najisikia kusisimka na raha zaidi lakini hafanyi chochote.
Nikiwauliza rafiki zangu wananiambia mume wangu ni bad lover kitu ambacho sikubaliana nacho kwani ukiacha sex mambo mengine ni shwari kabisa.

Nahisi kupoteza mood kabisa kwa hili tendo takatifu.
Je, nifanyeje ili mume wangu awe ananifanya ninavyotaka na kutamani na pia nitapataje mood na kuweza kufurahia ndoa yangu (sex)?

JIBU:
Dada inaonekana tangu mwanzo wa mahusiano yenu (uchumba) mlikuwa hamuongei masuala muhimu kama matarajio yako kuhusu sex na inawezekana ulidhani ukiolewa utaweza kuongea bila shida, hata hivyo umejikuta unaona ni ngumu kuongea masuala ya sex na mume wako.

Njia bora ni wewe kukaa na mume wako na kuongea wazi na kwa upendo bila kukefyakefya wala kulalamika.
Mwambie kile unapenda akufanyie na kinakufanya ujisikia raha na hatimaye kufurahia tendo la ndoa.
Inawezekana huwa anakuwa slow na haendi kwa speed kwa kuogopa kumaliza mapema hivyo mwambie wewe hutajali kama atafanya unavyotoka hata kama atamaliza mapema, wewe mhakikishie kwamba unamfurahia na unapenda iwe hivyo.
Sasa hapo hapo ulipo kabla hujamalizia kusoma hadi mwisho, chukua simu yako ya mkononi mwandikie message (sms) kwamba baadae una kitu kizuri unataka kumwambia hivyo mkifika nyumbani akukumbushe.

Huruhusiwi kuendelea kusoma kama hujatuma hivyo message au kumpigia simu kwani kutofanya hivyo ni kiburi na dhambi kama dhambi zingine, sitanii!

Pia njia nyingine ni wewe kuwa mjanja kumuomba mtumie milalo tofauti ambayo wewe ndo Utakuwa rubani wa airbus na kujihakikishia inapaa apende asipende.
Kwa mfano wewe mwanamke kuwa juu na yeye chini, kwa mlalo huu wewe mwanamke ndiye Utakuwa una control thrusting (speed, depth, angle nk) na masuala ya kuwahi kumaliza atajijua mwenyewe.
Pia kwa wewe kuwa juu anaweza kuendelea kuhudumia clitoris yako kwa kuipa stimulation kwa kutumia vidole au kidole huku wewe ukiendelea na rock and roll mbele na nyumba juu na chini.
Kwa njia hii unaweza kuimarisha excitement kwenye suala la mapenzi na kukuwezesha kufika kileleni haraka na kukupa mood zaidi ili kesho uhitaji zaidi.

Pia si vizuri kuombe ushauri kwa kila anayeitwa rafiki kwani rafiki ni wachache ila wanafiki ndo wengi na wengine wanamtaka huyo mumeo hivyo mlinde na mtunze na zaidi fanya kila mnaloweza kuhakikisha maisha yenu ya sex yanakuwa ya kuridhisha kwani kwa njia hiyo utajisikia ndoa yako inaridhisha.

Usikubali shetani aje kulala kitandani kwenu, mfukuze kwa maombi na pia kwa wewe kujifunza na kuongeza efforts kuwa innovative na creative idara zote hapo nyumbani.

Naamini kwa tips hizo unaweza kutatua tatizo lako, unaweza kuniuliza tena
Kama unaweza pitia posts za huko nyumba ambazo naamini zinaweza kukusaidia zaidi kuhakikisha maisha yako ya ndoa yanakupa kuridhika.
Ubarikiwe na Bwana!

5 comments:

Anonymous said...

Mmhh kaka pole na kuelimisha jamii,
Hivi haya maswali yoooote unayatoa wapi Mungu wangu kweli you are the talent Man keep it up and stay blssed
Yaahii huwa nafarijika sana pale ninaposoma blog yako, Please usiache kuendelea kutuelimisha namna hii?
Ubarikiwe na Bwana!

Lazarus Mbilinyi said...

Mdau hapo juu,
Maswali naulizwa na wale ambao wanakutana na mtatizo mbalimbali kwenye mahusiano yao.

Siwezi kutoa jina na pia huwa mengine yanajibiwa bila kupitia hapa "THE HILL OF WEALTHY" ni hiari ya mtu kwani wengine hupenda watu wote tujifunze kupitia maswali yao.

Ukiwa na swali unaweza kunitumie email (lazarusmbilinyi@gmail.com) naweza kukujibu wewe mwenyewe au ukitaka na wengine ila sitoi jina la mtu yeyote kwani ni confidential.

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima!

Jesse John said...

Umemjibu vizuri huyu dada kwani badala ya kumwambia mdhamini wake wa ndoa, anawambia marafiki zake.Pengine anaogopa akimwambia mume wake amsugue kwa nguvu, atamwona ameanza kua mjanja na kua na mashaka nae.

Anonymous said...

Umemjibu vizuri huyu dada manake si vyema kusema kwa marafiki.Bora angesema kwa wadhamini wake wa ndoa.Pia pengine anaogopa kumwambia mumewe amsugue kwa nguvu kwani atamuona ameanza kua mjanja na kua na mshaka naye.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Jesse,

Asante sana kwa maoni yako!

Kama mnaaminiana mke na mume ukweli unakuwa wazi kumwambia mpenzi wako unataka nini awe iweje, mawazo kwamba ataniona mhuni au mjanja hayana nafasi ila sema kama msingi wa mahusiano yenu ni kuogopana na hakuna uwazi na ukweli ndo issue anayotakiwa kuulizwa mpenzi wako unaenda kuwauliza rafiki zao.

Mawasiliano mazuri ambayo ni huru na wazi ni muhimu sana kwa mke na mume kwa maendelea ya ndoa yao.

Upendo daima