"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 1, 2009

Toolbox!

Kawaida kuna vitu au vifaa au mazingira ambavyo hutumika kuimarisha ufundi (techniques and skills) ukiwa na mke wako au mume wako wakati wa kuwa mwili mmoja na matokeo yake husaidia kila mmoja kujisikia raha na kuridhika na zaidi kuliko yote mnakuwa green (punguza carbon foot prints).

Kila jambo zuri huwa na maandalizi na maandalizi ni pamoja na kuhakikisha kila nyenzo muhimu inakuwepo kwa ajili ya shughuli muhimu iliyopo ili ilete raha na kuyapa maisha maana halizi.
Hapa hatuzungumzii sex toys bali tunazungumzia vitu muhimu ambavyo vikiwepo wakati wa sex basi huleta raha zaidi na kutengeneza mazingira yanayofanya kila mmoja ajisikia raha.

Lubricants:
Usiruhusu kuwa na ukavu wa aina yoyote sehemu za siri kwani huweza kumuumiza mwenzi wako hasa kwa wale (wanawake) ambao wana tatizo la kushindwa kuwa wet.

Mswaki na dawa yake au mouthwash:
Kwa ajili ya kuhakikisha kila mmoja anakuwa na kinywa safi kisicho na harufu inayifanya kila mmoja awe maili 5 kutoka kwa mwenzake.

Sabuni/ nzuri ya kuogea/ shampoo
Kabla ya tendo ni vizuri kuoga na kuwa safi na kila mmoja anavutia kimwili. Kuwa safi kimwili ni kiroho pia

Kiwembe/shaver
Si busara kuwa na msitu kwani uoto wa asili hutunzwa kwenye misitu asili na si katika mwili wa binadamu.
Ila inatokana na ladha ya wanandoa wengine wanapenda vichaka, it is up to you!

Vitambaa safi
Kujifuta kabla , wakati wa sex na baada ya sex.

Condoms
Kujikinga msije zaa watoto 35.

Chupi za kimahaba zinazovutia na kushawishi (Intimate lingerie)
Kama wewe ni mwanamke, kumbuka mwanaume huvutiwa kwa kile anaona au anaangalia.

Kioo kikubwa
Mwanamke unaweza kufurahia kufumba macho lakini yeye (mwanaume) mimacho itakuwa open na akijiona kwenye kioo basi anaweza kukufikisha mbali hadi kilele cha mliama kilimanjaro zaidi ya mara mbili.

Perfumes
Huweza kuchokonoa baadhi ya senses zake.

Taulo
Tandika chini kabla mvua haijaanza kunyesha hata kama baadae utafua mashuka yote.

Mwanga hafifu.
Kusiwe na mwanga mkali pia unaweza kuacha mwanga wenye harufu nzuri wa mishumaa maalumu (kama inapatikana - scented candles)

Usiri
Hakikisha mlango upo locked na simu imefungwa si busara kuacha kuwa mwili mmoja na kwenda kupokea simu na kurudi kuendelea tena (si ustaarabu na pia ni kukosa adabu)
Joto la kawaida
Kama baridi sana atahitaji kuvaa kitu na kama joto sana utamchosha (tumia ubongo)

Mood
Hii ndo ilitakiwa kuwa pale juu kabisa.
Je anapenda music aina gani wakati wa tendo takatifu ili kumliwaza na akukumbuke muda wote kupitia mazingira na huo muziki? naamini unajua.

Massage oil
Kumlainisha kwa uwezo wako wa kuwa (mwororo) tender.

Asali
Hutumika kwa kitu kinacholabwa kiwe kitamu zaidi.

Pipi/ Gum/mints
Kuondoa harufu mbaya mdomoni kabla na baada ya mahaba.

Maji
Wanasema sex ni zoezi la maana ambalo binadamu anaweza kupata hivyo kabla ya zoezi kunywa maji ya kiasi cha kawaida na baada ya sex kunywa pia, ingawa unashauriwa (mwanamke) kuwenda kukojoa (mkojo kila baada ya sex) usije pata UTI (urinary Track Infection)

Imarisha tendo la ndoa na mume/mke wako na kwa kutumia vitu vya kawaida kama hivyo unaweza kujihakikishia unakuwa na great sex na kutumiza ndoto za mwenzi wako.
Je viungapi vimetatwa hapo juu huwa unazingatia au ni kipi hakijatajwa ungependa wengine wajue?

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Unajua ile dhana ya VITU VIZURI NI VYA GHARAMA NA PENGINE SI "SAIZI" YETU inatuharibia saana
Wacha niendelee kujifunza juu ya vile vilivyo katika "reach" yangu kuniwezesha KUNOGESHA ndoa yangu.
Asante kwa hili na mengine tujifunzayo

Lazarus Mbilinyi said...

Mzee wa changamotO!
Issue ni kujua mazingira na kutumia kile kinapatikana katika mazingira yako na kufanya kweli kuboresha mahusiano yako so upo sahihi kwamba kile kilicho within your reach unaweza kukitumia kuboresha mahusiano yako na zaidi kutimiza ndoto za mpenzi wako.

Upendo daima