"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 25, 2009

Uchumba/Honeymoon ni mtoto!

Uchumba/honeymoon ni kitoto kichanga cha upendo wa kweli katika ndoa.Kizuizi cha faragha ya mapenzi (intimacy) kwa wanandoa.
Kukiwa na disappointment kwenye ndoa hasa mwanamke baada ya kuhisi yale alitegemea hakuna, huweza kuwa kizuizi kikubwa sana cha kujenga faragha ya mapenzi katika ndoa.
Kawaida ufahamu wetu kuhusu mapenzi (love) na ndoa kabla ya kuolewa au kuoa huwa unrealistic na si sahihi sana kwa kuwa tunakuwa bado tunakuwa hatujafika kwenye maisha ya kweli ya ndoa.
Kumbuka uchumba ni social activity ambayo unakuwa na interest kubwa ya kuwa na focus ya romantic yaani kila mmoja kumfurahisha mwenzake kiasi cha mwenzake kushindwa kuona hitilafu, kwa upande mwingine Ndoa ni task oriented work ambayo inahusisha kushirikiana katika uhalisi wa maisha ya kweli ya watu wawili imperfect.
Ikiingia kwenye ndoa unakutana na maisha halisi pande zote yaani positive na negative kama vile kuelewana na kuitoelewana, kupatana na migogoro, furaha na huzuni, kufurahishana na kuzozana, kufaulu na kushindwa.

Tatizo kubwa ni kwamba wengi huwa wanaingia kwenye ndoa na expectation za aina moja tu na akikosa vile alitegemea anakuwa frustrated na kujiona ameolewa au ameoa wrong partner, SI KWELI NI MTAZAMO WAKO TU UKIKUA UTAACHA NA UTAKUWA NA NDOA NZURI SANA.
Pia dunia ya sasa (modern society & information society/culture) imeathiri kwa kiasi kikubwa sana uelewa wetu kuhusu ndoa tofauti na wazazi wetu.
Chunguza jinsi media zinavyotudanganya kwa matangazo kuhusu wanawake, vijana na jamii kwa ujumla pia movie, TV, cartoons na romance novel vyote vinatupa hadithi za alinacha na kutudanganya kwamba sasa tunajua kuhusu ndoa.
Zinatudanganya kwamba mwanamke akimpata mfalme na yeye atakuwa malkia na atahudumiwa kama malkia na kwamba ameahidiwa kupata upendo wa kweli milele.

Fikiria kungekuwa na ndoa ambayo ziku zote ndani ya maisha mke na mume ni vilevile, si juu wa chini, hakuna disagreement kwa kuwa hakuna kitu cha kujadili na kutofautiana, hakuna mgogoro kewani wanaogopa kujieleza ukweli kwani mwenzake atakwazika.
Ukweli ni kwamba maisha yao yatakuwa shallow sana, hao ni wanandoa mfu, huwezi kupenda bila kukubali kwamba kawaida katika mahusiano kuna disappointment na conflict na pia ni mtazamo wako tu.
Wapo wanawake ambao kimtazamo wapo mbali kwa maana kwamba pamoja na disappointments, kuyeyuka kwa ndoto za yale aliahidiwa kabla ya ndoa bado huamua kuishi maisha ya furaha na kuendelea kutembea katika makusudi ya Mungu katika ndoa yake.
Wamefahamu kwamba masimulizi ya ukiolewa utakuwa princes ndani ya castle ya prince ni illusions ni vitu ambavyo vinaweza kuwa vipo au visiwepo.
Wanafahamu kwamba watu wazima wanaishi kwenye real world na kwamba upendo wa uchumba na honeymoon ni kitoto kichanga (infant) cha upendo wa kweli na kwamba kitahitaji kujifunza kutambaa, kutembea na kujigonda, kudondoka na hata kuumia ili siku moja hicho kichanga kiwe mtu mzima yaani TRUE LOVE
Wale wanaopingana na huu mtazamo hujikuta wakiruka toka mume mmoja hadi mwingine na kukutana na mambo yaleyale na walichofanya ni kubadilisha shape, size au rangi ya mwanaume ila matatizo yamekuwa mapya na makubwa zaidi.

Ni muhimu sana kuamini kwamba Mungu anao uwezo wa kufanya maajabu au miujiza katika magumu yote unapitia katika ndoa yako na anaweza kuiwezesha ndoa yako kuwa na upendo wa kweli.

Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa
ya mumewe.
Mithali 12:4

No comments: