"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, September 27, 2009

Una Uwezo wa kushangaza!

Mtu mwenye nguvu kuliko watu wote katika historia ya dunia alikuwa Samson, kama ingekuwa leo basi Samson angeitwa Mr. Universe au Mr. Israel.
Kama ni masumbwi basi Samson angebeba mikanda yote ya World Boxing Association (WBA) au World Boxing Council (WBC) au World Boxing Federation (WBF) au World Boxing Organization (WBO).
Hakuna cha akina Tyson wala Evander Holyfield au Wladimir Klitschko wote wangedundwa sekunde chache tu baada ya pambano kuanza.

Samson alikuwa shujaa (hero) kwa taifa la Israel, aliweza kuua simba kwa mikono mitupu, maelfu ya watu mikono mitupu pia na hata mageti ya vyuma yalishindwa kumfungia kwani aliyavunja bila huruma.

Samson alikuwa na ugonjwa na mabinti wa kifilisti (aliwapenda sana ingawa alionywa na kwake ikawa sikio lisiosikia...)
Mara ya kwanza alioana binti ambaye Biblia haimtaji jina na wengi huhisi hii ilikuwa ni Sababu tosha kwa Samsoni kuanzisha vita na wafilisti, ndoa haikudumu ilivurugika siku ya harusi hata hivyo Samson akampata mrembo mwingine kutoka kwa wafilisti, Delila ambaye hata hivyo wafilisti walimrubuni atafute siri ya nguvu za Samson.
Hata hivyo mke wa Samson yaani Delila alikuwa na nguvu kuliko Samson kama huamini subiri!

Huyu mwanamke alimaliza historia ya Samson na Samson akatoboa siri ya nguvu zake baada ya kuwekwa kufuani kwa Delila na matokeo yake akatobolewa macho na jina la Mungu wake likatukanwa.
Delila alitumia uwezo wake kama mwanamke kumshawishi Samson atoboe siri ya nguvu zake ambayo ilikuwa ni nywele zake kutonyolewa tangu utoto wake.
Baada ya kutoboa siri tu wafilisti wakamshika, wakamtoboa macho, wakamtesa na kumchezea kama mdoli na kumpa kazi ngumu.

Heading za magazeti ya KASHESHE, HABARI LEO, DAILY NEWS, THE GURDIAN, TANZANIA DAIMA, TAIFA LEO, MWANANCHI NA MENGINEYO YA WAKATI HUO HUKO ISRAEL yalipambwa na vichwa vya habari kuhusu Delila kummaliza Shujaa na Mbabe Samson, sipati picha!
(Kwa habari kamili kuhusu Samsoni soma Biblia kitabu acha waamuzi sura 13- 16)

Habari hii inatuelimisha au kutukumbusha kwamba uwezo alionao mwanamke kwa mume wake ni mkubwa ajabu na anaweza kufanya lolote anataka akijua jinsi ya kuchezesha kalata zake hasa kwa kujua mume wake udhaifu wake upo wapi.

Wanawake wote wanauwezo mkubwa sana juu ya wanaume tatizo kubwa wanawake wengi wameshindwa kutumia uwezo wao, ushawishi wao kuhakikisha mume anamuweka sawa au kufanya vile anapenda kwa sababu hawajajifahamu.
Hapa ninazungumzia kufanya yale ambayo mwanaume anaamini mume wake anazembea kama vile kuiweka ndoa katika mstari sahihi.

Ni kawaida kuwa na Generals, au Governors au Rais au mawaziri wanaume hata hivyo wengi wao hujikuta wake zao wakiwa chimbuko la uongozi wao na kwamba huwa wanawasaidia kutoa maamuzi ya mambo mengi.

Kuna usemi kwamba:
“A man’s wife has more power over him than the state”

Hata binadamu wa kwanza pale katika Bustani ya Eden alianguka baada ya shetani kumtumia Eva (mwanamke) kwa kumdanganya kula matunda na hatimaye amshawishi mume wake naye ale kwani alijua angemtumia mume ingekuwa ngumu sana mume kumshawishi mke akubali badala yake aliona mwanamke ni rahisi kumshawishi mume na akakubali.

Bottom line ni kwamba mwanamke anao uwezo mkubwa sana katika kuvumbua kile kilichomo ndani ya mume wake na kwamba mwanamke akitumia uwezo wake ambao Mungu amempa kuhusu mume basi anaweza kujenga mahusiano na ndoa imara na inayoridhisha.
Wapo wanawake kila kukicha ni kulalamika tu kwamba mume wangu mume wangu, acha kulalamika tumia uwezo wako wa kuwa mwanamke kumsaidia mume kuwa mume bora katika ndoa kwani Mungu amekupa uwezo wa ajabu ndani yako kiasi kwamba mume yeyote anaweza kumkubali kile mke anasema pale mke akitumia uwezo wake sawa na Mungu alivyompa.

2 comments:

Anonymous said...

WOOW HAPO NDO PENYEWE KABISA, NI KWELI KABISA BROTHER, MIMI KAMA MWANAMKE NIMEGUNDUA NINA MAJUKUMU MAKUBWA KUMSAIDIA MUME WANGU NA NIMEPEWA UWEZO NA MUNGU, SHIDA IPO WANAWAKE WENGI HAWAJUI KAMA WAMEPEWA UWEZO NAMUNGU WA KUWA WASAIDIZI, HATA KWENYE MAANDIKO MATAKATIFU BIBLIA, UKICHUNGUZA UTAONA WANAWAKE WALIOJISAHAU UWEZO WALIOPEWA NA MUNGU NA KUMSIKILIZA MUNGU WALISABABISHA MATATIZO KWA NDOA ZAO, MFANO SARAI NA ABRAHAM, SARAI ALISAHAU KAMA YEYE NA ABRAHAM NI MWILI MMOJA AKAMWAMBIA MUMEWE AMUINGILIE MJAKAZI HATIMAYE MJAKAZI ALIMDHIHAKI NA KUMDHARAU HAZAI,VISTA AKAACHWA AKAOLEWA ESTA,MKE WA LUTU AKASABABISHA WATOTO WAKE WAKALALA NA BABA YAO BAADA YA KUMNYWESHA KILEO, REBEKA UDANGANYIFU,EVA NA ADAM WAKAPOTEZA UTAJIRI WOTE WA EDEN NA TABU IKAANZA KWAO.
MUNGU TUSAIDIE WANAWAKE.
WANAWAKE TUOMBE SANA MUNGU ATUPE UWEZO, HEKIMA NA MAARIFA KUWA WASAIDIZI KWA NDOA ZETU.

KAKA LAZARUS NAKUUNGA MKONO KABISA MWANAMKE HAIPASWI KULALAMIKA NI KUINGIA MADHABAHUNI MWA BWANA TU NDO JAWABU NA KUNA SIRI KUBWA NA NGUVU YA MWANAMKE MWOMBAJI. MI NASEMA KAMA WANAWAKE WOTE WANGEJUA WAO NI KINA NANI NA KUFATA MWONGOZO WA MUNGU NA KUOMBA MAARIFA KWA MUNGU KUNGEKUWA HAMNA VIPIGO, TABU,VIMADA ,HAWALA KUINGILIA NDOA, MAANA MUNGU ANASEMA HAMNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA

MBARIKIWE WAPENDWA

MS GBENNETT

Lazarus Mbilinyi said...

MS GBENNETT,

Asante sana kwa comments zako ni kweli mwanamke ana uwezo wa ajabu sana na ukiwa ndani ya Kristo basi wewe una uwezo zaidi kwani Roho mtakatifu atakufundisha vyovyote unavyotaka kuwa.

Upendo daima